FAILI NAMBA 25
MWANDISHI:ROBIN MIHO
**********06*************
Remo aliondoka nyumbani kwa waziri Aidman kwa hasira,akajipakia katika gari yake na kutaka arejeshwe hotelini.
"Sikajula" hatimaye akaita baada ya mwendo wa takribani dakika kumi hivi.
"naam bosi"
"eti ukiwa na rafiki yako ukamsainia fomu ya kwenda chuo kikuu baada ya kushindwa kufika siku ya kusaini kutokana na kuumwa,ukamsamehe baada ya kumfumania akiwa na mchumba wako kitandani kwako"
"ukamlipia ada ya miaka miwili chuoni,ukampatia msaada wa hali na mali akaupata ubunge,ukatumia nafasi yako kama mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wa madini hapa nchini kutoa ushawishi kwa serikali kupendekeza rafiki yako ateuliwe kuwa waziri wa madini,hala......."
Remo alisita na kumtazama dereva wake,akatabasamu baada ya kuona akiwa kapunguza mwendoi na kutega sikio kwa umakini kuhakikisha hakuna neno linalompita,baada ya kuridhika kuwa alikuwa anasikilizwa kwa umakini aliouhitaji akaendelea.
"halafu rafiki yako huyo akiwa kama waziri wa madini,unakwenda kwake,unamwambia bwana tafadhali nahitaji kampuni ya mr.Kamuhanda ishinde zabuni ya uchimbaji dhahabu katika kitalu namba 135,endapo hilo litatokea nitajipatia hisa za kampuni hii kwa 30%" akasita na kulegeza tai yake.
"halafu rafiki yako huyo anakataa anasema anatetea maslahi ya nchi hii,maslahi ya wananchi,anataka kusimamia haki! Haki katika nchi hii,haki Katika nchi hii? Aaaaargh!" alibamiza dashbodi ya gari kwa hasira.
"eti Sikajula utamfanya nini rafiki yako huyu?" aliuliza na kumkazia macho Sikajula.
"nchi hii haina haki,atastahili kulipa kwa mazuri yote aliyoyapokea,siyo kweli kwamba hakuwa anafahamu kwanini umemsaidia hadi kuwa waziri wa madini,anajua!" alimalizia Sikajula.
Remo aliachia tabasamu la furaha akipiga makofi,aligeuka kuwatazama walinzi wake ambao nao walitikisa vichwa vyao kuonyesha kukubaliana na kauli ile.
"anastahili kulipa na atalipa",alizungumza Remo na kujiegesha kitini akazama katika tafakuri nzito.
*********
Hatimaye zilisalia siku mbili kabla ya mchakato wa uchaguzi wa mzabuni atakayepewa tenda ya kuuendesha mgodi mpya ulio kitalu namba 135.
likuwa katika sebule ileile na kama ilivyo ada Kamuhanda alikuwa amekaa katika kochi la pekee lililomuwezesha kuwatazama washiriki wa kikao hiki kwa ufasaha kabisa pasi na hitaji la kigeuza shingo.
"natumaini katika kikao hiki kila mmoja amekwishakutekeleza majukumu yake ipasavyo,nadhani ni wakati wa kujipongeza,nimekwishakuandaa mvivyo kwa ajili yenu hahahaha" alizungumza Dominc Kamuhanda na kuangua kicheko.
"hapana mkuu" alizungumza Makamu wa raisi Sospeter Nchunga.
"waziri mkuu,rafiki yangu,mlengwa wetu amenikataa kukubaliana na suala hili,nimetumia kila ushawishi lakini amegoma,amekataa katakata"
"amekataa fedha" alisema Dominic na kuachia tabsamu.
"Good na bwana Aidman"akauliza tena.
"samahani mkuu,nimej.........."
"Good bwana Remo,rafiki yako amekataa fedha,amekukataa rafiki yake" alisema Dominic.
"zimesalia siku mbili pekee na hatuna chaguo lingine zaidi ya kuondoa visiki ili barabara ipitike" alisema Dominic.
