Hadithi tamu: Hisia zangu

Hadithi tamu: Hisia zangu

jamani duuuh je nn kitatokea? mkuu itaipost lini tena?
 
Kumbe na wewe ulikuwa unaifuatilia, Lizzyy bana tangu atuache zawadi kalazwa hospital na baba yake alivyocharuka baada ya kujua bintie ana mimba hadi leo kimyaa, hope hata zawadi alishajifungua na bila shaka mwalimu alimuoa

Angalia usituache hewani km zawadi ya Lizzy
 
Last edited by a moderator:
Hisia Zangu-7
ILIPOISHIA...


Nilijua lazima hili lingetokea. Ni wiki tu tangu umeondoka, lakini tayari hisia za usaliti zimeanza kunukia. Nakuomba baada ya kusoma ujumbe huu, tafadhali endelea na maisha yako, nami niache na maisha yangu.
Siwezi kuendelea kulazimisha mapenzi mahali nisipopendwa. Kwa taarifa yako kwa sasa natafuta mwanaume mwingine ambaye ataweza kunithamini na kujua umuhimu wangu.
Kutokea muda utakaosoma ujumbe huu, ondoa kichwani mwako kuwa una mwanamke Tanzania anayeitwa Lilian.
Lilian.
Edo akaamua kujiridhisha tena kujua kama aliyetuma alikuwa ni Lilian. Ni kweli ulikuwa ujumbe kutoka kwa Lilian. Hilo alijihakikishia kwa asimilia mia moja!
SASA ENDELEA...

KICHWA cha Edo kilivurugika! Alianza kuhisi maisha yake machungu nchini Malaysia. Hakuwa tayari kumpoteza mpenzi wake, mwanamke ambaye aliingia moyoni mwake jumla!
Bado alikuwa na maswali mengi. Edo hakuamini kuwa Lilian, mwanamke wa ndoto zake ambaye walikaa muda mrefu na kuvumiliana, tena wakiahidiana mambo mengi amwambie kuwa asimtafute tena.
“Inawezekana kweli ikawa Lilian akanikataa kabisa? Mbona nachanganywa na hili jambo? Lilian amechanganyikiwa? Kinachompa kiburi ni nini? Imekuwa mapema sana kwake kufikia uamuzi huu.
“Sasa nimejua ni kiasi gani nampenda Lilian. Amejaa moyoni mwangu. Lilian ndiye mwanamke wangu. Amepatwa na nini jamani?” akazidi kuwaza.
Alipata wakati mgumu sana. Hakuwa na kitu cha kufanya zaidi ya kumjibu. Bado alitaka kusikia jibu kutoka kwa Lilian kabla ya kuyaaminisha moja kwa moja maneno aliyosoma kwenye waraka pepe.
Edo akamjibu.
Kwako,
Lilian. Nimesoma email zako, nimeelewa uamuzi wako lakini bado nashindwa kuelewa sababu hasa za wewe kuchukua uamuzi huo. Nimejiuliza maswali mengi lakini bado sijapata majibu.
Kweli Lilian umesahau mapema kiasi hicho? Kweli umesahau wema wangu wote? Sasa naanza kuamini kuwa, kumbe hukuwa na mapenzi ya dhati kwangu.
Nimeelewa ni kwanini ulikuwa unaninyima penzi lako. Bila shaka utakuwa umeshatolewa bikra ndio maana hukutaka nijue. Umeniumiza sana. Nahisi harufu ya damu mbichi ndani ya moyo wangu.
Hata hivyo, bado una nafasi ya kutafakari upya. Una muda wa kufikiri na kuamua vinginevyo kama utaona inafaa. Nakupenda sana kutoka ndani ya moyo wangu. Ahsante kwa yote lakini kumbuka sikupaswa kuachwa kwenye maumivu makali kiasi hiki, tena wakati huu wa mwanzoni kabisa wa masomo yangu huku Malaysia.
Moyo wangu unateseka!
Edo.
Kwa hakika Edo hakuweza kuvumilia, muda wote aliokuwa akiandika ujumbe ule, machozi yalikuwa yakimtiririka mashavuni mwake. Haikuwa rahisi kukubaliana na hali ile.
Hakuweza kufanya chochote tena, baada ya kutuma ujumbe ule kwa Lilian, alijitupa kitandani na kuanza kuvuta kumbukumbu za mpenzi wake upya kabisa.
Zilikuwa kumbukumbu za mateso sana. Lilian alikuwa amemtenda katika kiwango kikubwa sana!
***
Lilian aliingia kati. Lucy alikuwa na kazi ya ziada akimshawishi acheze. Kwa aibu akajikuta akicheza. Kwa mbali Pam na rafiki yake Big walikuwa wamekaa wakiendelea kukata kinywaji.
Walikuwa watu wenye fedha zao. Pam alikuwa akisubiri kwa hamu kukutanishwa na Lilian. Hilo ndio lilikuwa lengo lake. Usiku ule alikuwa Klabu Maisha kwa lengo moja tu, kukutana na Lilian.
Hiyo ilikuwa kazi maalumu aliyopewa Lucy aikamilishe. Latifa alikuwa beneti na Leila. Tayari alishamshawishi na kuonja mvinyo kidogo iliyomchangamsha!
Ni Lilian pekee ambaye alikuwa hajaonja kilevi mpaka muda ule. Lilian alivyozoea kucheza pale kwenye sehemu maalumu ya kucheza, Lucy alichepuka kidogo.
Hapo akamwonyesha Pam ishara na kwenda kuketi naye sehemu nyingine ambayo Lilian hakuwaona.
“Vipi mama lao?” akasema Pam akicheka.
“Poa baba lao!”
“Nataka kujua ulipofikia. Mambo yanakwenda vizuri?” akauliza Pam akionyesha wasiwasi kidogo.
“Usiwe na shaka baba, mambo yanaendelea. Hatua ya kwanza imeshafanyika. Si unamuona mrembo ndani ya nyumba? Kilichobaki hapa ni kuwakutanisha tu!”
“Utafanyaje sasa?”
“Hapa ndio nawaza, lakini nadhani nimpe pombe akilewa, wewe unamaliza!” akashauri Lucy.
“Hapana Lucy. Kumbuka mimi simhitaji huyo msichana kwa siku moja. Nahitaji aendelee kuwa wangu. Kumnywesha pombe halafu ndipo niondoke naye najua hatafurahia.
“Unaweza kuwa mwisho wa uhusiano wetu. Kwanini nisitumie njia za kistaarabu? Kitu pekee unachotakiwa kufanya ni kunikutanisha naye tu. Mambo mengine niachie mwenyewe.”
“Kweli Pam?”
“Kabisa.”
Lucy akarudi kuungana na akina Lilian kuendelea kucheza. Muziki ulikolea kwelikweli. Baadaye wakaamua kupumzika kidogo kwenye viti vyao.
Hapo Lucy akatoa wazo la kwenda kukaa na marafiki zake. Hakuna aliyejua hao marafiki ni akina nani isipokuwa Latifa tu. Wote wakakubali. Wakasimama na kuwafuata Pam na Big.
“Pam kutana na marafiki zangu, Leila, Latifa na Lilian,” akasema Lucy haraka kisha akawageukia rafiki zake na kuwaambia:
“Huyu ni rafiki yangu, anaitwa Pam!”
“Nashukuru kuwafahamu, warembo sana.”
Wakacheka!
“Huyu hapa ni rafiki yangu mkubwa hapa mjini, mfanyabiashara mwenzangu, anaitwa Big!”
“Tumefurahi sana kukutana nanyi,” Latifa akajibu akijifanya hawafahamu.
Ukweli ni kwamba Latifa aliwafahamu wote. Vinywaji viliendelea, Leila akiwa ameshazidi kuchangamka. Lilian alikuwa kimya akitumia juisi ya matunda muda wote.
“Kwanini unakunywa juisi muda wote? Nafikiri ungekunywa wine kidogo ili uchangamshe mwili. Siyo kali, ni laini kabisa,” Pam akamwambia Lilian.
“Mh! Naogopa mwaya,” akasema Lilian akionekana kujawa na haya.
“Huna sababu ya kuogopa, ni nzuri. Tafadhali jitahidi unywe hata glasi moja tu!” akazidi kushauri.
“Kweli kaka Pam? Unaniahidi siyo mbaya?”
“Acha ushamba bwana, kama ingekuwa inalewesha mimi ningekuwaje? Mbona nimekunywa muda wote na bado nipo poa,” sasa Leila alidakia.
“Haya bwana, ngoja nijaribu!” akajibu Lilian baada ya kupata ujasiri kutoka kwa rafiki yake Leila.
Bila kupoteza muda, Pam akachukua glasi mezani na kummiminia Lilian kisha akamkabidhi.
“Karibu ufurahie matunda ya mzabibu!” akasema Pam akijilamba midomo, tabasamu aliliachia.
Lilian akapokea akizidi kuonyesha aibu waziwazi. Akapiga funda moja kubwa. Akakunja uso kidogo kutokana na uchungu kiasi aliohisi kutoka katika mvinyo ule.
Maskini, hakujua hatari iliyokuwa mbele yake!
Itaendelea...


 
Keita................hapa tena mpaka tusahau. Big up na like kwa sana.
 
sawaaa..maskiniiii edoooooo....lily kashahalibu hukuuuu..mweeee
 
Chezea marafiki weye!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Lilian ameshaliwa tayari hapo!!!!!!!
 
HISIA ZANGU -8
ILIPOISHIA...
BILA kupoteza muda, Pam akachukua glasi mezani na kummiminia Lilian kisha akamkabidhi.
“Karibu ufurahie matunda ya mzabibu!” akasema Pam akijilamba midomo, tabasamu aliliachia.
Lilian akapokea akizidi kuonyesha aibu waziwazi. Akapiga funda moja kubwa. Akakunja uso kidogo kutokana na uchungu kiasi aliohisi kutoka katika mvinyo ule.
Maskini, hakujua hatari iliyokuwa mbele yake!
SASA ENDELEA...

Pam alitabasamu! Lilikuwa tabasamu pana ambalo halikujificha kabisa. Alikuwa na haki ya kutabasamu maana alikuwa na uhakika kuwa kazi yake sasa ilikuwa ikielekea kuwa nyepesi kuliko kawaida.
Uso wa Lilian ulikunjika sawasawa. Kwa tabu akameza funda moja kubwa la mvinyo. Ikaingia kooni taratibu kabisa! Akatikisa kichwa kwa nguvu!
“Mh! Nitaweza kweli?” akasema Lilian.
“No! No! No! Utaweza. Sikia... hutakiwi kunywa nusunusu, kwakuwa ni mara yako ya kwanza unatakiwa kumaliza hiyo glasi yote kwanza, halafu kutokea hapo ndiyo utaanza kuzoea.”
“Paaaam!” Lilian akasema akimwangalia Pam machoni.
“Yes! Ndiyo ukweli kama unahitaji kuzoea. Siyo chungu sana bwana!”
“Ngoja nijaribu.”
Lilian akanyoosha mkono wake kisha akachukua glasi na kuipeleka kinywani mwake. Aliigika ile mvinyo yote. Aliposhusha glasi ilikuwa tupu kabisa.
“Mnawezaje lakini?” Lilian akauliza.
“Acha hizo bwana, endelea kufurahi,” Leila akasema akionekana tayari ameshalemewa na mzigo mzito kichwani.
Haraka Pam akachukua chupa yenye mvinyo kisha akaijaza tena ile glasi ya Lilian. Akamwangalia kwa jicho la kumkaribisha kisha akarudisha macho yake kwa Lucy.
Wakatabasamu!
Kuna nini tena?
Kazi nyepesi kiasi gani?
“Karibu mama, endelea kufurahi,” akasema Pam.
Sasa Lilian akaichukua tena ile glasi, huku akionekana kuwa na uzoefu kidogo. Alikunywa kidogo, kisha akarudisha glasi mezani.
“Kweli sasa umekua mtoto wa mjini, na wewe inaonekana utazoea mapema sana!” akasema Lucy.
“Kweli wewe una akili sana. Umegundua hilo kama mimi?”
“Yeah, ndicho ninachokiona kwa Lilian,” akasema Latifa.
Kweli Lilian alionekana kuchangamka sana, glasi moja na nusu aliyokunywa tayari ilionekana kumbadilisha kabisa. Uchangamfu wake ukaongezeka ghafla. Hakuna ambaye hakujua kilichotokea.
Ilikuwa tabasamu la pombe!
Palepale Lucy akamwonyesha ishara Pam wasogee pembeni kwa ajili ya mazungumzo. Alianza Lucy kuondoka kisha akafuata Pam, wote wakisema kuwa wanakwenda msalani.
“Nipe changu,” akasema Lucy akitabasamu.
“Usijali, haina shida. Pesa yako utapata.”
“Lakini si umeniamini sasa?”
“Sana. Kinachofuata?”
“Kinachofuata nini tena? Chukua mzigo ondoka nao.”
“Hapana Lucy, kama nilivyokuambia, nahitaji kumchukua huyu mwanamke kwa ridhaa yake mwenyewe,” akasema Pam.
Lucy akabetua midomo yake. Akasema: “Sawa. Najua vizuri sana. Kwa hiyo?”
“Sitaki kumfanya mateka,” Pam akasema kwa sauti tulivu sana.
Ilikuwa sauti iliyoonyesha busara, hekima na uvumilivu. Ndani ya moyo wake hakuwa hivyo, Pam alikuwa mwanaume wa aina ya tofauti kabisa na mwonekano wake.
