Habib Mchange: ACT-Wazalendo tutaidhibiti vikali CHADEMA

Habib Mchange: ACT-Wazalendo tutaidhibiti vikali CHADEMA

Chadema tunafanya mikutano kila siku nchi nzima, hiki chama ni taasisi hakitegemei mtu mmoja sasa inamaana hawataki Chadema tufanye kazi zetu kwasababu wao wanafanya mkutano mwembe yanga?
 
Siasa za Tanzania ni rahisi sana aisee. Hivi hata Mchange naye ni mwanasiasa tegemezi ndani ya ACT-Wazalendo?? Huyu dogo aliongopa kuwa amezaliwa Kibaha Vijijini na akafurushwa. Akagombea Kibaha Mjini na akafanya mambo ya ajabu sana wakati ule akiwa CHADEMA. Yuko njiani kugombea tena Kibaha Mjini kwa tiketi ya ACT-Wazalendo. Karibu Kibaha Mchange ukumbushwe usaliti wako wa 2010

Kumbe yuko vizuri kama CHADEMA imewahi kumpa ridha ya kugombea jimbo kwa kumuona anafaa hapana shaka hili ni jembe. Sema mtu akishama kutoka CHADEMA hamkosi kumtupia maneno na sifa mbaya.
 
Last edited by a moderator:
Du ukwel daima ujitenga na uongo,huyu jamaa kapotea kisiasa kumbe naye kamkimbilia zitto kpnd kile kashndwa uenyekiti wa bavicha sababu ya mahusiano yake na zitto alipinga kama ni uongo,leo hi ni act naye! umepotea ndugu najua upo vzur kpolitics lakn uliko kimbilia ni her ungeenda ccm!
 
ACT ni sawa na mtu aliyejifunika shuka akajamba akidhani anawakomoa wengine kumbe anajikomoa mwenyewe.
Aibu sana kuwa na watu wenye fikra na maandishi kama haya. That why ccm itaendelea kuwatandika. Unakodi walevi waizomee ACT wakati ccm mmeshindwa kuwatoa. Very shame.
 
Kama alivyo saed kubenea kuwa think tanker wa cdm! Cmaajabu hayo!!
Naona ACT wanatafuta kick ya kutaka kufanikiwa kisiasa kwa kutumia mgongo wa CHADEMA.
Watu kama Habib Mchange ndio wamemuharibu kabisa Zitto.
Watu wanaomzunguka Zitto ni watu wenye kujaa Ujinga, Unafiki na Sifa mbaya.
Huyu Habib Mchange ndio miongoni mwa Think tanker wa
ACT, sasa hapo unategemea nini?
 
Duh! Pure naked hatred au ni nini? Mwembeyanga Temeke mpaka Kawe Kinondoni?
 
kinachommaliza zzk ni kufanya siasa kama za mrema
 
Katibu wa mipango na mikakati wa ACT-Wazalendo Habib Mchange amekionya CHADEMA kwamba huenda kikafutika katika historia endapo kama wataendelea kuifuatafuata ACT-Wazalendo.

Akizungumza na wanahabari makao makuu DSM Mchange amesema CHADEMA wamekuwa wakikodi watu kwenda kuwazomea kila wanakopita na akaonya chama hicho kikiendelea atawafanyia kitu kibaya sana ambacho hawatasahau katika maisha yao.

Mchange amesema Jumamosi kutakuwa na mkutano mkubwa wa Hadhara Mwembeyanga utakaoongozwa na Kiongozi Mkuu Zitto Kabwe na kuwaonya CHADEMA wakae mbali na mkutano huo.

Pia Mchange amesema katika kuonyesha CHADEMA inawafuatafuata baada wao kuitisha mkutano Mwembeyanga CHADEMA nao wameitisha mkutano Kawe ili kuikomoa ACT-Wazalendo.

Akili ya Kware!
 
Kila mtu ni jinias lkn kama utamjaji mmasai katika uwezo wa kuogelea baharini ataishi maisha yake kujiona mjinga na asie na akili.
 
mchange hana uwezo wa kibabe , kisheri wala kifedha wa kukoromea cdm , kwanza atueleze kwanini aliwadhulumu wale viongozi wa kusini ile mil 7 ya usaliti , tunawashukuru viongozi wa cdm kwa utu wenu wa kuwalipia nauli watu wale ya kurudi kwao baada kudhulumiwa .
 
Mbona huwa wanakataa kuwa huwa hawazomiwi,watu wanaoandaliwa na CHADEMA kuwazomea wanatoka wapi tena wakati hawajawahi kuzomewa?.
USALITI NI LAANA MBAYA SANA ! vijana wanajichanganya wenyewe kudadeki .
 
Hivi nyie mkipitia kipindi km cha chadema mtasalimika nyie?
Kujenga chama sio mchezo. Kundi la wasaliti wananunulika kila siku
 
Kama CHADEMA kiliundwa kukipoteza chama tawala CCM kwani ajabu gani kwa ACT kukipoteza CHADEMA? Ikumbukwe wazi kuwa CDM ni wale wote waliofukuzwa au kuhama CCM baada ya kwenda kinyume na chama,pia ikumbukwe ACT ni wengi wao waliofukuzwa au kutoka CHADEMA,hakuna cha ajabu kwa kila mmoja kukipiga vita chama alichotoka,Sasa mnanuna nini CHADEMA mkifanyiwa na ACT??au mtenda akitendewa??

Kwa akili kama hizi zako maendeleo Tanzania itakuwa ndoto
 
Siasa za Tanzania ni rahisi sana aisee. Hivi hata Mchange naye ni mwanasiasa tegemezi ndani ya ACT-Wazalendo?? Huyu dogo aliongopa kuwa amezaliwa Kibaha Vijijini na akafurushwa. Akagombea Kibaha Mjini na akafanya mambo ya ajabu sana wakati ule akiwa CHADEMA. Yuko njiani kugombea tena Kibaha Mjini kwa tiketi ya ACT-Wazalendo. Karibu Kibaha Mchange ukumbushwe usaliti wako wa 2010
Naona unaitukana Chadema angalia usifukuze huyu unayemponda leo alikuwa mgombea wenu uchaguzi uliyopita.
 
Last edited by a moderator:
Ana hasira, mkutano wake juzi na act yao ulionyesha wazi kwamba hana nafasi kwa wananchi wa kibaha kwenye upande wa ubunge
 
Back
Top Bottom