Hadithi tamu: Hisia zangu

Hadithi tamu: Hisia zangu

daaa jamani nanunua bikra kama kuna mwenye nayo ani PM.
 
Kutokana na watu wengi kuwa na kiu na hadithi hii, leo tena nimeamua kuileta mapema kabla hata kufika Jumatatu, nadhani umeburudika vya kutosha, ni miye mtumishi wenu Mommadou Keita.

HISIA ZANGU-16
ILIPOISHIA...

“Nakuhakikishia,” akasema Pam.
Lilian akajivuta kwa Pam, akalala kifuani mwake. Penzi jipya lilifumuka kwa wawili hao.
Waliamka kwa pamoja na kuelekea bafuni kuoga kisha wakavaa na kuondoka. Pam alimrudisha Lilian mpaka chuoni.
Lilian alikuwa na jambo moja tu kichwani mwake; angemwambia nini Edo kuhusu usichana wake? Hakuwa na jibu!
Huo ndiyo mtihani mgumu uliokuwa mbele yake.
SASA ENDELEA...

ULIKUWA zaidi ya mtihani. Siku zote alimwambia alikuwa na usichana wake, jambalo lilikuwa la kweli tupu. Ahadi yao ilikuwa ni kukutana faragha mara baada ya kufunga ndoa.
Ni msimamo ambao yeye ndiye aliyeushikilia zaidi. Kilichomuuma ni kuja kuutoa usichana wake kirahisi kiasi kile. Alijua wazi kuwa, hakuwa na mapenzi hata kidogo na Pam, ni fedha ndizo zilizomchanganya.
Moyoni alikuwa na majuto makubwa, tamaa ya fedha ndiyo mwanzo wa matatizo yote hayo. Hata hivyo moyoni alikiri kuwa, hakuwa na njia nyingine zaidi ya hiyo.
Isingekuwa rahisi awe na Pam, ampe fedha zake bila chochote kuendelea. Hilo lingekuwa jambo la ajabu sana.
“Sina namna, tayari nimeshaingia kwenye mambo ya kikubwa, siamini kama imekuwa rahisi kiasi hiki,” alijisemea wakati akitembea taratibu kuelekea hosteli.
Akiwa anatembea, simu yake ikaita, alipotupa macho yake kwenye kioo cha simu, akakutana na namba za mpenzi wake, Edo. Mara moja akapokea.
“Haloo!”
“Haloo mpenzi wangu, habari za huko?”
“Salama. Wewe je?”
“Mimi ni mzima, nashukuru naendelea vyema na masomo. Nimekupigia simu hii kwa ajili ya mambo mawili muhimu.”
“Mambo gani?”
“Kwanza kukuomba msamaha.”
“Msamaha?”
“Ndiyo mpenzi, kukuomba wewe msamaha.”
“Kwa kosa gani tena mpenzi?” akauliza Lilian akionekana kuwa na mashaka kidogo.
Alijaribu kuwaza kuhusu msamaha aliosema, akashindwa kuelewa kabisa. Kwa namna ilivyokuwa, yeye ndiye aliyetakiwa kuomba msamaha kutokana na kuvunja ahadi yao.
Kichwa kikamuuma, akawaza kuwa huenda Edo alikuwa akizungumza mambo kinyume. Kwamba huenda alikuwa akimaanisha yeye.
“Hata kama alikuwa akimaanisha mimi, itawezekanaje basi hata ajue? Yeye yupo Malaysia, mimi Tanzania, wapi na wapi? Hili ni jambo gumu kutokea bwana,” akazidi kuwaza.
“Lilian,” Edo akaita.
“Nakusikia Edo.”
“Nisamehe mpenzi.”
“Baby niambie bwana.”
“Jana ilikuwa siku yako ya kuzaliwa!”
“Najua Edo.”
“Kosa langu ni kutokupongeza mapema tangu jana, lakini nina sababu za msingi ingawa sipendi kukueleza, ila naomba ufahamu kuwa ninajua umuhimu wa siku yako hiyo na thamani yangu kwako kama mwanaume wako. Happy birthday Lilian,” akasema Edo kwa msisitizo sana.
“Thanks. Usijali, najua huko utakuwa na majukumu mengi, kwa hiyo kawaida tu, isikupe shida sana mpenzi wangu,” akasema Lilian.
“Nashukuru.”
“Ila kuna jambo kubwa sana nitakufanyia siku chache zijazo,” akasema Edo.
“Mh! Bwana unanitisha sasa. Ni jambo gani hilo?”
“Surprise, siwezi kusema chochote kwa sasa, muda ukifika utajua tu. Vuta subira mpenzi wangu,” akasema Edo.
“Poa mpenzi.”
Wakakata simu zao.
Lilian wakati akizungumza na simu alikuwa amesimama, hivyo alivyokata tu simu akaanza kutembea tena. Chumbani kwao aliwakuta Lucy, Latifa na Leila wakiwa bado wamejilaza. Hata hivyo hawakuwa kwenye usingizi.
“Mama lao nakuona!” akasema Lucy kwa sauti iliyoonyesha alikuwa akijua kilichoendelea.
“Mambo zenu,” akasalimia.
“Poa, pole mwaya!” akadakia Latifa.
“Pole ya nini tena?” Lilian akauliza akiwa ameukunja uso kidogo.
“Naona mwenzetu hujarudi kabisa jana!” akasema Latifa.
“Sasa ndiyo unipe pole?”
Wote wakacheka.
“Ungepewa nini sasa, maana wenzako wote kweli tuna mambo hayo, lakini hadi asubuhi?”
“Mh! Kweli mtu hawezi kuona tatizo lake, Latifa wewe hukulala na Big siku ile ukarudi kesho yake mchana? Bora hata mimi nimerudi asubuhi,” akasema Lilian kwa kujiamini.
Wakacheka tena.
Lilian akaamua kuingia bafuni, akaoga haraka kisha akatoka na kujitupa kitandani.
“Sitaki usumbufu leo, hata darasani sitakwenda, nahitaji kupumzika siku nzima ya leo,” akasema Lilian.
“Sawa mama, umesomeka!” Lucy ndiye aliyejibu.
Lilian akavuta shuka, kama vile alikuwa amelala usiku. Akajitahidi kuvuta usingizi.
***
WIKI MOJA BAADAYE
Lilian hakuamini macho yake, aliendelea kukaza macho yake kwenye kioo cha simu yake ili kupata uhakika wa alichokuwa akikiona, lakini bado kiliendelea kuwa vilevile.
Namba iliyokuwa ikimpigia ndiyo iliyomchanganya Lilian. Namba ya mpenzi wake Edo ya nchini Tanzania.
“Mh! Inamaana Edo yupo Bongo?” akajiuliza.
Alijiuliza sana, lakini baadaye akagundua maswali yake yasingekuwa na maana kama asingepokea simu na kuujua ukweli. Mara moja akabonyeza kitufe cha kupokea.
“Haloo,” akaita Lilian.
“Surprise! Surprise!” akasema Edo.
“Baby really?” akauliza Lilian.
“Yeah baby, nipo jijini Dar es Salaam,” akasema Edo kwa furaha.
“Uko wapi nikufuate mpenzi wangu?”
“Ha! Ha! Ha! Huo ni wimbo wa Ray C! Sikia nipo hapa chuoni.”
Lilian alihisi kuzimia!

Itaendelea wiki ijayo.

LILIAN yaani kama namuona vile anavyotaka kudondoka kwa hofu.

Na bila shaka haja ndogo inamtoka hapo pasipo kutarajia
 
Afanye mpango haraka amtafute Lameck (kizuizi) ampe dawa arudishe bikira otherwise patachimbika.
 
Afanye mpango haraka amtafute Lameck (kizuizi) ampe dawa arudishe bikira otherwise patachimbika.

Ahahahahh, nimechekaje vasbh asbh, ngoja tumwambie mizambwa amuombee kwa Lameck, Lily pole weee, na kwa hofu uliyonayo lazima eddo atagundua kitu, shauri yako
 
ILIPOISHIA...
Alijiuliza sana, lakini baadaye akagundua maswali yake yasingekuwa na maana kama asingepokea simu na kuujua ukweli. Mara moja akabonyeza kitufe cha kupokelea.
“Haloo,” akaita Lilian.
“Surprise! Surprise!” akasema Edo.
“Baby really?” akauliza Lilian.
“Yeah baby, nipo jijini Dar es Salaam,” akasema Edo kwa furaha.
“Uko wapi nikufuate mpenzi wangu?”
“Ha! Ha! Ha! Huo ni wimbo wa Ray C! Sikia nipo hapa chuoni.”
Lilian alihisi kuzimia!
SASA ENDELEA...

KWA sekunde kadhaa alibaki amesimama ameduwaa kabisa, bila kujua cha kufanya. Hakujua kama alikuwa na furaha au huzuni. Hakuna alichojua kuhusu tukio lile! Furaha ya Edo kuja na huzuni ya kuja kumtibulia penzi lake jipya kwa Pam!
Edo kuwa Tanzania, tena chuoni! Lilikuwa jambo kubwa na la kushtukiza kuliko kawaida. Alibaki hewani, akavuta pumzi ndefu sana kisha akazishusha taratibu kabisa.
Edo alikuwa amemchanganya sana.
“Baby are sure?” akauliza Lilian.
“Yes baby, kwani nina utani na wewe?” akasema Edo.
“Najua huna, uko maeneo gani sasa?”
“Kwani wewe uko wapi?”
“Utawala.”
“Hata mimi pia nipo hapa Utawala.”
Lilian akazidi kuchanganyikiwa. Kama ni mshtuko ulikuwa wa kipekee kabisa kuwahi kutokea katika maisha yao ya kimapenzi.
“Hebu geuka, angalia upande wa kituoni, kuelekea Survey!” akasema Edo.
Lilian akafanya hivyo!
Hakuamini!
Edo alikuwa amesimama upande wa pili. Ghafla Lilian akataka kuvuka barabara, Edo akamwonyesha ishara kwamba asifanye hivyo. Akatulia kwa muda, kisha Edo akavuka na kumfuata.
Walirukiana na kukumbatiana kwa nguvu. Kwa zaidi ya dakika mbili walikuwa wameng’ang’aniana bila kuachiana. Walikuwa na mengi ya kuongea.
“Mambo baby?” Lilian alimwambia Edo akijitoa kifuani mwake.
“Poa.”
Tayari macho ya Lilian yalikuwa yameshajaa machozi kila kona. Hakutegemea kabisa kukutana na Edo muda ule, ingawa kichwani mwake alikuwa na mawazo sana na mpenzi wake mpya Pam.
“Umependeza sana mpenzi,” akasema Lilian.
“Hata wewe pia mama, umependeza mpaka kidogo nikusahau!”
Wakacheka sana!
“Kwa nini umekuwa bonge hivyo? Unakula nini?” Edo akauliza tena.
“Kama kawaida, vyakula vya hapa chuoni si unavijua!”
Walizungumza mengi, mwisho Edo akamwambia Lilian watoke waende kwenye hoteli aliyofikia. Lilian hakubisha, alikubali haraka sana.
“Tusubiri daladala hapa,” akasema Lilian.
“No! Nimekuja na teksi.”
“Sawa, wapi sasa?”
“Tabata.”
“Sawa.”
Wakavuka barabara, Edo akampigia simu dereva ambaye alikuwa ameegesha kwenye maegesho, muda mfupi baadaye, gari aina ya Toyota Corolla liliegesha mbele yake. Edo akasogea na kufungua mlango wa siti za nyuma.
“Karibu malkia wangu,” akasema Edo akiachia tabasamu mwanana.
“Ahsante mfalme wangu!”
Wakacheka!
Baada ya Lilian kuingia ndani ya gari, alifuata Edo ambaye alibamiza mlango kwa nguvu. Dereva akawasha gari na kuliondoa kwa kasi.
Njia nzima walikuwa wakizungumza mambo mbalimbali kuhusu maisha baada ya kutengana kwa muda mrefu. Edo alikuwa akimpenda sana mpenzi wake. Alimweleza kila kitu kuhusu uzuri wa nchi ya Malaysia.
