Mtanzania,
Mkuu wangu kulingana na habari hiyo, mwenye Guest na hao waliowaliwiti watoto wa shule ya msingi wote wana makosa!..
Samwel Nijuavyo aliwajengea au ana mpango wa kujenga shule maana kwenye fundraising hata mie niliwachangieni tena si kitoto! Au hiyo shule nayo ni hewa?[/quote said:Womenofsubstance,
Usiwasikilize sana hawa vijana. Asante kwa kuchangia, naamini pesa zako zilifikishwa na kutumiwa vizuri.
Kuna shule nyingi sana zimejengwa Kyela kuanzia 2006 kuitikia wito wa Lowassa. Pia DC Mashimba kafanya kazi kubwa sana kwenye ujenzi wa hizo shule. Yeye ndiye alikuwa mfuatiliaji kwasababu mbunge muda mwingi hayuko Kyela.
Naamini viongozi wote akiwemo mbunge walishirikiana pamoja na wananchi kutimiza hilo lengo.
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu wangu sheria inaifahamu au unazungumza kwa kufikiria..
Kuna tofauti kubwa kati ya nyumba ya kupangisha na Guest house... Hii ni sehemu ya biashara na moja ya masharti yake ni pamoja na kulinda watoto.. Huyu Diwani hakupangisha jengo hilo kwa mtu yeyote ni biahsra yake na katika biashara hiyo ndipo kumefanyika matusi hayo.
Hapa kwetu Club zikilia risasi tu na akafa mtu club hufungiwa.. aliyeua sii mwenye Club, Club ikijulikana kunauzwa Unga hata kama mwenye Club hahusiki itafungwa na wahusika watapelekwa jela acha mbali mtu huyo awe kiongozi wa wananchi hao hao anaotakiwa kuwalinda.
Mkuu Mkandara,
Madai ni kwamba kuna wanafunzi walifanyiwa hivyo vitendo kwenye guest house ambayo mmiliki wake ndiye diwani wa Kyela mjini.
Sasa hapo mwenye kosa ni mmiliki wa guest au hao waliofanya kosa na kukamatwa?
Huyo jamaa ni Mkinga na pia haelewani na mheshimiwa. Ghafla kuna vita kibao juu yake na madai kama haya ya akina Nsesi. Juzi kwenye kura za Albino, wametuma vijana wao wakaandika jina la huyo diwani kama ni jambazi. Kuna maneno kibao ya kibaguzi yanaendeshwa. Ukienda kuangalia, huyo diwani anajituma kwenye maendeleo kuliko hata madiwani wengine. Lakini kwasababu sio Mnyakyusa tayari maneno, kwani waliomchagua mbona walijua hilo?
Ni siasa za Kyela tu na ujinga wa watu kutumia elimu zao, magazeti yao kuendeleza chuki badala ya umoja.
Tulikuwa na DC wa maana sana pale Kyela kwa ufuatiliaji na kafanya kazi kubwa kweli kwenye ujenzi wa shule. Kawabana watendaji, kafuatilia maendeleo lakini nasikia majungu yamepigwa mpaka jamaa kaondolewa. Nsesi alikuja hapa akaandika kahongwa gari na Kiwira Coal Mine, hivi hata anaijua Kiwira? Wafanyakazi wa Kiwira Coal Mine wako hoi mno, hata hizo pesa za kumnunulia gari mkuu wa wilaya watatoa wapi? Watu wanashindwa hata kutoa 70,000 ya kulipia ada za watoto wao kwa mwaka, kweli watamnunulia gari DC?
Kule kwetu nafikiri ifike mahali tupigane viboko, ujinga umekuwa mwingi sana.
Hizo nyumba zenyewe ni zile sijui hata uziitaje yaani control hakuna. Kama nchi yetu inafuata sheria nyumba kama hizo ni kufunga kabisa. Ziko nyingi kweli Kyela mjini, ni takataka tu. Kwasababu ya biashara ya Malawi basi hata nyumba za hovyo zinapata wateja.
Mkuu, una introduce a very interesting element katika suala zima la uandishi na michango yetu wanaJF. Hivi asiye mteule wa Dr. Mwakyembe anatakiwa aandike vipi, na wewe mwenzetu ni mteule wa nani? Fataki
Bahati nzuri nimeishi Kyela muda mrefu na nimeoa huku. Nazijua sana siasa za Kyela na Mkoa wa Mbeya. Mwakyembe kajitahidi kufanya yale aliyoyaweza ila hizi kelele mnazoziskia ni za wale wale walioko katika payroll ya mafisadi. Endapo wataendelea tutawafichua kwa kutoa vielelezo vya vikao vyao na namna wanavyo network ili kumhujumu Mwakyembe.
Engineer,Mtanzania,ntambaswala,
..majuzi si nilisikia Mwakyembe kawaita wana Kyela kuchangia mfuko wa elimu?
..lakini pia ni vizuri wananchi wa Kyela wakachambua mchango wake ktk kulihudumia jimbo lake.
Mi natokea Kyela nafanya kazi Karatu.Mbunge wetu Mwakyembe hajafanya chochote cha maana na baada ya kuona uchaguzi unakaribia unatapa tapa.Ufisadi ni swala la kitaifa zaidi na tulitaka mbunge wetu ashugulikie matatizo yetu kwa muda mwingi na kupambana na ufisadi 'in his spare time'.Mimi sio mpenzi wa chadema lakini namsifu Dr.Slaa ambaye yuko karibu sana na wapiga kura wake na utamuona jimboni hata siku za mwisho wa wiki bunge likiwa kwenye vikao.
Jamaa ni msanii wa kutupwa. Juzi kaitisha mkutano wa vijana wanaochangishana wanaitwa vijana wa Vikoba. Akaanza kuwaambia atafungua bank, atamwita Mengi na Mengi ana uwezo hata wa kuchangia milioni 100.
Baadaye akawaita wale washirika wake pale mjini na kuwauliza waelezee wanachokijua. Wakaanza kusema mipango ndio iko hatua za mwisho na ujinga mwingine mwingi tu.
Mtu unabaki kujiuliza, hawa ndio wasomi wa nchi hii, kwanini wanakuwa wahaba wa ukweli?
DC aliyeondoka ndiye alikuwa na wazo la kuunda bank ya wilaya lakini hakuungwa mkono. Sasa mheshimiwa anajifanya hilo ndilo lengo lake.
Kama atatekeleza ni vizuri, ingawaje kwa jinsi wanavyoongea, unajua ni usanii tu kwa ajili ya mwaka kesho.