Mkuu nadhani unasahau kwamba Rasimu ya Warioba sio Katiba, ni Mapendekezo ya awali ya Katiba Mpya ambayo yalikwama. Kuna kukubalika ama kukataliwa kwa sura, ibara au hata vipengele vyake. Hiinsio Katiba wala Hatujafika huko na hatutsfika kweli mkiendelea kulazimisha vitu visivyowezekana.
Exactly! ni framework . Kitu kilichokuwa dhahiri ni kwamba 2 tier government system is unsustainable
Nimesema Muundo wa Serikali 3 ulipigwa chini kutokana na Bunge litakuwa na viti 75 tu! nikasema hili haliwezekani na ndio sababu pendekezo hili la Serikali 3 haikufanikiwa. Viongozi hawatakubaliana nalo na hauakisi uhalisia kuwakilishinwa Wananchi mil.60 kwa Uchache kiasi hiki. Watu wenyewe sijui kama kweli unatujua?
Si kweli, nadhani hukufuatilia mchakato. Kilichokwamisha ni muundo wa Serikali 3 siyo contents za Serikali 3
CCM Unguja hawakutaka Serikali 3. Vurugu zilianzia NEC CCM walipomtisha JK. Unakumbuka ' Zanzibar siyo nchi ya machotara" the rest is history
3. Umesema Zanzibar wana structure kwa sababu wana Serikali yao,
Zanzibar wana structure kamili kwasababu kila jambo la muungano lina 'parallel' structure
Ndio maana wanakataa miswada ya JMT hadi ipitie BLW
Hivi unajua hivi karibuni wameanzisha Jeshi lao. Nenda you tube uone
unashindwa kuelewa kwamba Wabunge 272 ndio wawakilishi wa Bara na Serikali Kuu. Kwa hiyo Bunge hili Bara inapiga ndege wawili kwa jiwe moja.
Ni makosa! na hapo ndipo shida inapoanzia. Huwezi kuwa Tanganyika na Tanzania at the same time! dude!
Hata kama utakubali ni la Tanganyika, kwanini Wabunge 77 wanaamua mambo ya Tanganyika
Kwanini Wabunge wa Zanzibar wafanye shughuli za kamati za Bunge maeneo ya Tanganyika.
Wabunge wa Zanzibar wana athiri kura ndani ya Bunge la Tanganyika
Asilimia 99 ya Bunge la Jamhuri ni maswala ya Bara aidha tuwe na Serikali yetu au hii ya Muungano. Technically, Bunge hili kwa Asilimia 99 ni mfumo wa kusimamia maswala ya Serikali ya Bara.
Serikali ya Tanganyika haikwepeki kwa sasa, it's a matter of time. I can bet kama SSH hatakubali Tanganyika iwepo, muungano utafia mikononi mwake. In fact ni dhaifu sana kuliko wakati mwingine
5. Sielewi kwa nini bado hunielewi, nasema hivi kupendekeza Serikali ya Bara kuwakilishwa na Wabunge 50 tu Bungeni, pendekezo hili haliwezi kupita popote kwa sababu 2.
Ya kwanza Ubunge ni mradi wa Utajiri kwa viongozi, huwezi kuwaambia watoke 273 hadi 50 wakapitisha.
Ni hivi wabunge 50 ni wa Federal kama wale 9 wa EAC.
273 ni Watanganyika labda iniambia hawatakubali kwa muundo wa Tanganyika.
Ili uelewe na kutochanganya mambo: Serikali 3 ina Tanganyika, Zanzibar na Shirikisho(Federal)
Federal ina mambo 7 tu ambayo ukiondoa Katiba na Msajili wa vyama yanabaki 5 ikiwemo Ulinzi, mambo ya ndani, mambo ya nje, Fedha na jingine moja. Serikali kuu inashughulika na mambo yenye common interest
Serikali za washirika zitakuwa na mamlaka zake na hizo ndizo zitaamua structure ya mabunge yao kutokana na uzito wa shughuli zao.
Mwisho, Zanzibar hawaamui wao idadi ya Wabunge wa Kuchaguliwa. Majinbo nfio hutoa Wabunge wa Kuchaguliwa. Ukisema Zanzibar itakuwa na Wabunge 20 ina maana Zanzibar itakuwa na Majimbo 20 ya kupiga kura, Bara nako Wabunge = Majimbo 50. Hizo nyongeza za sijui nafasi za Rais na viti maalum hazina Upande. Wanaweza fhaguliwa toka upande wowote wa Muungano.
Narudia tena, Zanzibar inaweza kuamua idadi ya Wawakilishi katika BLW kwa kadri inavyotaka. Hakuna chombo au taasisi inayoweza kuzuia kwasababu BLW lipo kwa mujibu wa Katiba ya SMZ 1984 toleo 2010.
Tofautisha kati ya Wabunge na Wawakilishi.
Pili, Serikali kuu kwa mujibu wa Warioba itakuwa na Wabunge 75. 50 kutoka Bara na 25 kutoka visiwani kama sikosei. Uchaguzi wa hawa 50 utazingatia matakwa ya Katiba ya Tanganyika, na hao 25 wa Zanzibar utazingatia katiba ya SMZ. Kila upande utaamua njia za kupata Wabunge wake!
Mfano, EAC imetoa nafasi za kila nchi kupeleka Wabunge Arusha,, haikusema wapatikane vipi. Kila nchi ina utaratibu wake wa kupata hao 9. Tanzania tunawachagua kupitia Bunge , Kenya , Uganda na Rwanda wana utaratibu wao.
Usichanganye upatikanaji wa Wabunge wa serikali za shirikisho na Wabunge wa serikali kuu.