Hadithi kali Faili namba 25

Yani bora mtu uchungulie page ya mwisho then ndo kuanza kusoma. Leken kwa mtindo huu waandishi watalalama sana kutafuta LIKES
 
FAILI NAMBA 25

MWANDISHI:ROBIN MIHO

*************05*************


JULAI, 13, 2016. KIMARA, DAR ES SALAM.

Magari mawili aina ya Range rover discover ya rangi nyeupe na moja yenye rangi nyeusi yaliongozana kuingia katika geti la jumba kubwa la kifahari la mfanyabiashara maarufu wa mafuta na madini, Dominic Kamuhanda.

Baada ya gari hizo kusimama, alishuka mfanyabiashara wa madini Remo Kyaruzi, aliongzna na dereva wake aliyemuamini sana John Sikajula, walinzi wake binafsi, Issack Sembuyagi na Yusuph Kamkaze.

Gari ya pili yenye rangi nyeusi alishuka mkuu wa wilaya ya Geita, Baraka Kipingu, alikuwa pamoja na dereva wake, Ismail Haji.

Walinzi wa kasri hii hawakuwa nyuma kwani waliwalaki na kuwaongoza kuelekea katika mlango wa kuingilia ndani ya jengo kubwa la ghorofa moja lililokuwa mita chache toka lilipo kanisa Katoliki usharika wa King'ong'o.

Waliivuka sebule na kupandisha ngazi zilizowafikisha katika korido fupi, walinyoosha moja kwa moja wakiipita milango kadhaa hadi walipoufikia mlango mkubwa uliokuwa mwisho kabisa wa korido,

Dc Baraka kipingu na Remo kyaruzi wakaingia na kuwaacha walinzi wao wakipelekwa sehemu ya mapumziko.

Kuongezeka kwa watu hawa wawili katika chumba hiki kilichotawaliwa na samani za bei mbaya ulifanya idadi ya watu kuwa sita.

Mkuu wa wilaya ya Geita, Baraka kipingu, mfanabiashara maarufu wa madini ya dhahabu, Remo Kyaruzi, katibu mkuu wa chama cha Ukombozi (CCU) ambacho ndicho chama tawala,Innocent Kijazi, Mbunge wa Kondoa, Ipini Mwaijande, makamu wa Raisi, Sospeter Nchunga na Bwana Dominic Kamuhanda.

Wote walikaa katika makochi yaliyoizunguka meza fupi ya vioo, mwisho wa meza hii kulikua na kochi la mtu mmoja, alikaa bwana Dominic Kamuhanda.

"jamani napenda kuwakaribisha tena, ninashukuru na nimefurahi kuwaona tena mahali hapa"alisita akanywa funda la mvinyo uliokuwa pale mezani.

"wote mnafahamu ni kiasi gani nimekuwa nikiwaunga mkono kwa ajili ya maendeleo ya nchi hii, wote mnalijua hili right!..nimekuwa mwema kwenu marafiki zangu, nimetoa fedha nyingi kudhamini kampeni zenu, nimetumia fedha nyingi kudhamini teuzi zenu piaaa.... " akasita.

"mnafahamu ni juhudi kiasi gani nimewekeza ili kukipata kitalu namba 135 ambacho tangu kigunduliwe kuwa na hifadhi kubwa ya madini ya dhahabu hadi leo hii... Dakika hii bado kampuni yangu haijafanikiwa kupata zabuni za kuendesha uchimbaji katika ktalu hiki kipya"

"kibaya zaidi kampui yangu inakaribia kushindwa na kampuni ya magabachori wakoloni George Town Mining Company, kampuni ya wabelgiji, magabachori aaaaaargh" alimalizia kwa kupiga ngumi kochi.

"wapi mnakwama? Tatizo liko wapi? " aliuliza huku akiwatupia macho kwa zamu.

"tatizo lipo, sio tatizo bali mattizo"alizungumza Makamu wa raisi Sospeter Nchunga

"tatizo ni Waziri Mkuu Aloycius Mshana"

"Aaaaaloycius Mshana... Aloycius Mshana" Dominic Kamuhanda alirudia kuita jina la waziri mkuu huku akijiegesha kochini kivivu.

