Hadithi tamu: Hisia zangu

Hadithi tamu: Hisia zangu

Hivi jamani hakuna adhabu nyingine anayoweza kupata aliyeshindwa kuwa mwaminifu badala ya hii award ya HIV? Bro mleta maada naomba contact za Lily tumpime tena yumkini majibu aliyopewa sio yake!
 
Maskini Lily, mshahara wa dhambi ni mauti mamangu, pole sana
 
Wadau hebu muwe mnanishtua nayapenda sana haya mambo
 
DAAAA SIJUI NIMEKOSEA SEHEMU YA -20 AU SIYO?
“Uko wapi Pam?” akasema Lilian akionekana kulia.
Kilio chake kilisikika kupitia simu aliyokuwa akizungumza na Pam.
“Una nini? Kuna msiba au?”
“Bora ingekuwa msiba.”
“Tatizo ni nini?”
“Pam tuonane kwanza please!” akasema Lilian akizidisha kilio.
“Wewe una nini?”
“Pam kwa nini hukusema mapema?”
“Kusema nini?”
“Pam umeniua Pam, umenipa ukimwi. Umeharibu ndoto zangu, umesababisha mpenzi wangu hanitaki tena. Kwa nini Pam? Kwa nini?” akasema Lilian akizidi kulia.
Pam akacheka sana!
“Unanicheka?”
“Sikucheki bali unachekesha!” akasema Pam akizidi kukaukia kwenye simu.
Pam anacheka!
Lily analia!
Lilian alihisi dunia chungu, alitamani kuchimba shimo ili aingie humo, asionekane na mtu yeyote!
Hilo halikuwezekana!
SASA ENDELEA.

