HADITHI: KIZUIZI
SEHEMU YA TISA
Macho na masikio pekee ndio viungo vilivyokuwa huru kufuatilia tukio hili kikamilifu. Kichwani alipitisha maswali mengi lakini akakosa majibu, aliamini kuwa laiti kama angekuwa mzima wa afya hakika angepata cha kusema juu ya ndoa ile ya kifahari. Alipokumbuka juu ya uzima wake akawalaani wale mbwa waliomkimbiza, akataka kumlaani na dereva aliyemgonga na pikipiki lakini akakumbuka kuwa dereva yule alikufa hata kabla ya kufikishwa hospitali.
Laana zake akazihamishia kwa muuaji wa Deo.
Nani amemuua Deo? Alijiuliza tena.
Macho yake yakaitazama luninga akakutana na James
akimlisha mkewe keki kwa kutumia midomo. Hasira ikamkamata akataka kutukana, taya lililovunjika likamsaliti akauma meno kwa uchungu, chozi likamtoka kutokana na maumivu ya taya.
Jose B waukweli hapa sina ujanja aisee. Ila ngoja nipone.. Alikiri kimya kimya wakati kile kipindi kikielekea ukingoni.
Wagonjwa walivutiwa na kipindi kile, Jose B akafurahishwa na huduma bora kutoka hospitali binafsi. Laiti kama angekuwa hospitali ya serikali hata hiyo luninga asingeweza kuiona. Na hiyo ndoa ya James na mkewe asingepata fursa ya kuitazama pia.
ENDELEA...............
Ndege ilitua katika ardhi ya nchi ya Uganda katika jiji la Kampala, uwanja ndege wa kimataifa wa Entebbe. Haikuwa mara ya kwanza kwa James kutia mguu wake katika jiji hili. Lakini kwa upande wa Emmy ilikuwa mara yake ya kwanza.
Wapambe walioandaliwa jijini hapo waliwapokea kama wanavyopokewa maraisi ama viongozi wengine wa serikali.
Moja kwa moja wakaongozwa na kuingia katika magari kadhaa. Safari ikaanza, ilichukua takribani dakika arobaini na tano kutoka uwanja wa ndege hadi kuifikia hoteli ya kimataifa yenye nyota tano ya Sheraton.
Safari ya wapambe ikaishia katika chumba cha mwisho kabisa cha hoteli hii yenye ghorofa kumi na tano ikiwa na vyumba mia mbili na nane.
Emmy na James wakabaki peke yao katika chumba namba 208.
Chumba ambacho James alikichagua kwa sababu maalumu kabisa na alikilipia miezi miwili kabla ya siku hiyo.
Katika chumba hicho cha juu kabisa mteja anaweza kuiona kwa uwazi fahari ya Uganda, vilima vya Kololo na Nakasero ambavyo vinavutia sana kutazama.
Ilikuwa mara ya kwanza kwa mwanadada Emmy kuingia katika hoteli ya kifahari namna hii ambayo kwa usiku mmoja ilikuwa inalipiwa dola za kimarekani 440 ambayo ni zaidi ya shilingi laki tano za kitanzania.
Katika nafsi yake alikiri kuwa kuolewa na mtu mwenye pesa zake wakati mwingine ni jambo jema sana.
Angeyaona wapi haya kama angeolewa na kapuku kama fulani?
James hakuwa na haraka sana ya kutimiza haja yake. Haja iliyomfanya amuoe Emmy. Alikuwa mtulivu sana.
Baada ya kupumzika kwa takribani nusu saa, alimuongoza Emmy wakabadili nguo zao kisha wakatoka nje na kuchukua lifti ambayo iliwafikisha katika mgahawa mkubwa ndani ya hoteli hiyo ya aina yake katika jiji la Kampala na Afrika mashariki kwa ujumla.
Equator Lounge. Emmy aliyasoma maandishi makubwa mlangoni.
Huku walikula na kunywa huku James akionekana kumjali zaidi mkewe kuliko anavyojijali yeye.
Hali hii ilimfanya Emmy ajute sana kwa kitendo cha kutotimiza ahadi na kufanya uzinzi na Lameck.
Baada ya kula waliliendea bwawa la kyoga ambalo lipo pia ndani ya hoteli hiyo ya kimataifa.
Hapa ndipo simulizi ya kushangaza inapoanzia.
Emmy hakuwa mzoefu hata kidogo katika kuogelea, James alikuwa mzoefu sana katika mambo hayo. Akamchukua Emmy katika namna ya kumfundisha, Emmy alikuwa amevaa kinguo chepesi sana na James alikuwa na bukta yake maalumu kwa ajili ya kuogelea.
Akamshika Emmy kifuani, akaanza kuogelea naye taratibu.
Kila mara alivyojaribu kumweka sawa Emmy alifanya namna ya kuzitikisa chuchu zake ndogo za moto ambazo zilikuwa wima kama askari mkakamavu katika gwaride.
Kadri alivyozipapasa nazo zikazidi kuwa imara.
James akaingiwa matamanio, lakini hakusema.
