Hilipendo
Senior Member
- Sep 13, 2011
- 188
- 97
Katibu wa mipango na mikakati wa ACT-Wazalendo Habib Mchange amekionya CHADEMA kwamba huenda kikafutika katika historia endapo kama wataendelea kuifuatafuata ACT-Wazalendo.
Akizungumza na wanahabari makao makuu DSM Mchange amesema CHADEMA wamekuwa wakikodi watu kwenda kuwazomea kila wanakopita na akaonya chama hicho kikiendelea atawafanyia kitu kibaya sana ambacho hawatasahau katika maisha yao.
Mchange amesema Jumamosi kutakuwa na mkutano mkubwa wa Hadhara Mwembeyanga utakaoongozwa na Kiongozi Mkuu Zitto Kabwe na kuwaonya CHADEMA wakae mbali na mkutano huo.
Pia Mchange amesema katika kuonyesha CHADEMA inawafuatafuata baada wao kuitisha mkutano Mwembeyanga CHADEMA nao wameitisha mkutano Kawe ili kuikomoa ACT-Wazalendo.