KICHEKO! Vipi mtu acheke wakati amepewa taarifa mbaya! Jambo hilo kwa Lilian lilikuwa tatizo kubwa sana. Hisia zake zilivurugika hakika.
Alijiuliza maswali mengi sana bila kupata majibu ya moja kwa moja. Pam bado alikuwa hewani...
“Pam...” Lilian akaita.
“Nakusikia.”
“Una nini? Au unajua ulichokifanya?”
“Huna jipya Lilian, nadhani jambo la msingi kama ulivyosema tuonane, nitajua cha kufanya.”
“Utajua cha kufanya?”
“Ndiyo nitajua cha kufanya.”
“Unamaanisha nini?”
“Namaanisha kuwa nitajua cha kufanya baada ya kuonana na wewe.”
“Saa ngapi?”
“Leo jioni.”
“Sawa.”
Lilian alijihisi kuchanganyikiwa sana. Akachukua gari lililompeleka moja kwa moja chuoni. Aliposhuka, alitembea kwa kasi kulekea chumbani kwao. Bahati nzuri aliwakuta rafiki zake wote wapo.
Aliyekuwa na shida naye zaidi alikuwa ni ....... akamvaa...
“Nataka uniambie ulikuwa na maana gani?” akasema Lilian akitetemeka kwa hasira huku machozi yakiendelea kuchuruzika machoni mwake.
“Manaa gani kivipi?” akauliza.”
“Hujui eeh?”
“Ndiyo sijui.”
“Paaaaa...” kilikuwa kibao kilichotua shavuni mwa ..... barabara.
“Hivi wewe umechanganyikiwa? Kwanini unanipiga kiasi hicho?”
“Ni kwa sababu wewe ni muuaji?” akasema Lilian kwa kujiamini.
“Muuaji?”
“Ndiyo...wewe ni muuaji tena mkubwa sana.”
“Unasemaje wewe?”
“Paaaaa...” kibao kingine kikatua tena.
Hakuweza kukubaliana na jambo hilo. Naye akarudisha, Lilian safari hii alicharuka, akarusha ngumu, mwenzake naye akarudisha.
Zikapigwa!
Leila na mwenzake hakukubaliana na ugomvi ule, tena mbele ya macho yao. Wakaingilia kati na kuamulia. Mpaka ugomvi unaisha, hakuna aliyekuwa tayari kueleza kisa cha ugomvi ule.
Hata hivyo aliyekuwa na jibu alikuwa ni Lilian pekee ambaye alikuwa amecharuka kuliko mbogo!
***
Kilikuwa kipindi ambacho Lilian alihitaji kukaa peke yake kuliko kipindi chochote katika maisha yake.
Kwa Lilian kuwa na ukimwi ni sawa na kukata tiketi ya kifo. Akili yake ilivurugika kabisa. Alijitahidi kuusaka usingizi lakini haikuwezekana.
Akili yake yote ilikuwa kwa Pam. Huyu ndiye aliyekuwa na majibu yake yote. Aliusubiria kwa hamu kubwa sana muda alioahidiana na Pam wakutane.
***
Pam alikuwa mwenye tabasamu muda wote, jambo ambalo lilimkasirisha sana Lilian lakini hakuwa na la kufanya. Pam ni kama alikuwa anajua alichotiwa...
“Lilian...” Pam akaita baabda ya kumuona Lilian akilia muda wote.
“Abeee...”
“Tatizo ni nini hebu kuwa serious?”
“Lakini Pam kama ulikuwa unafahamu hali yako, kwanini ulinifuata na kufanya mapenzi na mimi?
“Umeniharibia kila kitu Pam, ndoto zangu za maisha zote zimeharibika. Ni kwa nini umenifanyia hivyo lakini?” akasema Lilian kwa sauti ya majuto lakini akionyesha heshima kwa Pam, akiwa na imani kuwa huenda akamsaidia.
“Ni kweli nimeathirika,” akasema Pam.
“Unasemaje?”
“Ni kweli kanisa nimeathirika lakini halikuwa kusudi langu kukuambukiza na wewe. Hili si kosa lako. Kuna mwanamke mmoja ndiye amesababisha matatizo yote haya.
“Kumbuka mimi kuna wakati huwa na mawazo kupindukia, sina mfariji yeyote ndiyo maana nikaona uwe wangu ili unipe raha. Lakini hata hivyo ukimwi siyo ishu kubwa kama unavyofikiria.
“Mimi naishi na ugonjwa huu, baada ya muda huwa nakwenda Afrika Kusini kubadisha damu. Hakuna kinachoshindikana. Angalia mpaka sasa naishi kwa amani kabisa.
“Nitakupeleka na wewe huko ukabadilishe damu. Haya mambo hayana nguvu mbele ya fedha. Sawa mama?”
“Paaaa...” Lilin aliinuka haraka sana, kisha akamshushia kibao kizito sana.
Eneo hilo halikuwa na maana tena kwake.
Aliinuka muda uleule kisha akaondoka zake.
“Ahsate sana, nashukuru sana Pam!” akasema Lilian wakati akiondoka zake.
Pam alijitahidi sana kumuita ili arudi wazungumze, lakini hilo halikuwezekana. Lilian alikuwa na maumivu ambayo hakuwahi kuyapata kabisa moyoni mwake.
***
Maisha ya Lilian yalibadilika, hakuw na uchangamfu kama aliokuwa nao awali. Akajikuta anakuwa mtu wa kukosea kila kitu kila wakati.
Masomo kwake yalikuwa magumu sana. Akiwa hana hili wale lile, akiwa amepoteza matumaini kabisa, siku moja akiwa amejifungia chumbani kwao, wenzake wakiwa wameingia kwenye kipindi, alisikia simu yake ikiita.
Alipotupa macho yake kwenye kioo cha simu yake, akagundua kuwa aliyekuwa akimpigia alikuwa ni Edo. Akastuka sana. Mapigo ya moyo wake yalibadilika. Mara moja akapokea...
“Lilian...” akaita Edo.
“Unasemaje Edo? Tafadhali naomba uniache na matatizo yangu, maumivu niliyonayo yananitosha...” akasema Lilian.
“Hapana nina jambo jipya kabisa la kukuambia.”
“Jambo jipya?”
“Ndiyo nina jambo jipya.”
“Jambo gani?” akasema Lilian akionekana kuwa na hamu ya kusikia jambo hilo kutoka kwa Edo.
“Nimekusamehe Lilian!” akasema Edo.
“Unasemaje Edo?”
“Nimekusamehe!”
Lilian alibaki kama aliyechanganyikiwa kabisa! Hakujua la kufanya.
 
