Hadithi tamu: Hisia zangu

Hadithi tamu: Hisia zangu

Nilisema hapa mimi kuna hackers wametumia account ya liliani kuwasiliana na eddo, pole Lily

Big up Mommadou Keita
 
Last edited by a moderator:

HISIA ZANGU -10
ILIPOISHIA...
MHADHIRI aliyekuwa mbele yake, alikuwa kama kopo. Hakuelewa chochote. Kichwa kilimuuma mno. Mawazo yake yalikuwa kwa Edo tu. Hakuwa tayari kumpoteza mwanaume wa maisha yake!
Alijaribu kufikiri labda huenda kuna mtu amevujisha kuwa ameanza kutoka usiku na alirudishwa na mwanaume, lakini jambo hilo halikumwingia akilini mwake maana ilikuwa ndiyo mara ya kwanza, tena siku ya kwanza tu!
Aliwaza zaidi kuhusu email. Hilo ndilo lililomkosesha raha!
“Kuna kitu kimejificha hapa, nitakijua tu!” akajipa moyo.
SASA ENDELEA...
Wingu zito lilitanda kichwani mwa Lilian. Alishindwa kuelewa hiyo email anayolalamikia mpenzi wake Edo ni ipi. Kichwa kilivurugika! Alitakiwa kutumia akili mpaka zile za akiba ili kujua kilichokuwa kikiendelea.
Mhadhiri aliendelea kufundisha mbele ya darasa lakini kichwa kilikuwa kizito sana. Hakuna kitu alichokuwa akikiingiza kutoka kwake.
Hakuona sababu ya kuendelea kuchanganyikiwa. Alikusanya vitu vyake, akasimama akiwa ameukunja uso wake, akatembea moja kwa moja mpaka mbele ya darasa.
Akanyoosha moja kwa moja kuelekea mlangoni. Hakutaka kuzungumza na Mhadhiri aliyekuwa mbele. Darasa zima likamshangaa. Si kwa sababu alitoka nje ya darasa bali namna alivyoonekana mwenye mawazo na uso uliokunjamana!
Alishuka kwenye ngazi fupi zilizokuwa mlangoni, kisha akanyoosha moja kwa moja hadi kwenye Jengo la Utawala. Hapo aliangalia kidogo ubao wa matangazo na kuondoka zake.
Alianza kutembea akielekea chumbani kwao. Alikuwa amechoka sana. Si kwa sababu ya pombe aliyokunywa jana yake, bali majibu ya Edo.
Wakati anatembea akielekea chumbani kwake, alijaribu kumpigia tena Edo mara kwa mara lakini hakupokea simu yake. Alihisi dunia yote imemgeuka.
Moyoni alikuwa na maumivu makali sana. Alivyoamua kuachana na simu ya Edo, simu nyingine iliingia. Alipoangalia kwenye kioo cha simu yake akakutana na jina la Pam.
“Mh! Ananipigia tena sasa,” akasema kwa sauti Lilian.
Hakupokea!
“Anataka nini huyu mbaba?” akajiuliza tena.
Lakini alihisi labda alikuwa na jambo muhimu la kumwambia, akaamua kupokea...
“Haloo...” ilikuwa sauti ya Pam kutoka upande wa pili.
“Haloo kaka Pam.”
“Najua uko chuo, vipi mambo yako?”
“Salama.”
“Nahitaji kukutoa kwa chakula cha jioni leo.”
“Mh! Wapi?”
“Siyo mbali, ni karibu na chuoni. Hapo Mlimani City, Samaki Samaki.”
“Peke yangu?”
“Peke yetu.”
“Unamaanisha?”
“Mimi na wewe.”
“Sawa.”
Wakakata simu zao.
Tayari alikuwa ameshafika chumbani kwake. Akaweka vitabu vyake kabatini kisha akajitupa kitandani. Mawazo yakaanza kufukuzana.
Alikuwa akimuwaza Pam.
***
Edo aliyatoa macho yake kwa mshtuko. Bado hakuamini kama kweli email ile mpya ilitoka tena kwa Lilian. Ni dhahiri Lilian alichanganyikiwa kabisa!
“Naanza kupata wasiwasi sasa,” akajisemea Edo.
Lilian alikuwa amemwandikia ujumbe wenye maneno makali sana. Ilikuwa vigumu kuamini kama ni kweli ujumbe ule ulitoka kwake.
Ujumbe wenyewe ulisomeka: Nashukuru kwa uamuzi wako. Usinitishe, mimi ni mwanamke niliyekamilika. Wewe ukiniona sifai, wapo wenzako wengi wanafukuzana kunitafuta ili waninase.
Huna jipya wewe. Kwanza nilikuvumilia tu kwa kipindi chote nilichokuwa na wewe. Sijawahi kufurahia chochote na sina cha kujivunia kutoka kwako.
Maisha mema.
Ndimi, msichana mrembo ninayejiamini,
Lilian.

Edo alirudia kusoma ile email zaidi ya mara tano, maneno yaliendelea kuwa yaleyale. Sasa aliamua kuchana na Lilian moja kwa moja. Hakuwa na wazo la kuwa naye tena katika maisha yake.
“Nimenawa mikono yangu sasa, siwezi kuwa na mwanamke wa aina hii. Atakuja kunisumbua tu huko mbeleni, lazima,” akajisemea kwa sauti Edo.
Alidhamiria kuhamishia akili yake yote kwenye masomo tu. Sasa aliamua kuachana kabisa na wazo kuwa ana msichana anayeitwa Lilian Tanzania.
***
Si Edo wala Lilian waliogundua kuwa kuna mchezo uliokuwa ukiendelea katika mawasiliano yao. Ilikuwa kazi ndogo sana kwa mtu ambaye alidhamiria jambo lake lifanikiwe.
Lucy ndiye aliyekuwa akijua mchezo ulivyokuwa. Edo hakuwa akiwasiliana na Lilian kwenye email. Aliyekuwa akiandika email zote alikuwa ni Lucy.
Kwa kushirikiana na mtaalamu wa kompyuta, Lucy alifanikiwa kuyateka mawasiliano ya email ya Lilian. Muda aliowaacha wakijisomea na wenzake, siku ambayo jioni yake walitoka na kwenda Maisha Club, ndiyo mchezo ulipofanyika.
Lucy alimwita mtaalamu ambaye alimmilikisha akaunti ya Lilian. Ujumbe wowote wa Lilian ulioingia uliingia kwa Lucy na alikuwa anaweza kumwandikia mtu yeyote kwa anwani ya Lilian.
Hilo halikujulikana!
Hii inamaana kuwa, ni Lucy ndiye aliyekuwa akimwandikia ujumbe wa hovyo Edo akiwa na lengo la kumkasirisha ili aachane na Lilian, sababu ikiwa ni kuwakutanisha kwa urahisi zaidi na pedeshee Pam.
Hiyo ilikuwa siri nzito.
Siri iliyojulikana na watu watatu tu; Lucy, Pam na mtaalamu aliyefanya kazi hiyo Rwegeshora. Hapakuwa na mtu wa nne.
***
Kazi ya kujikwatua ilikamilika ndani ya dakika ishirini. Akiwa amevalia gauni refu la rangi nyeusi na mtandio wa rangi ya buluu, Lilian alisimama mbele ya kioo kilichokuwa kwenye meza ya kujipambia.
Alimwangalia msichana aliyekuwa akionekana ndani ya kioo kile, kisha akatabasamu! Hakuwa na shaka kuwa, msichana yule alikuwa mrembo sawasawa.
Aligeuza shingo, akamwangalia. Akageuza upande mwingine tena, akaachama midomo yake. Akageuka upande, akachanganywa na hips za kuvutia kama bastola zilizochomoza pembeni mwa mapaja ya msichana yule.
Sasa akageuka nyuma!
“Mh! Msichana mzuri sana. Mrembo mwenye sifa zote. Anavutia hakika,” akasema akitabasamu.
Lilian alikuwa akimsifia msichana aliyekuwa ndani ya kioo mbele yake. Alikuwa akiangalia taswira yake mwenyewe kwenye kioo. Hakuwa na shaka kuwa, eneo lote la Mlimani City, jioni hiyo kusingekuwa na mwanamke mzuri aliyependeza kama yeye!
Mara simu ikaita!
Ni Pam alikuwa anampigia!
Akapokea...
“Nimeshafika mama, upo tayari?” Pam akamwuliza.
“Bila shaka, dakika mbili tu nitakuwa hapo barabarani,” akasema Lilian kisha akakata simu.
Mara moja akatumbukiza miguu yake kwenye viatu virefu kiasi. Akachukua mkoba na kuubamiza mlango!
Akatembea kama Twiga!
Itaendelea...
 
