Hadithi: Bila Passport Mtoto Hataingia Nchini

Newbies

JF-Expert Member
Jul 13, 2018
1,477
2,148
FB_IMG_1578828550814.jpg

Alfajiri ya tarehe 1, tulikuwa tumepanga safari ya kwenda nje ya nchi mimi na mke wangu, maandalizi yote ya safari yalikamilika vizuri na tulitarajia kusafiri pamoja na mtoto wetu kipenzi.

Tulikuwa tumepanga kwenda nchini Ugiriki katika mji wa Thessaloniki kwaajili ya mapumziko kupisha vuguvugu lililokuwa likiendelea nchini. Tulifika Airport mapema sana na tulikuwa abiria wa kwanza kuingia kwenye ndege ya shirika la ndege la Nairobi airways ambayo ingetufikisha Nairobi kisha tungechagua ama kusafiri na Qatari Airways inayoruka kutoka Nairobi hadi Athens Ugiriki au kupanda ndege nyingine ya shirika la ndege la Ethiopia airways ambayo ingetufikisha AdisAbaba Ethiopia kisha tuabiri ndege ya Fly Emirates inayoenda moja kwa moja hadi Ugiriki. Yote hayo yalikuwa machaguo yetu maana fedha tulikuwa nazo zakutosha, lakini mke wangu alishauri tutumie Qatari Airways tutakapofika Nairobi.

Nairobi katika uwanja wa ndege siku hiyo kulikuwa shwari na kwakuwa kutoka Dar es salama hadi Nairobi hakuna umbali sana basi hatukukawia kufika. Wafanyakazi wa pale uwanja wa Jomo Kenyatta ni wachangamfu sana hivyo haikutuchukua muda tulikuwa katika ndege ya Qatar Airways baada ya mda kidogo safari ilikuwa imekolea, tukipasua mawingu kwenda ulaya wakati wote huu Junior mtoto wetu alikuwa amelala fofofo.

Athens Ugiriki palikuwa shwari na muda mchache mji huu ulikuwa ukiwapokea wageni mbalimbali watakaofika na Qatari Airways na Mimi,mke wangu pamoja na mtoto wetu tulikuwa miongoni mwa wageni wa siku hiyo. Tulipanga tutakapofika Athens kwakuwa ni usiku tungelala katika mji huo huo na kesho yake tungefanya manunuzi kadhaa kisha kukodi ndege ya kibinafsi ya shirika la ndege la Aegean Airline inayoenda moja kwa moja hadi katika mji wa Thessaloniki ambapo ndipo tulikusudia kwenda.

"Hakuna safari isiyokuwa na mwisho" majira ya saa 7:30 usiku sana, tulitangaziwa kuwa nusu saa mbele tungewasili katika uwanja wa ndege wa Athens (Athens Airport. ATH) ambayo ni miongoni mwa viwanja vikubwa vya ndege pale Ugiriki. Saa 8:00 tulifika tamati. Kama ilivyo ada kuna Mgiriki alikuja kukagua passport zetu na ilivyofika zamu yetu akaanza na mke wangu kisha mimi, na kwakuwa mimi ndiye niliyembeba mtoto akaniuliza " passport ya Junior ikowapi? Nikamwambia hatukuwa nayo kwasababu Junior alikuwa bado mdogo.

Yule mgiriki alionesha kukerwa na kauli ile kisha akasema kwa sauti isiyokuwa na masihara hata kidogo "χωρίς διαβατήριο το παιδί δεν επέτρεψε την άφιξή του" alizungumza kwa Kigiriki tafsiri yake "BILA PASSPORT MTOTO HATAINGIA NCHINI" nilimtazama mke wangu ambaye alikwishatangulia kwa lifti nisijue lakufanya.

Ndugu msomaji una passport? Maisha tuyaishiyo ni safari na hapa duniani sio sehemu yetu. Tumesoma na kusikia katika maandiko matakatifu kuwa, kuna mbinguni au peponi ambapo ndiyo makao ya wale ambao waliishi maisha mema, kumwabudu Mungu wa kweli na kushika amri zake. Sehemu hiyo ni kwaajili tu ya wale waishio katika njia sahihi ambao ndio hupewa passport au kibali cha kupokelewa huko. Je unafikiri ninani atakubebea passport? Ni Mchungaji wako au Shekh au Padri?.

Junior katika hadithi hii alitutegemea sisi kumbebea na hatukuona ulazima wa kufanya hivyo, kwakuwa hatukuona athari ya kutobeba, passport zetu tulikuwa nazo na hivyo Junior peke yake ndiye hakuwa na uhalali wa kuingia Ugiriki. Tazama nakuusia kuwa kiongozi wako wa dini pamoja na maandiko ni wazazi wako kama ilivyo kuwa sisi kwa Mwenetu Junior lakini jukumu la kuhakikisha unapata kibali kwa Mungu ni lako Kwakufanya matendo mema, kuifanya ibada ya kweli, kumwabudu Mungu wa kweli
 
Hadithi tena ya uongo mkubwa wa kitoto. Hakuna safari za aina hiyo. Eti qatar air itoke nairobi direct to ugiriki. Mara Ethiopia air ikupeleke adis ababa halafu upande emirate moja kwa moja ugiriki jifunze kwanza safari za anga uzijue

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hadithi tena ya uongo mkubwa wa kitoto. Hakuna safari za aina hiyo. Eti qatar air itoke nairobi direct to ugiriki. Mara Ethiopia air ikupeleke adis ababa halafu upande emirate moja kwa moja ugiriki jifunze kwanza safari za anga uzijue

Sent using Jamii Forums mobile app
Hehehe

Route ajue ziko hivj
Ukipanda Qatar lazima upite Doha Ahmed International airport
Ukipanda KQ lazima upite Nairobi
Ukipanda Emirates/Etihad/Flydubai unapita Dubai ama ,Abu Dhabi
Ukipanda KLM unapita Amsterdam
Ukipanda Ethiopia unapita Bole Addis Ababa
Ukipanda Air Tanzania unapita Chato
 
Habari mambo naitwa Mr Equator Nimeandika ujumbe huu kuku omba swala moja tu!
Mimi nimetengeza website ya ku share story ambayo ni EquatorStory
Je umekuwa ukipata tabu kupost story zako hapa?
Hili ndo suluhisho lako.
Mimi nataka nkupe nafasi ya kuwa mmoja wapo wa kwanza kutumia hii website
unda account yako na uweze kupost story yako mpya.
 
Hadithi tena ya uongo mkubwa wa kitoto. Hakuna safari za aina hiyo. Eti qatar air itoke nairobi direct to ugiriki. Mara Ethiopia air ikupeleke adis ababa halafu upande emirate moja kwa moja ugiriki jifunze kwanza safari za anga uzijue

Sent using Jamii Forums mobile app
Iko sawa mkuu labda wewe ndiye hujawahi kupanda ndege
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom