Habib Mchange: ACT-Wazalendo tutaidhibiti vikali CHADEMA

Habib Mchange: ACT-Wazalendo tutaidhibiti vikali CHADEMA

Huyu kachoka kifikra, kuna watu watapata shida sana kuwajibu wajukuu zao watakapoulizwa wamelifanyia nini taifa hili majibu ya walikuwa vibaraka wa kuwamaliza wapinzani wa kweli hayavumiliki.
 
Mbona huwa wanakataa kuwa huwa hawazomiwi,watu wanaoandaliwa na CHADEMA kuwazomea wanatoka wapi tena wakati hawajawahi kuzomewa?.

Hapo sasa, a very good question!! Wanasema chama chao kinapendwa sana na hawazomewagi, sasa imekuwa tena wanazomewa!! Ujue hawa walijazana ujinga kuwa zitto kabwe anapendwa sana na watu wengi ndani ya Chadema, kiasi kwamba akihama nusu ya watu au robo tatu watamfuata, sasa anaona zero badala yake anazomewa. Wamechanganyikiwa, ndo tatizo la chama cha mtu mmoja
 
huyu amezungumza ukweli kwamba ACT ni chama cha kupambana na cdm. nimeamini act ni tawi la ccm. kwa siasa hizi act haitafika mbali kamwe...
 
ni mara nyingi wamekuwa wakikana kuzomewa. leo tumeujuwa ukweli.
 
Wakiambiwa ACT ni mpini wa CCM kuumaliza upinzani nchini, wanakasirika! Wanaudhibitisho gani wa wanaowazomea ni wafuasi wa Chadema na si wa NCCR Mageuzi, CCM ama chama kingine chochote ama ni wafuasi wa chama hicho cha ACT wanaounga mkono ACT Tanzania badala ya ACT Wazalendo!?
 
Nilishawahi kuuliza na nauliza tena kuhusu hiki chama kilichoanzishwa kwa lengo la kuibomoa CHADEMA,

Je, mpaka sasa kimefanikiwa kuibomoa CHADEMA?
 
ACT ya Membe.......Zana Za Kilimo ni kama kifutia matako tu hapo..!!
 
Ukweli sidhani kama wanasiasa wako kwa ajili ya kuleta maendeleo ila wako kwa ajili ya kutafuta maisha.Ndio hawa hawa walisema chadema ndio chama kitakacholeta maendeleo na ndio hao hao wanasema watu waondoke waende ACT.ila politics is a dirty game.
 
Kuibomoa kwa maana ipi? Hebu fafanua kidogo.
 
WAZALENDO Kamwe hawanampango wa kibomoa chama chochote, chama kitajibomoa chenyewe na si kuihusisha ACT, karne ya sasa ukiendekeza siasa za MUNGU MTU jua ipo siku utakibomoa chama usitafute mchawi nani wakati chama uhai wake ni UZEZETA WA WAFUASI. TEAM WAZALENDO
 
Mwenye Uwezo Wa Kuibomoa Chadema Ni Mungu Pekeake Wala Si Mwanadam Awaye Yote
 
Nilishawahi kuuliza na nauliza tena kuhusu hiki chama kilichoanzishwa kwa lengo la kuibomoa CHADEMA,

Je, mpaka sasa kimefanikiwa kuibomoa CHADEMA?

Je, wewe umeonaje wameweza?

Jana nimesikia kwenye vyombo vya habari wakisema walikatwa ccm hawaitajiki ACT kwa sababu hawataki matapishi. Ila ni baada ya EDDO kuonesha wazi hawezi kuhamia ACT coz hakijiwezi na hakina mtajii wa watu. Kipo hoi na tegemeo lao kubwa ilikua wanaohama ccm! kwa hiyo ACT sio tatizo kwa CDM ni kama kulinganisha kifo na usingizi
 
Ukweli sidhani kama wanasiasa wako kwa ajili ya kuleta maendeleo ila wako kwa ajili ya kutafuta maisha.Ndio hawa hawa walisema chadema ndio chama kitakacholeta maendeleo na ndio hao hao wanasema watu waondoke waende ACT.ila politics is a dirty game.
Wakipatikana watu wakuichambua siasa na vyama kama wewe mtakuwa na wafuasi wenye malengo na si haya mengine yenyewe kufuata mkumbo tu
 
Nilishawahi kuuliza na nauliza tena kuhusu hiki chama kilichoanzishwa kwa lengo la kuibomoa CHADEMA,

Je, mpaka sasa kimefanikiwa kuibomoa CHADEMA?

Wamefanikiwa kuibomoa CHADEMA, manake wamesababisha wanachama wa CHADEMA kuongezeka kwa kiwango cha kutisha, kutoka wananchama Milioni 5 hadi zaidi ya Milioni 8 hivi sasa. Kama tafsiri ya kubomoa ni hiyo basi wamefanikiwa hahaha...

Ukiona ACT mahali ujue umekutana na CCM. Hakuna tofauti ya ACT na CCM. Ni chama cha hovyo kimejaa wasaliti watupu!!
 
Back
Top Bottom