"Ndio akiwa pamoja na waziri wa madini mheshimiwa Aidman Mkunja wanapinga kwa nguvu zote pendekezo la kumpa kitalu namba 135 mzawa KMCL (Kamuhanda Mining Company Limited) hoja zao za msingi ni Uzoefu, masharti ya mkataba na mtaji"

"ni kweli kampuni yangu haina uzoefu na hii si hoja ya msingi, masharti ya mkataba yana nini? "

Mheshimiwa Sospeter Nchunga akalitwaa brifcase lake, akachakura kwa sekunde kadhaa, akaibuka na na nakala ya Maombi ya zabuni ya KMCL.

"kutokuwapo kwa ulinzi wa vyombo vya serikali, kupakia madini kwenda nje ya nchi kupitia uwanja binafsi, msamaha wa kodi kwa miaka mitano ya awali na sharti la mwisho ambalo mheshimiwa waziri Aidman Mkunja anapinga vikali ni kupunguzwa kwa asilimia ya gawio kutoka asilimia hamsni ya sasa mpaka asilimia thelathini na nane" alimaliza na kuvua miwani.

"swezi kukubaliana na hili, ni lazima kampuni yangu ipate zabuni hiyo ni lazimaa" aliongea Kamuhanda kwa hasira.

"Aloycius Mshana na Aidman Mkunja ni lazima mzungumze nao" alisema Kamuhanda,

"Sospeter Nchunga ni lazima uzungumze na waziri wako kwa namna yoyote ile hata akitaka hii nyumba yote nitampa nachohitaji Aloycius Mshana abadili msimamo wake"

"Aidman Mkunja.... " akamgeukia Kyaruzi.

"Kyaruzi nasikia Aidman ni rafiki yako sana, zungumza nae"

"nawakumbusha ni wiki moja tu imebaki kufanyika kwa mjadala wa mwisho kuelekea uteuzi wa zabuni" baada ya kauli hii Kamuhanda akainuka na kuelekea mlangoni akafungua na kuondoka.

Ukimya wa zaidi ya dakika tatu ulichukua nafasi katika chumba hiki, hatimaye ukazuka mjadala wa zaidi ya masaa mawili kabla hawajafikia muafaka na kuanza kuondoka mmoja baada ya mwingine.

Kwa upande wa Remo Kyaruzi alindoka huku kichwa kikimuwaka moto, kumshawishi Aidman Mkunja kuunga mkono suala la kuipa zabuni kampuni ya Kamuhanda.

Alimfahamu vizuri rafii yake huyu, alikuwa na misimamo mikali na haikuwa rahisi kubadili msimamo wa bwana huyu aliyependa kuitwa Msemakweli kutokana na tabia yake ya kusimamia haki na ukweli.

Tabia ya bwana Aidman ilipelekea mara kadhaa kuingia katika migogoro na wanasiasa wenzie waliokuwawakijaribu kutetea maslahi yao binafsi.

Vitisho vya hapa na pale vilikuwa sehemu mojawapo ya maisha ya bwana huyu, lakini hilo halikumrudisha nyuma.

"Sasa mimi nitakuwa nani? Kuweza kubadili msimamo wa Aidman juu ya sakata hili? Anyway nitajaribu"

"bosi kuna tatizo? Mbona unaongea peke yako" kamkaze ambaye alikuwa mlinzi na mtu wa karibu sana na bosi wake alimuuliza baada ya kuona bosi wake akizungumza peke yake.

Remo akatabasam kwa karaha baada ya kubaini ya kwamba mawazo yalitaka kumtia wazimu, akaitupia macho saa ya gari tayari ilishatimu saa moja ya usiku.

Akaitoa simu yake, akalitafuta jina la mr. Msemakweli akapiga na kuiweka simu sikioni.

"haloo" sauti ya uchamfu ya Aidma Mkunja ilisikika.

"haloo bwana msemakweli"

"msemakweli siku zote mpenzi wa mungu" kilifuatia kicheko kifupi.

"upo wapi bwana" aliuliza Remo.

"nipo vasco pub habari za Mwanza?"

"Mwanza wazima japo nipo hapahapa dar bwana"

"imekuaje tena swahiba unakuja mwanza bila hata taarifa kweli"

"si ndio nakutarifu lakini swahiba"

" hahaha sawa bwana karibu tupate kinywaji hapa Vasco pub"

"ninakuja bwana lakini nikukute kwako nina mazungumzo wewe bwana msemakweli"

"karibu sana bwana Remo utankuta bwana" alijibu Aidman huku akiinuka kuelekea kwake, ni mwendo wa dakika tano ungemfikisha nyumbani kwake nyuma ya kanisa la pugu kajiungeni.

Mbali na kuwa waziri wa madini Aidman Mkunja alipendelea kutembea maeneo ya jirani bila ya kuwa na walinzi wake.

"Sikajula pita Pugu kjiungeni kwa bwana Aidman" alisema Remo.

Uzoefu wa njia za mkato ulikuwa msaada mkubwa kwa Sikajula, hatimaye wakaingia mandela road, dakika arobaini ziliwakuta wakiwa getini kwa bwana Aidman.

Baada ya salamu za hapa ma pale kwa familia ya bwana Aidman, sasa wawili hawa walikuwa wameketi bustanini.

"muuza dhahabu umekuja na jipya gani leo maana huishiwagi maneno"alianzisha mazungumzo Aidman.

. "Aidman ni kuhusu KMCL"alijibu Remo huku akimkazia macho.

"KMCL hawa wanaotaka kuleta wizi na utapeli, huu ni moja ya uozo unaonuka na kuchukiza, wanataka kuiingiza nchi katika hasara, wabebe madini yetu wakauzie nje, wasafirishe madini kwa kupitia private airport, uozo! Uozo!"alilalamakwa hisia Aidman

"na hawatofanikiwa naapa tayari tumekwishakuama kuachana na hii kampuni inayojiita ya mzawa, mzawa kitu gani mbele ya maslahi ya nchi hi? "

"tafadhali nisikilize Aid" Remo alimkatiza waziri wa madini Aidman Mkunja.

"ni kwamba KMCL inamilikiwa na Kamhanda pamoja na mimi hivy..... "

"Niipitishe KMCL" alimalizia Idman na kuangua kicheko.

"Remo wewe ni swahiba wangu lakini tangu lini tumeanza mazoea kama haya ya kuelekezana majukumu,KMCL hata ingelikuwa ya baba yangu mzazi bado nisingelikubali kuiacha ikihodhi rasilimali za nchi kwa maslahi ya upande mmoja"alijibu Aidman akionekna kukerwa na bwana Remo.

"hahahaha nafahamu bwana Aid nafahamu sana bwana kwamba hata ingelikuwa ya baba yako bado usingelikubali, lakini katika hili tafadhali bwana nisaidie swahiba wako" aliongea Remo kwa kwa msisitizo.

"kwa huko unakoelekea bwana Remo tutazika hata urafiki wetu tafadhali kywa muelewa" aliongea kwa sauti ya upole Aidman

"kumbuka hadi hapa ulipo Aid ni wazi bila msaada wangu usingekuwa hapa, nimejitoa sana kwa hali na mali kugharamia juhudi za kisiasa, leo hii ni waziri wa madini, minister of minarals of the united republic of Tanzania tafadhali nisitiri swahiba wako"

"natambua mchango wako bwana lakini ktika hili nitakuwa dhidi yako hadi mwisho, marfiki hawawezi kubaliana katika kila jamo Remo"

"Endapo KMCL itapata zabuni hisa asilimia thelathini zitakuwa zangu, nimanzia mbali sana kuwashawishi wanaumoja wa wafanyabiashara wa madini kuiunga mkono KMCL leo hii nakuja kukwamishwa na rafiki yangu mwenye" alizungumza kwa maskitiko.

"samahani" alijibu Aidman bila kumtazama Remo.

kwa hasira Remo aliinuka na kukisukuma kiti alichokalia, kisha akamtazama rafiki yake kwa sekunde kadhaa.

"misimamo yako ipo siku itakuja kukupoteza katika uso wa sayari hii na kuiacha familia hii unayojivunia" alizungumza na kuondoka.
*******************************
KITALU KIPYA NAMBA 135 KIMEZUA KIZAA ZAA, TUKUTANE KESHO
 
Miguu ya Kuku mwambie jamaa aisogeze angalau tufike kwenye chapter ya 16 halafu ndio aanze kudai mkwanja.Mbona hii story ndio kwanza tu imeanza?
 
NAOMBA RADHI RATIBA ZILIINGIKIANA NAAHIDI KESHO TUTAKUWA PAMOJA, MNIWIE RADHI SANA NDUGU ZANGU.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom