Nianze hivi, nadhani nyuma kidogo nilikwambia kwamba Muungano wa nchi zetu ulikuwa wa kujenga UMOJA wa KITAIFA (Unitary State) sio wa Shirikisho (Federal Union).
Nakubaliana nawe kwasababu Mwalim Nyerere alidhani baada ya muda mrefu tutafikia hiyo Unitary state.
Ni kwa bahati mbaya hakuwa na partner upande wa Zanzibar.
Watanganyika walikubali hilo na hadi 2010 hawakuwa na habari na Muungano. Wazanzibar waliowaamsha kwamba ni mazezeta ,Wakoloni, wanaionyonya Zanzibar, hawana uchungu na nchi yao n.k.
Watanganyika wakahoji moja baada ya jingine na kubaini wameubeba Muungano na kuibeba Zanzibar. Wakabaini Zanzibar haina mchango wowote wa maana kwa maisha yao. Wakahoji gharama za Muungano ukilinganisha na faida. Hilo likazua hoja moja muhimu, hivi Tanganyika inapoteza nini bila muungano!
Na nadhani Wanasiasa, wasomi na hata Wananchi wengi hawaelewi hilo ndio maana wanachukuwa ya Muungano wa Shirikisho kuzungumzia Muungano wetu wakihoji hata Muundo wa Serikali 2 tumetoka wapi sio Shirikishi!
Wananchi wanatambua kwamba muungano ni unsustainable , wanazungumzia alternative ili kuzuia collapse ambayo sasa ni imminent
Nirudi kwenye hoja. Matatizo ya Muungano wetu yameanzia wapi? Nitasema ni baada ya mabadiliko ya Katiba ya mwaka 1992 hasa baada ya kutoka report ya Nyalali 1991 ambayo maoni ya watu wengi wali base kwenye kuutazama Muungano wetu kama ni Shirikisho. Kwa hiyo, mabadiliko mengi yalofanyika 1992 yalitokana na report ile kwa.kuzingatia Muungano wetu, pamoja na kuongeza mambo yale 11 ya ziada, lengo ni kuimarisha mshikamano wa Watanzania Bara na Visiwani.
Si kweli hata kidogo! Mwaka 1991-1992 Aboud Jumbe hakuwepo madarakani kabisa.
Kilichomuondoa Jumbe ni Muungano tena hoja ya serikali tatu. Baada ya miaka mingi kwa mara ya kwanza Tume ya Warioba ilipotoa rasimu ya serikali 3, Jumbe alionekana hadharani akisema amekuwa vindicated
Hata kabla ya vyama vingi tayari kulikuwa na vugu vugu la kina Shaaban Mloo na wengineo chini chini
Madai ya Katiba Mpya yakaanza upya kwa kushinikiza Muungano wa Mkataba (Confederal Union) na Shirikisho (Federal Unioni) dhidi ya Serikali moja. Yote hii ni kutokana na makosa tulofanya 1992, kutotenganisha Kikatoba mamlaka ya Mihimili na hasa Mamlaka ya rais kutokuwa na mkono ndani ya Mihimili mingine, tulijikuta katika Utawala wa Kiumla (Authoritarian).
Again, si kweli. Muungano wa mkataba haikuwa hoja Tume ya Warioba ilipoanza kukusanya maoni.
Hoja ya Maalim Seif ilikuwa serikali 3 , CUF walipofikisha rasimu yao haraka haraka chini ya huyu DC Mtatiro madai yalikuwa Kurudi kwa Tanganyika.
Maalim Seif akaambiwa kurejea kwa Tanganyika kutaifanya Zanzibar dhaifu . Hapo akaleta hoja ya Muungano wa mkataba. Ni hoja ya kipuuzi sana aliyotoa Maalim Seif kwasababu mara zote hakuwahi kuitetea kwa mantiki. Mkataba utahusu nini na una faida gani kwa Tanganyika! hakuweza kujibu
Hata leo ukimuuliza Jussa, OMO na wengine hakuna anyeweza kukuambia Mkataba ni wa nini na unafaidisha vipi pande zote mbili za Muungano! hawawezi kwasababu ilikuwa hoja ya kipuuzi iliyojengwa kipuuzi na kwa bahati mbaya tunakumbatia upuuzi huo kama hoja muhimu. Huuni moja ya upuuzi wa Maalim Seif, tuiache
Wapambe wake akina Jussa, walisema Kijiografia Zanzibar itabaki katika kivuli cha Tanganyika kwa maana kwamba, Tanganyika ina provide huduma za Ulinzi na Usalama , Budget support, inatoa ajira kwa Wazanzibar kuliko SMZ, ni soko la biashara la Zanzibar kiutalii na kibidhaa. Ni eneo lililobeba Wazanzibar wengi kuliko Zanzibar yenyewe.
