Hadithi tamu: Hisia zangu

Hadithi tamu: Hisia zangu

Mommadou Keita

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2013
Posts
230
Reaction score
238
HISIA ZANGU

...Sikujua mwisho wangu ungekuwa hivi

EDO aligeuka tena. Kwa mara ya tatu anafanya hivyo wakati akielekea bafuni. Safari hii alimwangalia Lilian kwa macho yaliyojaa ubembe wa huba.
Alihisi moyo wake ukienda mbio kama saa mbovu!
Lilian alikuwa mbichi kabisa. Mwanamke mrembo kuliko neno lenyewe. Kwa namna Lilian alivyokuwa akimwangalia Edo aliyekuwa akisitasita kuingia bafuni, alionekana dhahiri hakuwa na mpango wa kubadili maamuzi yake.
Moyoni alionekana wazi kusimamia alichopanga. Hakuwa tayari kuyumbishwa! Kweli alimpenda sana Edo, lakini isingekuwa rahisi kwake, kutokana na upendo huo avunje agano lake.
Hapo Edo naye alikuwa na mawazo yake, alijaribu kufikiria ni kwa namna gani angemlaghai Lilian akubali kubadili maamuzi yake.
Kwa hakika ilikuwa kazi ngumu. Kazi ngumu kwelikweli. Pengine ingekuwa rahisi zaidi tairi la gari kupita juu ya mguu wa binadamu bila kuuvunja kuliko jambo lililokuwa mbele yao kufanyika.
Msimamo thabiti!
Lilian alikuwa amekaa kitandani, amevaa gauni zuri, refu la rangi ya buluu ya kung'aa. Tangu ameingia katika chumba cha hoteli hiyo na Edo, saa mbili zilizopita, hakuonekana kuwa na wazo la kutoa nguo zake.
Ni kama alipanga kulala nazo. Ahadi ya wawili hawa ni kutokukutana kimwili hadi watakapofunga pingu za maisha. Ni msimamo ambao Lilian alijiwekea siku zote.
Si kwamba walikutana siku hiyo... la hasha! Hawa ni wapenzi wa siku nyingi; uhusiano wao sasa umefikisha miaka mitatu. Kwa muda wote huo, hakuna siku waliyowahi kukutana kwenye uwanja wa huba.
Lilian pamoja na kuwa na umri wa miaka 22, bado alikuwa hajawahi kumjua mwanaume. Bado alikuwa amefungwa kwenye makaratasi. Kichwani mwake alisema: "Mtu pekee ambaye anapaswa kuchukua zawadi hii ni mume wangu pekee. Siwezi kumwamini Edo, hata kama nampenda.
"Edo atakula vinono vyangu ikiwa atatimiza ahadi yetu ya ndoa. Najua tunasoma, acha tutengeneze maisha yetu kwanza, baada ya hapo atanifaidi tu. Mimi ni wake tu."
Au ataniacha? Lilian akawaza tena.
"Mwenzetu vipi? Mbona umeganda hapo mlangoni?" Lilian akamwuliza Edo ambaye bado hakuwa na dalili za kutaka kuingia bafuni.
"Naingia mama, kwani kuna ubaya gani mtu kumwangalia mpenzi wake?" akajibu Edo.
"Hakuna ubaya kwa kweli, si vibaya mtu kumwangalia mpenzi wake. Nakubaliana na wewe lakini muda baby. Bado hatujala mpaka sasa hivi."
"Najua...njoo basi tuoge wote ili tuokoe muda."
"Edo wewe! Acha utani wako bwana...unajua kitakachotokea. Utaniudhi sasa..." akasema Lilian kwa sauti ambayo haikueleweka ilikuwa ya ukali au kudeka.
Haraka Edo akashika kitasa cha mlango wa bafuni. Akakinyonga kwa nguvu, kisha akasukuma mlango. Akaingia. Muda mfupi baadaye kilichosikika ndani ya bafu lile ilikuwa ni maji yakitiririka kutoka kwenye bomba la mvua.
Bado Edo alikuwa anapanga mashambuzi.
***
Edward Mhagama au Edo kama alivyojulikana na wengi alikuwa kijana mtanashati hasa. Hakuwa mtu wa wasichana sana. Mpaka anamaliza kidato cha nne alikuwa hajawahi kukutana na msichana yeyote kimapenzi.
Alipoingia kidato cha tano, Shule ya Sekondari Lutengano, Tukuyu, Mbeya ndipo alipoanza utundu. Alijikuta akikutana kimapenzi na wasichana tofauti tofauti kwa muda mfupi.
Alipoanza tu kujua mapenzi, akajikuta amechanganyikiwa ghafla. Akiwa anamaliza kidato cha sita, alijishangaa amebadilika ghafla.
Hakutaka tena kuendelea na tabia yake ile ya kupenda wanawake. Kwa bahati nzuri, alipata alama nzuri na hivyo ikawa rahisi kwake kupata nafasi ya kuendelea na masomo ya chuo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) sehemu ya Mlimani.
Hapo ndipo alipokutana na Lilian, yeye akiwa mwaka wa mwisho wa masomo, wakati Lilian akiingia mwaka wa kwanza. Alipata shida sana kufanikiwa kumnasa Lilian kwenye himaya yake.
Lilian hakuwa mtu wa wanaume kabisa. Hakujua chochote kuhusu mapenzi. Bahati nzuri kwa Edo ni kwamba alikuwa mcheza mpira wa kikapu mzuri sana, mchezo ambao Lilian alipenda kuungalia.
Hapo ndipo mwanzo wa uhusiano ulivyokuwa lakini sharti lilikuwa moja tu. Wasingekutana faragha mpaka watakapoingia kwenye ndoa.
Lilikuwa sharti gumu sana kwa Edo, lakini aliamua kulipokea kwa sababu alimpenda sana Lilian na ndani ya moyo wake alikuwa na uhakika kuwa hakutaka kuwa naye kwa ajili ya kujifurahisha tu bali kuingia kwenye ndoa.
Pazia la uhusiano wao likafunguka.
***
Mlango ulifunguka. Edo akatoka bafuni akiwa bado ana maji mwilini mwake. Hakuwa na nguo yoyote zaidi ya taulo kiunoni. Akatembea taratibu hadi ilipokuwa kabati ya kujipambia.
Ilikuwa siku ngumu sana kwao, ni siku ambayo walikubaliana kulala pamoja kwa vile tu, siku inayofuata, Edo alikuwa na safari ya kwenda Malaysia kwa ajili ya masomo. Wazazi wake waliamua kumpeleka nchini humo kutafuta Shahada ya Uzamili.
Hiyo ilimaanisha kuwa, Lilian angebaki pekee nchini kwa muda wote huo wa masomo. Mipango ilikuwa mizuri, Edo asingerejea nchini mpaka atakapomaliza masomo yake, maana wazazi wake walikuwa wameshamtafutia kazi ya muda kwa kipindi chote atakachokuwa likizo na siku za mapumziko.
Ratiba yake ilikuwa imebana kabisa. Walikuwa pamoja kwa ajili ya kuagana. Ahadi ikiendelea kutunziana heshima kwa kipindi chote hicho. Ndivyo makubaliano yao yalivyokuwa.
Edo hakujali, kama vile hapakuwa na mtu. Alijitoa taulo na kuanza kujikausha maji mwilini. Baada ya hapo akachukua manukato ya ngozi, akajipulizia mwili, kisha akatoa nguo na kuvaa.
Lilian alifumba macho. Aliona haya kumwangalia Edo. Alijua wazi kama angeendelea kumwangalia ni jambo gani lingejitokeza. Hilo alilijua kwa hakika kabisa.
Edo alitumia dakika mbili tu kujikamilisha. Akamfuata Lilian na kumshika mikono...
"Wewe, yaani umefumba macho kweli?" akauliza.
"Ndiyo!"
"Kwa nini?"
"Wewe hujui? Sitaki matatizo bwana."
"Nenda basi na wewe ukaoge."
"Nitafanya hivyo kwa sharti moja tu."
"Sharti gani?"
"Kama utaondoka na kwenda mgahawani, uniache mimi nioge peke yangu na nijiandae kabisa, nikiwa tayari nakufuata."
Edo akatulia kwa muda, akamwangalia Lilian kwa macho yaliyokuwa yanafikisha ujumbe fulani, kisha akamjibu: "Sawa."
Hakusubiri zaidi, alisimama na kuufuata mlango kisha akafungua na kuubamiza kwa nguvu. Ni kama alikuwa amechukia. Lilian hakujali. Akasimama na kwenda kuufunga ule mlango kwa ufunguo kisha akarudi ndani.
Akavua nguo na kuchukua taulo kisha akaelekea bafuni. Alioga kwa uhuru sana. Alipomaliza kila kitu, alitoka na kumfuata mpenzi wake mgahawani.
"Umeniagizia chakula?" Lilian akamwuliza.
"Sasa nitajuaje unapenda chakula gani?"
Jibu lile lilionyesha chuki dhahiri iliyokuwa moyoni mwa Edo. Lilian akatulia kwa muda. Akanyoosha mikono yake na kuivuta ya Edo.
"Niangalie machoni," Lilian akamwambia Edo.
Edo akafanya hivyo.
"Nakupenda sana na ninajua malengo yetu yalivyo. Amini usiamini, kama utalazimisha unachotaka kitokee, nakuhakikishia tutauvunja uhusiano wetu wenyewe."
"Kwa nini unasema?"
"Umevumilia kwa miaka mingapi mpenzi wangu? Si mitano? Eeeeh? Kuna tatizo gani kusubiri kwa hiyo miaka miwili tu iliyobaki? Kuna haraka gani?
"Hivi utaniamini vipi mimi kuwa sitakuwa na mwanaume mwingine? Sikia dear, mimi sijawahi kukutana na mwanaume yoyote tangu kuzaliwa kwangu. Hii ni zawadi yako mpenzi.
"Ona...ukiniacha na hii hali itakuwa ni usalama na ulinzi wa kweli kwako. Siwezi kumpa mtu. Nitakupa wewe tu muda ukifika. Maana yake ni kwamba, ikiwa leo utanitoa usichana wangu, ukiondoka kesho, hata kama nikikutana na mwanaume mwingine huwezi kujua mpenzi.
"Nipe uhuru, niamini. Mbona mimi nakuamini mpenzi? Au huwa unafanya na wengine? Ni heshima kunioa nikiwa msichana kamili. Mpenzi wangu, acha papara!" alisema Lilian kwa sauti lakini kwa harakaharaka.
"Nimekuelewa mpenzi."
"Kweli?"
"Ndiyo."
"Umeagiza nini?"
"Nafurahi kula ugali na makange."
"Makange ya nini?"
"Unapenda nini?"
"Wewe umeagiza ya nini?"
"Samaki, sato."
"Uko sahihi kabisa mpenzi."
Mazungumzo yao yakabadilika, sasa ikawa ni kuhusu maisha yao yajayo na namna ya kudumisha uhusiano wao. Bado kichwani mwa Edo kulikuwa na matumaini.
Ni kweli alimpenda sana mpenzi wake Lilian, lakini alitamani sana japo apate fursa ndogo tu ya kujifurahisha nafsi yake. Ni jambo baya, alikiri lakini japo kidogo tu.
"Nitazungumza naye zaidi. Haiwezekani niwe naye kwa muda wote huo, nimevumilia. Leo nataka kusafiri kwenda Malaysia nimuache hivihivi, hapana bwana. Nitafanya kila njia," akajisemea moyoni mwake.
Itaendelea...
 
