Hadithi tamu: Hisia zangu

Hadithi tamu: Hisia zangu

MOMMAdoukeita heb njoo tuoe mambo watu presha juu juu jamani
 
Last edited by a moderator:
Hisia Zangu 18
ILIPOISHIA...

“Kwa nini usifikiri labda mimi ndiye naonekana nina ukimwi? Tunahitaji kuwa waangalifu mpenzi. Tuna mipango mingi sana mbele yetu kuhusu maisha yetu. Hatuwezi kuwa rahisi kiasi hiki. Kama kweli unanipenda, tutoke sasa hivi, twende tukapime tuwe na uhakika na afya zetu kisha tuendelee na mambo mengine,” akasema Edo.
“Sawa,” akasema Lilian kwa hasira, akainuka kitandani na kukimbilia bafuni ambapo alioga, alipotoka alimkuta Edo ameshavaa anamsubiri yeye.
“Haya twende,” akasema Lilian.
“Ok!”
Edo akabamiza mlango, akaingiza ufunguo kwenye kitasa, akafunga. Wakaanza safari ya kwenda kituo cha afya.
SASA ENDELEA...

MOYONI Edo alikuwa na mawazo mengi sana. Alijaribu kumfikiria Lilian wake, si yule mwenye msimamo tena. Nini kimetokea hadi msimamo wake ubadilike? Ni kweli alikuwa na hisia, tena hisia kali sana za kimapenzi, lakini isingekuwa rahisi kuingia kwenye mtego wa namna ile.
Alikuwa na wasiwasi mwingi sana moyoni mwake. Hakujua ilivyokuwa, lakini alijishangaa kwa namna alivyoingiwa na wasiwasi wa ghafla.
“Siwezi kuwa mjinga kiasi hiki, lazima kuna kitu,” akajisemea moyoni mwake Edo wakati akipiga hatua kutoka kwenye chumba chake na kushika korido kuelekea nje.
Lilian alikuwa akitembea bila wasiwasi kabisa, hakuonekana kufikiria jambo lolote baya kichwani. Alikuwa katika hali ya kawaida kabisa.
“Lilian na msimamo wake wote ule? Leo anawezaje kubadilika? Anawezaje kukubali kirahisi namna hii? Lazima atakuwa ameshaanza haya mambo. Angekuwa bado ningejua tu...hapa kuna kitu,” akazidi kuwaza Edo.
Edo hakuwa na gari, hivyo walitoka kwa miguu hadi kwenye kituo cha teksi, wakaingia kwenye mojawapo.
“Wapi bro?” dereva teksi akauliza.
“Tabata Health Centre.”
“Sawa, si pale kwa Dk. Manungu?”
“Sina hakika, naijua tu hiyo hospitali, sifahamu jina la mmiliki.”
“Sawa. Kaka, huyo ni daktari maarufu sana, alikuwa Muhimbili, sasa ni mstaafu ndiyo akaamua kufungua senta yake hapa Tabata.”
“Kikubwa ni kutufikisha hapo kaka, kanyaga mafuta tafadhali,” akajibu Edo akionekana kutohitaji maneno mengi kutoka kwa dereva yule.
Gari likapepea!
Hapakuwa mbali sana, dakika kumi tu baadaye, teksi hiyo aina ya Toyota Carina, lenye rangi nyeupe na mstari wa kijani pembeni, iliegeshwa mbele ya hospitali hiyo ambayo iliaminika sana katika Kitongoji cha Tabata.
“Kiasi gani?”
“Elfu tano zinatosha bro.”
“Sawa.”
Edo akaingiza mkono mfukoni, akatoa pochi yake kisha akachomoa noti moja ya elfu kumi kati ya nyingi zilizotunisha pochi hiyo. Akamkabidhi dereva, kisha akamshika mkono Lilian na kuondoka.
“Chenji yako kaka...” akasema dereva yule akitoa noti moja ya elfu tano kupitia dirishani.
Edo akageuza shingo kumwangalia, akaachia tabasamu changa ambalo alijitengenezea. Akachanganya midomo, akasema: “Ni lini utakunywa soda wewe? Kazi njema!”
Dereva akachekelea!
Hakuwa amezima gari lake, lilikuwa silence! Alichokifanya ilikuwa ni kuachia mguu aliokanyaga breki taratibu, mikono yake ikiwa kwenye usukani, kisha akahamisha mguu wake wa kulia kwenye kibati cha mafuta, akakanyaga taratibu, teksi ikayoyoma!
“Pesa bwana...kweli pesa inaongea,” akajisemea dereva yule wakati akiendelea kuongeza spidi kurejea kituoni kwake.
Siku yake ilikuwa inakaribia kuisha vizuri.
***
“Karibuni tafadhali,” sauti ya dada mrembo, aliyekuwa mapokezi katika hospitali hiyo ilitoka akiwatazama Edo na Lilian.
“Ahsante, tunahitaji huduma ya ushauri na kupima.”
“Oooh! Karibuni sana, bila shaka kabisa. Huduma inapatikana, piteni na hii korido, mtakata kulia pale mbele, room ya kwanza mtaiacha, mtaifuata ya pili ambayo mlangoni imendikwa VCT. Ni hapo mtaingia.”
“Ahsante sana.”
Edo akamshika mkono Lilian kisha wakaongozana kuelekea chumba cha mshauri. Kwa namna walivyoelekezwa, haikuwa vigumu kufika.
Edo akagonga mlango, kisha wakaingia. Wakapokelewa na mshauri mmoja aliyekuwa amekaa kwenye kiti cha kuzunguka. Akawakaribisha na tabasamu mwanana kabisa.
“Karibuni na mjisikie huru!” akasema mshauri huyo.
“Ahsante sana.”
“Karibuni tena...mimi naitwa Dk. Siwema, ni mwanasaikojia, mtaalamu wa ushauri nasaha kwenye mambo mengi katika jamii lakini kwa sasa nimebobea zaidi kwenye elimu rika na ukimwi. Naomba tufahamiane tafadhali,” akasema Dk. Siwema akitabasamu.
“Mimi ni Edward lakini nimezoeleka zaidi kama Edo, huyu ni mpenzi wangu, yeye anaitwa Lilian au Lily.”
“Nimefurahi sana kuwafahamu Edo na Lily, acha nami niwaite hivyo,” akasema Dk. Siwema huku akicheka.
Wote wakacheka.
“Ndiyo! Sasa naomba niwasikilize.”
“Sisi tumekuja hapa kwa ajili ya kupima afya zetu.”
“Kivipi?”
“Tunataka kupima virusi vya ukimwi.”
“Vizuri sana, hilo wazo mmeamua pamoja au kuna mmoja amekuwa na shinikizo kwa mwenzake?” Dk. Siwema akauliza.
Wote walibaki kimya, ni kama walikuwa wanategeana hivi...
“Aaaah! Nataka swali hili anijibu Lily.”
“Siwezi kusema kama kumekuwa na shinikizo lakini lilikuwa wazo la mwenzangu. Sijaona kama ni vibaya, ni wazo zuri tu, ndiyo maana nimeamua kuja naye hapa.”
“Je, mmewahi kukutana kimapenzi?” akauliza Dk. Siwema.
“Hapana,” wakajibu wote kwa wakati mmoja.
“Kwa nini?”
“Tulikubaliana kufanya hivyo siku tutakapoona,” akajibu Edo.
“Je, sasa mpo tayari kuoana?”
“Tutaona tu, lakini muda bado. Wote bado tunasoma. Mimi nipo Malaysia na mwenzangu anamalizia UD (University of Dar es Salaam), lakini kwa kweli uzalendo umetushinda, tukaamua kuliko kusalitiana ni bora tuanze tu wenyewe.”
“Sawa. Je, mpo tayari kushauriwa pamoja majibu mpokee pamoja?”
“Ndiyo, tupo tayari.”
“Vizuri sana. Najua siku hizi elimu ya ukimwi ipo wazi sana hivyo hakuna mambo mengi sana mapya ya kuwafundisha hapa. Jambo la msingi mnalotakiwa kujua ni kwamba, kwanza mmefanya vizuri sana kuamua kujuana afya zenu kabla hamjaanza kufanya chochote.
“Ni wazo zuri, lakini vizuri pia mkiendelea kuwa makini hata baada ya majibu yenu. Mnapaswa kuwa waaminifu katika uhusiano wenu, hapo ndipo mtakapoona raha ya uhusiano. Sasa turudi katika suala lenu. Vipi kama ikitokea mmekutwa wote mmeathirika?”
“Ikiwa tutakuwa tumeathirika wote, kwa kweli tutaumia sana, lakini itabidi tuendelee na uhusiano wetu huku tukipeana moyo,” akajibu Edo.
“Niwatoe hofu, ukimwi usiwaogopeshe sana, hata kama mkikutwa nao au mmoja wenu akawa ameathirika, hampaswi kuchanganyikiwa. Mkifuata ushauri vizuri, mtu anaweza kuishi zaidi ya miaka ishirini baada ya kujua kama ana maambukizi.
“Ninao marafiki wengi sana ambao wameathirika na maisha yao yanaendelea kama kawaida. Msijali. Kupima ni kujua ukweli wa afya zenu. Hata kama msipojua leo, kuna siku mtajua mkiwa mmeshachelewa.
“Ni afadhali mjue mapema, muanze kufuatilia masharti mapema na kwa usahihi ili muweze kuishi maisha marefu. Nasisitiza, msiwe na wasiwasi, sawa jamani?”
“Sawa dokta.”
“Sasa mpo tayari nichukue vipimo vyenu?”
“Ndiyo!”
Itaendelea wiki ijayo...
 
Sheeeee.... Huyu dokta maneno meeengi hajui kuna wengi twangoja majibu hapo ya huyo mama PAM
 
Presha inapanda presha inashuka
 
Akili ya Edo ni kwmb kw nin Lily amekuw na hisia kali za mpnz hapo ndipo palipo na mtihan kw Edo.
 
Edo na ujasiri wake mara yeye ndo mwenye ngwengwe maana mwanzo alikua player haswa.
 
ILIPOISHIA...
“Niwatoe hofu, ukimwi usiwaogopeshe sana, hata kama mkikutwa nao au mmoja wenu akawa ameathirika, hapaswi kuchanganyikiwa. Ukifuata ushauri vizuri, mtu anaweza kuishi zaidi ya miaka ishirini baada ya kujua ana maambukizi.
“Ninao marafiki wengi sana ambao wameathirika na maisha yao yanaendelea kama kawaida. Msijali. Kupima ni kujua ukweli wa afya yako. Hata kama usipojua leo, kuna siku utajua ukiwa umeshachelewa.
“Ni afadhali ujue mapema, uanze kufuatilia masharti mapema na kwa usahihi ili uweze kuishi maisha marefu. Nasisitiza, msiwe na wasiwasi, sawa jamani?”
“Sawa dokta.”
“Sasa mpo tayari niwapime?”
“Ndiyo!”
SASA ENDELEA...

HOFU kuu iliwavaa wote. Ingawa ni kweli walikuwa tayari kwa vipimo, lakini kwa ndani hawakujiamini.
Lilian alijua wazi kuwa yeye hakuwa bikra. Tayari alishavunja ahadi yake kwa kutoka na Pam. Hilo lilikuwa kosa kubwa maana hakumjua vizuri Pam.
Hata hivyo, hofu yake haikuwa kubwa kutokana na kwamba, hakuwa na ufahamu sana na habari za maambukizi ya ukimwi. Kwa Edo kulikuwa na mashaka zaidi.
Edo pamoja na kwamba alikuwa mwaminifu katika kipindi chote alichokuwa na Lilian, kabla yake alishawahi kutoka na wasichana kadhaa.
Hilo lilimpa hofu kidogo, lakini akajipa moyo.
“Ni vizuri kujijua afya yangu. Nafikiri ni sahihi kupima,” akawaza.
“Ok! Nafikiri tunaweza kuanza sasa,” akasema Dk. Siwema.
Muda huohuo Dk. Siwema akaweka vifaa tayari, haikuwa kazi kubwa, maana alitumia kifaa kidogo na kwa urahisi. Aliwatoboa vidole, kisha akachukua damu na kuweka kwenye kipimo ambacho majibu yake hutoka haraka, wateja wakiwa hapohapo.
Zoezi lilipokamilika, Dk. Siwema aliwaangalia. Wote wakaonekana kuwa na wasiwasi sana.
“Majibu yenu yapo tayari, naweza kuwapa sasa?” Dk. Siwema akaanza kuzungumza.
“Tupo tayari kabisa, tupo tayari,” akasema Lilian.
“Kama tulivyokubaliana, naomba iwe vilevile. Majibu yote ni majibu, kwa hiyo naomba muyapokee kama yalivyo, sawa jamani?” akasema Dk. Siwema.
“Sawa...” wote wakajibu.
“Majibu yaliyopatikana kwenye damu ya Edo yanaonyesha kuwa, Edo huna uambukizi...” akasema Dk. Siwema kisha akatulia kwa muda.
“Uko negative, hongera sana kwa hilo,” akasema tena.
Edo alitabasamu, Lilian akawa anasubiri kwa majibu yake. Uso wa Dk. Siwema ni kama ulikuwa na ujumbe tofauti ambao alikuwa akijaribu kuuficha au kutafuta mbinu sahihi za kuufikisha.
“Kwa upande wako Lilian...” akasema Dk. Siwema kisha akameza funda kubwa la mate.
Akaendelea: “Damu yako inaonekana ina matatizo kidogo... na ni kweli kabisa kuwa damu yako ina maambukizi ya ....” kabla Dk. Siwema hajamalizia kusema, Lilian alimkatisha.
“Haiwezekani, nasema haiwezekani. Nyie mna njama zenu. Unasemaje? Oooooh! Pam... Pam umeniua Pam,” akasema kwa sauti ya juu.
Edo aliinamisha kichwa chini, machozi yakimwagika machoni mwake kama mfereji unaomwaga maji kutoka mlimani!
Edo ndiye aliyechanganyikiwa zaidi, akasimama na kumshika Lilian mikono yake. Naye akasimama. Wakajikuta wamekumbatiana. Wote walikuwa wakilia.
“Lilian kwa nini lakini, kwa nini?” Edo akasema akipiga kelele kwa uchungu.
“Edo siyaamini haya majibu, siyaamini kabisa,” akasema Lilian.
“Naomba mtulie kwanza jamani, hebu ketini,” akasema Dk. Siwema kwa sauti ya kusihi sana.
Wakaketi.
“Sikilizeni...” akasema tena Dk. Siwema.
“Sina sababu ya kudanganya kwa lolote. Ninyi nyote ndiyo najuana nanyi kwa mara ya kwanza leo hii.
“Kusema kuwa naweza kuandka majibu ya uongo, haiwezekani. Halafu Lilian unapaswa kutulia kama nilivyosema awali. Hakuna kitu cha kutisha hapo.
“Ni kweli umeathirika, lakini siyo mwisho wa maisha yako. Bado kuna mambo mengi ambayo unaweza kufanya bila kuathiri maisha yako. Tulia...nawahitaji mje tena hapa kesho kwa ushauri zaidi.
“Lilian unatakiwa kupima pia kinga zao za mwili ili kujua mahali pa kuanzia na kukuweka katika hali salama, uendelee kuyafurahia maisha kwa muda mrefu zaidi,” akasema Dk. Siwema.
Yalikuwa maneno makali sana kwa Lilian. Alihisi kichwa kumgonga kabisa. Hata hivyo hakuwa na namna zaidi ya kukubaliana na hali halisi.
Ni kweli kabisa, alikuwa ameathirika. Kwa shingo upande, Edo akimwongoza, kutoka nje ya chumba cha daktari. Safari yao ikawa moja kwa moja hadi barabarani walipochukua teksi iliyowarudisha hotelini.
***
“Nataka uwe mkweli kwangu Lilian,” akaanza kusema Edo.
“Ndiyo.”
“Ulinisaliti?” akauliza Edo kwa ukali.
“Haikuwa dhamira yangu Edo mpenzi nilileweshwa!”
“Nataka kujua, ulinisaliti?”
“Ndiyo!”
“Na nani?”
“Kuna baba mmoja hivi, anaitwa Pam. Ni yeye tu ndiye niliyetoka naye, sikuwa na mwingine zaidi yake. Ilitokea kwa bahati mbaya. Rafiki zangu walitaka nitoke nao kwenda klabu, huko ndiyo mwanzo wa yote.
“Walinidanganya nikanywa pombe, nilipolewa ndiyo akanishawishi, baada ya hapo sikuweza tena kuachana naye. Sikujua kama angekuwa na maambukizi. Najuta mimi,” akasema Lilian akilia.
“Nakupenda sana kutoka ndani ya moyo wangu, sijui nitaishi vipi bila wewe. Angalia...umeharibu ndoto zangu. Umenipotezea dira ya maisha yangu. Kwa nini umenitenda hivyo?” akasema Edo kwa uchungu sana.
“Nisamehe mpenzi wangu. Najua huu ni mwisho wa mapenzi yetu, lakini tafadhali naomba unisamehe. Hata kama utakuwa na mwanamke mwingine badala yangu, lakini nisamehe kwa kukuumiza moyo wako.
“Naomba radhi kwa kukutesa hisia zako. Nisamehe tafadhali, haya yaliyotokea sikuyajua kabisa,” akasema Lilian.
Edo alibaki kimya!
“Umenisamehe Edo?” akauliza Lilian.
“Sikia, nakupenda sana. Hata moyo wangu unajua hilo, akini kwa hili samahani sana...hebu nipatie muda nipumzike kidogo kwa sasa.
“Tafadhali naomba uondoke hapa hotelini. Niache peke yangu. Nahitaji muda wa kuwa mwenyewe kwa sasa,” akasema Edo.
Lilian hakutaka kubishana naye. Alijiandaa na kujichukulia vitu vyake pale chumbani kisha akatoka nje, ambapo umbali mfupi sana kabla ya kulifikia geti alimpigia Pam.
Simu ya Pam iliita mara moja tu, akapokea: “Yes dear, niambie mama.”
“Uko wapi Pam?” akasema Lilian akionekana kulia.
Kilio chake kilisikika kupitia simu aliyokuwa akizungumza na Pam.
“Una nini? Kuna msiba au?”
“Bora ingekuwa msiba.”
“Tatizo ni nini?”
“Pam tuonane kwanza please!” akasema Lilian akizidisha kilio.
“Wewe una nini?”
“Pam kwa nini hukusema mapema?”
“Kusema nini?”
“Pam umeniua Pam, umenipa ukimwi. Umeharibu ndoto zangu, umesababisha mpenzi wangu hanitaki tena. Kwa nini Pam? Kwa nini?” akasema Lilian akizidi kulia.
Pam akacheka sana!
“Unanicheka?”
“Sikucheki bali unachekesha!” akasema Pam akizidi kukaukia kwenye simu.
Pam anacheka!
Lily analia!
Lilian alihisi dunia chungu, alitamani kuchimba shimo ili aingie humo, asionekane na mtu yeyote!
Hilo halikuwezekana!
Itaendelea.....
 
Dah najifunza kitu hapa
 
Pombe zishamtoka anajuta peke yake sasa...shenzi taip
 
Back
Top Bottom