Hadaa ya Mihimili ya Serikali

Hadaa ya Mihimili ya Serikali

Dola ndo Ina Mihimili Mitatu siyo serikali

Sema serikali inaingilia sana mihimili Mingine
Mara Nyingi Serikali ya Tanzania /Serikali Kuu imeonekana kuingilia mihimili mingine - Bunge na Mahakama. Kumbuka Tanzania ina "separation of powers" kwenye katiba, lakini kwenye vitendo wakati mwingine mistari imekuwa ukungu.

mfano tu hata bila kuchimba sana

1. Kuingilia Bunge
1. 2016-2020 - Kusimamisha wabunge na kufuta hotuba
Spika wa Bunge alipiga marufuku wabunge kadhaa wa upinzani kusema Bungeni kwa kipindi kirefu. Hoja ilikuwa "kutunza heshima ya Bunge". Wabunge kama Tundu Lissu, Zitto Kabwe, Halima Mdee walinyimwa haki ya kuzungumza kwa miezi. Hapa Serikali kupitia Spika ilionekana kudhibiti mjadala wa Bunge.

2. 1992 - Katiba ya Vyama Vingi
Mchakato wa kuleta vyama vingi ulisukumwa sana na Nyerere wakati wa Rais Mwinyi + CCM. Bunge lilipitisha sheria haraka sana baada ya kamati ya Nyalali kutoa mapendekezo. Wakosoaji walisema Bunge lilikuwa "rubber stamp" - lilipitisha tu bila mjadala wa kina. Lakin ndo Mpaka sasa inatutesa

3. 2019 - Sheria za Bunge kuhusu vyombo vya habari na NGOs
Bunge lilipitisha sheria za Media Services Act na sheria za NGOs ambazo zilipa Waziri madaraka makubwa ya kufunga magazeti/kuvuta leseni. Mahakama baadaye ilipinga baadhi ya vifungu, lakini awali Bunge lilikuwa limepitisha kile Serikali ilitaka.

2. Kuingilia Mahakama
1. 1994 - Kesi ya James Mapalala vs AG
Mahakama Kuu iliamua kuwa kifungu cha katiba kinachozuia vyama vya siasa kisipitishe mgombea mmoja ni kinyume na katiba. Serikali ilikasirika sana. Baada ya hapo kulikuwa na mjadala mkubwa wa "Mahakama inakiuka Bunge". Ilionyesha mgogoro wa mihimili.

2. 2017-2018 - Kesi za uhaini na "sedition"
Wanasiasa na wanaharakati kadhaa walipeleka mahakamani kwa kesi za uhaini. Wanaharakati wa haki za binadamu walisema mahakama ilikuwa inatumika "kunyamaza" wakosoaji. Mfano: kesi za Lissu, Freeman Mbowe. Serikali ilikanusha, ikasema ni utekelezaji wa sheria tu. Lakin Samia na Magufuli wana mkono kwenye kesi za Kipuuzi hizo

3. 2006 - Teule la Majaji
Rais ana katiba uteue Jaji Mkuu na majaji wa Rufaa. Wakati mwingine uteuzi huu ulilalamikiwa kuwa "kisiasa". 2006 Rais Kikwete alipoteua majaji kadhaa bila kushauriana sana na Tume ya Huduma za Mahakama. Wanashiria walisema inathiri uhuru wa mahakama.

4. 2020 - Kesi ya Kupinga Matokeo ya Uchaguzi
Baada ya uchaguzi 2020, kesi kadhaa zilizopinga matokeo zilitupiliwa mbali na mahakama kwa "technicalities". Upinzani ulisema mahakama ilikuwa inaogopa Serikali. Jaji Mkuu alijibu kuwa mahakama inafanya kazi kwa mujibu wa sheria.

Mambo 3 ya kuelewa:
1. Katiba inaruhusu kuingiliana kidogo: Rais anateua Jaji Mkuu, Bunge linapitisha bajeti ya mahakama. Hivyo "kuingilia" kabisa na "kuingiliana kwa utaratibu" ni tofauti.
2. Uhuru wa Mahakama umeimarika zaidi: Tangu 2000, mahakama imekuwa ikipinga Serikali kwenye kesi kadhaa kama kesi za ardhi, haki za binadamu. Lakin simu zinapigwa toka juu! Mfano juzi tarehe 2/06/2026 Simu kutoka kwa msaidizi wa Samia alimpigia afisa mkuu wa Magereza na pia akipiga kwa Hakimu kujiridhisha kuwa je Lissu wamuachie kwa Mbinu gani! Mkuu wa Gereza yeye hakuwa na la kusema anasema TUNATEKELEZA MAAGIZO YATOLEWAYO MKUU TUNASUBIRIA

3. Tafsiri inatofautiana: Serikali husema "tunatekeleza sheria", Wakosoaji husema "ni kuingilia". Hivyo serikali ujificha kwenye kutekeleza sheria kumbe wanaingilia mahakama.

