Hadithi tamu: Hisia zangu

Hadithi tamu: Hisia zangu

Utaipata hapa Jumamosi (Jumapili), kila Ijumaa inatoka kwenye Gazeti la Mwanaspoti.

Kama ilivyokuwa kwa EDO na sisi trutasubiri tu Jumamosi au jumapili mbona siyo mbali???

Tofauti na miaka miwili aliyoambiwa EDO asile kitumbua kile!!! mmmhhhhhhh

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Hisia zangu-3

AKAMSOGELEA Edo.
Ilikuwa nafasi ya dhahabu. Edo alimvuta Lilian upande wake na kumkumbatia sawasawa. Alikuwa akitetemeka kwa hisia kali za huba.
Kwa namna hali ilivyokuwa, ilikuwa vigumu sana kukubaliana na ukweli kuwa alitakiwa kulala na mpenzi wake katika hali ile lakini bila kuvunja sharti walilokubaliana.
Sharti la kutokukutana kimwili hadi watakapofunga ndoa.
“Nikuambie kitu Lilian?” Edo akasema.
“Niambie mpenzi.”
“Ikiwa usiku wa leo hutanipa penzi lako, kesho nitakwenda Malaysia nikiwa sina mchumba niliyemuacha Tanzania. Sitajali muda niliopoteza kwako, ninachotaka ni penzi lako tu!” akasema Edo, safari hii machozi yakianza kutiririka machoni mwake.
Lilian hakujibu kitu!
ENDELEA...