Hamad Rashid alisema wapo Wazanzibar 1.2 Milioni Tanganyika wakinufaika na huduma za kila aina bila ubaguzi. Kuwarudisha hawa Zanzibar kutazua mgogoro wa resources na chuki zitarudi
Ilipokuja report ya Warioba, na Bunge la Katiba hapo ndio tukatibua kabisa donda ndugu. Dhahiri Sasa tulitaka Muungano wa Shirikisho (Federal Union) dhidi ya Muungano uloasisiwa (Unitary Union). Na Vyama.vingi gimekuww kama Challenge kwa rais mwenye mamlaka yote.
Hapa si sahihi. Hakuna Tume iliyoundwa ya matatizo ya Muungano iliyokuja na maoni tofauti na ya Warioba. In fact Warioba alipitia rejea za Tume za Nyalali, Shelukindo, Kisanga, Amina n.k. na zote zilikuwa na jibu moja, muundo wa sasa haufai na Serikali 3 ni jawabu.
Warioba alikusanya maoni ya Wananchi akapata jibu lile lile. Kumbuka ilikuwa ni lazima kuwa na jibu la nini kifanyike, na ingekuwa wendawazimu kusema tofauti . Jitihada za kufanya muungano kama taboo zilikuwa za kipuuzi na ndizo zimetufikisha hapa! Warioba sioni kosa lake
Kibaya zaidi ni pale Upinzani walipounda UKAWA wakaanza kuhoji hata Muungano, Hati ya Muungano, Mambo ya Muungano yaloongezwa na madai kwamba Zanzibar imetawaliwa na Tanganyika! Msemaji mkuu akiwa huyu huyu Tundu Lissu mnayemsifia leo. Mbunge aloapa kuilinda.na kuitetea Katiba ya JMT
Mkuu ukilinda Katiba ya JMT haina maana usiwe na maoni tofauti . Huu ndio ujinga uliotamalaki. M
abunge yaliyopita badala ya kutafuta jawabu wanasema wameapa kulinda Katiba.
Ni uongo kwasababu katiba waliyoapa kuilinda ni kwa pale tu wanapotaka. Magufuli alisigina sana Katiba mbona hatukusikia hoja ya kuilinda Katiba. Hata sasa imesigina sana Katiba, hivi kusema ni kosa.
Kuitetea katiba ni pamoja na kusema pale inapoonekana kuna tatizo si kukaa kimya au kuwa 'ndiyo mzee'' kwasababu tu mtu aliapa.
Katiba ya Jamhuri imesha kote kudhaurika bara na Visiwani. Wazanzibar wamesha anza kujitika madaraka, Wamesha ondoa baadhi mambo ya Muungano wasoyataka. Wamempa heshima kubwa ya Kitafa rais wao huku wakidai nchi yao huru na kibaya zaidi Tuliwa support, leo wanaanza kutekeleza yao kinyemela mnashangaa kama hawa ni Watanzania? Alaaa!
Mwaka 2010 tukiwa hapa Jamvini tulimuonya JK kwamba kuwafurahisha Wazanzibar kwa kuruhusu katiba yao iwe juu ya katiba ya nchi ni hatari. JK kama kawaida ni mtu wa kupendeza watu.
Leo Zanzibar wana Jeshi lao, yaani wana Chuo cha Monduli. Wameanzisha Chuo cha Uhamiaji. Hakuna Taasisi isiyo na mbadala. Wanapotaka maziwa na asali za Tanganyika wanabeba vitambulisho vya NIDA, wakirudi kwao si Watanzania. Huu ndio upuuzi uliotufikisha hapa, Watanganyika hawana cha kulaumiwa
Nimalizie kwa kusema hivi hivi, both sides Tunatumia UTANZANIA pale tunapokwazwa ama penye maslahi na Manufaa kwetu,
Watanganyika wanatumia Utanzania kwa faida gani kutoka Zanzibar
Mkuu usijaribu ku balance kuwa mkweli! Ukweli ni kama upembe wa ng'ombe haujifichi
Hatari ninayoiona ni kwamba Viongozi wa sasa ni kama wameridhia kwamba muungano ufikie tamati, na kwa Watanganyika walivyochoshwa si dhani kama kuna miaka 3.
Kumbuka wao ndio wamebeba muungano na hawana cha kupoteza! silent majority! mark my words