Hadaa ya Mihimili ya Serikali

Hadaa ya Mihimili ya Serikali

Mbona warioba alipropose wabunge 75 nchi nzima. 50 bara, 25 zanzibar. Hakutokuwa na viti maalum.

Ikumbukwe kwa sasa zanzibar wana baraza la wawakilishi ila bado linapeleka wabunge dodoma. So kwa zanzibar dual system ni sawq ila ikija Tanganyika ndio issue ya gharama inatajwa!!
Huwezi kuwa na Bunge la watu 75 ikiwa tuna Majimbo 314! Lazima kila jimbo lipate mwakilishi wake katika Bunge la Jamhuri na Bunge la Serikali yao. Ndio maana unaona Zanzibar ina Wabunge wa Serikali yao na Wabunge wa Jamhuri wakila hela tu miaka yote.

Na hata huo Umoja wa Kitaifa Zanzibar ni viongozi kugombania nafasi chache zilizopo wakaunda Umoja huu kukidhi ambitions za watu wabinafsi lakini haiwasaidii chochote wananchi wa Wazanzibar zaidi ya kutuliza Uhasama wao wa Kisiasa. Matajiri Wakubwa Zanzibar siku hizi ni Viongozi wao.
 
Huwezi kuwa na Bunge la watu 75 ikiwa tuna Majimbo 314! Lazima kila jimbo lipate mwakilishi wake katika Bunge la Jamhuri na Bunge la Serikali yao.
Muungano lingekua na 75 tu maana si linakutana kujadili mambo ya muungano tu. Sasa kama zanzibar inaleta wabunge 50 huku bara ukiweka na viti maalum wanaotoka zanzibar na bara zaidi ya 100 utagundua tu hiyo 75 inakua offset na viti maalum vitakavyofutwa na hivyo viti vya zanzibar vinavyopungua kutoka 50 hadi 25.

Usiseme haiwezekani maana bunge hilo litakua specifically kujadili mambo ya muungano tu so halina mambo direct sana ya grassroots kulinganisha na la tanganyika. Itakua equivalent ya bunge la EAC tu
 
Na hata huo Umoja wa Kitaifa Zanzibar ni viongozi kugombania nafasi chache zilizopo wakaunda Umoja huu kukidhi ambitins za watu lakini haiwasaidii chochote wananchi wa Wazanzibar zaidi ya kutuliza Uhasama wao wa Kisiasa.
Lakini mkuu unasahau hta nafasi za DC zilikua zinafutwa na hesabu zilipigwa na humphrey polepole pale Nkrumah Hall kwa msaada wa BOT na hakukua na extra cost.

Kuhusu zanzibar hata majimbo 50 ni makosa, population na geography wise yalitosha majimbo 20 pekee. So tunaweza kuwa na serikali 3 zilizopunguzwa post za kisiasa ili kuwa na ufanisi ila kulinda muungano otherwise iwe serikali moja tu.
 
Huwezi kuwa na Bunge la watu 75 ikiwa tuna Majimbo 314! Lazima kila jimbo lipate mwakilishi wake katika Bunge la Jamhuri na Bunge la Serikali yao. Ndio maana unaona Zanzibar ina Wabunge wa Serikali yao na Wabunge wa Jamhuri wakila hela tu miaka yote.

Na hata huo Umoja wa Kitaifa Zanzibar ni viongozi kugombania nafasi chache zilizopo wakaunda Umoja huu kukidhi ambitions za watu wabinafsi lakini haiwasaidii chochote wananchi wa Wazanzibar zaidi ya kutuliza Uhasama wao wa Kisiasa. Matajiri Wakubwa Zanzibar siku hizi ni Viongozi wao.
Majimbo siku hizi wanapeana kama zawadi kila siku yaongezwa na hakuna cha maana

Pia ubunge umekua ajira ya kudumu mtu akiingia humo hatoki

Ibara ya 104 ya katiba ya Kenya inaruhusu mbunge kutolewa na wananchi kabla ya wakati wake kuisha hii inaitwa Right to Recall...

Kwenye rasimu ya katiba waliwela hichi kitu ibara ya 123

Alafu ulitegemea wabunge wa Ccm wapitishe kirahisi tuu
 
Muungano lingekua na 75 tu maana si linakutana kujadili mambo ya muungano tu. Sasa kama zanzibar inaleta wabunge 50 huku bara ukiweka na viti maalum wanaotoka zanzibar na bara zaidi ya 100 utagundua tu hiyo 75 inakua offset na viti maalum vitakavyofutwa na hivyo viti vya zanzibar vinavyopungua kutoka 50 hadi 25.