"ni lazima wafe,hili niachieni mimi,katibu mkuu chama cha ukombozi,inno na makamu wa raisi Sospeter nadhani mnafahamu wazi kilichopp mbele yetu na nini kinahitaji kufanyika"alimalizia Dominic.
***********
Siku moja kabla ya kikao cha maamuzi ya mwisho ya uchaguzi wa mzabuni stahiki anayestahili kupewa zabini ya uchimbaji madini katka kitalu namba 135.
Vifo vya kutatanisha vya waziri mkuu Aloycius Mshana na waziri wa madini Aidman Mkunja,kesi yao ilikuwa ni nyepesi sana,walikufa kwa ajali ya gari.
Gari ya waziri wa madini Aidman Mkunja ikiwa imempakia pia waziri mkuu Aloycius Mshana iliacha njia na kugonga nyumba hatua chache toka chuo cha mipango IRDP,Dodoma,
Habari iliishia hapo,ilielezwa kuwa waziri Aidman pamoja na waziri mkuu waliwataka walinzi na madereva wao kuwasubiri hotelini hapo,Arican dream hotel.Mlimwa hill area D.
Ikiwa ni siku moja tu kabla ya kikao cha mwisho cha kamati kutolea maamuzi kuhusiana na sakata la kitalu namba 135 na mzabuni yupi alistahili kupewa hasa zabuni hii ya uchimbaji wa madini katika kitalu hiki,
Ugunduzi wa uwepo wa mamilioni ya tani za dhahabu hakika uliziumiza kichwa kampuni mbalimnali za kigeni,mchujo mkali ulipitishwa baada ya uwepo wa maombi ya zabuni zaidi ya thelathini, hatimaye zikasalia kampuni mbili pekee.
Kampuni ya mzawa,Dominic Kamuhanda (KMCL) hii ni kampuni changa lakini ikiwa na historia ya kuvutia katika uchimbaji wa dhahabu nchini,ufanisi wa kampuni hii ulimjengea jina bwana Kamuhanda kiasi cha kuweza kuzipiga kikumbo kampuni za kigeni na ilibakiza hatua chache tu kushinda zabuni hii muhimu.
Dominic kwa mgongo wa uzawa kwa makusudi aliweka masharti ambayo yatamwezesha kupata mianya mingi ya kutorosha madini na kukwepa kodi.
sharti jingine ambalo waziri mkuu na waziri wa madini walilipinga wazi wazi lilikuwa ni msamaha wa kodi kwa miaka mitano ya mwanzo.
George Town Mining Company,kampuni ya wabelgiji yenye makao makuu katika mji wa mkuu wa Malaysia,George town,ni kampuni maarufu ya uchimbaji dhahabu na mafuta,iliendesha shughuli zake katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo,Malaysia,Canada,Afrika ya kusini,Zimbabwe na jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
GTMC iliweka masharti mepesi na yenye manufaa kwa pande zote,hili ndilo lililowaunganisha waziri mkuu na waziri wa madini kuiunga mkono kampuni hii,hivyo kwa pamoja waliazimia kumpatia zabuni hii mgeni dhidi ya mzawa KMCL.
Kutokana na kifo cha waziri wa madini,Aidman Mkunja na Waziri mkuu Aloycius Mshana,mchakato wa utoaji wa zabuni ililazimu usitishwe kwa muda kupisha taratibu za uteuzi wa mawaziri kujaza nafasi zilizoachwa na viongozi hawa.
Miezi minne baadaye ilimkuta Mbunge wa Geita Ipini Mwaijande akiwa amekalia kiti cha waziri mkuu na mkuu wa wilaya ya Geita,mheshimiwa Baraka Kipingu akiwa amekalia kiti cha waziri wa madini.
Fedha ilifanya kazi,kitalu namba 135 kilikuwa chini ya KMCL,hisa asilimia thelathini zilikuwa mikononi mwa Remo Kyaruzi.
**************************
KUMEKUCHA! HII SIO YA KUIKOSA TUKUTANE SEHEMU YA SABA...