Britanicca
Samahani, naomba kuelezwa tafsiri ya DOLA?
 
Shukran sana, unajua sikuwepo hapa kijiweni mida na dhumuni langu haswa ni kutafuta suluhisho bora zaidi, na ndio maana nikaanza na kuuliza swali.

Hata nilipokosa majibu nilirudi kuhitimisha dhamira yangu kwa sababu watu wengi wanalilalamikia Bunge kuwa butu wakati hawajui Bunge hilo hilo ni sehemu ya Serikali (Executive). Na nikaeleza pia kuhusu Mahakama zetu huwezi mlalamikia CJ ambaye mhimili wake upo dhani ya Serikali.

Nimepitia muundo wa Serikali nyingi kutazama muindo yao lakini kote nilikutana na hitilafu za Kifalme ama PM pamoja na CJ kuwa sehemu ya Bunge. Hapa huwezi kupata 'Separation of Power' bali ni nchi ambazo wana Utaifa na walindana wenyewe.

Kutokana na experience tulizopitia toka wakati wa Mwalimu hadi Sasa, njia pekee tunayoweza kupata mabadiriko ya kweli ni kuanza na muundo mpya wa Utawala wetu ili tuwe na Separation of Power katika mihimili yetu na muundo pekee unaoswihi kisheria katika mazingira yetu ni huu wa Marekani.

Nilitegemea zaidi kutoka kwenu wakongwe kujadilli muundo huo zaidi ya kuitafuta Katiba Mpya kwa mijadala ya Serikali ngapi, sijui Tume Huru wakati rais wa nchi Ndiye aloshika Mpini. Rasimu ya Warioba ilikwama kwa sababu hii na sidhani kama itakuja kurudishwa mezani while the President is a supreme leader.

Kwa muundo tulonao, katu hatuwezi kuwa na Bunge Huru wala Mahakama huru ikiwa Serikali ina mkono wake ndani ya Mihimili hii. La ziada labda badala ya sisi pia kuwa na Baraza la Senate sisi tuote Baraza la Wazee kama ilivyo kwa Zanzibar wao.mbali Naraza la Wawakilishi wana Baraza la Mapinduzi.

Itasaidia sana pale Bungeni haipiti Sheria yeyote kwa kutegemea Wabunge, lazima Baraza la Wazee nao wapitishe na wanaweza ku veto au kumhoji rais kwa maamuzi yeyote yanayoonekana kinyume cha Katiba.

Maasalaam
Case study nzuri ni Kenya kwa ukanda huu wa Africa mashariki
 
Case study nzuri ni Kenya kwa ukanda huu wa Africa mashariki
Haswaaa, lakini nako tatizo lao Kiutawala liko wapi haswa? maana Ruto na Trump kama wanafanana vile! Je, ni support ya Wananchi, The Elites au inatoka kwenye mihimili yenyewe (Lobbyist na Rushwa)
 
Mkuu ahsante kwa mada fikirishi !
Naona swali limekuwa gumu kujibika kwa sababu Katiba yetu haisemi maneno hayo isipokuwa Ibara ya 4(1-3) inasema Shughuli zote za Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kudhibitiwa na mihimili hiyo kwa pande mbili za Muungano.sehemy
Swali ni gumu kwasababu mfumohauel eweki. Katika mifumo ya utawala na serikali hatuna pa kusimama. Kwanza, Head wa government ni Head of State pia tukifuata presidential system kama USA.

Parliamentary system kuna Head of Gov anayeshughulikia mambo ya serikali tu ndani ya Bunge halafu kuna Head of State. Sasa Rais wa Tanzania ni sehemu ya Bunge kama Parliamentary system inavyosema akiwa Head of Gov.

Wakati huo huo kuna ni Head of state kama presidential system inavyosema. Hapa ndipo tatizo linapoanzia

Mihimil imetamkwa kama ulivyonukuu kutoka Katiba kwa makusudi kabisa kutokana na mkanganyiko wa kati ya presidential system na Parliamentary system.