ILIPOISHIA...21
Alipotupa macho yake kwenye kioo cha simu yake, akagundua kuwa aliyekuwa akimpigia alikuwa ni Edo. Akashtuka sana. Mapigo ya moyo wake yalibadilika. Mara moja akapokea...
“Lilian...” akaita Edo.
“Unasemaje Edo? Tafadhali naomba uniache na matatizo yangu, maumivu niliyonayo yananitosha...” akasema Lilian.
“Hapana nina jambo jipya kabisa la kukuambia.”
“Jambo jipya?”
“Ndiyo nina jambo jipya.”
“Jambo gani?” akasema Lilian akionekana kuwa na hamu ya kusikia jambo hilo kutoka kwa Edo.
“Nimekusamehe Lilian!” akasema Edo.
“Unasemaje Edo?”
“Nimekusamehe!”
Lilian alibaki kama aliyechanganyikiwa kabisa! Hakujua la kufanya.
SASA ENDELEA...

DIRA ya maisha ya Lilian ilibadilika kabisa. Kama ni basi, lilikuwa limegeza uelekeo. Ni kama liligeukia upande lilipotokea.
Alijiona asiye na thamani tena. Kujitunza kote katika maisha yake hapakuwa na maana tena. Lilikuwa tendo la siku moja tu, mara moja tu, lililogharimu maisha yake yote.
Rafiki zake akina L, aliwaona kama nuksi katika maisha yake. Aliyemchukia zaidi alikuwa ni Lucy. Kampani yake yote ya Lucy, Latifa na Leila aliichukia kabisa.
Pamoja na yote hayo, simu ya Edo aliyekuwa akizungumza naye, ambaye alimwambia alimsamehe, ilimshangaza na kumshtua. Zilikuwa habari mpya kwake. Pengine ni habari njema lakini zisizo na uthibitisho.
Hajui kilichopo moyoni mwa Edo.
“Edo ananichora au ni mkweli?” akawaza.
Edo anisamahe mimi? Akawaza tena. Ulikuwa wakati wa kuwaza na kuwazua. Wakati wa kujiuliza maswali na kujijibu mwenyewe.
“Edo...” Lilian akaita simuni.
“Yes darling...” (Ndiyo mpenzi) akaitikia Edo.
“What?” (Nini?) akang’aka Lilian.
Kuitwa mpenzi lilikuwa jambo jingine jipya na la kushangaza hasa.
“What’s wrong with you my dear?” (Una tatizo gani mpenzi?) akauliza Edo kwa kimombo.
“You calling me darling again?”
(Unaniita mpenzi kwa mara nyingine?) akaualiza Lilian.
“Kwani kuna tatizo gani?” akauliza Edo.
“No!” (Hapana) akajibu Lilian.
“Why not?” (Kwanini hapana?)
“Kwa hakika sifai tena kuwa na wewe, niache nife na ukimwi wangu. Niache nife peke yangu...” akasema Lilian, tayari machozi yalianza kumwagika machoni mwake.
“Inawezekana unachowaza ni sahihi lakini pia si ajabu ikawa si sahihi. Naomba nikutane na wewe tuzungumze.”
“Kukutana na mimi?”
“Ndiyo.”
“Lini?”
“Leo.”
“Saa ngapi?”
“Muda wowote jioni. Hebu panga wewe.”
“Sawa...saa moja usiku vipi?”
“Ni sawa tu, wapi?”
“Kwa sababu umechagua muda, pendekeza na eneo pia mpenzi.”
“Pendekeza wewe.”
“Mh!” akaguna Edo.
Kimya cha muda kikapita, baadaye Edo akaanza kuzungumza simuni: “Acha nitajua mwenyewe. Cha msingi, saa moja juu ya alama uwe tayari, nitakuwa hapo chuoni.”
“Sawa.”
“Zingatia muda tafadhali.”
“Nimekuelewa Edo.”
Wakakata simu zao.
***
Hakuna jambo gumu kama kulazimisha furaha, lakini Lilian alilazimisha furaha. Kichwani mwake, alihisi ameshafika mwisho wa maisha yake.
Hakuwa na elimu sahihi juu ya maambukizi ya virusi vya ukimwi na ukimwi. Hakujua tofauti ya virusi vya ukimwi na shambulio la ukimwi. Kifupi hakujua lolote kuhusu ugonjwa huo.
