Hadithi: Gamboshi

Hadithi: Gamboshi

SEHEMU YA SITA
Ikiwa ni jioni ya jumatano ikiwa bado siku mbili watu washereke sikukuu ya kusafishwa lakini kwa muda mrefu toka mzee kunti kashika madaraka yote ya kijiji hicho hiyo sherehe aliifuta sababu yeye alikuwa anaamini ni sherehe ambayo watu huwa wanaotelewa kafara, ivyo aliagiza kila mwaka watu watakuwa wanatumia hiyo siku kukumbuka watu waliowapoteza lakini sio kusafishwa kama inayotakiwa. Siku iyo john alikuwa anataka kuongea na baba yake akiwa basi alielekea mpka alipokuwa baba yake ikiwa ni jengo kubwa kijijini likiwa linafamika kama [Luiku ya mizimu ] ikiwa inamaanisha makao makuu ya mizimu mida ya saa sita mchana alifika ndani ya jengo hilo akiwa kafalia nguo ndefu zana haina kama wanazo vaa mapadri alipofika alipiga goti na kumsalimia baba yake . Mzee kunti akiwa kakaa kwenye kitu cha mizimu pembene akiwa na washauri wake ambao walikuwa ni wazee wa miaka 70 na kuendelea
“Shikamoo baba” alitoa salama kwa baba yake akiwa kainamisha kichwa chini huku akiwa kapiga
“Maharaba” mzee kunti alijibu salama kwa kituo bila kutaka kujua mwanae ni nini kafata
“Nahitaji baraka zako kesho nisafishe watu” aliongea kinyenyekevuy huku kichwa kikiwa bado kakiinamisha
Mzee kunti alikaa kimya akiwa anawaza lipi ni jibu sahihi kwa kijana wake
“Hapana haiwezekani” Alijibu moja ya wazee washauri wa kunti
“Kunti mizimu ishapinga hicho na wewe kijana ujafika umri wa kusafisha watu” Mzee yule mshuari alienndelea kuongea
“Basi kakuelewa unaweza kwenda” mzee kunti alijibu huku akiwacha wazee wakimtaza kama wanasubiri aseme kitu
John alisimama na kutoa heshima kwa baba yake na kuondoka
“Kijana wako anahitaji kuadhibiwa” alikuwa sauti mzee mwingine mshauri wake
“Tunahitaji afikishe kwa mizimu aweze kuadhibiwa awezi kuja kwako kwa kujiamini kiasi hicho” mzee mwingine mshauri aliendelea kuongea
Lakini kunti alinyoosha kidole kimoja na washauri wake wote walikaa kimya na kumskiliza kunti anakipi cha kusema
“Naomba tutawanyike mpka saa moja jioni” aliongea hayo maneno kusimama kwenye kitu na kuondoka kwenye makau makuu ya mizimu
Aliacha washauri wake wote wakiwa wanamtazama wakijiuliza anashida gani?
Sababu ya mzee kunti kuacha kumjibu kitu chochote mwanae alijua mwanae anaweza kuongea vitu mbele ya wazee ambavyo angetaka wajue kinachoendelea,alijua na kutambua kwa nini mwanae alikuja kwa makao makuu ya mizimu na sio kumtafata faragha.
Mzee alipotea kwa siku iyo hamna aliejua ameenda wapi ,ikiwa mida ya jion saa kumi na moja john aliingia kwenye chumba alichokuwa analala mama na baba yake na kukuta kukiwa kimya ikimanisha hamna mtu yoyote alitembea mpka kwenye mlango wa chumba ambacho babu yake alikiita dhahabu
Sababu alijaribu kufungua lakini kilikuwa kimefungwa alitoa karatasi na kunuia maneno ambayo yalikuwa kwenye maandisha kisha mlango ulifunguka, hakuamini alingia hatua moja na kunuia maneno mengine tena mishumaa yote iliwaka kwenye jengo lile kukawa na mwanga mkali alitembea atua nyingine na akandelea kutembea alikuwa akitazama michoro tofauti tofauti iliyokuwa imechorwa ukutani kwa kutimia damu,alifika mpka sehemu husika aliona sahani lile likuwa linamaji mengi sana siku iyo tofauti siku ile lakini siku iyo alikuta hamna kuta zilizokuwa na vitabu kama siku ile aliangalia kwenye karatasi yake na kunuia maneno mengine tena ghafla kuta zilifunguka zikiwa zina namba mpka 10 alisogea mpka kwenye kuta ulioandikwa “3” alisamama pale na kunuia maneno mengine yaliyo kuwa kwenye karatasi ile palifunguka na kutoa kitabu alichukua na kuparudishia kwa kunuia maneno aliyonuia mara ya kwanza kabla haja funga kuta zote alisogea mpka ilipokuwa sahani lenye maji mengi alichukua kidumu kidogo alichokuwa amekuja nacho na kuchotaka maji yake lakini kipindi anachukua yale maji mkono wake uligusa bila yeye kujua madhara yake alipo maliza kujaza kidumu alifunika na kurudisha kwenye kimkoba kidogo ambacho pia alitumia kuweka kitabu alichochukua alinuia kwa mara nyingine tena kuta zote zilijifunga na alianza safari ya kuondoka pale kipind akiwa anamaliza kufunga mlango kwa kunuia mdogo wake wa anaefuata anaefamika kama katerina alikuja chumbani hapo akiwa anamtafuta mama yake lakini alimkuta kaka yake
“JOHN?”Alimwita kwa sauti kubwa
“Naam!” aligeuka huku akiwa tayari anaogopa kakamatwa
“Unafanya nini chumbani kwa mama” aliuliza swali akiwa anamsogelea
“Na huo mkoba umebeba nini”Aliongezea swali jingine
“Huu..” Alitahamaki huku akishika ndani
“kuna..” Alipo shika ndani ya mkoba alihisi kitu cha duwara alipotoa lilikuwa ni tunda la Tofaa[apple] yeye mwenyewe hakumbuki akiweka apple kwenye ule mkoba
“Kumbe umeleta apple alafu unataka kula peke yako” Alisogea karibu na kumpokonya lile apple na kung’ata kipande
John alibaki kazubaa haelewi tunda limetoka
“Naomba jingine” akiwa anakula aliomba tunda jingine
“Hapana ilo linakutosha” aliongea hivyo na kumpiga kikumbo na kutokomea akiwa bado anajiuliza apple limetoka wapi
“Mchoyoo!”alimwambia huku akishuhudia akiwa anaishiria
John aliekea mpka chumbani na kufunga milango akiwa bado anajiuliza aliweka ule mkoba kitandani na yeye akakaa kitandani mara ghafla alisikia mlango ukigongwa akauliza nani lakini hakujibu ukaendelea kugongwa alihisi kama balaa siku iyo aliweka ule mkoba uvunguni na kwenda kufungua mlango alikuta ni mdogo wake anjella
“Nimeambiwa una apple ziko wapi”
“Apple?” Akijiuliza mdogo wake alimsukuma kidogo na kuingia chumbani
“Ndio, katerina kanambia una apple nyingi kwenye mkoba”
“Sina apple na toka kwenye chumba changu” John aliongea huku akimwonesha mlango wa kutokea lakini ghafla apple liliseleleka kutoka mfunguni mwa kitanda
“Hili ni nini” Aliliokota na kunga’ta alipo maliza aliinama kutaka kujua kuna nini chini ya uvungu
Alipo inamana aliona mkoba na kufikisha mkono wake ndani alipo utoa tu john alitahamaki na kumshika nao lakini dada akuelewa kwa nini john kabadilika ghafla wakiwa wanapelekesha chupa ya plastiki yenye maji aliotoa kile chumba cha siri yalianguka, anjella alimwachia ule mkoba kaka yake kuokota yale maji bila kujua ni ya nini alifungua na kupiga pafu moja ndipo john alihisi kuchanganyikiwa bila kujua afanye nini alijikuta anampiga ngum, anjella alianguka na kuzilahi maji yalimwagika kabla hayaisha yote aliwahi na kukifunga kile kikopo na kuchukua mkoba haraka na kuondoka chumbani akimwacha mdogo yake akiwa hana fahamu
 
Mtanisamehe sehemu ya saba haiko tayari kwahiyo mpka jumatatu mtanisamehe wapendwa
 
Nimepata matatizo jamani lakini ntarudi na nyiny hivi karibuni
 
Naombeni radhi wapenzi wa gamboshi na ahid kuanzia jumatatu ijayo tutaendelea tulipo ishia mungu awabariki!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom