Habari njema kwa wenye matatizo ya usikivu hafifu

mvuv

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
2,758
2,000
Kama una upungufu wa kusikia au unamjua ndugu, jamaa au rafiki yako mwenye upungufu wa kusikia, tafadhali mjulishe kuwa chama cha kuhudumia viziwi Tanzania kitatoa vifaa vya kusaidia kusikia bure kabisa bila malipo yoyote, jumatano ya tar.19 June 2019 katika mji wa Dodoma.
FB_IMG_1560335550327.jpeg
 

mwanamimi

Senior Member
Oct 30, 2017
164
225
Mwanza ilikuwa jumapili na jumatatu, kifaa kinaitwa shime sikio au aering .aids,Kazi yake ni kukusaidia kunasa mawimbi ya sauti na kuyasafisha kwenye sikio,ili mtu asikie vizuri
 

MLUGURU

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
1,777
2,000
Vifaa ni bure ila lakini mpaka upimwe kwanza kujua baki yako ya usikivu ndio itapendekezwa upewe kifaa cha uwezo gani.

Wananchi hatuna budi kuunga juhudi kama hizi hususani kwa ndugu zetu ambao wana uhitaji (walemavu) kwani changamoto kama hizi zinawakwamisha mno kwenye maendeleo yao ya kimaisha hasa ya kielimu.
 

mvuv

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
2,758
2,000
Mwanza ilikuwa jumapili na jumatatu, kifaa kinaitwa shime sikio au aering .aids,Kazi yake ni kukusaidia kunasa mawimbi ya sauti na kuyasafisha kwenye sikio,ili mtu asikie vizuri
Umekipata?
 

mvuv

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
2,758
2,000
Mimi walinipa mwaka 2012.nilikosea kwenye kuweka tarehe mwanza ni jumapili kwa wasio wanafunzi na jumatatu ni kwa wanafunzi tu,watakuwa shule ya msingi nyanza kuanzia saa12asubuhi
Vip kimekusaidia?
Unawashauri na wengine wachukue, na je ukikivua hali inakuaje.?

Mpauko
 

mwanamimi

Senior Member
Oct 30, 2017
164
225
Mki
Vip kimekusaidia?
Unawashauri na wengine wachukue, na je ukikivua hali inakuaje.?

Mpauko
[/QUOTEkiminisaidia kiasi,ila tatizo limekuwa kubwa kwangu, katika tatizo la kutokusikia limegawanyika katika makundi matatu,kundi la kwanza ni wale ambao hawasikii kabisa,hawa Hata hakiwa na machine hizo tatizo halitapona,kundi la pili hawa sikio halina uwezo wa kuvuta mawimbi ya sauti hivyo kumfanya mtu asisikie vizuri ,huyu akipata machine tatizo lake linatibika kabisa,kundi la mwisho hawa wanauwezo wa kusikia sauti ila kuelewa maana ya sauti hiyo ndio shida,hii inasababishwa na mishipa ya fahamu kucheza,tiba ya hili tatizo ni kufanya upasuaji na kuwekewa machine maalimu (inaitwa sound booster) ambayo itawekwa kwenye sikio na nnje ya sikio na mgonjwa atapona kabisa. Kuhusu machine nashauli watu waende kuchukua kwani hapo watapimwa kwanza hivyo kufahamu tatizo lake liko kwenye aina ipi, pili kuhusu machine ukiitoa unakuwa kama kawaida tu ,lakini pia kama mtu tatizo lake ni LA aina ya tatu asitumie machine maana ataongeza tatizo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom