Hadithi kali Faili namba 25

skfull

skfull

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2013
Messages
2,550
Points
2,000
skfull

skfull

JF-Expert Member
Joined Dec 24, 2013
2,550 2,000
Mkuu unatupa vipande vidogo mno halafu ratiba yenyewe haieleweki,, kiukweli story hii ni nzuri ila umfumo unaotumika kuifikisha kwa wasomaji unachosha sana mkuu kiasi cha wakati mwingine kutamani kuachana nayo
 
Miguu ya kuku

Miguu ya kuku

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2019
Messages
524
Points
1,000
Miguu ya kuku

Miguu ya kuku

JF-Expert Member
Joined Jun 18, 2019
524 1,000
Mkuu unatupa vipande vidogo mno halafu ratiba yenyewe haieleweki,, kiukweli story hii ni nzuri ila umfumo unaotumika kuifikisha kwa wasomaji unachosha sana mkuu kiasi cha wakati mwingine kutamani kuachana nayo
NAPENDA KUTANGULIZA SAMAHANI WAKUUKUNA CHANGAMOTO BINAFSI ZA KIMAISHA ZINANIKABILI,HALI YANGU KIAFYA SI NZURI KWA SASA,NIPATAPO MUDA HUJITAHIDI KUSONGA MBELE LAKINI CHANGAMOTO ZINANIKWAMISHA,NATAMANI KUWAPA KITU KIZURI SANA.
 
MR KUO

MR KUO

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2016
Messages
668
Points
1,000
MR KUO

MR KUO

JF-Expert Member
Joined Jan 8, 2016
668 1,000
NAPENDA KUTANGULIZA SAMAHANI WAKUUKUNA CHANGAMOTO BINAFSI ZA KIMAISHA ZINANIKABILI,HALI YANGU KIAFYA SI NZURI KWA SASA,NIPATAPO MUDA HUJITAHIDI KUSONGA MBELE LAKINI CHANGAMOTO ZINANIKWAMISHA,NATAMANI KUWAPA KITU KIZURI SANA.
Nyoosha maelezo mkuu unahitaji kuchangiwa??
 
skfull

skfull

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2013
Messages
2,550
Points
2,000
skfull

skfull

JF-Expert Member
Joined Dec 24, 2013
2,550 2,000
Pole sana mkuu mungu akusaidie utengemae kiafya mkuu
NAPENDA KUTANGULIZA SAMAHANI WAKUUKUNA CHANGAMOTO BINAFSI ZA KIMAISHA ZINANIKABILI,HALI YANGU KIAFYA SI NZURI KWA SASA,NIPATAPO MUDA HUJITAHIDI KUSONGA MBELE LAKINI CHANGAMOTO ZINANIKWAMISHA,NATAMANI KUWAPA KITU KIZURI SANA.
 
Miguu ya kuku

Miguu ya kuku

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2019
Messages
524
Points
1,000
Miguu ya kuku

Miguu ya kuku

JF-Expert Member
Joined Jun 18, 2019
524 1,000
Nyoosha maelezo mkuu unahitaji kuchangiwa??
Unaweza nisaidia pia mkuu,namba yangu ni 0677421378 tigo

Yeyote atakayeguswa kunisaidia anaweza nipata kwa namba hiyo.
 
Miguu ya kuku

Miguu ya kuku

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2019
Messages
524
Points
1,000
Miguu ya kuku

Miguu ya kuku

JF-Expert Member
Joined Jun 18, 2019
524 1,000
FAILI NAMBA 25.
MWANDISHI:ROBIN MIHO
************07**********
Kitendo cha kuliangusha taulo kilifuatiwa na teke kali lililotua moja kwa moja katika nyeti za Abdulkarem,Abdul akatoa mguno hafifu wa maumivu makali na moja kwa moja akapiga magoti bila kupenda,Fred akamrukia pale chini na kumtia roba kwa nguvu zake zote,alitambua hiyo ndiyo nafasi pekee kujikomboa.

Abdul alijaribu kuivua kabali ya ya Fred bila mafanikio hatimaye alilegea na kutulia tuli,macho akiyatoa kama mjusi aliyenaswa na mlango huku haja kubwa ikimtoka kifo cha aibu!.

Fred akaufuata mlango na kuufunga kwa ndani akaziendea nguo za Abdul na kuzivaa,alikuwa na bahati kwani zilimkaa vilivyo,akaitoa simu ya Abdulkarem kwa bahati nzuri haikuwa imefungwa kwa nenosiri,akaingiza tarakimu kadhaa na kuipachika sikioni.

"Halo Fred hapa"

"Namba ya nani tena,nilikuambia tumia namba ile pekee kunitafuta" sauti ya Cliff ililalama.

"Cliff nimetekwa na wale wakora,nusura niliwe kiboga nahitaji msaada wa haraka"

"Hey fred unasema umetekwa"

"Ndio fanyeni hima mje Cliff muda ni mali,majengo ya kiwanda cha nguo cha Ndindichi mbele ya godauni la buluu kuna nyumba yenye vigae vyekundu"

"Dakika sifuri" sauti ya Ckiff ilisikika.

Fred akakata simu na kuketi kitandani,woga na hamaki vilimjaa huku harufu kali ya kinyesi ikimghiribu vikali.

uvumilivu ulimwisha akaamua kwenda kukaa bafuni ,alishukuru kimoyomoyo wajenzi wa nyumba hii kukifanya chumba kile kuwa chenye kujitegemea choo na bafu.


Muungurumo wa gari ulimgutusha Fred,akatoka bafuni na kwenda dirishani,gari nyeusi aina ya Verrosa ilipaki pembeni ya godauni la buluu hatua chache toka ilipokuwa nyumba hii.

Protas akaonekana akitembea kuelekea ilipo ile verrosa alipoifikia akainama akionekana kuzungumza na dereva wa Verrosa.

Baada ya majibizano ya nusu dakika hivi,protas akazama mfukoni na kutoa simu akaipachika sikioni,sekunde sifuri simu ya Abdulkarem iliyokuwa mikononi mwa Fred ikaanza kuita,Fred akaitupia macho na kuona namba iliyoseviwa P.

"Aargh mambo yanaharibika sasa atakuwa yeye tu"

alisema Fred huku kijasho chepesi kikianza kumtoka,alichanganyikiwa haswa, ilikuwa ni takribani dakika 20 tu toka ampigie Cliff.

haja ndogo ilibisha hodi,akakimbilia maliwatoni ajabu haja haikutoka ilikata gafula,akaachia msonyo wa kukereka.


Gafla tabasamu hafifu likamtoka,akaikata simu iliyokuwa ikiendelea kuita na kwenda sehemu ya ujumbe mfupi wa maneno,akachapa ujumbe mfupi "tusisumbuane mbwa wewe" akautazama kwa sekunde chache kisha akautuma lakni uligoma.Akajaribu tena kwa kutumia laini nyingine ujumbe ukakubali,Fred akashusha pumzi na kujongea dirishani,alimuona Protas akiwa amekaa kwenye boneti ya Verrso huku akionekana kuandika andika katika simu yake.

Kuingia kwa ujumbe katika simu ya Abdulkarem kulimgutusha Fred,akaacha kumsanifu Protas na kuufungua ujumbe ule, bahati nzuri ulitoka kwa P,

"Kuna mgeni wako hapa,jamaa wa usalama " ,Fred akajibu "dakika 15 tu nakuja" ,Protas akaonekana akisogea upande wa dereva na kusemezana naye kidogo kisha akarudi kukaa katika boneti.
************************
Baada ya taarifa za kutekwa kwa kijana wa Cliff safari ya kwenda ilemela iibidi iishie pale gari ikageuzwa kurudi tulipotoka tayari ilishakuwa saa nane na dakika ishirini usiku.

Barabara ilikuwa nyeupe tulipishana na malori machache tu,hali hii ilikuwa msaada sana kwetu,gari ilitembea kwa kasi kwelikweli.

tulifika eneo yalipo majengo ya kiwanda mfu cha Ndindichi,tukaiacha barabara ya kuingilia kiwandani hapo na kwenda kusimama mita kadhaa mbele. Kando ya barabara ya Sirali-mbeya.

kila mtu akaitwaa bastola yake, tukaanza kurudi kwa mguu kuelekea lilipo geti la kuingilia.

Kiwanda hiki kilizingirwa na vichaka na nyasi,kikiwa na ukuta mkubwa na mrefu,kulikuwa na mageti mawili,upaande wa mbele na upande wa nyuma,hii iliwia vigumu kuona kinachoendelea ndani yake.

"Fred yupo humu,kuna nyumba yenye vigae vyekundu mbele ya godauni lenye rangi ya buluu" Clif alitoa maelekezo.


"Okay sasa mimi na clif tutaingilia hapa,Makusu wewe zunguka geti la upande wa mashariki" Harold alizunguza.


"Kumbuka ukiwa katika himaya ya maadui huruhusiwi kutulia jina asilia" aliongeza na kuikoki siraha yake.


Nikashika njia kuelekea upande wa masharikii lilipokuwa geti jingine,nikatoa tochi ndogo yenye mwanga hafifu na kuvipita vichaka na nyasi ndefu zilizoachwa bila kupunguzwa na kuharibu mandhali ya eneo hili.


Nililifikia geti kubwala rangi nyeusi iloanza kumezwa na wekundu wa kutu,eneo hili lilionesha uhai kwani palikuwa na njia iliyoonekana kutumika mara kwa mara.

nililisogelea geti na kubaini kuwa lilkuwa wazi na liliacha upenyo mkubwa katikati,nilichungulia katika uwazi na kuona ni nyumba moja pekee kuu kuu yenye vigae vyekundu iliyoonekana kuwa na umeme.

Majengo mengi chakavu yalitawaliwa na kiza totoro, isipokuwa godauni kubwa la buluu lililokuwa mbele ya nyumba ile.

simu yangu ilitoa mtetemo na uzuri ni kwamba haikuwa ikitoa mwanga nikaitwaa na kuiweka sikioni.

"Code E04 naongea" Cliff alisikika.
'Code E03 nipe ripoti"
"Godauni la buluu mbele ya nyumba yenye vigae"
"Naliona"
"Nyoosha moja kwa moja hadi katika godauni jeupe upande wa kushoto kila kitu kipo safi over"


Nikatembea kwa hadhari kulivuka geti,kiza kizito kilinisaidia kunificha,nikaambaa kuyavuka mapagale yaliyoonekana kuwa yalitumika kama nyumba za wafanyakazi.

nikiwa nimebakiza takribani hatua tano hivi nilisita baada ya kusikia sauti ya mtu akizungumza,nikanyata kwa tahadhari hadi nilipolifikia godauni jeupe lililopakana na godauni la buluu,nikasogelea kona ilikotokea sauti ile.

"Ndio bosi mmoja tayari aliyesalia muda mfupi ujao naye ataenda kuwasalimu babu zake"
Niliitambua vilivyo sauti hii alikuwa ni Cliff, toka ilipokuwa kona niliyojibanza hadi lilipokuwa lango la kuingilia katika godauni jeupe alipokuwa amesimama Cliff palikuwa na umbali wa hatua kumi hivi.

nilichokiona sikuamini kabisa macho yangu,nilimuona Harold Mnembuka akiwa kalala chini huku damu zikimtoka,alikuwa amepigwa risasi ya paji la uso.

wanaume wawili walifika eneo lile na kuzungumza harakaaraka na Cliff,kisha wakaubeba mwili wa Harold na kuuingiza katika godauni na kurudishia mlango.
"Tulia hivyo hivyo"
Sauti nzito ikifuatiwa na mguso wa kitu cha baridi kisogoni kwangu iliunguruma,kijasho chembàmba kikanitoka..!
*********************
TUKUTANE SEHEMU YA NANE HAPO KESHO.
 

Attachments:

Forum statistics

Threads 1,336,620
Members 512,670
Posts 32,545,449
Top