Muda wote, Lilian alikuwa na mawazo na Pam, hakujua ingekuwaje kama angempigia. Hakutaka kabisa kitu hicho kitokee.
“Kifupi bado kidogo tu nimalizie masomo yangu. Nimefurahi kukukuta mzima mpenzi wangu. Najua unakosa misaada yangu kwa kipindi hiki lakini usijali mambo yanakaribia kuwa mazuri na utaratibu utaendelea kama kawaida,” akasema Edo.
“Najua baba, wala hupaswi kuniambia mpenzi wangu. Najua mazingira ya nje.”
“Nashukuru kwa kuelewa.”
Ukweli uliokuwa ndani ya Lilian, ni kwamba hakuwa na shida ya pesa hata kidogo, Pam alikuwa akimwezesha kwa kila kitu. Kutokana na mazungumzo ya hapa na pale, Tabata hapakuwa mbali sana.
Walifika wakiwa hawajachoka hata kidogo, ni kama hawakuwa kwenye safari. Walishuka garini, Edo akamlipa dereva kisha wakatembea wakiwa wameshikana mikono wakielekea ndani ya hoteli aliyofikia Edo.
Walipoingia tu chumbani, walivutana kwa nguvu kisha wakaanza kubadilishana mate. Muda mfupi baadaye, wote wakiwa wanahema kwa kasi, wakajikuta wakiwa watupu! Hakuna aliyekuwa na hiyari ya kufanya tendo hilo.
Jambo lililomshangaza Edo ni kwamba, Lilian alionyesha dalili zote za kuhitaji tendo la ngono. Ilikuwa ni maajabu sana kwa Edo. Lilian ambaye siku zote alikuwa mgumu akionyesha msimamo, iweje leo akubali kirahisi namna hiyo?
“Hapana, kuna kitu. Lazima...” akajisemea moyoni mwake.
“Baby please, I’m hot,” Lilian akasema kwa Kimombo.
Wote walikuwa kama walivyozaliwa, ilikuwa kazi ngumu sana kwa Edo, lakini alijitahidi sana kuzuia hisia zake. Mara moja akajiondoa mikononi mwa Lilian.
“Vipi?” Lilian akauliza akiwa amekunja uso wake kwa hasira.
“Siyo makubaliano yetu Lilian.”
“Najua mpenzi, lakini mwili wangu umewaka kwa tamaa ya mapenzi, sina namna. Nisaidie mpenzi.”
“Lilian, lakini wewe ni bikira.”
“Najua mpenzi, nimeamua kukupatia hii zawadi leo.”
“Hapana.”
“Lakini si wewe ulikuwa unang’ang’ania kila siku tukutane? Iweje leo unakataa tena unakuwa mkali kiasi hicho?” akasema Lilian.
“Tutafanya hivyo lakini mpaka tupime ukimwi.”
“Kwahiyo mimi naonekana nina ukimwi siyo?”
“Kwa nini usifikiri labda mimi ndiye naonekana nina ukimwi? Tunahitaji kuwa waangalifu mpenzi. Tuna mipango mingi sana mbele yetu kuhusu maisha yetu. Hatuwezi kuwa rahisi kiasi hiki. Kama kweli unanipenda, tutoke sasa hivi, twende tukapime tuwe na uhakika na afya zetu kisha tuendelee na mambo mengine,” akasema Edo.
“Sawa,” akasema Lilian kwa hasira, akainuka kitandani na kukimbilia bafuni ambapo alioga, alipotoka alimkuta Edo ameshavaa anamsubiri yeye.
“Haya twende,” akasema Lilian.
“Ok!”
Edo akabamiza mlango, akaingiza ufunguo kwenye kitasa, akafunga. Wakaanza safari ya kwenda kituo cha afya.
Nini kitatokea? Utamu ndiyo kwanza unaanza. Usikose Jumatatu ijayo hapahapa.
 
lilian ameathirika wallai pam simwamin kabisaaaaa
 
ebana da mm sithemi kitu nenden tu mkapime wajameni.....
 
Edo mkaree..anaambiwa "baby am hot,anaanza kuleta maswala ya kupima ngoma..
 
Edo alishindwa nn kutumia condom, hii nafasi hatokaa aipate tena.!!#!
 
Back
Top Bottom