Usiseme haiwezekani maana bunge hilo litakua specifically kujadili mambo ya muungano tu so halina mambo direct sana ya grassroots kulinganisha na la tanganyika. Itakua equivalent ya bunge la EAC tu
Hapana mkuu nadhani mnachanganya Mamlaka ya Taasisi na Madaraka ya mtu. Isitoshe report ya tume sio maneno ya Warioba bali ni Maoni ya wananchi.l waloyakusanya.

Yeye binafsi alitaka Serikali 1 na ndio maana tulipoanza Muungano, tulikuwa na Mambo 11 ya Muungano kisha yakafika 22 kama sikosei ili kuelekea Serikali 1 na tuki deal na chngamoto za Utaifa moja baada ya nyingine. Kaitafute yale mahojiano yake na Jenerali akizungunzia jinsi Unija wa Kitafa wa Zanzibar walivyokiuka Katiba ya JMT.

Ok, ni hivi - Rais wa Jamhuri ana Madaraka nchi nzima iwe kule mnajadili Elimu, lakini fedha itatoka Janhuri. Bunge la Jamhuri litakuwa na Bajeti ya Taifa kuhusiana na Elimu au jambo jingine lolote kulingana na ahadi za Chama tawala. Tofauti ni moja tu, Utekelezaji wa shughuli za Elimu au jambo jingine ndio unabakia kwenye mamlaka yenu na Mambo yasiyokuwa ya Muungano. Kwanhiyo mnapikea fedha za Elimu, nyie ndio mnapanga hizi zitajenge nini kulingana na mahitaki ya kwenu. Hampangiwi uendeshaji wala sheria na Serikali ya Jamhuri.

Kwa hiyo tukitaka Serikali 3, lazima Bunge la Jamhuri liwe na Wabunge 314 sawa na Serikali uloundwa. Bunge haliwezi kuzungumzia swala lolote la Kitaifa pasipo mwakilishi wa jWananchi kutoka jimbo hata moja. Basi huyo hatakuwa rais wa Jamhuri ya Tanzania bali rais wa Kifalme.

Chukulia Bunge Marekani au hata Canada japokuwa wana Mambo yasiyokuwa ya Muungano lakini kila jimbo lina Mwakilishi wake Bunge la federali. Na kule kwao kuna mbunge vile vilevile wa jimbo katika Bunge lao.

Nimalizie kusema hivi, kama nia na dhamira ni Kuuvunja Muungano basi chukueni Serikali 3. Sio kila Maoni ya Wananchi ndio yawe suluhusho au mwelekeo wetu Kitaifa. Wananchi walikataa kuundwa Vyama vingi kwa Aslimia 80, lakini Mwalimu alichagua asilimia 20 na tukaunda Vyama vingi, leo tunazungumzia Demokrasia.

Siku tutakayo unda Serikali 3, ndio Siku tutajuana huyu Mtanganyika yule Mzanzibar. Tutawafukuza Wazanzibar wote kwa sababu Sheria yao Mtanganyika hawezi kumiliki ardhi Zanzibar.

Tutaziona gharana zinazobebwa na Bara kama mzigo tusioweza kuubeba! Uhasama utashika kasi na haitaweza kutokea tena Mzanzibar kuwa rais wa Jamhuri kwa sababu hesabu yetu kubwa na hatutajali anatika Chama gani cha Chama cha Siasa.

Kutakuwa na Wazanzibar na Wazanzibara, Wapemba na Waunguja. Watanganyika nao wataanza kujitazama nani mzigo? Huyu asili yake wapi? Mtwara watadai Gas yao iwanufaishe wao, Kanda ya ziwa nao Dhahabu yao kea nini Dodoma inajengeka kuliko Kahama! Yote haya yahahitaji cheche moja tu iwashe. Serikali 3.

Anzisheni - Mtanikumbuka

Maasalaam..
 