Pumzi za Emmy zikaanza kupishana kwa kasi ya ajabu kama ambaye anatapatapa kujiondoa katika hatari fulani ama aliyemaliza mashindano ya riadha ndefu.
James akaganda kama kinyago. Hali ilikuwa mbaya sana.
Juhudi za kufanya subira zikashindikana.
Upesi kabla ya lolote la kuwatia aibu kutokea alimtwaa Emmy mpaka nje ya maji. Akamfuta hovyohovyo kisha wakakimbilia ndani katika lifti. Ikawarejesha chumbani.
Kitanda kikubwa cha kisasa chenye mashuka meupe sana kikawapokea.
James akamnyanyua Emmy na kumrusha kitandani.
Emmy aliyekuwa anathema juu juu akakata ghafla pumzi hizo na kurejewa na pumzi zake za kawaida.
Jimmy...noooo.... akamzuia mwanaume yule aliyetaka kumvamia pale kitandani.
James kimya. Akashangaa.
Naomba nipumzike kidogo mume wangu...utaniua ujue... aliongea kwa kubembeleza huku moyoni akikiri kuwa alikuwa katika uhitaji mkubwa wa hicho anachohisi.
Lakini asingeweza kumruhusu, kuna sharti moja alikuwa hajatimiza.
James akiwa katika upole hakuwa na cha kupinga, akamkubalia Emmy.
Msichana huyu akajifanya amepitiwa na usingizi, James akasinzia kweli.
Emmy akanyanyuka na kuelekea bafuni, kwa siri kubwa akatoa kisabuni kilichopigwa lebo ya KAISIKI
Kaisiki ni sabuni ambayo alipewa na Lameck. Alitakiwa kujiosha na sabuni hii masaa kadhaa kabla ya tendo, ni jambo hili alikuwa hajalifanya.
Akafanya kisha akarejea kitandani baada ya kuwa ameificha.
Saa nane usiku, Jimmy akahisi anapapaswa, aliposhtuka alikuta ameelekezewa bastola mbili fupi zinazofanana. Alikuwa ametekwa.
Hofu kuu ikatanda. Bastola zile zikamsogelea na sasa zikamgusa, mapigo ya moyo yakapanda maradufu, hakutegemea kama anaweza kutekwa kutoka usingizini bila hata dalili za kutekwa.
Bastola zile badala ya kutoa risasi zikamchomachoma kifuani na kuunda joto kali.
James akaamua kupambana. Akazishika zile bastola mbili kutoka katika kifua cha Emmy.
Kilichoendelea hapo, makelele ya kuigiza yaliyopigwa na Emmy na mengine yote.
Si mimi wala wewe anayeweza kuyasimulia lakini vilima vya Kololo na Nakasero vilishuhudia kila kitu, hata wakati muhudumu anapewa pesa ya ziada kwa ajili ya kufua mashuka yaliyotiwa doa na damu vilima vilishuhudia pia.
James akatimiza azma yake.
Hatimaye, sasa aliyangoja majibu.
Baada ya majuma mawili. Mume na mke wakarejea nyumbani baada ya kuwa wametumbua mamilioni kadhaa katika hoteli ya kifahari ya nyota tano. Sheraton.
Walipotua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu nyerere, walikuwa mume na mke halali kabisa.
Likafuatia fungate la nyumbani, James akatulia na Emmy kwa siku kumi kabla ya kuanza shughuli zake.
Katika siku hizi kumi, Emmy akaongeza baraka katika familia. Emmy alikuwa mjamzito.
Habari hii ilipokelewa na James katika namna ya kustaajabu, hakutegemea kabisa kupokea taarifa hii mapema kiasi kile.
Hakuweza kumueleza mtu yeyote ni kwa jinsi gani ameipokea taarifa ile. Lakini alielewa kuwa ilikuwa nzito na ya kushangaza.
Zawadi ya kipekee kwa wakati muafaka.
Mwisho wa Emmy kutumia SHABU,na NDIMU.
****
Mazoea hujenga tabia. Na tabia kuibadilisha hasahasa kwa mtu mzima ni jambo gumu sana.
Wanasema samaki mkunje angali mbichi, ukimngoja akauke atavunjika ukithubutu kumkunja.
Ilikuwa hivi kwa huyu kijana ambaye mazoea yake ya kupenda kujua mengi tangu utotoni yaligeuka kuwa tabia yake ya ukubwani.
Hakujali kama alivunjwa mguu katika ajali ya pikipiki huku taya nazo zikipisha na sasa alikuwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kwa matibabu baada ya hospitali za jijini Mwanza kushindwa kumuhudumia ipasavyo.
Akiwa katika kufanya mazoezi ya mguu wake ambao ndio ulikuwa ndio kwanza umetolewa bandeji gumu, maarufu kama P.O.P. Jose B wa ukweli anakutana na jambo ambalo linakuwa kama ndoto.
Akajiuliza kama anaota kile kipindi alichokiona katika luninga kikionyesha ndoa ya kifahari ama anakiona kweli kikiendelea.
Aliyapikicha macho yake lakini alipoyaacha wazi bado aliziona zile sura ambazo aliziona katika luninga zikitabasamu.
James na mkewe. Ni siku ambayo walikuja kupima mimba na ikagundulika mwanadada yu mjamzito....Jose B anawaona.
Ushakunaku ukampanda kichwani, akajikongoja na magongo yake ili aweze kupata mawili matatu yasiyomuhusu, aliwaza juu ya kizuizi, akahisi bado kuna nafasi ya kumpatia shilingi mbili tatu.
Jose B waukweli akajisogeza kwa tabu hadi akalikaribia eneo walilokuwa James na mkewe, wakiwa na daktari, wote walikuwa na furaha.
Baada ya mazungumzo James aliagana na daktari na mke wake kisha akatoweka.
Hiyo ikawa nafasi ya kipekee iliyokuwa inasubiriwa na Jose B waukweli.
Kutoweka kwa James kukamfanya abakie na sura ngeni zisizomtambua.
Shida yake ikawa juu ya yule msichana mrembo ambaye alimuona katika luninga akilishana keki kwa kutumia midomo na bwana james.
Jose B akaupima mguu wake akahisi una masalia ya nguvu za kutembea japo kwa kuchechemea kidogo.
Akajikongoja hadi nje akiwa kama anayefanya mazoezi.
Baada ya dakika kadhaa yule mwanamke akafika akaangaza huku na kule akamuita dereva taksi, Jose B naye akafanya vilevile.
Mfukoni alikuwa na akiba kiasi fulani ya pesa.
Hakuwa mwenyeji sana wa jiji la Dar es salaam, alimuagiza dereva kufuata taksi iliyoanza kuondoka.
Jose B akaanza kumfuatilia mke wa James.
Emmy John.
Ilikuwa siku ya mapumziko hapakuwa na foleni kubwa barabarani. Safari ikaishia katika mitaa ambayo ilikuwa na watu wengi wakijishughulisha na biashara ndogondogo.
UBUNGO TERMINAL Jose B aliyasoma maandishi makubwa, kisha moyoni akajisemea. Kumbe hapa ndio Ubungo.
Hivi nilipotoka panaitwaje vile? alimuuliza dereva huku akijiandaa kumlipa.
Muhimbili hospitali.
Emmy aliposhuka na yeye akashuka baada ya kulipa akaanza kumfuatilia. Alijikaza asichechemee sana lakini alilazimika kuchechemea.
Kuna wakati alijiuliza anafuatilia ili iweje lakini tabia kamwe haibadiliki kirahisi, akajiona yupo sawa tu.
Emmy mbele, Jose B mbele.
Wasiwasi ulioonyeshwa na Emmy wakati akitembea ulizidi kumvutia kijana huyu wa Mwanza.
Hatimaye wakafikia mahali pakiwa na nyumba ya kulala wageni yenye hadhi ya uswazi. Jose B akaduwaa, hakuamini malaika kama Emmy anaweza kuwa anaenda kukutana na mtu katika nyumba ile isiyokuwa na hadhi ya kumuhifadhi malaika kama yeye.
Akiwa bado anatafakari, alimuona mwanamama yule akifanya mawasiliano katika simu na baada ya dakika kadhaa kikajitokeza kipande cha mtu kikiwa na misuli iliyokakamaa na mwili wa mazoezi ambao haujatepeta.
Jicho la Jose B likakumbwa na sintofahamu.
Umbea wake ukamuwasha zaidi, akatamani kujua zaidi kinachoendelea.
Hakujali kama ametoroka hospitali ama la. Alijiona yupo sawa kabisa.
Roho wa kiherehere alikuwa amemteka na kumpelekesha atakavyo.
Kipande cha mtu kikamkumbatia Emmy, binti akaona aibu lakini hakuwa na budi akapokea lile kumbatizi mwanana.
Jose B akakumbwa na wivu asiojua ni wapi umetokea.
Akatamani kupiga kelele, lakini hazikuwa na tija. Akajikausha.
Wawili wale wakakokotana hadi chumbani. Jose B akachungulia kwa mbali.
Ule uzuri wa gesti bubu ukawa faida kwa Jose B.
Chumba namba 18!!
Jose B akaweza kukisoma kile chumba walichoingia wawili hawa.
Lazima nijue kunani humo ndani haiwezekani yanipite. Jose B akajiapiza huku akikumbwa na hasira kana kwamba yanamuhusu ama ni mkewe ameingizwa humo ndani.
Uswazi ni uswazi tu. Upande wa nyuma wa ile nyumba ya kulala wageni ilikuwa ni chochoro ya kupita watu.
Jose B akashtukia huo mchezo.
Huku akichechemea akaanza kupiga mahesabu ya kupata udaku.
Laiti kama angekuwa mwandishi wa habari hizo. Basi angekuwa maarufu sana.
******************************************
****JOSE B waukweli kutoka MWANZA mpaka DAR anasafiri na USHAKUNAKU......je atayaweza ya jijini???
***Kipande cha mtu kinaingia guest bubu na mke wa mtu....kulikoni EMMY???
***JAMES amemjaza mimba EMMY mapema kuliko kawaida.....kuna usalama hapa...
**MAMU hajajitokeza katika simulizi......je huyu ni nani???
ITAENDELEA