Tanzania, Rais ana nguvu za uendeshaji wa Mahakama na Bunge.
Nguvu hizo ni Budget! Rais anateua Katibu wa Bunge na Mawaziri. Rais anateua Majaji anavyoona

Mahakama na Bunge hazisimami kama ''pillar'' bali 'branch' za Serikali.
Yes nakubaliana nawe kuna tatizo la kimfumo linalonyima Bunge na Mahakama Uhuru. Unapochanganya na teuzi za Uchawa, tatizo ni kubwa

Mzee Warioba aliliona! bahati mbaya wakampiga stop! ili waendelee kutawala kwa kutokuwa na checks and balances. Matatizo tunayotaona sasa ni matokeo ya mfumo mbovu usio na checks and balance

Mimi najua sababu moja kubwa Tume ya Warioba walipo kosea ni kujadili maoni ya Wananchi kuhusiana na tuunde Serikali ngapi? Kana sikosei Warioba alimuuliza JK akamwambie go ahead knowing vyovyote itakavyokuwa, yeye atapigilia msumari hapo hapo..

Mtazamo wangu miye hili lisingekuwepo kabisa kwenye Rasimu ile, kwa sababu ni moja ya NGUZO kuu kabisa iloasisiwa na Wazee wetu toka 1922 hata kabla ya Mwalimu. Watu wengi hawaelewi kwamba African Association ilianzishwa kwanza Zanzibar na Dar es Salaam. AA ndiye babu mzazi wa Afro shiraz na TANU walomzaa hii CCM.

Kihistoria hapo awali Ushirika wao (Bara na Visiwani) ulikuja kujengwa nguvu zaidi na Pan Africanism na wakafungua tawi Ukombozi Pan-African Freedom Movement of East and Central Africa (PAFMECSA). mapinduzi.ya Zanzibar hayakuwa ya ghafla au sijui Okello laaa, Yalipangwa kutokea IF.

Kama sikosei swala la Serikali 3, ndilo lilomweka Marehemu Abdul Jumbe kifungo cha nje maisha Kigamboni na kumpelekea Mzee wetu Malecela balaa wakati ule Afro Shiraz ilijaa wana Mapinduzi wa African Association ya Zanzibar ambao hata Salim A Salim walimkataa kuwa rais wa JMT kwa imani yao kwamba hoja ya serikali 3 ni hoja ya wafuasi wa Hizbu na lengo lao ni kutengua Umoja wa Bara na Visiwani ulosababisha Mapinduzi ya 1964. Rasimu nzima ikapigwa vita.

Tuliposimama leo hii, tumekalia kuti kavu. Muungano upo matatani japokuwa Viongozi wote wa mihimili yote wameapa kuitetea na Kuilinda Katiba! Na katika vitu vyote vilopewa kipaumbele zaidi ndani ya Utaifa wetu ni MUUNGANO.

Maadam tumekalia kuti kavu, tunapitia mitihani kama Wa South hawaamini kama walisaidiwa kuupata Uhuru wao. Generation hii ni Chako chako Changu Changu, njaa kali Na viongozi wengi wanavunja miiko yote waziwazi kuwajaza Wananchi CHUKI na HOFU. Leo tunashughulikiana wenyewe badala ya kutafuta suluhu ya matatizo yetu Kitaifa, tunaanza kugawana Kuti.
 
Mimi najua sababu moja kubwa Tume ya Warioba walipo kosea ni kujadili maoni ya Wananchi kuhusiana na tuunde Serikali ngapi? Kana sikosei
Tume ya Warioba iliundwa kuchukua maoni ya Wananchi. Kumbuka wenye Nchi si viongozi ni Wananchi. Nyerere aliwahi kuonya, msipuuze maoni ya Wananchi hata kidogo. Maoni ya Wananchi ndio nguzo ya Muungano.
Hadi Tume inaundwa ilishapita miaka 40 na viongozi waliona tatizo na kubaini hali si ''sustainable''
Hakuna Tume yoyote iliyoundwa ikaja na proposal tofauti na Warioba. In Fact miaka 20 baada ya Tume ya Nyalali kusema, maoni yale yale yalirudiwa na Tume ya Warioba, Wananchi wanasema
Warioba alimuuliza JK akamwambie go ahead knowing vyovyote itakavyokuwa, yeye atapigilia msumari hapo hapo..
JK alikumbuna na tatizo la Muungano. Katika watu waliodhoofisha ni yeye kwasababu hakutaka kuwa mkweli bali kuwapendeza Wazanzibar! Tatizo sasa ni kubwa kuliko alipokuwa kiongozi
Mtazamo wangu miye hili lisingekuwepo kabisa kwenye Rasimu ile, kwa sababu ni moja ya NGUZO kuu kabisa iloasisiwa na Wazee wetu toka 1922 hata kabla ya Mwalimu
Huwezi kufunika kidonda na taulo ukasema unatibu. Dawa ya kidonda ni kukifunua na kusafisha
Miaka 60 na ushee leo Muungano ni dhaifu kuliko wakati wowote. Uwezekano wa Muungano kuvunjika ni mkubwa kuliko kuimarika hasa zama hizi za ''zamu' yetu.
Kama sikosei swala la Serikali 3, ndilo lilomweka Marehemu Abdul Jumbe kifungo cha nje maisha Kigamboni na kumpelekea Mzee wetu Malecela balaa wakati ule Afro Shiraz ilijaa wana Mapinduzi wa African Association ya Zanzibar ambao hata Salim A Salim walimkataa kuwa rais wa JMT kwa imani yao kwamba hoja ya serikali 3 ni hoja ya wafuasi wa Hizbu na lengo lao ni kutengua Umoja wa Bara na Visiwani ulosababisha Mapinduzi ya 1964. Rasimu nzima ikapigwa vita.
Well, je, Jumbe, SAS n.k. kuwekewa vikwazo kume solve tatizo?
Tuliposimama leo hii, tumekalia kuti kavu. Muungano upo matatani japokuwa Viongozi wote wa mihimili yote wameapa kuitetea na Kuilinda Katiba! Na katika vitu vyote vilopewa kipaumbele zaidi ndani ya Utaifa wetu ni MUUNGANO.

Maadam tumekalia kuti kavu, tunapitia mitihani kama Wa South hawaamini kama walisaidiwa kuupata Uhuru wao. Generation hii ni Chako chako Changu Changu, njaa kali Na viongozi wengi wanavunja miiko yote waziwazi kuwajaza Wananchi CHUKI na HOFU. Leo tunashughulikiana wenyewe badala ya kutafuta suluhu ya matatizo yetu Kitaifa, tunaanza kugawana Kuti.
Hapana! Kwa miaka mingi Watanganyika hawakuwahi kuwa na tatizo na muungano. Tatizo limeanza baada ya Uzanzibar kuwa mkubwa kuliko Utanzania. Watanganyika wanajiuliza kipi hasa wanachonufaika nacho katika muungano walioubeba wenyewe?

Kama umepita mitandaoni leo kuna Mtanganyika analalamika kwamba Leseni yake ya udereva haitambuliwi Zanzibar. Trafiki anayeikataa analipwa na Wizara ya mambo ya ndani inayogharamiwa na Tanganyika. Leseni ya Tanganyika inakubalika Uganda, Kenya, Malawi, Zambia! Vipi ikataliwe Zanzibar
Ujinga kama huu unawafanya watu wajiulize, huu muungano ni wa kitu gani! na Watanganyika wananufaika na nini, na watakosa nini ikiwa haupo!
 
Hoja ya msingi hapa ni kujiuliza Serikali ambayo ina Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Inaongozwa na nani?
Nadhani Jamhuri (Republic) ndiyo yenye mamlaka ya kuiweka Serikali madarakani. Jamhuri ndio yenye serikali

Bila shaka jibu ni Rais wa Jamhuri, kisha ukienda kwanye Mhimili wa Serikali pia kiongozi wake ni rais.
Kwa hiyo, ile dhana ya kwamba Serikali ina mihimili mitatu inayojitawala ni dhana Potoshi kwa sababu neno Mihimili ni sawa na kusema MATAWI ya Serikali, na matawi haya hayapo huru kwa sababu yote yapo chini ya Mamlaka ya rais.
Kituko ni kwamba katika Presidential system Rais (executive branch) hawezi kuvunja Bunge kama ilivyo USA. Tanzania Rais ni sehemu ya Bunge na ana uwezo wa kulivunja Bunge kama ilivyo kwa Parliamentary system ambayo Waziri Mkuu ana uwezo wa kuvunja Bunge.

Rejea hotuba ya Nyerere kwa Taifa alipozungumzia suala la Wabunge kupinga Bajeti ! Nyerere alisema ''kama hamtaki kupitisha Bajeti nina uwezo wa kulivunja Bunge, turudi kwa Wananchi na nina uhakika wa kurudi''
Wabunge wakanywea
Huwezi kuwa na Bunge huru ikiwa rais na mawaziri wake ni sehemu ya Bunge
Huwa najiuliza hivi ni kwanini Katibu wa Bunge anateuliwa na Rais? I mean kwamba Bunge haliwezi kuajiri au!
, na huwezi kuwa na Mahakama huru ikiwa majaji wa Mahakama ni wateule wa rais. Huu ni muundo nadhani wa Kiingereza ambao Serikali yao Kifalme yenye mihimili mitatu chini ya Ufalme huo.
Hapa kuna kituko kingine. Tume ya uajiri ya Mahakama huteua majina ya ''Majaji watarajiwa wengi''. Rais huweka majina katika data base na kitokea nafasi anachagua kutoka humo. Hii maana yake ni kuwavutia ''Watarajiwa ' kwamba wakimfurahisha Mhe. majina yao yatateuliwa. Majaji waliopo katika data base hiyo wana kazi moja tu '' UCHAWA''.
 