“Utafanyaje?”
“Nashauri tuwarudishe chuo, nitachukua namba yake ya simu kutokea kwake mwenyewe, halafu sasa nitawasiliana naye mwenyewe. Sitaki ajisikie kuwa amekubali kwa kulazimishwa au kwa kisingizio cha pombe.
“Nahitaji ridhaa yake mwenyewe. Nataka yeye akubali bila shinikizo la mtu mwingine. Nimeshasema nina malengo naye!”
Lucy akacheka!
“Mbona unacheka?” Pam akauliza.
Lucy akacheka tena.
“Mbona sikuelewi? Kwa nini unanicheka?”
“Wewe unaweza kuwa na malengo na mwanamke wewe? Haya...umeanza lini mwenzetu?”
“Fahamu hivyo Lucy, naomba ukubaliane na mikakati yangu maana najua mwisho wake utakuwa mzuri.”
“Sawa, acha nikubaliane na wewe.”
Wakarudi kujumuika na wenzao!
***
Pombe ilikuwa imewakolea sawasawa. Saa 8:30 usiku, waliamua kuondoka klabu na kurudi hosteli. Lilian na Leila walikuwa hawajiwezi kabisa kwa ulevi.
Lucy na Lilian waliingia kwenye gari la Pam, Leila na Latifa, wakaingia kwenye gari la Big, safari ya kuelekea chuoni ikaanza. Mazungumzo njia nzima yalikuwa ya kilevi.
Lilian alikuwa amekaa siti ya mbele ya Pam. Muda wote huo, Pam hakuwa na haraka ya kumweleza hisia zake. Waliposhika Barabara ya Sam Nujoma kwenye mataa ya Mwenge, Pam akaanza kuchombeza...
“Lilian, wewe ni mwanamke mrembo sana. Mwanaume yeyote ambaye atapata nafasi ya kukumiliki atakuwa mwenye bahati sana!” akasema Pam.
“Mh! Kweli?”
“Kabisa.”
“Ahsante.”
“Leila,” Pam akaita tena kisha akatulia.
“Abee...”
“Natamani sana uwe mtu wa karibu yangu, hata kama haitakuwa mambo ya mapenzi lakini nitajisikia fahari kukusaidia katika mambo yako. Wewe ni mwanamke mrembo, hutakiwi kuteseka hapa mjini wakati wanaume tunaojitambua wenye fedha zetu tupo,” akasema Pam.
“Ahsante, haina shida, kama si kwa ubaya ni sawa tu.”
Hapakuwa na magari usiku huo, dakika tano baadaye gari lilikuwa limeegesha jirani na jengo la hosteli ambalo wanaishi akina Lilian. Muda mfupi baadaye Big naye alisimamisha gari.
Kwanza alishuka Lucy, kisha akafuata Lilian lakini kabla hajafanya hivyo, Pam alichomoa burungutu na kumkabidhi!
Zilikuwa milioni mbili!
“Zitakusaidia hizi!” akasema Pam kwa sauti yenye ushawishi wa fedha.
“Ahsante,” Lilian akaitika akizichukua zile fedha.
Akashuka garini na kumbusu mashavuni Pam. Mwanaume wa watu alisisimka sana. Alihisi kama shoti ya umeme ikimtembelea. Wakaongozana hadi kwenye gari la Big.
Latifa alikuwa tayari ameshashuka, Leila aligoma. Alitaka kuondoka na Big. Wote wakashangaa. Ni muda mfupi tu wamekutana na kuzungumza.
Kutoka Masaki mpaka chuoni tayari walishakuwa wapenzi! Lilikuwa tukio jipya kwa Lilian. Bado aliendelea kuwaza kuhusu burungutu la pesa alizopewa na Pam! Big akaondoa gari Leila akiwa pembeni yake.
Range Rover ya Pam ikaunguruma, akaingiza gia namba moja, akakanyaga mafuta!
Ikapepea!
Itaendelea...



 
Watu wanaokamata hisia za watu kupitia kazi zao za sanaa wanapoamua kwa makusudi kuchezea hisia za watu hawana tofauti na Interahamwe...Mommadou Keita chonde chonde...em maliza hii maneno!
Mkuu Rich Pol usiwe na wasiwasi hii hadithi itakuwa hapa kila Jumatatu, najua kiu mliyonayo, bado sijafikia hata robo ya kuitwa Interahamwe.... aaaah aaaah...
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom