Tetesi: Habari za hivi punde: Kinana ameandika barua ya kujiuzulu

respect wa boda

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
4,538
2,000
Nadhani Mzee umri umeenda sana,

Ni muda muafaka kupumzika kiungwana na kistaarabu. Kwa kuzingatia zama hizi, nadhani Kinana anastaafu bila kinyongo. Nisiwe mnafki, Busara za Kinana zimesaidia kwa namna fulani kutufikisha hapa tulipo kama Taifa.

Niko kipepeni hapa kuangalia safu ya kukabidhi Nchi kwa Wapinzani itayoundwa na Bwana mkubwa hivi karibuni.

Imagine, Hivi ile ccm ya Mukama, ingekuwa wapi hivi sasa.......

BACK TANGANYIKA
 

zionale

Member
Oct 13, 2012
25
75
Licha ya makandokando yasiyothibitishwa, bado amekuwa mtu muhimu sana kwa chama na taifa na kwa kipindi cha miaka zaidi ya 15. nadhani ni wakati muafaka kupumzika ili safu mpya iandaliwe na wengine nao waoneshe uwezo wao. nchi hii ina utajiri sana wa wanasiasa wa aina zote.
 

Maghayo

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
6,994
2,000
Huu ni uzushi toka mtaa wa ufipa
kama lizaboni kapinga hii habari ujue labda ni uongo. Kwasabab huyu jamaa ni hatari mwanzon nilizan msela mwenzetu. Ila sasa hiv niko naye chonjo na sasa hivi anavyoposti hivi anaposti kutoka kijitonyama
 
  • Thanks
Reactions: nao

ISIS

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
92,306
2,000
Safi mzee dentist......ila huku Arusha hatukutaki ishia huko dodoma,Tembo wetu ukija hawatakuwa salama
Kwa hilo nakuunga mkono. ..hata hofu ya MWENYE ENZI MUNGU hawana. ..wao ni kuua tu tembo zetu....hicho kitendo nakilaani kwa laana zote!
 

martin mwamlima

Senior Member
Oct 31, 2013
148
225
Nikiwa ndiyo nakimalizia kukisikilizia kipindi cha morning magic, nimesikia wakitangaza kwa ufupi mnoo kuwa
Kinana ameandika barua ya kujiuzulu.

Mwenye taarifa zaidi.... Kipi kilichopelekea mpk kuomba kujiuzulu..
Karibu tujadili.

ndio utaratibu wa chama. Katibu mkuu anaandika barua ya kujiudhuru kwa niamba ya viongozi wote ili kumpa mwenyekiti mpya kupendekeza atakaofanya nao kazi. NI KWAHERI TU NA SIO KWASHARI.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom