Hadithi kali Faili namba 25

S

Simon Mkirene

Senior Member
Joined
Jul 16, 2019
Messages
129
Points
250
S

Simon Mkirene

Senior Member
Joined Jul 16, 2019
129 250
Siraha = silaha
FAILI NAMBA 25

MWANDISHI:ROBIN MIHO
***********06************

Fred baada ya kutoka saluni alizunguka njia iliyokuwa nyuma ya kanisa na kurudi barabara kuu ya Kenyatta, Land cruiser Hardtop ilikuwa nyuma yake.

Akanyoosha yalipo majengo ya kiwanda cha Pepsi,akiwa anamalizia kuyapita majengo ya kiwanda ghafla,land cruiser ikampita kwa kasi na kuziba njia.

Kwa haraka wanaume wawili walishuka wakiwa wameelekeza bastola zao katika gari ya Fred huku wakitoa ishara ya kumwashiria kusimama.

Fred hakuwa na namna ujanja ulimuisha akasimama hatua tano toka walipokuwa wamesimama wanaume wale,kitendo cha kufumba na kufumbua alikuwa amezingirwa na vijana watano wakiwa na siraha za moto.

Kijasho kilimtoka haswa,jambo pekee alilolifanya ni kubonyeza kitufe chekundu katika dashibodi na kutulia huku akitetemeka kwa mbali,hakika Fred aikua amekwama haswa.

"shuka chini" Hassan Kuku aliyekuwa amesimama upande wa dereva aliamuru huku wakifungua milango iliyosalia na kuambulia patupu.


"yupo peke yake" Hassan kuku alizungumza huku akiwatazama mabwana wale waliosimama nyuma ya Landcruiser hardtop iliyomfuatilia Fred.


"mmechezewa shere Abdulkarem na Maliki,mmepotezwa" Hassan aliongea,Abdul na Maliki walitazamana.

"hata hivyo hatuna cha kupoteza,Fidelis na Gerald kagueni gari yao kisha pigeni kiberiti.Protas na Swalehe chukueni huo mzoga mtarajiwa tuondoke.

Abdulkarem,Maliki,Swalehe, Protas na Hassan kuku walijipakia katika Land cruiser ya kina Abdulkarem wakiwa na Fred.

Wakachukua uelekeo wa round about ya Sirali-mbeya,hadi wanaingia barabara ya B6 hakuna aliyekuwa amezungumza.

"mnanipeleka wapi" Fred aliuliza

"hapo tu sio mbali" alijibu Hasan Kuku,akamgeukia Fred.

"unadhani kwanini tunaelekea mafichoni kwetu huku hatujakuziba macho? Kwanini hakuna aliyekupiga wala kuongea na wewe?" Kuku aliuliza.

"hapana sijui"

"ni kwa sababu huwa hatuongei na mzoga,aendaye huku huwa harudi hahahaha" Hassan kuku alisema na kuangua kicheko cha kukereka

"hapana kaka tafadhali msiniue"

"naitwa Hassan kuku,utakufa kijana utakufa tu nakuambia,hakuna aliyejaribu kuingia katika mikono hii akatoka salama"

"tafadhali jamani mwenzenu mama anaumwa nipo hapa kwa ajili ya kutafuta pesa za matibabu ya mama yangu tu sina ubaya na mtu" Fred alizungumza huku machozi yakianza kumtoka.

"huna ubaya na mtu?"

"ndio sina ubaya na mtu"

"we fala nitakupasua domo lako hilo,huna ubaya na mtu na kwenye ile gari ulifikaje" Abdulkarem aliyekuwa nyuma ya usukani aliuliza kwa hasira.

"nilibadilishana na Cliff saluni,yeye na wenzie walichukua Gari yangu"

"ili mtupoteze sio? Halafu huna ubaya na mtu?? Hak'yamungu nazaa na wewe leo" Abdulkarem alisema.

"nisamehe brother"

Hakuna aliyejibu,gari iliyaacha makutano ya sirali-mbeya na kuchukukua barabara ya Sirali,dakika thelathini mbele walikuwa wakiingia katika magofu ya kiwanda cha NDICOL(Ndindichi Company Limited).

Walielekea katika nyumba pekee iliyokuwa katikati ya majengo chakavu ya kiwanda hiki cha nguo kilichojifia miaka mingi.

"huyu mzoga tukaufungie stoo" Swalehe aliuliza baada ya kuona wanaingia sebuleni wakiwa pamoja na Fred.

"Hapana mpelekeni bafuni akaoge" Abdulkarem alisema,Swalehe akatabasamu na kumtazama Fred.

"twen'zetu tukaoge kaka" akamshika mkono na kupotelea katika korido.

Abdulkarem,Hassan kuku na Protas walibaki sebuleni wakinywa pombe na kuvuta Cocaine,dakika kumi na ushee Swalehe alirejea akiwa na Fred aliijekuwa na taulo tu.

"kaa hapo Fred" Hassan kuku alimwambia Fred.

"unaitwa nani?"

"Fred Baltazar"

"Fred mama anaumwa?" Abdulkarem aliuliza.

"ndio mama anaumwa sana,anahitaji upasuaji kuziba tundu katika moyo"

"Good wewe ni polisi?"

"hapana mimi hufanya mishe mishe tu za mtaani dili za hapa na pale"

"hapa hapa mjini?"

"hapana,Dar es salaam hapa Mwanza niliitwa na Cliff na nafanya tu kila anachoniambia kukifanya naye hunilipa vizuri"

"Cliff ni nani?"

"Askari"

Abdulkarem na wenzake wakatazamana,

"anachunguza nini hasa?"

"kwa kweli sijui na huwa simuulizi zaidi ya kupokea maagizo tu"

Abdulkarem akaitwaa simu ya Fred iliyokuwa mezani na kuitazama kwa sekunde kadhaa.

"afande Cliford Ndimbo" akaita huku akiendelea kutazama majina katika simu ya Fred.

"okay nifuate" akainuka na kuelekea katika korido hadi katika mlango wa mwisho kulia,akafungua mlango na kumtaka Fred aingie.

"Hakuna kiumbe aliyeingia nyumba hii akatoka akiwa hai,wewe utatoka hai endapo tu hutakuwa na makuu" alizungumza Abdulkarem huku akivua nguo.

Akatwaa kichupa kidogo kilichoandikwa KY jelly,akamsogelea Fred na kufungua taulo aliyoivaa huku akimtazama kwa macho ya uchu,dakika chache zilizofuata miguno ya maumivu ilikuwa inasikika kwa mbali!
*************************
JE FRED ATAOLEWA?,KINA CLIFF WAKO WAPI? JE! KITUFE CHEKUNDU ALICHOKIBOFYA FRED KILIKUWA CHA NINI? TUKUTANE SEHEMU YA SABA.
 
skfull

skfull

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2013
Messages
2,547
Points
2,000
skfull

skfull

JF-Expert Member
Joined Dec 24, 2013
2,547 2,000
Mimi nashauri FAILI NAMBA 25 lifutwe rasimi maana limeshindwa kukidhi matakwa ya walaji nimegeuka kuwa teja aliekosa unga kila saa nachungulia kwa pusha kama mzigo umeingia lakini nakuta hola au begi limepotelea airport?
 
moneytalk

moneytalk

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2017
Messages
4,672
Points
2,000
moneytalk

moneytalk

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2017
4,672 2,000
Mimi nashauri FAILI NAMBA 25 lifutwe rasimi maana limeshindwa kukidhi matakwa ya walaji nimegeuka kuwa teja aliekosa unga kila saa nachungulia kwa pusha kama mzigo umeingia lakini nakuta hola au begi limepotelea airport?
 
Millie Mhb

Millie Mhb

Senior Member
Joined
Jun 29, 2016
Messages
147
Points
225
Millie Mhb

Millie Mhb

Senior Member
Joined Jun 29, 2016
147 225
Mimi nashauri FAILI NAMBA 25 lifutwe rasimi maana limeshindwa kukidhi matakwa ya walaji nimegeuka kuwa teja aliekosa unga kila saa nachungulia kwa pusha kama mzigo umeingia lakini nakuta hola au begi limepotelea airport?
Alsema hali yake kiafya sio nzuri jaman
Let's keep waiting!
 
Songa Heri

Songa Heri

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2016
Messages
1,712
Points
2,000
Songa Heri

Songa Heri

JF-Expert Member
Joined Feb 6, 2016
1,712 2,000
Faili namba 25 limegeuka kuwa faili namba bashite
 

Forum statistics

Threads 1,336,594
Members 512,670
Posts 32,544,694
Top