Alichojua yeye, ukimwi ni kifo. Alijua hilo tu. Alichofundishwa ni kwamba ukimwi unaua. Hakuwa na kitu kingine kichwani mwake. Kugundulika kuwa virusi hivyo vilikuwa vinaishi ndani ya damu yake, kuliharibu kila kitu.
Mazungumzo yake na Edo kidogo yalimpa faraja, aliamini kama mpenzi wake, mtu ambaye alimwamini, kumheshimu na kumpenda, mtu ambaye ndiye pekee aliyejua siri ya ugonjwa wake, yupo pamoja naye na anahitaji kukutana naye, kidogo angepunguza uzito wa mzigo aliokuwa nao moyoni mwake.
Furaha ya kutengeneza ikaonekana. Alisubiri kwa hamu sana muda wa kutoka na Edo ufike. Ni kweli muda ulikwenda taratibu sana. Sana. Sana.
Lakini hata hivyo, saa 12 jioni ilifika. Muda ambao alitakiwa kuanza kujiandaa. Hakutumia muda mwingi sana. Ajipambe kwa lipi? Ajirembe kwa sababu gani? Alichokifanya ni kuingia bafuni, akaoga haraka na kutoka. Alivaa simpo tu. Suruali ya jeans nyeusi na blauzi nyekundu. Akajifunga kilemba kichwani, kisha mkoba wa rangi ya bluu ya kung’aa.
Tayari mshale wa saa ulikuwa umegota kwenye 6, wa dakika ukiwa kwenye 23, wa sekunde ukiendelea kutembea. Zilibaki dakika 37 tu kufikia muda wa miadi.
Akayazuia machozi yake kwa nguvu. Akaficha hisia zake za maumivu. Kwa kuhofia kujiumiza sana moyo wake na fikra za mateso zilizojaa majuto, muda huo akaamua kuutumia kusoma kitabu.
Akafungua kabati dogo, kisha akachukua kitabu cha nguli wa riwaya Afrika Mashariki, Ben Mtobwa. Kiliitwa Roho ya Paka. Alishakisoma mara nyingi sana, hakuona tabu kukirudia. Akafungua ukurasa wa kwanza kabisa wa hadithi ilipoanzia, akaanza kusoma tena.
‘Ilikuwa ghafla, kama pigo la kisu ambalo lilipenya mwilini na kuujeruhi moyo wa Inspekta Kombora. Kati ya yote aliyoyatarajia jioni ya leo, simu kama hiyo, ya maafa, haikuwamo kabisa akilini mwake. Kwa jumla, ilikuwa kama iliyopigwa muda huu kwa ajili ya kumsimanga au kumdhihaki....’
Ndivyo macho yake yalivyoanza kutembea juu ya maandishi ya kitabu cha gwiji huyo. Akaendelea kusoma zaidi. Kama utani, Ben Mtobwa akafanikiwa kumteka Lilian.
Sekunde moja tu ilisababisha asahau mzigo wa mawazo uliokuwa kichwani mwake.
Akazama katika hadithi hiyo ya kusisimua....
***
Mlio wa simu ulimgutusha. Akapuuza. Mawazo yake yalikuwa kwenye kitabu. Ikaita tena kwa mara nyingine, kichovu sana, akachukua simu yake na kuangalia mpigaji!
Akashtuka!
Alikuwa ni Edo!
Tayari alikuwa ameshasahau kabisa kuwa alikuwa na miadi na Edo. Mara moja akabonyeza kitufe cha kijani kuruhusu simu, kisha akaipeleka sikioni.
“Nimeshafika mpenzi, bila shaka upo tayari,” akasema Edo.
Lilian akachanganywa tena na neno ‘mpenzi’. Lakini hakuwa na la kufanya, akajibu kichovu: “Ndiyo, nipo tayari tangu nusu saa iliyopita.”
“Sawa njoo basi twende.”
“Nakuja.”
Lilian alipoyatupa macho yake kwenye saa iliyokuwa ukutani, akagungua kuwa tayari ilikuwa saa 1:18 usiku. Akarudisha kitabu kabatini, akatoka nje.
“Edo ana habari gani mpya?” akawaza akimfuata.
Itaendelea..
 