Ina maana tuna muhimili mmoja tu, hiyo mingine ni vivuli vya muhimili mkuu.
Yes!, hili sio tuu nimelisema wazi humu bila kumungunya maneno!, Je, wajua kuwa Rais wa JMT ndie Serikali, Bunge na Mahakama? Yuko juu ya Mihimili yote 3. Je, kuna uwezekano Rais wa JMT pia yuko juu Katiba?, bali pia nikaliandikia makala ya gazetini
1780782116785.png

P
 
Kwa hiyo tukitaka Serikali 3, lazima Bunge la Jamhuri liwe na Wabunge 314 sawa na Serikali uloundwa. Bunge haliwezi kuzungumzia swala lolote la Kitaifa pasipo mwakilishi wa jWananchi kutoka jimbo hata moja. Basi huyo hatakuwa rais wa Jamhuri ya Tanzania bali rais wa Kifalme.
Hii figure ya 314 unaitoa wapi? Walishasema NEC ingepunguza majimbo kubakia 75 pekee na wabunge viti maalum pamoja na DCs kufutwa. So ondoa hii hypothetical figure ya watu 314.

Pia sijaelewa unaposema hakuna wawakilishi? Kwani nchi haiwezi kuwa na wabunge 75 pekee??
 
Nimalizie kusema hivi, kama nia na dhamira ni Kuuvunja Muungano basi chukueni Serikali 3. Sio kila Maoni ya Wananchi ndio yawe suluhusho au mwelekeo wetu Kitaifa
Of course wengi wanataka serikali moja ila sasa zanzibar hawataki na wao ni autonomous wakati Tanganyika ishamezwa na muungano. So kama hawataki 1 basi serikali 3 ila hizi mbili ni complicated sana unless zanzibar iwe jimbo tu kma Hong-Kong au Macau.
Wananchi walikataa kuundwa Vyama vingi kwa Aslimia 80, lakini Mwalimu alichagua asilimia 20 na tukaunda Vyama vingi, leo tunazungumzia Demokrasia.
Hawakukataa walikua wametishwa sana, mimi nikiwa mdogo kule kijijini kwetu mpaka makanisani tulikua tunaambiwa vyama vya upinzani vikishika nchi tutaingia vitani, makanisa yatafugiwa mbuzi n.k tuliogopeshwa mpaka nakumbuka tumewahi kuomba aisee kama lisaa hivi wapinzani washindwe, watu mpaka wanalia kabisa. Hofu ilikua kubwa kuliko ya corona, so kwa mazingira hayo lazima tu wananchi wangekataa upinzani.

Pia hatukuwa na elimu so hata hatuelewi demokrasia ni nini wala bunge lina kazi gani. Ila waliotoa maoni kwa warioba ni kizazi cha waliosoma na kuelewa matunda ya demokrasia na changamoto za muungano.

Na kuweka rekodi sawa sio maoni yote yalichukuliwa, mfano wananchi wengine hasa zanzibar walitaka muungano wa mkataba lakini ikapigwa chini, kuna wengi walitaka serikali ya majimbo hasa kwenye ngome za chadema huku zanzibar ikiwa jimbo ila warioba alipiga chini.
 
Hii figure ya 314 unaitoa wapi? Walishasema NEC ingepunguza majimbo kubakia 75 pekee na wabunge viti maalum pamoja na DCs kufutwa. So ondoa hii hypothetical figure ya watu 314.

Pia sijaelewa unaposema hakuna wawakilishi? Kwani nchi haiwezi kuwa na wabunge 75 pekee??
Now you talkin, kwa hiyo rasimu ilipendekeza Majimbo yote Bara yatakuwa 75? Ok, nambie nini hasa dhamira ya kupunguza Majimbo?

Bila shaka utasema kupunguza idadi ya Wabunge na gharama zake! Ufanisi je? Ikiea leo hii hawa Wabunge 314 wa Bunge hili wanachemsha wanapiga domo tu, fikiria Wabunge 75 ndani ya Bunge wakijadili maswala ya Kitaifa ambao bado watamtegemea rais kufikisha maendeleo maeneo ambayo haya hawayajali.

Infact, Bunge la JMT leo hii linashughulikia Mambo yote ya Bara, Inafanya kazi kama ni Serikali ya Tanganyika chini ya Waziri Mkuu! Malalamiko mengi ninkwa nini Wazanzibar wapo Bungeni kujadili mambo ya Tanganyika! Hizi ni cheche zinazosubiri moto ushike kasi.

Kifupi Mkuu wangu, leo hii ni kama tuna Serikali 3 tayari isipokuwa sio Official na ndio maana Zanzibar wamebadilisha mambo mengi kwao kinyume cha Katiba ya JMT.

Narudia kusema rasimu ya Warioba ilikuwa nzuri baadhi ya maeneo lakini iligusa pia maeneo ambayo hatukutakiwa Wananchi kuyajadili.

Binafsi naamini Katiba ni Mwongozo wa nchi hautakiwi kuuliza Wananchi kwa sababu ni Sheria Mama ambayo wao wote watawajibika.

Sasa ukianza kuuliza Wananchi kuna watakao kataa na wakisema hapana ukalazimisha itaingia chuki. Kumbuka Bunge la Katiba lilivunjika kwa sababu ya ambi mawili tu muhimu. 1. Muundo wa Serikali 3 na 2. Kumpunguzia rais madaraka.

Solution ya yote haya ni Kuyagawa mamlaka baina ya Mihimili yetu (Separation of Power) iwe Huru kimamlaka ili wasimamiane "Check and Balance" ndio ombwe kubwa tulokuwa nalo sasa hivi. Hope unanielewa kwa undani nachozungumzia

Maasalaam
 
Tutaziona gharana zinazobebwa na Bara kama mzigo tusioweza kuubeba! Uhasama utashika kasi na haitaweza kutokea tena Mzanzibar kuwa rais wa Jamhuri kwa sababu hesabu yetu kubwa na hatutajali anatika Chama gani cha Chama cha Siasa
Gharama zinatoka wapi? Wakati walikua wanapunguza positions na departments zinazo overlap. Mfano sahivi mbona matumizi mfano gharama za serikali kama mishahara, posho, magari, safari yaani recurring budget zinapanda kila mwaka ilihali ni serikali mbili? Maana yake hakuna correlation kati ya idadi ya serikali na gharama kuongezeka au kupungua.

Yaani watanganyika wasivunje muungani sahivi ambapo tunagharamikia muungano kwa 95% alafu tuje kulalamika baadae? Si itakua utoto. Hayo malalamiko yapo tayari maana tunaona mfano hta mkopo wanapewa mgao ila kulipa ni serikali ya muungano kupitia kutukamua wabara ila mbona hatujavunja muungano.

My point is Muungano utavunjika kwa sababu zingine kma kero za muungano, zanzibar kuelemea bara, kukosekana usawa mfano kumiliki ardhi zanzibar etc na wala hazihusiani na ikiongezwa serikali ya 3.
 
Solution ya yote haya ni Kuyagawa mamlaka baina ya Mihimili yetu (Separation of Power) iwe Huru kimamlaka ili wasimamiane "Check and Balance" ndio ombwe kubwa tulikuwa nalo sasa hivi. Hope unanielewa kwa undani nachozungumzia
Hii haiwezekani mpka katiba mpya iwepo na automatically itapunguza mamlaka ya Rais.

Mfano huwezi sema Bunge liwe huru ilihali kwenye katiba rais ana mamlaka ya kuvunja bunge kama likipinga bajeti au kusema huwezi kubaki bungeni bila chama maana yake ukipinga serikali wakikuvua uanachama sio mbunge tena maana hatuna wagombea binafsi. Maana yake hakuna bunge huru, sasa rasimu ya warioba iliondoa hizo clauses.

Pia Rais kuteua majaji moja kwa moja kunaondoa uhuru wa mahakama sasa ili kutenganisha mihimili lazima katiba mpya ili ipunguze hizo mamlaka za rais kuingilia mahakama. Imagine mpaka bajeti yao wanamlilia rais unategemea itakuaje? Ila katiba mpya inaweza demarcate authority, independence and accountability of the judiciary arm.

Hapa ni mutual exclusive, huwezi kuwa na mihimili huru na wakati huo huo Rais awe na mamlaka makubwa!!
 
.
Sasa ukianza kuuliza Wananchi kuna watakao kataa na wakisema hapana ukalazimisha itaingia chuki. Kumbuka Bunge la Katiba lilivunjika kwa sababu ya ambi mawili tu muhimu. 1. Muundo wa Serikali 3 na 2. Kumpunguzia rais madaraka.
[/COLOR]
Nimetoa mfano kuwa wananchi wengi walitaka muungano wa mkataba ila mbona Warioba aliweka serikali 3 na sio suala la mkataba? Mbona issue ya serikali za majimbo lilipigwa chini? Maana yake maoni yote walichukua ila walichakata na mengine kuyatoa na baadhi kubakiza.

Mwananchi kumsikiliza ni muhimu ila kuchukua au kuacha maoni yake ni suala jingine kuliko kutomsikiliza kabisa.
 
Gharama zinatoka wapi? Wakati walikua wanapunguza positions na departments zinazo overlap. Mfano sahivi mbona matumizi mfano gharama za serikali kama mishahara, posho, magari, safari yaani recurring budget zinapanda kila mwaka ilihali ni serikali mbili? Maana yake hakuna correlation kati ya idadi ya serikali na gharama kuongezeka au kupungua.

Yaani watanganyika wasivunje muungani sahivi ambapo tunagharamikia muungano kwa 95% alafu tuje kulalamika baadae? Si itakua utoto. Hayo malalamiko yapo tayari maana tunaona mfano hta mkopo wanapewa mgao ila kulipa ni serikali ya muungano kupitia kutukamua wabara ila mbona hatujavunja muungano.

My point is Muungano utavunjika kwa sababu zingine kma kero za muungano, zanzibar kuelemea bara, kukosekana usawa mfano kumiliki ardhi zanzibar etc na wala hazihusiani na ikiongezwa serikali ya 3.
Mkuu tusibishane kwa sababu unataka kubishana wakati tujadili kwa lengo la kufahamishana. Pale usiponielewa uliza nami nisipokuelewa nitakuuliza. Hakuna sababu ya kupandisha.

Usichukue majibu yangu kama ni kinzani wakati mimi nakueleza nachokiona kama tutafanya hivi ama vile basi tutegemee haya, ni.mtazamo wangu kutokana na experience nilonayo.

Ok, Ni hivi mpaka sasa ghrama zoote za kuendesha Serikali ya JMT zinachukuliwa na Bara kwa asilimia zaidi ya 95 kamanulivuosema.

Tutakapo unda serikali ya 3 bado gharama hizo zitabebwa na Bara lakini Serikali ya Tanganyika itaongeza gharama nyinginezo. Zanzibar tayari wameshakuwa na Serikali yao mchango na gharama zao wanazijui.

Kwa mfano, Dodoma ni makao makuu ya Kitaifa gharama zake tunazibeba sisi, tukiunda Serikali ya Tatu rais wa Tanganyika tuseme atakuwa Magogoni. Lazima tutampa heshima na huduma za Urais kama taasisi. Tutakuwa na Sijui Waziri Kiongozi au sijui jina gani? Mawaziri wa Bara watatakiwa kupata makazi yao, ofisi zao sijui tutatimia zile zilizokuwa zamani hapo Dar.

Na kule Dodoma Makao Makuu, mchezo ni ule ule. Hili la Kuvunja Muungano trust me, wont take even 5 years! Ukiwa na mke mkaamua kulala vitanda tofauti, basi ndoa hiyo ina matatizo.

Maasalaam
 
Bila shaka utasema kupunguza idadi ya Wabunge na gharama zake! Ufanisi je? Ikiea leo hii hawa Wabunge 314 wa Bunge hili wanachemsha wanapiga domo tu, fikiria Wabunge 75 ndani ya Bunge wakijadili maswala ya Kitaifa ambao bado watamtegemea rais kufikisha maendeleo maeneo ambayo haya hawayajali.
[/COLOR]
Rasimu ya warioba ingeleta tume huru so wananchi wangechagua kiongozi makini na kama angefeli wameweka namna ya wananchi kumfanyia impeachment mbunge na sio kusubiri miaka 5 so hofu ya kuwa impeached na kushindwa uchaguzi unaofuata ingewafanya wabunge kusimama na wananchi bila hofu ya bunge kuvunjwa au kuvuliwa uanachama maana anabaki kama mgombea binafsi.

Hapa kungekua na accountability kubwa sana. Hao wabunge wala sio kama hawana akili ila wanalinda vyeo maana wanahofia kukatwa kama mpina, ila kupitia mgombea binafsi na tume huru mtu anauhakika wakurudi bungeni so ana deal tu na wananchi anakua haogopi vyama wala Rais.

Na kwa sababu mawaziri hawaruhusiwi kuwa wabunge ina maana ile kujikomba ili kupata uwaziri isingekuwepo tena. Watu wangekua wanajua hakuan teuzi so una deal na wananchi tu.
 
Hii haiwezekani mpka katiba mpya iwepo na automatically itapunguza mamlaka ya Rais.

Mfano huwezi sema Bunge liwe huru ilihali kwenye katiba rais ana mamlaka ya kuvunja bunge kama likipinga bajeti au kusema huwezi kubaki bungeni bila chama maana yake ukipinga serikali wakikuvua uanachama sio mbunge tena maana hatuna wagombea binafsi. Maana yake hakuna bunge huru, sasa rasimu ya warioba iliondoa hizo clauses.

Pia Rais kuteua majaji moja kwa moja kunaondoa uhuru wa mahakama sasa ili kutenganisha mihimili lazima katiba mpya ili ipunguze hizo mamlaka za rais kuingilia mahakama. Imagine mpaka bajeti yao wanamlilia rais unategemea itakuaje? Ila katiba mpya inaweza demarcate authority, independence and accountability of the judiciary arm.

Hapa ni mutual exclusive, huwezi kuwa na mihimili huru na wakati huo huo Rais awe na mamlaka makubwa!!
Ndugu yagu huwezi kubadilisha muundo wa Serikali pasipo kubadilisha ndaninya Katiba iliyopo. Ndani ya Katiba hii ibara ya 4 imeeleza shughuli za Mihimili hiyo na kama nia ni kuifanya iwe Huru ina maana Rais hatakuwa na uwezo wa kuvunja Bunge Unless kuna sababu na vigezo ambavyo vitamruhusu rais kulivunja Bunge.

Vile vile Mahakama na Bunge wana uwezo wa kumuondoa rais Madarakani kwa mamlaka walokuwa nayo. Kumbuka hizi organs will be checking each other kuhakikisha hakuna mhimili unakiuka Katiba. Hakuna atakae kuwa juu ya Sheria.

Na hilo la Mahakama nimesema Mahakimu watapendekezwa kisha watapitia Usaili kwa kuzingatia sifa zao kitaaluma na misimamo. Ndivyo wanavyofanya nchi.nyinginezo. kila mhimili utakuwa na limits zake hawaruhusiwi kuvivunja.

Kwa hiyo tunaandika Ibara yote ya 4 juu ya Utawala hasa maeneo hayo nyeti, trust me tukiweza kuwa control hawa Viongozi wakahofia nafasi zao madarakani, mengine yooote yatakuwa rahisi kuyakabiri.

Utawala wowote wa Kidikteta hutakiwa kuwapokonya madaraka ukampa mwingine ambaye anaweza kuwa Dikteta vile vile. rais Wa Tanganyika anaweza kuwa Dikteta na msimfanye kama ilivyo sasa, unaondoa kabisa Mamlaka yake, hana mkono wake Bungeni na Mahakamani ndio maana inaitwa Separation of Power.

Kama tunavyozungumzia Mambo yasokuwa ya Muungano. Haya ni Mamlaka walopewa marais hawa kwa mujibu wa Katiba na hawaingiliani katika usimamizi wa shughuli zao.
 
Huwezi kuwa na Bunge la watu 75 ikiwa tuna Majimbo 314! Lazima kila jimbo lipate mwakilishi wake katika Bunge la Jamhuri na Bunge la Serikali yao. Ndio maana unaona Zanzibar ina Wabunge wa Serikali yao na Wabunge wa Jamhuri wakila hela tu miaka yote.
Mkuu Mkandara with all due respect kuna eneo hulifahamu kabisa au unafanya makusudi kupotosha

Katiba ya Warioba inasema kutakuwa na Wabunge 75 wa Federal Government. Serikali washirika zitatafuta namna ya kuwapata. Mfano wa sasa ni Wabunge 5 kutoka Baraza la Wawakilishi wanavyopatikana Dodoma

Kuhusu majimbo 314 kwamba Bunge litakuwa na mara mbili ni upotoshaji au kutojua jua.

Zanzibar wana Baraza la Wawakilishi lenye wajumbe 50 tu. lakini Wabunge wao ni zaidi ya 100.
Sababu kubwa ni moja, Wabunge wanaokuja Dodoma wanalipiwa na Tanganyika hata kama watakuja 1000 haihusu uchumi wa Zanzibar. Wale 50 wanaolipiwa na SMZ ndio maana ni wachache

Leo ukiwaambia Wazanzibar walipie Wabunge wao wanaokuja Dodoma idadi itapungua kwasababu ni mzigo kwa SMZ. Kwabile wanalipiwa na fedha za Watanganyika basi wanagawa mitaa ya watu 3000 kuwa jimbo.
Kwa upuuzi hu urakosaje wabunge 314.

Kukiwa na Serikali ya shirikisho, Zanzibar watakuwa na utaratibu wao wa kupata Wabunge wa Muungano na BLW.
Tanganyika itakuwa na utaratibu wake. Kuna uwezekano kuwa 100 au 200 kwasababu ni utaratibu tu wa kugawa majimbo.

Watanganyika wataamua Bunge lao liwe na Wabunge wangapi si suala la kusema sasa ni 314 wakati huo watakuwa 628.

Marekani ina Wabunge wa majimbo 400 ikiwa na population ya watu milioni 300. Kwanini Tanzania iwe na Wabunge 300. I mean ni ulafi tu wa kujigawiwa majimbo si suala la utendaji au gharama.

Katika hao 314 unaosema wapo kutoka Zanzibar wanaowakilisha watu 3,500 na Wapo wanaowakilisha Watu 800,000 huku bara. Najaribu kulkuelewesha kwamba hakuna Formula ni ulafi tu, serikali za nchi husika zinapaswa kuamua zenyewe. Angalia mfano wa Kenya, seneti na Wabunge wanavyopatika
 
Gharama zinatoka wapi? Wakati walikua wanapunguza positions na departments zinazo overlap. Mfano sahivi mbona matumizi mfano gharama za serikali kama mishahara, posho, magari, safari yaani recurring budget zinapanda kila mwaka ilihali ni serikali mbili? Maana yake hakuna correlation kati ya idadi ya serikali na gharama kuongezeka au kupungua.
Mkandara haelewi suala la gharama. Kwasasa hivi kila Wizara na idara hadi jeshi zina mbadala Zanzibar.

Maana yake, Wizara kama Afya , Elimu , Utalii , mifugo n.k. ni za JMT kwa ubatizo , kiuhalisia ni za Tanganyika. Kama sivyo, kwanini tuna mbadala huo kule Zanzibar?

Mfano anaotoa wa Bunge anajichanganya sana, sina uhakika kama alielewa Rasimu ya Warioba.

Kwa mfano, Warioba anasema kutakuwa na Bunge la Shirikisho lenye Wabunge 75. kama sikosei 35 kutoka Zanzibar 40 kutoka Tanganyika. Kila mshirika ataweka utaratibu wa kupata Wabunge hao.

Mfano , Tanganyika itaweka utaratibu katika Wabunge 40 kila mkoa utachagua Mbunge mmoja. Watakaobaki 10 watapatikana kwa utaratibu kutoka Taasisi kama vyama vya Wafanyakazi, wakulima na makundi maalum. Gharama za Wabunge 40 zitalipiwa na zile za sasa za Wabunge 100 wa Zanzibar wanaokuja Dodoma kulala tu kwasababu 97% hayawahusu. Gharama zitaongezeka au kupungua!!!

Kuhusu Bunge la Tanganyika, nalo litakuwa na Wabunge kulingana na mgawanyo utakaowekwa si huu wa sasa. Ukiondoa Wabunge 100 wanaokuja kula na kula kutoka Zanzibar, Wabunge wa Tanganyika leo hii ni 300

Kuna uwezekano wa kuPunguza Wabunge kama tutazingatia population na si maeneo.
Gharama zitaongezeka vipi?

Ukiondoa Wabunge 100 kutoka Zanzibar unapunguza mzigo kwa Mtanganyika. Mbona Baraza la wawakilishi lina Wawakilishi 50 kwa Zanzibar ile ile.

Kwasasa Wabunge wa Zanzibar wanachaguliwa na watu 3,500 yaani Mbunge anakuja Dodoma anawakilisha watu wachache kuliko Faculty of law au CoE pale Chang'ombe wala si UDOM au MUHAS!

Pili, Wizara haziwezi kuongeza gharama kwasababu hadi sasa tunazo zile zile! Serikali ya shirikisho itachangiwa na Washirika katika Wizara zisizodi 3. Wizara zingine kama kilimo ni za Washirika

Labda gharama anayosema ni kwa Zanzibar kwasababu free ride ya kuleta Wabunge wanaochaguliwa na watu 3,500 haitakuwepo. Dezo la gharama za Muungano halitakuwep pia

Kitakachoua muungano ni mzigo anaobeba Mtanganyika. Mtanganyika analipa kodi kumlipa Mbunge kutoka Zanzibar aliyechaguliwa na watu wachache kuliko Diwani wa Tanganyika.
Mbunge huyo wa Zanzibar akija Dodoma hana mchango wowote ni haya ya YUDA.

Mbunge wa Znz anayechaguliwa na Watu 3,500 ana kura sawa na Mbunge wa Ubungo anayechaguliwa na watu 400,000. Mkandara anachanganya Umma eti kutakuwa na ongezeko la gharama.

Tena Mbunge wa Zanzibar anaweza kukwamisha Bajeti ya mambo ya Tanganyika yasiymhusu kama atakuwa amemaliza hoja ya YUDA.

Katika umasikini, ujinga na maradhi anayozungumzia Mkandara yupo aliyevuka bahari na idea moja tu YUDA! Gharama zake zinabebwa na Mtanganyika!

Narudia kusema rasimu ya Warioba ilikuwa nzuri baadhi ya maeneo lakini iligusa pia maeneo ambayo hatukutakiwa Wananchi kuyajadili.
Yaani Wananchi wenye katiba na nchi kuna maeneo hawatakiwi kujadili, Kumbe Kuna Wananchi na Wenye-nchi ?

Hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kuyaficha au kukanusha hayapo.
 
Hapana mkuu nadhani mnachanganya Mamlaka ya Taasisi na Madaraka ya mtu. Isitoshe report ya tume sio maneno ya Warioba bali ni Maoni ya wananchi.l waloyakusanya.

Yeye binafsi alitaka Serikali 1 na ndio maana tulipoanza Muungano, tulikuwa na Mambo 11 ya Muungano kisha yakafika 22 kama sikosei ili kuelekea Serikali 1 na tuki deal na chngamoto za Utaifa moja baada ya nyingine. Kaitafute yale mahojiano yake na Jenerali akizungunzia jinsi Unija wa Kitafa wa Zanzibar walivyokiuka Katiba ya JMT.

Ok, ni hivi - Rais wa Jamhuri ana Madaraka nchi nzima iwe kule mnajadili Elimu, lakini fedha itatoka Janhuri. Bunge la Jamhuri litakuwa na Bajeti ya Taifa kuhusiana na Elimu au jambo jingine lolote kulingana na ahadi za Chama tawala. Tofauti ni moja tu, Utekelezaji wa shughuli za Elimu au jambo jingine ndio unabakia kwenye mamlaka yenu na Mambo yasiyokuwa ya Muungano. Kwanhiyo mnapikea fedha za Elimu, nyie ndio mnapanga hizi zitajenge nini kulingana na mahitaki ya kwenu. Hampangiwi uendeshaji wala sheria na Serikali ya Jamhuri.

Kwa hiyo tukitaka Serikali 3, lazima Bunge la Jamhuri liwe na Wabunge 314 sawa na Serikali uloundwa. Bunge haliwezi kuzungumzia swala lolote la Kitaifa pasipo mwakilishi wa jWananchi kutoka jimbo hata moja. Basi huyo hatakuwa rais wa Jamhuri ya Tanzania bali rais wa Kifalme.

Chukulia Bunge Marekani au hata Canada japokuwa wana Mambo yasiyokuwa ya Muungano lakini kila jimbo lina Mwakilishi wake Bunge la federali. Na kule kwao kuna mbunge vile vilevile wa jimbo katika Bunge lao.

Nimalizie kusema hivi, kama nia na dhamira ni Kuuvunja Muungano basi chukueni Serikali 3. Sio kila Maoni ya Wananchi ndio yawe suluhusho au mwelekeo wetu Kitaifa. Wananchi walikataa kuundwa Vyama vingi kwa Aslimia 80, lakini Mwalimu alichagua asilimia 20 na tukaunda Vyama vingi, leo tunazungumzia Demokrasia.

Siku tutakayo unda Serikali 3, ndio Siku tutajuana huyu Mtanganyika yule Mzanzibar. Tutawafukuza Wazanzibar wote kwa sababu Sheria yao Mtanganyika hawezi kumiliki ardhi Zanzibar.

Tutaziona gharana zinazobebwa na Bara kama mzigo tusioweza kuubeba! Uhasama utashika kasi na haitaweza kutokea tena Mzanzibar kuwa rais wa Jamhuri kwa sababu hesabu yetu kubwa na hatutajali anatika Chama gani cha Chama cha Siasa.

Kutakuwa na Wazanzibar na Wazanzibara, Wapemba na Waunguja. Watanganyika nao wataanza kujitazama nani mzigo? Huyu asili yake wapi? Mtwara watadai Gas yao iwanufaishe wao, Kanda ya ziwa nao Dhahabu yao kea nini Dodoma inajengeka kuliko Kahama! Yote haya yahahitaji cheche moja tu iwashe. Serikali 3.

Anzisheni - Mtanikumbuka

Maasalaam..
Muungano hauna faida yoyote kama wananchi hawautaki
 
Back
Top Bottom