ALILIA kama mtoto mdogo. Machozi yalitiririka machoni mwa Edo. Pamoja na mwanga hafifu chumbani mle, Lilian aliweza kuyaona vizuri machozi ya mpenzi wake.
Alikuwa analilia mapenzi. Edo alionekana hakuwa tayari kuondoka Tanzania na kumwacha mpenzi wake wa muda mrefu bila kukutana naye kimwili.
Lilian alichanganyikiwa sana. Hakutaka kumuudhi mpenzi wake, lakini pia hakuwa tayari kuvunja ahadi yake. Bado moyo wake ulimwambia alitakiwa kufanya hivyo baada ya kuingia tu kwenye ndoa yao.
“Edo mpenzi wangu,” Lilian akaita.
“Maneno yako hayatakuwa na maana yoyote kwa sasa.”
“Nisikilize kwanza mpenzi.”
“Lilian najua unaweza sana kuongea. Najua ulivyo na maneno ya ushawishi. Ninachokuomba kama kweli una nia na mimi, kama kweli unanipenda, ikiwa kweli mimi ndiye mwanaume wako wa dhati, nakuomba sana, usikatae ninachokitaka.
“Utaniacha na mateso makubwa sana ya moyo. Sijui kwa nini moyo wangu una mashaka kiasi hiki. Sina amani hata kidogo. Najua utanisaliti tu Lily, utanisaliti mama,” alisema Edo akionesha msisitizo wa hali ya juu katika kile alichokiongea.
“Siwezi kufanya hivyo baba, mimi nakupenda wewe tu, sina mwingine na wala sifikirii kuwa na mwanaume mwingine zaidi yako. Kubaliana na maneno yangu nakuomba,” alisema Lilian.
“Unasema kweli?”
“Kweli Edo.”
“Kwa nini hutaki kukutana na mimi sasa?”
“Si kwa nia mbaya kama nilivyokuambia, nafanya hivyo kwa sababu nzuri. Kwani huwezi kulala na mimi bila kunigusa?
“Hebu vuta picha, itakuwa furaha kiasi gani kama siku ambayo utakuwa unafunga ndoa na mimi unikute nikiwa na usichana wangu? Sitaki kumkasirisha mama yangu.
“Aliniambia nihakikishe jambo hili nalisimamia. Sipendi kumkosea. Tafadhali kubaliana na mimi mpenzi wangu. Nakupenda Edo, wewe ni wangu wa pekee,” alisema Lilian kwa sauti tamu, laini ikionyesha kumaanisha alichosema.
Edo alinyamaza kwa muda. Alitakiwa kutafakari kwanza. Ni kama Lilian alikuwa makini na maneno yake na alijipanga kwa kila neno moja lililotoka kinywani mwake.
Pamoja na yote hayo, Edo alijikuta akiguswa sana na maneno ya mpenzi wake. Ni kweli alivumilia muda mrefu. Kwa nini kipindi hicho kifupi tu?
Alilegeza masharti moyoni mwake, akakubali kumuacha mpenzi wake Tanzania bila kumgusa kabisa. Hilo alilipasisha moja kwa moja moyoni mwake.
“Lilian,” akaita Edo.
“Abee Edo, mpenzi wangu.”
“Sikiliza maneno yangu.”
“Nakusikiliza baba.”
“Tazama macho yangu...”
“Nayaona baba.”
“Unaona nini?”
“Machozi.”
“Machozi yapo kweli, hakuna kingine unachokiona zaidi ya machozi?”
“Kwa kweli sioni kitu zaidi ya machozi.”
“Angalia kwa makini Lilian,” akasisitiza Edo.
Lilian akatulia. Hapo sasa akaamua kumwangalia kwa makini zaidi. Alimwangalia tena na tena.
Hola!
Hakuna alichokiona!
Aliishia kuona kilekile...
Aliona machozi ya Edo.
“Bado hujaona tu baby?”
“Tafadhali naomba uniambie.”
“Sikia, nakupenda sana. Nakupenda kuliko utakavyoweza kufikiria. Nakupenda kwa moyo wangu wote na ninaamini hizi hisia zangu. Sijui kama nawe unanipenda mpenzi.”
“Nakupenda sana Edo, sina cha kusema au cha kukuonyesha ni kwa kiasi gani nakupenda, lakini fahamu kuwa nakupenda. Kitu pekee kitakachothibitisha kuwa nakupenda ni kukutunzia heshima yako mpaka siku tutakayofunga ndoa.
“Naamini hapo utakubaliana nami kuwa kweli nakupenda. Kwa sasa huwezi kuelewa mpenzi. Usichana wangu ndiyo zawadi ya pekee yenye thamani kuliko zote mpenzi wangu. Niamini baba, nenda salama chuoni, utanikuta. Mimi ni wako,” akasema Lilian.
“Kweli?”
“Niamini mpenzi.”
“Nakuamini mama.”
Edo alitulia tena, ni kama alikuwa katika lindi fupi la mawazo. Aliikunja mikono yake kidogo, akanyoosha mguu wake mmoja, akiwa ndani ya blangeti, alijivuta hadi alipokuwa amelala Lilian.
Walitenganishwa na mto uliokuwa katikati yao. Edo aliunyakua haraka na kuurusha mgongoni mwake. Sasa walikutanisha miili yao. Kwa kasi ya ajabu, alimvutia Lilian kwake.
Akaenda mzimamzima!
Lilian hakuwa na nguvu lakini bado alikuwa akitaka kuona kitakachofanywa na Edo. Mwanaume wa maisha yake. Midomo ya Edo ikaanza kucheza.
Alikuwa anazungumza: “Mpenzi wangu Lilian, lazima nikueleze kuhusu hili. Siwezi kuacha kusema maana naona inaweza kusababisha matatizo siku za baadaye.”
Lilian akashtuka!
Alitaka kujitoa kifuani mwa Edo, akamdhibiti. Haikuwa rahisi kuponyoka mikononi mwa mwanaume yule aliyekuwa mshirika wa kudumu wa mazoezi ya viungo.
“Tulia...” akasema Edo.
“Niambie ni nini baba?”
“Naheshimu sana hisia zangu za ndani. Sijui kwa nini nafikiria hivyo, lakini nahisi kama nikikuacha huku Tanzania lazima utanisaliti. Kama hisia hizi si za kweli, tafadhali naomba uthibitishe kwa kuwa mwaminifu.”
Lilian alihisi moyo wake ukiingiwa na ubaridi kama wa maji ya barafu. Hakutegemea kusikia maneno hayo kutoka kwa mpenzi wake Edo. Yalikuwa maneno mazito sana yaliyomchanganya.
“Edo?! Kweli unaweza kunifikiria hivyo baba?”
“Lazima nikuambie kilichopo moyoni mwangu.”
“Naomba uwe na amani mpenzi wangu, usinifikirie vibaya hata kidogo. Mimi ni wako na nitaendelea kuwa wako milele. Tafadhali, safiri ukiwa na amani moyoni mwako kuwa nitakuwa salama na nitahifadhi mali zako!” akasema Lilian.
“Ok! Acha nikuamini. Nakupenda mpenzi. Tulale sasa, umeshakuwa usiku, kesho tutazungumza zaidi.”
“Sawa mpenzi wangu.”
Ilikuwa kama kifaranga cha kuku kikiwa kimekumbatiwa na mama yake, Lilian alilala kifuani mwa Edo. Ahadi yao iliendelea kuwa ileile, kwamba hawatafanya chochote usiku huo.
Ni ahadi ambayo ilitekelezwa!
***
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ulikuwa bize sana jioni hiyo. Watu walikuwa katika pilikapilika za kusafiri au kupokea wageni wao kutoka ndani na nje ya nchi.
Edo na Lilian walikuwa miongoni mwao; kwao ilikuwa siku yenye maumivu makali ya moyo. Edo alikuwa anaachana na mwanamke wake akiwa na uhakika wa kutoonana naye kwa miaka miwili! Kilikuwa kipindi kirefu sana.
Kilikuwa kipindi ambacho Edo aliamini kingetosha kabisa kubadilisha historia ya uhusiano wao. Aliuona usaliti waziwazi kabisa. Kweli Lilian amvumilie kwa muda wote huo?
Miaka miwili?
Ilikuwa mingi sana. Ni muda ambao ungeweza kubadilisha chochote na akampoteza mpenzi wake. Alikuwa na mizigo yake, tayari kuingia chumba cha ukaguzi na kuendelea na taratibu nyingine za safari.
Walisimama wakiwa wanaangaliana, kila mmoja alionekana kuwa na mawazo yake kichwani. Edo alivumilia yote. Alikubaliana na yote. Alimwacha Lilian aamua mwenyewe. Amsaliti au amtunzie heshima.
“Nakuambia kwa mara nyingine nakupenda sana mpenzi wangu. Naondoka nikiwa nimekuacha na usichana wako, tafadhali nikirudi nikukute nao,” akasema Edo akimwangalia Lilian kwa hisia kali za mapenzi.
“Nakuahidi mpenzi wangu. Nimeshasema mengi, sina ya kuzungumza zaidi. Nakupenda sana, nakutakia safari njema!” akasema Lilian.
Haikuwa rahisi, lakini ndivyo ilivyokuwa na ilipaswa kuwa hivyo. Edo aliachiana na Lilian, akasogea kwenye foleni ya kuingia chumba cha ukaguzi.
Edo akageuza kichwa na kumwangalia Lilian, alichokutana nacho, kilimtisha sana. Alipigwa na butwaa!
Itaendelea Ijumaa ijayo...

ILIPOISHIA

heeeee...jamaniiii..ijumaaa gani tena momma zaidi ya hiiiii...tafadhali hebu kuja huku ..usinipe mshituko mieeeeeeeeeeee........
 
[MENTION]
Mommadou Keita[/MENTION]

Yaani tumekuwa kama EDDO na sisi kusubiri muda mrefu..................
 
  • Thanks
Reactions: ram
ILIPOISHIA...
Hipsi zilikuwa kivutio kingine, mwisho ni milima ya haja iliyokuwa nyuma ya viuno yao! Hakika walifungasha. Kufungashia huko hakukuwa na maana kuwa walifanana na majimama, la hasha!
Milima yao iliendana kabisa na maumbo yao. Kwa mifanano ya maumbo walikuwa sawa, tatizo likawa kwenye tabia. Hasa kwenye maisha yao ya kimapenzi.
Leila na Lilian walikuwa na misimamo inayofanana. Leila alikuwa na mpenzi wake mmoja anayejulikana aliyeitwa Michael, maarufu zaidi kama Mike, Lilian yeye alitoka na Edo ambaye awali alikuwa akisoma naye chuoni hapo.
Latifa na Lucy wao habari zao zilikuwa nyingi! Hawakutulia na wanaume kabisa. Mikesha na kwenda klabu ilikuwa ndiyo michezo yao. Pamoja na yote hayo, bado wote kwa pamoja walikuwa na juhudi sana darasani na walikimbiza wenzao katika masomo yote.
Lilian alikuwa akitembea kwa pozi kama vile alikuwa akizionea huruma ngazi alizokuwa akitembea. Bado alishindwa kuondoa Edo kichwani mwake.
SASA ENDELEA...