Mkuu salama? wengine hatujaona sehemu ya 8 na 9

Sent from my iPhone using JamiiForums mobile app
 
mhhhhhh....shikamooooooooo kaka momma...ebu endelea kidogo tuuuu
 
uyo lily nae mjinga tuuuu...inaaana ameshidwa kabisa kuingia kwenye email yake kusoma kilichoandikwa...password czilezile..alaaaaaa...ameniboaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa...mxuuuu..
 
Eddo alifanya kosa kubwa kuiacha bikra et imsubiri mm nngeivunja hata kwa nguvu looh....hadith tamu kweliiii
 
Wanafunzi wa chuo siku hizi wanafanana na wanasisa wa TZ! Huyu Liliani na yeye ni kilaza Edo alimweleza kuwa kuna ujumbe wa barua pepe, kwanini asiingie kwenye akaunti yake ajiridhishe. Maana hacker akimaliza lazima anafuta sent items au kama hacker naye ni kilaza angeziacha and so angegundua shida ilipo!

What I am saying mtunzi, angeenda mbali kuondoa hili, ili hadithi ijae uhondo! Other wise good story!!

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Maskini Lily na Eddo ndo mmeshaachanishwa hivyo!
Hivi Lilian, eddo alivyokwambia umemtumia email mbona hata hujajishughulisha kuingia kwenye email yako kuhakiki badala yake unatoka kwena kwa pedeshee, why? msomi gani hujiongezi mama
 
Yaah! N kweli alipaswa afanye hvyo ili kujua n k2 knaendelea kwenye email yake
 
  • Thanks
Reactions: ram

Hisia Zangu – 11
ILIPOISHIA...
LILIAN alikuwa akimsifia msichana aliyekuwa ndani ya kioo mbele yake. Alikuwa akiangalia taswira yake mwenyewe kwenye kioo. Hakuwa na shaka kuwa, eneo lote la Mlimani City, jioni hiyo kusingekuwa na mwanamke mzuri aliyependeza kama yeye!
Mara simu ikaita!
Ni Pam alikuwa anampigia!
Akapokea...
“Nimeshafika mama, upo tayari?” Pam akamwuliza.
“Bila shaka, dakika mbili tu nitakuwa hapo barabarani,” akasema Lilian kisha akakata simu.
Mara moja akatumbukiza miguu yake kwenye viatu virefu kiasi. Akachukua mkoba na kuubamiza mlango!
Akatembea kama Twiga!
Sasa endelea...

Ni saa 10:00 alasiri, muda ambao kipindi kilikuwa kimemalizika. Kama walioambiana, Lucy na Latifa walitoka kwa pamoja darasani. Wakashuka ngazi taratibu wakianza kutembea kuelekea hosteli.
Tangu wanatoka darasani mpaka wanafika barabara kubwa ya lami, hakuna cha maana walichozungumza zaidi ya stori za hapa na pale.
Lakini baadaye, Latifa akaamua kuvunja ukimya. Akaanza kumzungumzia Lilian...
“Vipi mwenzangu, ulimuona Lilian alivyotoka darasani?” akauliza akionekana kuwa na shauku ya kusikia jibu kutoka upande wa pili.
“Nilimuona sana.”
“Unadhani ana nini?”
“Anajua mwenyewe lakini kwa vyovyote vile, mapenzi ya Pam yatakuwa yameshaanza kumkolea. Unafanya mchezo na pesa?”
“Lakini kweli...”
“Si unamuona Leila, si alijifanya mjanja na mwenye msimamo, yuko wapi sasa? Si aling’ang’ania kuondoka na Big jana. Kuna mjanja kwenye pesa?” akasema.
Wote wakacheka!
Ilikuwa dili!
Kwao ilikuwa furaha, maana fedha ilikuwa inaingia kama kawaida.
“Lakini Pam amenitumia ujumbe nikiwa darasani,” Lucy akasema.
“Amesemaje?”
“Mambo mazuri, leo ana mtoko na Lilian. Watajuana wenyewe. Unajua ninachompendea Pam, hana papara na anajua anachokifanya.”
“Kweli kabisa.”
“We subiri, siku mbili hizi usikie kama utamsikia Lilian akizungumza habari za Edo tena. Kila kitu kitafunikwa na fedha za Pam, niamini mimi.”
“Kwa nini nisiamini wakati dalili zinaonekana wazi?”
“Umeanza kuwa mjanja sasa, unaona maneno hayo?”
“Wewe! Kwani tangu lini nikawa mshamba?”
“Haya bwana, ratiba ya leo vipi?”
“Kiukweli sitaki hata kujichosha sana. Tukapumzike, usiku twende tu hapo Udasa tukale mbuzi choma na ndizi, kisha tushushie na wine, nadhani itakuwa poa!”
“Sawa.”
Wazo likapita!
Fedha kwa wasichana hao ilikuwa jambo dogo sana. Walikuwa na uhakika wa kufanya chochote bila kutegemea fedha zinazoingizwa kwenye akaunti zao na serikali kwa ajili ya matumuzi ya kawaida.
Walitumia usichana wao kujipatia fedha na kufanya kila aina ya anasa za mjini. Ni jambo moja tu walijua, pamoja na yote hayo, vichwani mwao walikuwa na madini ya ajabu.
Walikuwa wakifanya vizuri sana kiasi kwamba, wengine waliamini walikuwa wakitoa rushwa ya ngono kwa wahadhiri ili wawafaulishe. Haikuwa hivyo.
Ukweli ni kwamba, walijua vizuri kujisomea na kujadiliana katika kundi lao. Cha kushangaza ni kwamba, hawakutaka mtu yoyote aungane nao kwenye kundi zaidi ya wao wanne tu; Leila, Lucy, Latifa na Lilian.
Ndivyo msimamo wao ulivyokuwa!
***
Hakutaka lakini alijishangaa akitaka kuingia kwenye anwani pepe yake. Hiyo ni baada ya kuamua kujisomea kwa nguvu na kuachana kabisa na mawazo ya Lilian.
Edo alishaamua kuachana na mambo ya mapenzi. Kichwani mwake aliamini kuwa, Lilian hakuwa mwanamke sahihi kwake, hivyo alijipa muda kutafakari na pengine kutafuta mwingine ambaye angekuwa na penzi la dhati.
Lakini sasa uamuzi huo aliupinga ghafla. Kuna kitu alihisi kikizunguka kichwani mwake. Alitakiwa kujiridhisha tena kupitia maandiko yale kwenye email yake.
“Lilian anaweza kunitusi mimi? Anaweza kunikejeli? Napata shaka na jambo hili. Kuna kitu kipo nyuma kinafanyika. Kipo, naamini kipo,” akawaza.
Muda huo huo akafungua email yake, kisha akaenda kwenye ujumbe wa mwisho kutoka kwa Lilian. Kwa uchungu moyoni, akarudia tena kuusoma. Sasa aliamua kusoma kwa sauti kabisa.
Hakuna kilichobadilika. Maneno yalikuwa ni yaleyale. Alihisi kupasuka kichwa kwa mawazo. Akapata wazo lingine la haraka. Alitakiwa kuzungumza na Lilian muda uleule ili amwulize vizuri kuhusu email alizokuwa akimtumia.
Ni Lilian pekee ndiye angemaliza utata uliokuwa umemzunguka kichwani mwake. Akachukua simu yake mezani kisha akampigia. Simu ikaita kwa muda mrefu sana, lakini haikupokelewa!
Akarudia kupiga kwa mara nyingine, bado haikupokelewa!
“Shiiiiit!” akasema kwa sauti na kuishusha simu hiyo kwa hasira.
Hakuweza tena kuendelea kusoma, alibadilisha nguo, akavaa suti za michezo, akatoka na kwenda uwanjani kwa ajili ya mazoezi ya viungo.
***
Alifungua mlango na kuingia ndani ya gari. Alikutana na tabasamu pana lililodhihirisha fedha kutoka kwa Pam. Lilian akakaa, huku akijishangaa namna woga ulivyoanza kumuondoka kwa kasi.
“Karibu mrembo!” Pam akasema.
“Ahsante. Pole na kazi.”
“Nashukuru, nawe pole kwa masomo.”
“Ahsante sana. Siku yangu haijawa nzuri sana leo, kichwa kimekuwa kizito sana.”
“Usijali, amini kwamba utaimaliza siku vizuri sana.”
“Nashukuru Pam.”
Gari likaungurumishwa!
Walikuwa wanaelekea Mlimani City. Hapakuwa mbali, dakika tatu tu Pam alikuwa anaegesha gari kwenye maegesho eneo hilo. Akashuka, kisha akazunguka upande wa pili haraka na kumfungulia mlango Lilian.
Akashuka!
Wakaongozana hadi Samaki Samaki. Wakapata chakula cha jioni kisha vinywaji vikafuata. Kwa mara ya pili Lilian alikunywa mvinyo. Kidogo alianza kuuzoeazoea!
Hawakukaa sana, saa nne usiku, Pam alimrudisha Lilian chuoni. Akiwa ameegesha gari nje ya jengo la hosteli anayoishi, Pam alitoa bahasha na kuchomoa maburungutu matatu ya fedha na kumkabidhi.
Zilikuwa milioni tatu!
Lilian akasita kupokea.
“Chukua tu!”
“Hapana Pam. Kwa nini unanifanyia yote haya? Hebu niambie ukweli, unataka nini kwangu?” Lilian akamwuliza.
“Unataka kujua ukweli?” Pam akamwuliza akiwa amemkazia macho.
“Ndiyo niambie ukweli Pam, kuwa wazi...” akasema Lilian akionekana kukolea kwa kilevi kidogo.
Itaendelea wiki ijayo...
 
