UTANGULIZI
Ni hadithi inayohusu kijiji kilichopo mkoa wa simiyu wilaya ya bariad ambacho kiko umbali wa takribani kilometa 12 za mlaba kutoka simiyu mjini, kama hili jina litakuwa geni kwako na hujawahi kuliskia kabisa basi ngoja nikufamishe kidogo.
Gamboshi ni kijiji kinachofahamika kwa uchawi nchi Tanzania kikifahamika ni makao makao makuu ya wachawi ukiachana na mkoa wa sumbawanga basi kwa lugha nyingine unaambiwa ni kitovu cha wachawi yani mizimu yote inapatikana huko, ndo kijiji pekee unaambiwa mchana giza usiku ulaya.
Julai mwaka 1999 serikali ilichukua maamuzi ya kukitenga kijiji hicho baada ya vifo vya zaidi ya watu hamsini [50] vilivoketea ndani ya siku moja ikiaminika ilikuwa na uhusiano na mambo ya kishirikina basi watu waliambiwa kuhamaka makazi na kutafuta sehemu zingine za kuishi.
Kwa muda wa takribani miaka ishirini [20] hamna ambae amekuwa na taarifa zozote kuhusu eneo hilo basi ndo mda serikali kutoka kwenye ofisi ya rais, ilitumwa barua kwa mkuu wa mkoa wa simiyu barau ya agizo la kukifungua kijiji hicho kwa upya ikiwezekana atume maaskari mara moja na kufunguliwe kituo kidogo cha polisi nae mkuu wa mkoa wa simiyu alitii maagizo yaliyo kuwa yametoka kwa rais na kuitisha kikao cha maaskari wa jeshi la polisi, kutoka wilaya zote za simiyu.
Mkuu wa mkoa kwa kutambua kuwa askari wengi wangekuwa na uonga wa kufanya kazi kijiji kule lakini bado ilikuwa inamlazimu kuchagua sababu pia alikuwa na mamlaka ya kufanya hivyo, basi alifanya maamuzi na kumchagua Mwita Choma na Baraka Kulwa kama maaskari teule kwenda kijijini gamboshi.
Lakini bila kufaham wamejiigiza kwenye shida kubwa nao walikuba kazi ile kwa mikono yote.
SEHEMU YA KWANZA
Tarehe 13 mwezi wa sita mwaka 2019 saa kumi na mbili afajiri [06:00am] akiwa amelala kwake kengele ya mezani [ Alarm] ilikuwa ikipiga kelele kumanisha mda wa kuamka umefika nae taratibu akijinyoosha kutoa uchovu wa usiku, akamudu kufungua macho huku akiwa anatazama aliona mtu akija ghafla kurukia kitandani kama kwa kishindo alishutka sana maana alikuwa na wenge la usingizi lakini hakuwa mwingine bali mke wake Mwita choma
“Habari za asubuhi, mme wangu”. alikuwa ni mke wake mwita akitoa salam huku akilukia kwa kitanda alipo mume wake
“ unajua umenishutua” mwita alimuliza mke na kueka kituo bila kujibu salam yake
“ kumbe umeogopa, basi pole mume wangu”anaomba radhi huku sura yake ikiwa inatabasamu kama anataka kucheka .
“ Umeamkaje kipenzi changu” bado aliuzua huku sura yake ikiwa na tabasamu lilelile
“ salama tu mke wangu.” alijibu salam ya mke wake akaambatanisha na swali,
“mbona umeamka mapema sana leo”
“ kuna kitu konki nimekuandalia kabla ya hujaondoka” alimjibu swali la mume akimtazama kwa ukalibu
“Aah konki” mwita alianza kumtenkenya mke wake huku akirudia neno “konki”
Konki! konk, konki! konki! Mwita aliendelea kumtenkenya huku mke wake akicheka na kumwomba aache anahisi atajikojolea!
Mwita aliacha huku mke wake akiwa ameweka sura ya kununua nae alijirudi na kumwambia
“ kumbe umeumia, basi pole mke wangu” huku sura yake ikiwa inatabasamu kama anataka kucheka
Wakiwa bado wapo kitandani mke wake hakujibu chochote bali alisogeza uso wake karibu na kushika kidevu cha mume wake na kumpiga busu la wakika, na kulikatisha haraka huku akishuka kitandani na kumwambia mume wake amfate bafuni. Nae Mwita alishuka kitandani haraka akiwa na boxer tu na kuelekea bafuni, basi huko kilikuwa ni kitendo cha kuendelea kudumisha ndoa yao ambayo imeishi kwa muda wa miaka mitano sasa wakiwa bado hawajafanikiwa kupata mtoto.
Mwita choma ni kijana wa miaka therathini [30] kabila mkulya urefu wake nin wastani, akiwa na miaka 25 alibahatika kupata mke aitwae ni Janeth. akiwa na miaka 27 aliteuliwa kuwa ofisa msimamizi wa kituo kidogo kilichopo wilaya ya bariadi mkoani simiyu alifanya kazi kwa waminifu huku sifa zikimndondokea kama kijana jasiri. Badaa ya kutumikia jeshi la polisi kwa kipindi wa muda mrefu akiwa ofisa msimamizi alipewa kazi ya kwenda kuwa mkuu wa kituo kijijini gamboshi kama ilivotoka kwa ofisi ya raisi kuwa wateuliewe askari wawili waende wakafanye kazi kijijini huko.