ILIKUWA ndiyo kwanza siku ya pili inakatika baada ya kuagana na Edo. Hadi muda huo hakuwa na mawasiliano yoyote na Edo ingawa alimtumia waraka pepe tatu na zote hakujibu. Kwa mbali akawaona rafiki zake akina L wakiwa wamekaa kivulini wanajisomea.
Ni palepale pa siku zote!
Kwa kawaida walizoea kusomea sehemu moja. Lilian alikazana na kuwafikia. Lilikuwa kundi zuri sana la majadiliano kutokana na namna wote walivyokuwa na mtazamo mkubwa na uwezo wa kuelewa.
“Mambo zenu warembo?” Lilian akasalimia.
“Poa Lilian, vipi mwenzetu?” Leila alikuwa wa kwanza kuitikia salamu.
“Safi tu.”
“Karibu mrembo, tunatengeneza maisha hapa, hatupo tayari kuendelea kunyanyaswa na wanaume, elimu ndiyo mkombozi wetu wa kweli,” Latifa naye akasema.
“Kweli kabisa,” akajibu Lilian kisha akaketi na kutoa vitabu vyake.
Jambo lililomshangaza ni kwamba, muda wote aliofika hapo, Lucy hakusema kitu chochote! Lilian hakumfikiria vibaya, aliamini ni masomo ndiyo yaliyokuwa yamembana. Akanyamaza kimya na kuanza kupiga kitabu.
Wote wakawa kimya!
Dakika tano baadaye, Lucy alionekana kuchukua bahasha kwenye begi lake la vitabu na kumkabidhi Lilian. Alipokea kwa mshangao. Ilikuwa bahasha ndogo kiasi lakini iliyonona. Ilionekana ndani yake kuwa na makabrasha muhimu ila yaliyojaa.
“Ni nini?”
“Utafungua baadaye.”
“Kama ni bomu je?”
“Mh! Wewe naye, nani wa kukuwekea bomu sasa mtoto wa kike?”
“Niambie ni nini basi?”
“Mtoto una haraka sana wewe. Haya fungua!” akasema Lucy.
Lilian akafungua. Alikutana na burungutu la noti za elfu kumikumi!
Bahasha ilikuwa imejaa kiasi kwamba haikuwa rahisi kufungika vizuri.
“Zimetoka wapi?”
“Hapo sasa tutazungumza baadaye.”
“Hapana Lucy, chukua pesa zako.”
“Acha upuuzi wewe, lini utakuwa na akili? Huyo Edo unayemn’ang’ania, unajuaje kuwa naye hakusaliti? Kwanza sasa hivi hayupo nchini, una wasiwasi gani? Tumia urembo wako vizuri mtoto, la sivyo utabaki unang’aa macho tu mjini hapa,” akasema Lucy kwa msisitizo.
Lilian hakuwa mtoto, alishajua kuwa zile fedha zilitoka kwa mwanaume. Kwa Lucy na Latifa, kubadilisha wanaume lilikuwa jambo la kawaida kabisa.
“Lucy tunaheshimiana sana mimi na wewe, kumbuka kinachotukutanisha hapa ni masomo tena ni kwa vile hili ni kundi letu la kujisomea na ni zuri. Tuishi kwa kuelewana na kuheshimiana.
“Ni vyema kila mmoja akaheshimu hisia za mwenzake. Kwanini unataka kunilazimisha nifanye kitu ambacho sikipendi? Chukua pesa zako,” Lilian akasema kwa ukali sana.
“Sitaki, kama unaweza kuzichoma labda ufanye hivyo. Huo ushamba utakutoka lini? Kwani kula pesa ya mtu ndiyo kumkubali? Acha ujinga, kula maisha hayo, mambo mengine baadaye,” akasema Lucy akijiandaa kuinuka.
Ni kweli aliinuka.
Alikusanya vitabu vyake na makabrasha mengine, akaondoka zake. Pale akawaacha Latifa, Leila na Lilian wakimshangaa.
Ama kweli alishangaza!
“Sikia shosti, kwani wewe umeomba hela?” akasema Leila.
“Ndiyo nashangaa!”
“Sasa huna haja ya kushangaa, chukua mzigo utumie. Ni nani anaweza kukufuata kukudai? Kwani umekopeshwa? Tumia lakini akikuambia mambo ya wanaume kataa,” akasema Leila na kuungwa mkono na Latifa:
“Kweli kabisa, sioni tatizo.”
“Wewe na yeye ni walewale tu!” akasema Leila.
“Jamani hebu tusomeni basi, kwani Lilian ni mtoto? Kwanini tunatofautina kwa mambo binafsi? Yeye ni mtu mzima na anaweza kuamua chochote kwa utashi wake,” akasema Latifa.
Lilian alikuwa kwenye mzigo mzito wa mawazo lakini alipotafakari sana, hakuona sababu ya kukataa hizo fedha. Akaziweka kwenye mkoba wake na kuendelea kujisomea.
“Kibaya ni kumsaliti Edo, kama ni pesa sioni tatizo lake,” akajisemea moyoni mwake akiendelea kujisomea.
***
Edo alifika jijini Kuala Lumpur, nchini Malaysia salama kabisa. Alikuwa na maelekezo yote, hivyo haikuwa vigumu kwake kufika chuoni. Alipokelewa vizuri na kuelekezwa chumbani kwake kisha taratibu nyingine zikafuata.
Alikuwa mchovu sana kutokana na safari ndefu ya kutoka Tanzania hadi Malaysia. Siku tatu baadaye ndipo alipopata utulivu wa akili kidogo. Akiwa chumbani kwake, akakumbuka kuwasiliana na mpenzi wake.
Bado hakuwa na mawasiliano ya simu ya mkononi, simu alikuwa nayo lakini alikuwa bado hajapata usajili wa namba kutoka moja ya kampuni za simu nchini humo.
Alifungua laptop yake na kuingia kwenye akaunti yake ya waraka pepe. Alikutana na ujumbe kutoka kwa watu wengi sana, akiwemo Lilian ambaye alimwandikia mara tatu. Akaanza kusoma mmoja baada ya mwingine.
Hello,
Edo. Najua umefika salama mpenzi wangu. Pole na safari baba. Napenda kukuhakikishia kuwa, moyoni mwangu umejaa wewe pekee na hakuna nafasi ya mwingine zaidi yako. Nakupenda sana.
Ukipata ujumbe wangu, tafadhali unijibu.
Lilian.

Edo akavuta pumzi ndefu sana kisha akazishusha taratibu kabisa. Akatulia kwa muda. Baadaye kidogo akafungua ujumbe unaoufuata.
Ujumbe huo ndiyo uliomshtua sana moyo wake. Aliuma meno kwa nguvu, akarudi kuangalia jina na anwani ya mtu aliyemtumia ili ajiridhishe kuwa Lilian ndiye aliyemtumia.
Ni kweli alikuwa ni Lilian!
Akazidi kuchanganyikiwa!
Itaendelea…
 
Back
Top Bottom