ILIPOISHIA...22
Lilian akachanganywa tena na neno ‘mpenzi’. Lakini hakuwa na la kufanya, akajibu kichovu: “Ndiyo, nipo tayari tangu nusu saa iliyopita.”
“Sawa njoo basi twende.”
“Nakuja.”
Lilian alipoyatupa macho yake kwenye saa iliyokuwa ukutani, akagungua kuwa tayari ilikuwa saa 1:18 usiku. Akarudisha kitabu. kabatini, akatoka nje.
“Edo ana habari gani mpya?” akawaza akimfuata.
SASA ENDELEA...

UZURI wa Lilian bado uliendelea kuonekana kwa nje lakini ndani yake hakuwa msichana mrembo tena. Alitembea kivivu, bila mpangilio kama zamani. Alijitoa thamani kabisa.
Mikogo yote ilikaa pembeni, ndani ya moyo wake kulijaa majuto. Hakuchukua muda mrefu tayari alikuwa ameshafika barabarani ambapo Edo alikuwa ameegesha gari lake.
Edo alipotupa macho yake na kumuona Lilian akimfuata, alijawa na huzuni moyoni. Alimuona Lily hana furaha kabisa. Lilian alionyesha wazi kilichokuwa ndani yake.
Alikuwa kwenye majuto makubwa. Lilian alikuwa mpya kabisa. Mpya kwa kila kitu. Taratibu alivuta mlango wa siti za nyuma, ukafunguka. Akaingia.
“Habari yako Edo?”
“Poa.”
“Mbona huna furaha?”
“Nipo sawa Edo.”
Edo hakuzungumza kitu, aliangalia pembeni, nje kupitia dirisha la upande wa kushoto ambao alikuwa amekaa, aliporudisha macho yake ndani, akakutanisha macho na dereva wa gari lile.
“Twende kaka,” akasema Edo.
Gari likawashwa, likaanza kuondoka.
“Lakini huna sababu ya kuwa na mawazo kiasi hicho mpenzi.”
“Sifurahishwi na namna ninavyokuona. Natamani kuona tabasamu lako tena. Kwa nini unakuwa hivi?” akauliza Edo.
“Edo, unajua kila kitu. Unafahamu kuhusu malengo yetu, unajua kuhusu makubaliano yetu. Sasa angalia...kila kitu kimebadilika. Kila kitu kimeharibika. Nawezaje kufanya chochote tena Edo?
“Kumbuka mimi sina thamani tena kwako, siyo kwako tu sina thamani kwa mwanaume yeyote kwa sasa. Maisha yangu yamebadilika kabisa,” akasema Lilian kwa sauti iliyojaa uchungu moyoni.
“Hapana, usiseme hivyo. Ungekuwa huna thamani kwangu, nisingekuwa na wewe muda huu. Ni kwa sababu una thamani ndiyo maana uko na mimi muda huu,” akasema Edo kwa sauti tulivu.
“Unachokifanya sasa ni kunipa moyo tu. Hilo baasi. Siyo zaidi ya hivyo,” akasema Lilian.
“Nikuombe kitu?” akauliza Edo.
“Ndiyo.”
“Tusizungumze chochote muda huu mpaka tufike tunapokwenda, sawa?”
“Sawa,” akajibu.
Hapakuwa na mazungumzo zaidi. Gari lilishika njia hadi kwenye mzunguko wa Mlimani City, kwenye makutano ya Barabara ya Ardhi na Sam Nujoma. Dereva akakata kushoto kuifuata Barabara ya Sam Nujoma kuelekea Mwenge.
Dakika moja tu baadaye, tayari walikuwa kwenye mataa ya Mwenge, zilipokutana Barabara za Sam Nujoma, Ali Hassan Mwinyi, Bagamoyo na ile ya Coca Cola.
Taa ya kijani ilipowaka, dereva akanyoosha kuifuata Barabara ya Coca Cola. Mbele kidogo kabla ya kukifikia kiwanda cha soda alikata kulia na kupitia jirani kabisa na salon maarufu ya Naznat.
Wote walikuwa kimya kabisa, wakafika kwenye Barabara ya Mwai Kibaki, jirani kabisa na Clouds Media. Wakaishika barabara hiyo, ambapo mbele kidogo, mkono wa kulia, dereva alikata na kuegesha.
“Jack’s Pub...” Lilian alisoma maandishi kwenye bango dogo barabarani wakati dereva akikata kuelekea kwenye Pub hiyo.
“Kumbe tulikuwa tunakuja hapa?” Lilian akauliza.
“Ndiyo...hujapenda?”
“Pazuri, haina shida.”
Wakashuka garini na kuelekea kwenye meza iliyokuwa na viti viwili tu. Ilionekana wazi meza za namna hiyo zilitengwa maalum kwa ajili ya wapenzi au watu wawili pekee waliokuwa na mazungumzo ya siri.
Yule dereva alikaa sehemu nyingine. Muda mfupi baada ya kukaa, alifika mhudumu na kuwasikiliza.
“Juisi ya embe ipo?” akauliza Edo.
“Ipo ya maembe peke yake, kuna nyingine imechanganywa na maziwa na nanasi. Utapenda ipi?”
“Embe pekee, glasi mbili tafadhali.”
“Sawa bosi,” akaitikia yule mhudumu.
“Sikia Lilian...nimekuita hapa ili kuzungumza na wewe. Najua ni kiasi gani una maumivu, lakini lazima tuzungumze. Nimegundua jambo moja muhimu,”alianza kuzungumza Edo akimwangalia Lilian usoni.
“Kwa sasa uko kwenye majuto. Najua una maumivu na unahitaji mtu wa kukupa faraja. Nina uhakika, mwanaume uliyetoka naye, hawezi kukupa faraja. Bado mimi ni wako na ninakupenda,” akasema Edo.
Lilian akaanza kulia.
“Stop crying please!” (Acha kulia tafadhali)
“Niache nilie Edo.”
“Hapana. Unakosea. Nini kinachokuliza? Hakuna unachoweza kubadilisha...” akasema Edo, kisha akakatisha baada ya kumuona mhudumu akifika mezani kwao.
“Tutayarishie makange ya kuku na ugali dona tafadhali,” akasema Edo.
“Sahani mbili?”
“Ndiyo.”
Edo akaendelea: “Mimi ndiye wa kukupa faraja. Nimeshakuambia...nimekusamehe kutoka moyoni. Bado nipo na wewe. Hata kama haitakuwa kimapenzi tena, lakini sitakubali kuona furaha yako inaondoka kwa sababu yangu.
“Mimi ni wako, wewe ni wangu. Naomba uwe na amani na uendelee na masomo vizuri. Wiki ijayo narudi Malaysia. Tafadhali nataka nikuache ukiwa na amani. Acha kujifikiria peke yako. Hata mimi nina maumivu makali. Nami pia naumia. Ndiyo maana nataka kuwa sawa na wewe.”
Lilian akainuka!
Edo naye akasimama.
Lilian akazunguka upande wa pili aliokuwa amekaa Edo. Akamsogelea, wakakumbatiana.
“Ahsante kwa msamaha wako, nimekuelewa. Itakuwa hivyo Edo,” akasema Lilian.
“Unaniahidi?”
“Nakuahidi Edo.”
Baadaye kidogo chakula kilifika mezani, wakaanza kula huku wakizungumza. Walishasahau kabisa machozi na huzuni walizokuwa nazo muda mfupi uliopita.
***
Edo alirudi Malaysia. Kwa taabu Lilian aliweza kufuatilia masomo yake kwa miezi miwili ya mwazo. Baadaye hakuweza tena. Kila alipokumbuka kuwa anaishi na VVU, alihisi akili yake ikimruka.
“Sitaweza kuendelea na masomo kwa staili hii. Nitachekwa nikifeli. Ni afadhali nipumzike kwa muda kwanza,” akawaza Lilian.
Uamuzi alioufikia ulikuwa ni kuandika barua ya kuomba kuhairisha mwaka wa masomo hadi mwaka uliofuata. Katika barua yake, alieleza sababu mbalimbali za kutunga, uongozi wa chuo ukakubaliana naye.
“Sitakwenda nyumbani, nitakuwa hapahapa Dar,” alijisemea Lilian akiwa kitandani, akisoma barua ya majibu aliyopewa na uongozi wa chuo ambao ulikubaliana na maombi yake.

Je, nini kitaendelea? Usikose kufuatilia Ijumaa ijayo.
 
Maskini lily, kuwa na VVU sio mwisho wa maisha
 
Back
Top Bottom