Niseme Ukweli:-
Wakati Pascal Mayalla anamuuliza Magufuli swali gumu kwenye mkutano wa Waandishi wa Habari, mimi nilikuwa nimeshakaa pembeni JF kwa sababu JPM alikuwa mtu wangu , sikupenda ubishani ulokuwa ukiendelea hapa.

Niliandika hoja zangu FB zaidi na hata nilijibu hoja ya Mayala kule FB kwa kuzingatia Mamlaka alokuwa nayo Magufuli japo watu wengi hawakuelewa kuwa muundo wa Serikali yetu ndio unampa mamlaka hayo.

Isitoshe katika sakata lile rais ana Mamlaka ya kutunga Sheria ndani ya mhimili wake (Executive Order au Presidential decree) kupunguza matumizi holela ya fedha ndani ya Serikali.

Na mpaka leo naamini Magufuli alihujumiwa sana wakati akiwa madarakani kutokana na misimamo yake. Kwangu miye Magufuli alikuwa Kiongozi mwenye Vision, IQ ya juu kabisa na mwenye kuthamini UTU wa Watanzania.

Naandika haya nikijua MADONGO yanakuja lakini imani yangu ilikuwa ipo kabisa mpaka kesho, na katokea Polepole kuniwekea MHURI wa Kiimani kuwa Hisia na Fikra zangu zilikuwa on the right track.

Matatizo yoote ya Kiutawala tulokuwa nayo yanatokana na MUUNDO wa Mihimili yetu. Ndio unampa Kiongozi Udikteta (kuwa Baba au Mama wa Taifa) sisi sote tuko chini yake. Ndio ulojenga Machawa wakitegemea sauti zao zitawapandisha katika utumishi na matumaini ya nafasi za juu kwenye ajira n.k.

Mabadiriko lazima yaanzie hapa kuhakikisha vyombo na taasisi zote zinazotakiwa kuwa HURU hazipati maelekezo kutoka Juu. Hatuwezi kuwa na Check and Balance kwa mwendo huu. Tunahitaji Mabadiriko sasa.

Leo hii Kiongozi yeyote hawezi kumgomea Rais pale anapoona Sheria imepindishwa ama Katiba imekiukwa - Utatumbuliwa.

Kupata Viongozi kama Mzee Warioba alomgomea Nyerere na Nyerere akajishusha kidogo sii rahisi kabisa nyakati hizi. Wajibu wa Mihimili ni KATIBA na Katiba ndio Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bila Katiba hatuna JMT. Leo hii Katiba inapuuzwa, inabagazwa kiasi inaitwa ni Kitabu, hakika ni kwa sababu ya Muundo wa Serikali (Dola).
 
Hili ni swali kwa wahenga wa jukwaa hili la Siasa. Naomba pia ufafanuzi wake.

Ni Sura au Ibara gani ya Katiba ya JMT inayosema hivi: -

Serikali ina Mihimili mitatu.
1. Bunge -Parliament
2. Mahakama - Judicial
3. Serikali - Executive
Zamani ndio ilikuwa hivyo ila saizi, president ndo kila kitu.
 
Hili ni swali kwa wahenga wa jukwaa hili la Siasa. Naomba pia ufafanuzi wake.

Ni Sura au Ibara gani ya Katiba ya JMT inayosema hivi: -

Serikali ina Mihimili mitatu.
1. Bunge -Parliament
2. Mahakama - Judicial
3. Serikali - Executive
Asante kurejea kihenga,

Hili jambo tuliisha lijadili sana humu Nani Zaidi Kati ya Bunge na Mahakama?!. The Doctrine of "Separation of Powers" Nothing, Just a Myth!

Hali hii ni. kufuatia tulipopata uhuru ile 1961, katiba ya uhuru ilitoka UK, Malkia ndie alikuwa the head of State, Waziri Mkuu the head of the Government, Spika the head of the legislature, na CJ the head of the Judiciary,

Kazi zao zilikuwa Bunge kutunga sheria, Mahakama kutafsiri sheria na Serikali kutekeleza sheria. Bunge linaundwa na Malkia na Kuvunjwa na Malkia, CJ anateuliwa na Malkia na kuidhinishwa na Bunge, Spika anachaguliwa na wabunge .

Mfumo huu unalifanya Bunge kuwa na nguvu kuisimamia serikali, CJ ana nguvu ya kulizuia Bunge na serikali.
Mwaka 1962, tukawa Jamhuri, yale madaraka yote ya malkia, akapewa President, na madaraka yote ya PM, akapewa president, hivyo sasa president akawa an executive president mwenye madaraka yote, rais wa kifalme. Rais akawa ndio kila kitu! kama nilivyo eleza hapa Je, wajua kuwa Rais wa JMT ndie Serikali, Bunge na Mahakama? Yuko juu ya Mihimili yote 3. Je, kuna uwezekano Rais wa JMT pia yuko juu Katiba?

Ile siku nimemuuliza JPM swali hili Ikulu,
View: https://youtu.be/Ta0URHvUlko?si=r3IMbnd_90GeZHEu
Akanijibu kuna mhimili, umejichimbia chini zaidi,

Bunge la Tanzania ni Bunge Zuga Tuu!, halitungi sheria, sheria zote zinatungwa na serikali, kisha zinapelekwa bungeni kuwa rubber stamped na Bunge kuzuga limetunga sheria, Je, Bunge letu ni Bunge Butu?. Angalia Bunge la Uingereza lenye meno linavyong'ata Serikali. Je, Kuna ubaya tukiiga?

Nishauri PreGE2025 - Watanzania tusiruhusu tena Bunge Kibogoyo dhaifu kama hili, lisilo na Meno, kukosa Kambi ya Upinzani na kushindwa kuisimamia Serikali kikamilifu!

Nimeandika sana humu kuhusu hili Bunge.
  1. Wabunge Wetu wa Ajabu!, Wanaachaje Bunge Lijipendekeze Kwa Serikali!, Wanajua Wajibu Wao?. Check 'n' Balance Itoke Wapi?
  2. Sehemu ya Pili: Je, Bunge letu tukufu linajipendekeza kwa Serikali?
  3. Bunge letu ni Bunge la ovyo? Bunge linafanya Uhuni? Wabunge Wetu ni Wahuni? Tumshauri Spika naye aanze kuita Watu kwenye Kamati, au waachwe tu?
  4. Watanzania tutaendelea kusubiri mpaka lini Bunge likitunga Sheria batili na kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu? Tufanye nini?
  5. View attachment 3602001Je, wajua kuwa Rais wa JMT ndie Serikali, Bunge na Mahakama? Yuko juu ya Mihimili yote 3. Je, kuna uwezekano Rais wa JMT pia yuko juu Katiba?
  6. Bunge jipya lina hali mbaya! Serikali itafanaje kuliokoa Bunge ili kuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni?
  7. View attachment 3602004
  8. Je, Bunge Litimize Wajibu Wake KikamiliIfu Ikiwemo Kutunga Sheria, Au Liendelee Kuwa "Rubber Stamp" ya Kupitishia Miswada ya Serikali Bila Kuhoji?
P

Ina maana tuna muhimili mmoja tu, hiyo mingine ni vivuli vya muhimili mkuu.
 
Nyerere aliwahi kutuasa juu ya Katiba hii ya mwaka 1977 lakini wengi hawakumuelewa.
Alituasa lakini hakuibadilisha sababu ilimnufaisha na aliacha makusudi kubadilisha Ili kukilinda chama chake cha Ccm.

Absolute power corrupts Absolutely...
 
Alituasa lakini hakuibadilisha sababu ilimnufaisha na aliacha makusudi kubadilisha Ili kukilinda chama chake cha Ccm.

Absolute power corrupts Absolutely...
Nyerere sio alotakiwa kubadilisha muundo wa Serikali ya JMT kwa sababu mageuzi yalikuja baada ya yeye kung'atuka. Badala ya Makamu wa rais kuendelea kuwa ndiye rais wa Zanzibar tukawa na rais wa Zanzibar, Zanzibar wakaandika Katiba yao kinzani na Katiba ya JMT. Ukazaliwa upya sisi Wazanzibar na wale Watanganyika!

Miiko na Maadili ya viongozi ikafutwa bila mfumo wa kudhibiti na kuwajibisha viongozi watakao kiuka Katiba. Ujio wa Vyama vingi ukazaa fitna na Uadui ambayo inatutesa mpaka leo.

Hatua zote hizi hazikuzingatia muundo wa Serikali kwa sababu huo ndio ulikuwa wakati wa Viongozi kutoka katika Umaskini na kujitajirisha. Kulizaa Ubwana viongozi kuitwa Waheshimiwa. Misingi ya Uongozi ikageuzwa kutoka Ujamaa kuhudumia Wananchi ukawa Biashara.

Matokeo yake huduma muhimu kama Maji, Afya na makazi viligeuzwa kuwa biashara na mpaka leo hii ni biashara kubwa ambayo tumeshindwa kuondokana na Ujinga, maradhi na Umaskini. Umimi umetamalaki kiasi kwamba sasa hivi tunaanza kujinasibisha na Dini, Kabila, Asili na Ukanda.

Naamini kabisa haya yote yametokana na marekebisho mengi ya Katiba ya Mwaka 1977 yalofanyika yalikuwa kwa faida ya Watawala badala ya kubadilisha mfumo wa Uongozi.

Na kama sikosei baada ya Mwalimu kunga'atuka, hotuba zake nyingi alizozitoa na zenye mvuto mpaka mpaka leo ni zile alozungumza wakati huo.
 
Katika Sura kama hii nadhani wameweka vema isipokuwa pale kwenye kumpunguzia rais Madaraka sijui abakie na wizara chache za serikali kusimamia. Tukimpunfuzia mamlaka yake tutayapeleka wapi? Hii itatuvuruga na kupata marais wengine pembeni wenye mamlaka ya juu.
Mkuu kumpunguzia Rais madaraka ni kuondoa mambo yasiyomhitaji. Kwa mfano, Rais anabaki na madaraka ya mambo ya Kitaifa, Wizara ya Ulinzi, Mambo ya Nje, Fedha, Wizara ya mambo ya ndani na taasisi zake.

Mengine kama Elimu, utamaduni, Kilimo, ushirika, maliasili n.k. yatashughulikiwa na serikali washirika
Unapaswa kuelewa dhana yakumpunguzi madaraka inakwenda sambamba na uundwaji wa serikali 3
Katika mfumo wa sasa haiwezekani kwasababu yasiyomhusu hayana pa kupelekwa

Sioni tatizo kwasababu hata sasa hivi tuna serikali 3. Ukiacha Wizara ya fedha, ulinzi , mambo ya ndani mengine yanayojadiliwa Dodoma ni ya Tanganyika yamevalishwa koti la Tanzania ili ku accomodate Wazanzibar.
Wabunge wa Zanzibar pale Dodoma wanapswa kukaa wiki 2 tu kwasababu 97% hayahusu

Kwasababu mambo yanayojadiliwa hayahusu ndio maana hoja zao huwa vituko kama yale ya YUDA.
Hawana kazi! wanapokea posho na mishahara tu.

Waziri Mkuu pale Bungeni anasimamia mambo ya Tanganyika, Zanzibar wana serikali na Bunge lao
Waziri Mkuu hana mamlaka na mambo ya Zanzibar

Tayari tuna serikali 3 ingawa tunajidanganya ni 2. Wananchi wanataka kurasimisha serikali 3 ili ya Tanganyika iwe wazi na iwe na mipango yake.

Tayari tuna serikali 3 ingawa tunajidanganya ni 2. Wananchi wanataka kurasimisha serikali 3 ili ya Tanganyika iwe wazi na iwe na mipango yake.
Naona zipo serikali mbili (Tanganyika na Zanzibar), ila hiyo serikali ya Tanganyika ndio imevikwa koti la muungano.

Naamini Ccm wanataka huu mfumo ubakie kama ulivyo maana umekaa zaidi kichama kuliko kitaifa.

JokaKuu zitto junior
 
Mkuu kumpunguzia Rais madaraka ni kuondoa mambo yasiyomhitaji. Kwa mfano, Rais anabaki na madaraka ya mambo ya Kitaifa, Wizara ya Ulinzi, Mambo ya Nje, Fedha, Wizara ya mambo ya ndani na taasisi zake.

Mengine kama Elimu, utamaduni, Kilimo, ushirika, maliasili n.k. yatashughulikiwa na serikali washirika
Unapaswa kuelewa dhana yakumpunguzi madaraka inakwenda sambamba na uundwaji wa serikali 3
Katika mfumo wa sasa haiwezekani kwasababu yasiyomhusu hayana pa kupelekwa

Sioni tatizo kwasababu hata sasa hivi tuna serikali 3. Ukiacha Wizara ya fedha, ulinzi , mambo ya ndani mengine yanayojadiliwa Dodoma ni ya Tanganyika yamevalishwa koti la Tanzania ili ku accomodate Wazanzibar.
Wabunge wa Zanzibar pale Dodoma wanapswa kukaa wiki 2 tu kwasababu 97% hayahusu

Kwasababu mambo yanayojadiliwa hayahusu ndio maana hoja zao huwa vituko kama yale ya YUDA.
Hawana kazi! wanapokea posho na mishahara tu.

Waziri Mkuu pale Bungeni anasimamia mambo ya Tanganyika, Zanzibar wana serikali na Bunge lao
Waziri Mkuu hana mamlaka na mambo ya Zanzibar

Tayari tuna serikali 3 ingawa tunajidanganya ni 2. Wananchi wanataka kurasimisha serikali 3 ili ya Tanganyika iwe wazi na iwe na mipango yake.
Hapana hapo siafiki mabadiliko haya na nadhani swala hili nimewahi kulizungumzia hapa wakati ule wa tume ya Katiba, kuhusiana na Mamlaka ya rais kupunguzwa.

Haihitaji kumpunguzia rais madaraka yake bali tupungu
ze mamlaka kwa kuunda mgawanyo wa mamlaka wa Serikali zetu kwa mujibu wa Katiba (Separation of Power) lengo haswa ni kudhibiti viongozi.

Unapoyaondoa madaraka ya rais na kuyapeleka kwenye Serikali zake ina maana unazaa marais wengine madikteta kwenye hizo Serikali ikiwa Bunge na Mahakama hazipo Huru. Kwanza tuvipe vyombo hivi meno badala ya kuendelea kulalamika.

Halafu, kuhusu Serikali 3, hiyo pia mimi siafiki kabisa kwa sababu ya GHARAMA ya kuendesha Serikali 3. Kumbuka kila Jimbo litatoa Wabunge wawili wa bunge la Muungano na Bunge la Serikali (State). Kama leo Bara ina Wabunge 314 basi tutakuwa na Wabunge 628 ambao wote watapokea Mishahara, posho na sijui magari ya thamani maana watu wenyewe ndio sisi hakuna Mbunge atakaye kubali kupokea sijui mil. 5 kwa mwezi.

Pili, watu wanadhani unapoondoa madaraka ya rais ndio njia sahihi lakini hawaelewi kwamba hata Marekani Federal Government bado ina wizara zote ndani yake isipokuwa mamlaka ya Sheria na uendeshaji ndio upo chini ya States. Kama Waikikwama kifedha ama any other emergency wanaomba msaada Serikali Kuu.

Kwa mfano, Nenda tazama Elimu na Afya utazikuta wizara hizo zipo Federal. Bila shaka unamkumbuka Dr. Fauci wakati wa Covid 19 huyu alikuwa Federal. Kwa hiyo tunakuwa na wizara nyingi upande wa Janhuri na upande wa nchi. Itazame vizuri Serikali ya Zanzibar leo ni mfano upo mbele yetu lakini hatuuoni.

Kwa hiyo, huwezi kumuondolea rais madaraka ya upande wa Elimu na Afya wakati rais anagombea kufuta Ujinga na Maradhi, anagombea kufuta rushwa na mikataba mibovu! Kutakuwa hakuna sababu kabisa ya Kumchagua rais Tanzania ikiwa hana madaraka hayo.

Nitaendelea kufafanua ikibidi.

Maasalaam
 
Na

naunga mkono hoja
 
Mbona warioba alipropose wabunge 75 nchi nzima. 50 bara, 25 zanzibar. Hakutokuwa na viti maalum.

Ikumbukwe kwa sasa zanzibar wana baraza la wawakilishi ila bado linapeleka wabunge dodoma. So kwa zanzibar dual system ni sawq ila ikija Tanganyika ndio issue ya gharama inatajwa!!
 
Kwa kuongezea, sehemu pekee inayotakiwa kudhibitiwa katika madaraka ya rais (Executive) ni teuzi zake zote lazima zifanyiwe Usaili iwe Mawaziri, Majaji, Mkuu wa Polisi, Majeshi, Usalama na hata Tume ya Uchaguzi na CAG wote lazima wawe na sifa za kushika madaraka hayo.

Tukiwa na Baraza Wazee Bungeni walokunywa maji ya Uhuru, wenye Hekima na Busara wawakilishi both Bara na Viziwani. Hapatakuwa na ujinga unaonendelea
 
Haswaaa, lakini nako tatizo lao Kiutawala liko wapi haswa? maana Ruto na Trump kama wanafanana vile! Je, ni support ya Wananchi, The Elites au inatoka kwenye mihimili yenyewe (Lobbyist na Rushwa)
Mahakama ipo huru katiba yao imeweka mpaka namna ya kupata funds za mahakama...
 
Back
Top Bottom