Hadithi: Wakili wa moyo

Hadithi: Wakili wa moyo

Jamani naomba tuungane wote kuwaomba hawa waheshimiwa watumalizie huu utamu.
Pliiiiiz waku. Mmetuachia ukiwa
 
Kwa nini mnatufanyia hivi lakini.
Yaani ni sawa na kulipia chumba hotel alafu demu anasema yupo period.
Msitufanyie hivyo wazee
 
Kwa nini mnatufanyia hivi lakini.
Yaani ni sawa na kulipia chumba hotel alafu demu anasema yupo period.
Msitufanyie hivyo wazee

Katika hili mheshimiwa mizambwa amenikwaza hakika. Ningekuwa na uwezo ningesusa kusoma hadithi zake zingine ila najua hata nikisusa mimi wengine wengi tu watasoma ko sina jinsi inabidi nisome tu...
 
Last edited by a moderator:
Katika hili mheshimiwa mizambwa amenikwaza hakika. Ningekuwa na uwezo ningesusa kusoma hadithi zake zingine ila najua hata nikisusa mimi wengine wengi tu watasoma ko sina jinsi inabidi nisome tu...

Kweli kabisa mkuu.
Wakati mwingine shida inakufanya uwe mtumwa
 
Last edited by a moderator:
Wakili wa moyo-50

Kuondoka ghafla kwa familia ya Hans
ilizidi kumshtua Mage na kujikuta
akitaka kususa sherehe. Ilibidi
achukuliwe na kupelekwa pembeni
na kuelezwa ukweli kuwa mpenzi
wake kachukuliwa na polisi.
Aliomba kupelekwa kituo cha polisi
ili akamuone mpenzi wake kwa
kuamini kupitia kwa rafiki wa baba
yake mkuu wa polisi atatoka.
Alifikishwa kituo cha polisi na
kupelekwa chumba alichokuwemo
mpenzi wake na kuonana naye.
Mage akiwa amechanganyikiwa
macho yakiwa yamemvimba kwa
sababu ya kumlilia mpenzi wake
ambaye hakujua yupo pale kwa kosa
gani.
“Vipi mpenzi kuna nini?”
“Mmh! Mambo magumu.”
“Kivipi?”
“Ile ishu imebumburuka.”
“Ishu gani?”
“Off air”
“Mungu wangu! Sasa itakuwaje?”
“Sijui, lakini naamini imekaa vibaya
kwa vile kuna ushahidi mkubwa wa
kunimaliza naamini siwezi kutoka.”
“Kwa nini?”
“Kila kitu kipo wazi lazima nitaozea
gerezani.”
“Sasa harusi yetu itakuwaje?”
“Mmh! Itategemea muujiza wa
ngamia kupita katika tundu la
sindano.”
“Yupo ba’ mkubwa naamini utatoka
tu,” Mage alimtia moyo mpenzi
wake.
“Nami ndicho ninachokiomba.”
“Hebu subiri.”
Mage alichukua simu na kumpigia
baba yake mkubwa Mkuu wa Polisi,
Kamanda Clarence. Baada ya kuita
ilipokelewa upande wa pili.
“Haloo.”
“Haloo baba,” Mage alisema huku
akilia.
“Vipi mama, mbona unalia?”
“Baba mchumba wangu
amechukuliwa kwenye ‘send off’
yangu na kuwekwa ndani.”
“Kwa kosa gani?”
“Hakuna kosa lolote zaidi ya
uonevu.”
“Naomba kuzungumza na mkuu wa
kituo.”
“Sawa baba.”
“Mpenzi nimeshazungumza na baba
utatoka sasa hivi ngoja nipeleke
simu kwa mkuu wa kituo,” Mage
alimueleza mpenzi wake huku
akielekea kwa mkuu wa kituo.
“Hakuna tatizo.”
“Samahani kaka kuna simu kutoka
kwa mkuu anataka kuzungumza na
mkuu wa kituo,” alimwambia askari
mmoja aliyekuwa kaunta.
“Mkuu gani?”
“Mkuu wa polisi wote.”
“Nenda chumba cha pili mkono wa
kushoto.”
Mage alikwenda hadi mlangoni na
kuingia bila hodi kitu
kilichomkasirisha mkuu wa kituo na
kutaka kumfukuza.
“We binti toka nje unaingiaje kama
msalani.”
“Kuna simu yako toka kwa mkuu wako
unatakiwa kuzungumza naye.”
“Mkuu gani?”
“IGP.”
“He! Nipe,” mkuu wa kituo Aloyce
Jacob alishtuka na kuichukua simu
haraka, aliweka sikioni na kusema
kwa sauti ya juu.
“Samahani afande.”
“Bila samahani pole na majukumu.”
“Asante mkuu.”
“Kuna kijana mmemkamata usiku
huu akiwa kwenye send off ya
mchumba wake?”
“Ndiyo mkuu.”
“Kwa kosa gani?”
“Lile la mauaji tulilokuwa
tukipeleleza.”
“Sasa yeye anahusika vipi?”
“Ndiye mtuhumiwa mkuu.”
“Una uhakika?”
“Kila kitu kipo wazi, kesho faili lake
tunalifikisha mahakamani.”
“Nipe huyo binti.”
Simu alipewa Mage aliyekuwa
akifuatilia mazungumzo ambayo
yalimtisha na kuona tatizo la mpenzi
wake lilivyo zito lakini aliamini
kupitia wadhifa wa baba yake
mkubwa lazima ataachiwa tu.
“Haloo baba.”
“Sasa mama suala la mpenzi wako
lipo kisheria sana, hivyo nakuomba
rudi nyumbani ili vyombo vya dola
vifanye kazi yao.”
“Sasa baba harusi yangu itakuwaje?”
“Naomba urudi nyumbani, kesho
nitakuja.”
“Sawa baba.”
Mage alirudi kwa Hans kumweleza
alipofikia, Hans aliamini hali ilivyo
kulikuwa hakuna dhamana mpaka
upelelezi ukamilike. Aliamini
ukikamilika lazima utamtia hatiani
na kufungwa.
Ilibidi Mage arudi nyumbani kwao
akiwa amechanganyikiwa kutokana na
tukio lile aliamini ndoa hakuna na
atakuwa amepoteza mwana na maji
ya moto. Kwa vile sherehe ilimalizwa
alirudi nyumbani. Mama yake naye
aliona sherehe ya mwanaye imeingia
nuksi alitaka kujua kipi
kilichompeleka mchumba wake polisi.
“Si lile tatizo lililoniweka ndani.”
“La kifo cha mke wa Hans?”
“Ndiyo.”
“Sasa yeye anahusika vipi?”
“Eti kahusika kumuua mkewe.”
“He! Ili iweje?” mama Mage alishtuka
kusikia habari zile.
“Mimi sijui, eti mama mtu
akishitakiwa kwa kosa la kupanga
mauaji hukumu yake ipo vipi?”
“Kama hajatenda hawezi kufungwa
lakini kama kweli amehusika hukumu
yake ni miaka 30 au jela maisha.”
“Mungu wangu nimekwisha!” Mage
alisema kwa sauti ya kukata tamaa.
“Mbona unasema hivyo?”
“Mashtaka ya Hans ni ya kupanga
njama za kifo cha mkewe.”
“Sasa wasiwasi wako nini ikiwa
haimuhusu, nitampigia simu baba
yako mkubwa yataisha.”
“Mama nilizungumza na baba na
kutaka kuzungumza na mkuu wa
kituo baada ya mazungumzo
aliniambia mashtaka yapo kisheria
hivyo tuache vyombo vya dola
vifanye kazi yake.”
“Mmh! Kama baba yako kasema hivyo
itabidi tuwe watulivu.”
“Mama nina wasiwasi huenda harusi
yangu haitakuwepo.”
“Kwa nini?”
“Nina wasiwasi mpenzi wangu
atafungwa.”
“Kwa nini unasema hivyo?”
“Hata sijui, mama hivi nikimfuata
Colin atakubali kweli kunirudia?”
“Mage umefikiria nini tena mama!
Kwa nini umefikia huko, mchumba
wako yupo ndani na hana kosa
alilotenda, atatoka tu.”
“Sasa tutafanyaje?” Mage aliuliza.
Itaendelea wiki ijayo.
 
ILIPOISHIA:
“Nina wasiwasi mpenzi wangu
atafungwa. ”
“Kwa nini unasema hivyo?”
“Hata sijui , mama hivi
nikimfuata Colin atakubali
kweli kunirudia ?”
“Mage umefikiria nini tena
mama! Kwa nini umefikia
huko , mchumba wako yupo
ndani na hana kosa alilotenda
atatoka tu. ”
“Sasa tutafanyaje?” Mage
aliuliza.
JIACHIE MWENYEWE . ..
Mara simu ya Mage iliita
ilikuwa ikitoka kwa mama Hans ,
alichukua na kuiweka sikioni.
“Haloo mama.”
“Nina imani sasa umefurahi .”
“Nifurahi nini mama?”
“Haya sasa mwanangu
anafungwa kwa ajili yako, haya
fanya sherehe kwa vile dhamira
yako imetimia , umekuwa kama
jini wa kutumwa humuachi mtu
mpaka uone amefukiwa .”
“Mama utanionea bure. ”
“Tunashukuru kwa
ulichotufanyia ila Mungu yupo ,”
baada ya kusema vile alikata
simu na kumuacha Mage
kasimama kama sanamu kitu
kilichomshtua mama yake .
“Nini tena?”
“Mama huu mkosi gani?” Mage
alisema huku akilia .
“Kwani kuna nini tena
mwanangu mbona unataka
kuniuguza presha?” mama yake
alitaharuki .
“Siamini maumivu ninayosikia
juu ya mpenzi wangu kuwekwa
ndani na kubambikiwa kesi
nzito halafu familia yake
inasema eti nimefurahi! Mimi
Mage nifurahi kufungwa kwa
mpenzi wangu ?” Mage
alimuuliza mama yake huku
akibubujikwa na machozi ya
uchungu.
“Nani amekuambia hivyo ?”
“Mama Hans .”
“Unaona mwanangu ile siyo
familia badala ya kukuonea
huruma ndiyo kwanza
wanakulaumu, ufanye vile ili
iweje ungeweza kuvuruga ndoa
yako kama mtu humpendi .”
“Mama nakuapia Hans akinioa
sitaki kuwaona ndugu wa
mume.”
“Mage mwanangu hayo siyo
maneno, bado tunataka
kuonesha upendo kwa wenzetu
kipindi hiki kigumu. ”
“Mama wakati Hans yupo ndani
nataka kuzungumza na Colin
naamini ananipenda sana .”
“Ukishazungumza naye?”
“Ili nikamate huku na huku
kama Hans atafungwa basi niwe
na Colin . ”
“Na Hans akitoka gerezani na
kukuta umeolewa?”
“Nitajua, nina imani Colin
nammudu, nitamweleza ukweli
kuwa kwake nilikuwa najiegesha
na nimpendaye karudi. Mbona
anajua kuwa kwa Hans
nimekufa nimeoza .”
“Mage kumbuka ukianzisha
uhusiano na Colin mpaka
kufikia kufunga ndoa lazima
watu watasema umehusika
kumfunga mpenzi wako hapo
ndipo utaongeza uhasama na
familia ya kina Hans .”
“Nitafanya kwa siri .”
“Colin akitaka kukuoa ?”
“Nitamvuta kwa muda ili
kumsubiri Hans , kama
anafungwa maisha sina jinsi
kama miaka saba nitajishikiza
kwa Colin .”
“Ulivyomuacha atakukubali
kweli, ha. .ha ..lafu leo kaingia
na msichana mrembo ni nani
yake?”
“Mpenzi wa raafiki yake ,” Mage
aliongopa.
“Mmh ! Ili kutengeneza
mazingira mazuri unatakiwa
kujipendekeza kwa mama
Colin. ”
“Nitafanya hivyo , najua yule
mama ananipenda sana
nikimfuata na kumweleza
nimerudi kwa mwanaye nina
imani atapiga vigelegele.”
“Mmh ! Haya. ”
Mage aliachana na mama yake
na kwenda chumbani huku
mawazo yake yote yakiwa kwa
Colin kutokana na kuujua
ukweli wa kesi ya Hans kwa
kuamini kutoka kwake kutakuwa
ni muujiza.
Alipanga kuanza kujipendekeza
kwa familia ya kina Colin wakati
akisubiri hukumu ya mpenzi
wake.
***
Colin alimpeleka Cecy chuo cha
urembo ambako alisoma kwa
miezi mitatu , muda wote
walikuwa kama kumbikumbi kila
mmoja alionesha mahaba
mazito. Taarifa ya kukamatwa
mchumba wa Mage iliwafikia na
kushangaa taarifa ya kukamatwa
kwake kuwa alihusika na kifo
cha mkewe na mwanaye ili tu
amuoe Mage .
“Colin yaani naomba kama
mama yako atasababisha
tutengane usifanye kama
mpenzi wa Mage alivyofanya.
Heshimu uhai wa mtu, kama
ipoipo tu , Mungu ana maajabu
yake ameweza kutukutanisha
pamoja bila sisi wenyewe kujua.
Kwa hivyo ni makosa
kulazimisha kitu .”
“Cecy kila dakika nakuwa
mwanafunzi wako, wewe ni
zaidi ya mwanamke pamoja na
umri mdogo lakini Mungu
amekupa busara na hekima .”
“Kwa kweli kama ni kweli
mpenzi wa Mage anahusika
kutenda unyama ule kwa ajili ya
Mage atakuwa ametenda
dhambi kubwa sana .”
“Mi’ siamini mtu anaweza
kumuua mke na mwanaye kwa
ajili ya mpenzi wake .”
“Kwa hiyo ungemuoa Mage ,
mimi ningekuwa na nafasi gani
moyoni mwako ?” Cecy
alimuuliza swali la kizushi .
“Cecy tuachane na hayo ,
unakumbuka wiki ijayo ndiyo
onesho lako la kwanza la
mavazi, mazoezi yako yamenipa
matumaini ya kuishtua dunia.”
“Mmh ! Nitafunikaje maana
nguo zote nilizojipima hadi
mwenyewe najionea wivu , si
vibaya kujisifia mi ’mzuri
bwana. ”
”Siyo mzuri bali ni mrembo ,”
Colin alimrekebisha .
“Bwana eeh, urembo
unatengenezwa lakini uzuri ni
wa asili .”
“Sawa mama umeshinda.”
Wiki moja baadaye liliandaliwa
onesho la kwanza la mavazi la
kampuni ya Colin ambalo
litaoongozwa na Cecy.
Matangazo yalirushwa mwezi
mzima katika vyombo vyote vya
habari na kufanya watu wengi
wavutike na kuapa kutolikosa .
Miongoni mwa watu walipanga
kwenda kwenye onesho hilo la
kwanza la kimataifa alikuwa ni
Mage na shoga yake Brenda .
Washiriki walikuwa wengi
kutoka ndani na nje ya nchi na
kufanya onesho lile lizidi
kuvutia watu wengi.
Siku ya onesho ilipowadia ,
Mage na shoga yake Brenda
walikuwa miongoni ma watu
waliohudhuria onesho hilo
lililojaza watu wengi. Muda
ulipofika maonesho yalianza
kwa kuanza kupita wageni
ambao walionesha mavazi ya
kigeni na kuwafanya watu
walipuke mayowe.
Baada ya kumaliza wageni
lilianza vazi la Kitanzania
kuanzia vazi la vitenge, khanga
na vikoi .
Walianza kutangulia mabinti
ambao nao walikuwa katika
kampuni hiyo. Baada ya kupita
wote ikafika kipindi akatokea
Cecy katika vazi la kitenge
chenye kilemba kirefu na
kufanya ukumbi ulipuke
mayowe.
Alipita kwa mavazi zaidi ya
kumi ya ubunifu na kuacha
historia kwenye onesho
hilo.
Itaendelea wiki ijayo .
 
aisee,mi huwa napitaga hapa mara moja moja,ila hii kitu imenigusa sana hebu malizia mkuu
 
Mh. Mmary asante kwa kulikomboa jahaz lililokuwa likizama kwa kukata tamaa. Ila sasa na wewe usije kututupa km wengne mkuu
 
Huyu Magie mwehu kamili anayejua kuoga tu changanya na mama yake uuuuuuwwwwwwwwwwwiiiii nakosa neno.
 
kunakipande kimerukwa maana hatukualikwa sendoff tumeshangaa watu wamekamatwa na police
 
Back
Top Bottom