Habari njema kwetu Tanzania Prisons kuelekea mechi ya leo dhidi ya Yanga Sc

ninosi

Senior Member
Jun 30, 2022
151
333
Kuelekea mechi ya leo kati ya Yanga SC na Tanzania Prisons.. Msemaji wa Tanzania Prisons anena haya wakati akihojiwa na kituo kimoja cha redio:-

Mtangazaji: Kuelekea mechi ya leo, je katika timu yenu kuna majeruhi yoyote?

Msemaji: Benjamini Asukile yupo salama.. Pia wachezaji wenzake wote wako salama.

Hii ni habari njema sana kwetu sisi mashabiki lia lia wa Tanzania Prisons.

Kila la heri Wajelajela
 
Mpira hauchezwi mdomoni, subiri dakika 90 watapigika na kuchakaa.

Mimi ni Simba lialia ila hao Prisons hawana timu ya kuizuia Yanga.

Mkuu hii Yanga ambayo mpaka kipa afanye makosa ndo ishinde una imani nayo?

REFERENCE: Mechi dhidi ya KMC.
 
Mkuu hii Yanga ambayo mpaka kipa afanye makosa ndo ishinde una imani nayo?

REFERENCE: Mechi dhidi ya KMC.
Mbona Simba haijawafunga Yanga kwa miaka kadhaa?, kwa sasa Yanga ndio timu bora hapa nchini.
Binafsi Simba yangu siioni ikichukua chochote msimu huu vinginevyo tuliibe kombe la Azam Federation cup.
 
Prisons ni tawi la Utopolo hamna jipya.Wanafadhiliwa na tawi la GSM.
 
Mbona Simba haijawafunga Yanga kwa miaka kadhaa?, kwa sasa Yanga ndio timu bora hapa nchini.
Binafsi Simba yangu siioni ikichukua chochote msimu huu vinginevyo tuliibe kombe la Azam Federation cup.

Yanga mawazo yao yote yapo mechi ya week ijayo katika michuano ya loosers. Hivyo leo tegemea kuwaona kina Ambundo, Mauya, Farid n.k ambao mbele ya kina Asukile ambao hawana cha kupoteza lazima watwangwe VIRUNGU tu.
 
Prisons ni tawi la Utopolo hamna jipya.Wanafadhiliwa na tawi la GSM.

Mkuu Tanzania Prisons ni timu inayomilikiwa na SERIKALI tofauti na Toto Africa au Singida Big Stars. Huyo GSM ana uwezo wa kuihonga SERIKALI?
 
Hii mechi Yanga atashinda bila shida yeyote Prison hawezi kuwazuia hata wakihaidiwa nyumba na usafiri kila mchezaji.
NB.Mimi ni mnyama na nilishasema sitabishana mpira na shabiki ambaye timu yake haishiriki Super League, period
 
Back
Top Bottom