Na ndo ilikuwa siku yenyewe akiwa ameamka salama akiwa nyumbani kwake na mke wakiwa bafuni wanamlizia kuoga. Akiwa amejifunga taulo kiunoni alisikia sauti ya simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita aliishika na kuangalia jina lilikuwa ni rafiki yake Baraka kulwa alikuwa anapiga alikuwa amemsave [ Partern in crime] alipokea na kuongea nae
“Kaka, habari yako” ndo kitu cha kwanza aliskia alipo pokea simu ilikuwa ni salam kutoka kwa rafiki yake
“ salama kaka, kwema?”
“uko wapi”
alijibu salam huku akikaa kitandani. Akaongezea swali jingine
“Kwema! Niko nyumbani napata breakfast” baada ya kujibu swali mwita alicheka na kuuliza
“Haha haha”
“Hivi mdogo wangu huna mpango wa kuoa kabisa!”
“Maana kila siku ujipikie mwenyewe ufue kwa nini usioe?”
Aliuliza na kubaki kusubiri atasema nini
“Mimi ntaoa tu kaka ata usijali ni mipango tu”
“Sawa, wahi kituo sababu tutakuwa tunaondoka mapema si unalewa sehemu tunayoenda unaambiwa usiku ni ulaya” alikubali kisha kumpa taarifa nyingine
“Haha haha, sawa kaka” alicheka kidogo kwa taarifa mwita aliyompa kisha akakubali na kukata simu maongezi yakawa yameishia hapo
Mwita akaweka simu kitandani iliavae nguo za jeshi la polisi ambazo zilikuwa zinamkaa vizuri sana sababu pia ya mwili wake uliokuwa umekaa kimtindo wenye mpangilio na kwenda kupata chai ambayo mke alikuwa kamwandalia, alikuta janeth akiwa anamsubiri seblen akiwa tayari kashaweka chai mezan alikuwa kavaa kitenge tu.
“Karibu chai mme wangu” alimkaribisha chai mme wake kwa tabasamu nzuri kabisa huku akimtengenezea kiti aweze kuketi
“Ahsante mke wangu” alishukuru na kuketi kwenye kiti huku mke wake akiwa ubavu wake wa kushoto
Hakika kilikuwa chakula kitamu ambacho hata mwita alishambulia kama hana akili timamu
“wewe umeshakula mke wangu” aliuliza huku akiendelea kula
“ hapana babo ntakula baadae kidogo, saivi nataka nikae karibu na wewe” alimjibu mme wake na kuongezea shida yake kwa huo mda
Mwita alitambua kwa nini mke wake alisema maneno yale na alikuwa hana jinsi zaid ya kumfariji
“ usijali mama angu, mimi ni wako siku zote “ alimwambia maneno mazuri akiwa anambembeleza kwa kumshika shavu akitumia mkono wake wa kushoto
Janeth alisimama na kumwambia mme wake asuburi na kuelekea chumbani alipo rudi alikuwa na kiboski kidogo ambacho kilikuwa kimefungwa vizuri
“ Kwa ajili yako mme wangu” alimpatia kwa mikono miwili likiabatinishwa na taabasam kama ilivyo kawaida yake kutabasamu
“Ahsante mke wangu” mwita alifurahi alionesha kabisa kashukuru alisamama na kumpatia busu mke wake, alipo jaribu kufungua mke wake alikataa na kumwambia utaifungua baadae
“kuna nini kwani “ akaongezea na swali
“ utaona tu, lakini usikifungue hapa” alimwambia akiwa anamtazama machoni bila kupepesa
“ sawa” mwita alikubali lakini alibaki na maswali kutakuwa na nini kwenye boski maana kilikuwa kidogo sana chenye urefu wa 5 na upata wa 3
tayari kamaliza kupata chai alichukua begi lake la mgongoni lilokuwa mezani na kuelekea nje akiwa anatoka alimgeukia mke wake na kumwambia
“ usisahau kufunga milango mda wa kulala na ukiwa unatoka”
“ na ukiwa na shida yoyote nipigie mimi kwanza”akaongezea huku akiwa anafungua mlango
“sawa , mme wangu” alikubali huku akimtazama mme wake akielekea kupanda gari la jeshi la polisi aina ya toyota landa cruiser ikiwa inafahamika kama [ Defender ]
Mwita aliwasha injini ya gari na kushusha vioo huku mke wake akiwa bado anasubiri aondeke
“ kwaheri, ubaki salama” alimwaga akiwa anamtazama kwa mbali
“ sawa, safari njema mme wangu” alimjibu na kuingia ndani
Mwita alipandisha vioo na kuondoa gari kuelekea kituoni.