Hisia Zangu – 11
ILIPOISHIA...
LILIAN alikuwa akimsifia msichana aliyekuwa ndani ya kioo mbele yake. Alikuwa akiangalia taswira yake mwenyewe kwenye kioo. Hakuwa na shaka kuwa, eneo lote la Mlimani City, jioni hiyo kusingekuwa na mwanamke mzuri aliyependeza kama yeye!
Mara simu ikaita!
Ni Pam alikuwa anampigia!
Akapokea...
"Nimeshafika mama, upo tayari?" Pam akamwuliza.
"Bila shaka, dakika mbili tu nitakuwa hapo barabarani," akasema Lilian kisha akakata simu.
Mara moja akatumbukiza miguu yake kwenye viatu virefu kiasi. Akachukua mkoba na kuubamiza mlango!
Akatembea kama Twiga!
Sasa endelea...

Ni saa 10:00 alasiri, muda ambao kipindi kilikuwa kimemalizika. Kama walioambiana, Lucy na Latifa walitoka kwa pamoja darasani. Wakashuka ngazi taratibu wakianza kutembea kuelekea hosteli.
Tangu wanatoka darasani mpaka wanafika barabara kubwa ya lami, hakuna cha maana walichozungumza zaidi ya stori za hapa na pale.
Lakini baadaye, Latifa akaamua kuvunja ukimya. Akaanza kumzungumzia Lilian...
"Vipi mwenzangu, ulimuona Lilian alivyotoka darasani?" akauliza akionekana kuwa na shauku ya kusikia jibu kutoka upande wa pili.
"Nilimuona sana."
"Unadhani ana nini?"
"Anajua mwenyewe lakini kwa vyovyote vile, mapenzi ya Pam yatakuwa yameshaanza kumkolea. Unafanya mchezo na pesa?"
"Lakini kweli..."
"Si unamuona Leila, si alijifanya mjanja na mwenye msimamo, yuko wapi sasa? Si aling'ang'ania kuondoka na Big jana. Kuna mjanja kwenye pesa?" akasema.
Wote wakacheka!
Ilikuwa dili!
Kwao ilikuwa furaha, maana fedha ilikuwa inaingia kama kawaida.
"Lakini Pam amenitumia ujumbe nikiwa darasani," Lucy akasema.
"Amesemaje?"
"Mambo mazuri, leo ana mtoko na Lilian. Watajuana wenyewe. Unajua ninachompendea Pam, hana papara na anajua anachokifanya."
"Kweli kabisa."
"We subiri, siku mbili hizi usikie kama utamsikia Lilian akizungumza habari za Edo tena. Kila kitu kitafunikwa na fedha za Pam, niamini mimi."
"Kwa nini nisiamini wakati dalili zinaonekana wazi?"
"Umeanza kuwa mjanja sasa, unaona maneno hayo?"
"Wewe! Kwani tangu lini nikawa mshamba?"
"Haya bwana, ratiba ya leo vipi?"
"Kiukweli sitaki hata kujichosha sana. Tukapumzike, usiku twende tu hapo Udasa tukale mbuzi choma na ndizi, kisha tushushie na wine, nadhani itakuwa poa!"
"Sawa."
Wazo likapita!
Fedha kwa wasichana hao ilikuwa jambo dogo sana. Walikuwa na uhakika wa kufanya chochote bila kutegemea fedha zinazoingizwa kwenye akaunti zao na serikali kwa ajili ya matumuzi ya kawaida.
Walitumia usichana wao kujipatia fedha na kufanya kila aina ya anasa za mjini. Ni jambo moja tu walijua, pamoja na yote hayo, vichwani mwao walikuwa na madini ya ajabu.
Walikuwa wakifanya vizuri sana kiasi kwamba, wengine waliamini walikuwa wakitoa rushwa ya ngono kwa wahadhiri ili wawafaulishe. Haikuwa hivyo.
Ukweli ni kwamba, walijua vizuri kujisomea na kujadiliana katika kundi lao. Cha kushangaza ni kwamba, hawakutaka mtu yoyote aungane nao kwenye kundi zaidi ya wao wanne tu; Leila, Lucy, Latifa na Lilian.
Ndivyo msimamo wao ulivyokuwa!
***
Hakutaka lakini alijishangaa akitaka kuingia kwenye anwani pepe yake. Hiyo ni baada ya kuamua kujisomea kwa nguvu na kuachana kabisa na mawazo ya Lilian.
Edo alishaamua kuachana na mambo ya mapenzi. Kichwani mwake aliamini kuwa, Lilian hakuwa mwanamke sahihi kwake, hivyo alijipa muda kutafakari na pengine kutafuta mwingine ambaye angekuwa na penzi la dhati.
Lakini sasa uamuzi huo aliupinga ghafla. Kuna kitu alihisi kikizunguka kichwani mwake. Alitakiwa kujiridhisha tena kupitia maandiko yale kwenye email yake.
"Lilian anaweza kunitusi mimi? Anaweza kunikejeli? Napata shaka na jambo hili. Kuna kitu kipo nyuma kinafanyika. Kipo, naamini kipo," akawaza.
Muda huo huo akafungua email yake, kisha akaenda kwenye ujumbe wa mwisho kutoka kwa Lilian. Kwa uchungu moyoni, akarudia tena kuusoma. Sasa aliamua kusoma kwa sauti kabisa.
Hakuna kilichobadilika. Maneno yalikuwa ni yaleyale. Alihisi kupasuka kichwa kwa mawazo. Akapata wazo lingine la haraka. Alitakiwa kuzungumza na Lilian muda uleule ili amwulize vizuri kuhusu email alizokuwa akimtumia.
Ni Lilian pekee ndiye angemaliza utata uliokuwa umemzunguka kichwani mwake. Akachukua simu yake mezani kisha akampigia. Simu ikaita kwa muda mrefu sana, lakini haikupokelewa!
Akarudia kupiga kwa mara nyingine, bado haikupokelewa!
"Shiiiiit!" akasema kwa sauti na kuishusha simu hiyo kwa hasira.
Hakuweza tena kuendelea kusoma, alibadilisha nguo, akavaa suti za michezo, akatoka na kwenda uwanjani kwa ajili ya mazoezi ya viungo.
***
Alifungua mlango na kuingia ndani ya gari. Alikutana na tabasamu pana lililodhihirisha fedha kutoka kwa Pam. Lilian akakaa, huku akijishangaa namna woga ulivyoanza kumuondoka kwa kasi.
"Karibu mrembo!" Pam akasema.
"Ahsante. Pole na kazi."
"Nashukuru, nawe pole kwa masomo."
"Ahsante sana. Siku yangu haijawa nzuri sana leo, kichwa kimekuwa kizito sana."
"Usijali, amini kwamba utaimaliza siku vizuri sana."
"Nashukuru Pam."
Gari likaungurumishwa!
Walikuwa wanaelekea Mlimani City. Hapakuwa mbali, dakika tatu tu Pam alikuwa anaegesha gari kwenye maegesho eneo hilo. Akashuka, kisha akazunguka upande wa pili haraka na kumfungulia mlango Lilian.
Akashuka!
Wakaongozana hadi Samaki Samaki. Wakapata chakula cha jioni kisha vinywaji vikafuata. Kwa mara ya pili Lilian alikunywa mvinyo. Kidogo alianza kuuzoeazoea!
Hawakukaa sana, saa nne usiku, Pam alimrudisha Lilian chuoni. Akiwa ameegesha gari nje ya jengo la hosteli anayoishi, Pam alitoa bahasha na kuchomoa maburungutu matatu ya fedha na kumkabidhi.
Zilikuwa milioni tatu!
Lilian akasita kupokea.
"Chukua tu!"
"Hapana Pam. Kwa nini unanifanyia yote haya? Hebu niambie ukweli, unataka nini kwangu?" Lilian akamwuliza.
"Unataka kujua ukweli?" Pam akamwuliza akiwa amemkazia macho.
"Ndiyo niambie ukweli Pam, kuwa wazi..." akasema Lilian akionekana kukolea kwa kilevi kidogo.
Itaendelea wiki ijayo...

Shikamoo....
 
lily unaniuziiiiii ahaaaaaa.....hebu pokea simu uko upewe mashitaka yako.pesa zisikufanye uuze utu wako..thamani ya penzi lako ni kubwa kuliko pesa ambazo ukitumia zinaisha...mxxxuuuuuuuuuu...
 
  • Thanks
Reactions: ram
Back
Top Bottom