HISIA ZANGU -2
"Umeniagizia chakula?" Lilian akamuuliza.


"Sasa nitajuaje unapenda chakula gani?"

Jibu lile lilionyesha chuki dhahiri iliyokuwa moyoni mwa Edo. Lilian akatulia kwa muda. Akanyoosha mikono yake na kuivuta ya Edo.


"Niangalie machoni," Lilian akamwambia Edo.


Edo akafanya hivyo.


"Nakupenda sana na ninajua malengo yetu yalivyo. Amini usiamini, kama utalazimisha unachotaka kitokee, nakuhakikishia tutauvunja uhusiano wetu wenyewe."

"Kwa nini unasema hivyo?"

SASA ENDELEA...


KILIKUWA kipindi cha ukimya mfupi. Lilian alimwangalia Edo kwa muda. Macho yake yalishatoa taswira ya kilichokuwa moyoni mwake.
Lilian alishajua mwenzake alikuwa katika hasira. Alikasirishwa na jambo ambalo lilikuwa na faida kwao wote wawili. Kukubali jambo lile lifanyike, kulimaanisha kukubaliana na kusitishwa kwa uhusiano wao.

Msimamo wake ulikuwa wa hali ya juu sana. Kuliko akubali kuuachia mwili wake utumike na Edo, hata kama alikuwa na mzigo wa mapenzi moyoni mwake, ilikuwa bora waachane.

Moyoni alijaa Edo pekee. Kuachana halikuwa jambo zuri kwa hakika. Uundaji wa maneno ukaanza kichwani mwake. Alitakiwa kuwa na maneno mazuri ya kumwambia Edo ili akubaliane na msiamo wake ambao tayari Edo alishaonekana kuushindwa!

Aliendelea kuung'ang'ania mkono wa Edo. Macho yake bado yalikuwa usoni mwa Edo ambaye naye alimwangalia kwa makini akisubiri ujumbe kutoka kwa mpenzi wake. Alijua ujumbe wenyewe usingekuwa mzuri sana kwake, lakini alitaka kusikia chochote kutoka kwake!
Macho ya Lilian yalitingishika, kope zikacheza kidogo kuruhusu usafi wa macho yake. Taratibu alifungua kinywa chake.

Meno yake meupe peee yakaonekana.


Akauuma ulimi wake, akaanza kuzungumza: "Edward."
Edo akashtuka! Hakumbuki mara ya mwisho Lilian kumwita jina lake lote kikamilifu bila kulikatisha na kumwita Edo.
"Nakusikia."
"Mbona umeshtuka?"
"Nimeshangaa ulivyoniita jina langu lote maana si kawaida yako."
"Ni kweli, nimefanya hivyo kutokana na umuhimu wa jambo ninalotaka kukuambia."
"Sawa nakusikiliza."
"Mpenzi wangu jamani, mbona una hasira hivyo? Kuwa na utulivu kidogo basi baba!"
"Lilian nakusikiza."
"Ok! Nikuulize swali moja?"
"Uliza."
"Unanipenda?"
"Hata moyo wako unajua hilo," akajibu Edo akilengwa na machozi.
Ni kweli alikuwa amezungumza hisia zake za ndani kabisa. Hakuwa kwenye maigizo wakati akimwambia Lilian kuwa anampenda na moyo wake unatambua hilo!

Ni kweli, moyo wa Lilian ulitambua hisia za Edo.
"Najua baba. Kama ndivyo, hebu naomba unisikilize kwa makini... umevumilia kwa miaka mingapi mpenzi wangu? Si mitano? Eeeeh? Kuna tatizo gani kusubiri kwa hiyo miaka miwili tu iliyobaki? Kunah araka gani?

"Hivi utaniamini vipi mimi kuwa sitakuwa na mwanaume mwingine? Sikia dear, sijawahi kukutana na mwanaume yoyote tangu kuzaliwa kwangu. Hii ni zawadi yako mpenzi.

"Ona...ukiniacha na hii hali itakuwa ni usalama na ulinzi wa kweli kwako. Siwezi kumpa mtu. Nitakupa wewe tu muda ukifika. Maana yake ni kwamba, ikiwa leo utanitoa usichana wangu, ukiondoka kesho, hata kama nikikutana na mwanaume mwingine huwezi kujua mpenzi.

"Nipe uhuru, niamini. Mbona nakuamini mpenzi? Au huwa unafanya na wengine? Ni heshima kunioa nikiwa msichana kamili. Mpenzi wangu, acha papara!" alisema Lilian kwa sauti laini lakini haraka haraka.
Edo akatulia kwa muda.

"Kubaliana na mimi baba. Kubaliana na hii heshima mpenzi wangu."
"Nimekuelewa mpenzi wangu," akajibu Edo kwa sauti ya utulivu sana.
"Kweli?"
"Ndiyo."
"Umeagiza nini?"
"Nafurahi kula ugali na makange."
"Makange ya nini?"
"Unapenda nini?"
"Wewe umeagiza ya nini?"
"Samaki, sato."
"Uko sahihi kabisa mpenzi."
"Nawe utapenda kula kama mimi?" Edo akauliza.
"Ni lini tumekuwa pamoja tukala vyakula vya aina tofauti?"
"Ok! Ngoja nimwite mhudumu."
Edo akamwita mhudumu na kumuagizia mpenzi wake chakula kama alichoagiza yeye.

"Vije kwa wakati mmoja!"

"Sawa," mhudumu akaitikia akiondoka zake.
Mazungumzo yao yakabadilika, sasa ikawa ni kuhusu maisha yao yajayo na namna ya kudumisha uhusiano wao. Bado kichwani mwa Edo kulikuwa na matumaini.

Ni kweli alimpenda sana mpenzi wake Lilian, lakini alitamani sana japo apate fursa ndogo tu ya kujifurahisha nafsi yake. Ni jambo baya, alikiri lakini japo kidogo tu.

"Nitazungumza naye zaidi. Haiwezekani niwe naye kwa muda wote huo, nimevumilia. Leo nataka kusafiri kwenda Malaysia nimuache hivihivi, hapana bwana. Nitafanya kila njia," akajisemea moyoni mwake.
"Mbona kama unaonekana una mawazo sana?" akauliza Lilian.
"Hapana usijali, nipo sawa mpenzi wangu."
"Vizuri kama ndivyo."

Muda mfupi baadaye chakula kilikuwa mezani. Walifurahia sana chakula hicho. Makange ya sato yakikutana na mtaalamu anayejua kutengeneza, walaji lazima wafurahie.

***
Kadi iligusishwa kwenye kitasa cha mlango. Ukasikika mlio mdogo, Edo akausukuma, ukafunguka. Aliingia mara moja, kisha nyuma yake Lilian akafuatia.
Akasukuma mlango na kuchomeka kadi pembeni ya mlango kulipokuwa na sehemu maalumu ya kuhifadhi. Baada ya hapo Edo akaenda kujilaza kwenye sofa kubwa lililokuwa ndani ya chumba kile.

Bado kichwani mwake alikuwa akiwaza namna ya kumpata Lilian.
"Lakini mpenzi, kwa nini unaonekana una mawazo sana?" Lilian akauliza.
"Lilian, siyo jambo rahisi kutengana kwa muda mrefu kiasi hicho. Miaka miwili ni mingi sana mpenzi wangu. Nafikiria kuhusu usalama wa penzi langu.
"Sina hakika kama utaweza kuvumilia kwa muda wote huo. Nalazimisha kuamini lakini moyo wangu unakataa kabisa mpenzi."
"Kwani ni muda gani tumekuwa pamoja baba?"
"Miaka mitatu."
"Katika kipindi chote hicho, kuna wakati ulihisi nakusaliti?"
"Hapana."
"Kwa nini kipindi hiki?"

"Hata mimi nashangaa, ngoja nijaribu."

Edo alisimama na kuvua tisheti yake, akatoa na suruali kisha akabakiwa na bukta na fulana nyepesi ya ndani. Akajitupa kitandani.
Aliingia ndani ya blangeti na kujikunyata. Ujanja wa joto la Dar es Salaam, ulizimwa na kiyoyozi kilichokuwa kikisambaza hewa taratibu ndani ya chumba kile. Lilian akasimama kwa muda akijishauri.

Akachukua taulo na kujifunga kifuani, kisha akaanza kuvua nguo zake huku akiwa amejikinga na taulo. Akachukua gauni la kulalia, akavaa na kwenda kitandani.
Aliingia kwenye blangeti na kuungana na Edo. Kwa ushawishi wa baridi, Lilian akajikuta akihitaji joto zaidi ya blangeti lililokuwa juu ya mwili wake.
Akamsogelea Edo. Ilikuwa nafasi ya dhahabu. Edo alimvuta Lilian upande wake na kumkumbatia sawasawa. Alikuwa akitetemeka kwa hisia kali za huba.
Kwa namna hali ilivyokuwa, ilikuwa vigumu sana kukubaliana na ukweli kuwa, alitakiwa kulala na mpenzi wake katika hali ile lakini bila kuvunja sharti walilokubaliana. Sharti la kutokukutana kimwili hadi watakapofunga ndoa.
"Nikuambie kitu Lilian?" Edo akasema.
"Niambie mpenzi."
"Ikiwa usiku wa leo hutanipa penzi lako, kesho nitakwenda Malaysia nikiwa sina mchumba niliyemuacha Tanzania. Sitajali muda niliopoteza kwako, ninachotaka ni penzi lako tu!" akasema Edo, safari hii machozi yakianza kutiririka machoni mwake.
Lilian hakujibu kitu!
Itaendelea Ijumaa...
 
Miye ni binaadamu lolote linaweza kunitokea hadithi hii inapatikana katika Gazeti la Mwanaspoti la Kila Ijumaa...
 
Nzuri very sexy and fun I like it.

Sent from my BlackBerry Q10 using JamiiForums
 
Umetulia sana mkuu, hongera zako ni kazi nyingine nzuri utachukua muda wangu sana tu.
 
Mommadou Keita leo ni jumamosi nami nataka pasaka kwa kupata hisia zangu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom