Tatizo la Usikivu Hafifu Tanzania

T Kaiza-Boshe

Member
May 27, 2013
20
39
Usikivu hafifu ni tatizo kubwa na linalokua Tanzania; lakini linaweza kupungua kama mamlaka husika zikitimiza wajibu wao kisheria kwa dhati.

Naanza na mfano mdogo wa kuonesha ukubwa wa tatizo. Kwa mujibu wa Mwongozo wa Kitaifa wa Udhibiti wa Kelele na Mitetemo wa 2022, utafiti wa 2019 wa Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili (MUHAS), kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma katika viwanda vya nguo viliyopo Dodoma, walibaini kuwa zaidi ya asilimia 58 ya wafanyakazi wamepoteza usikivu.

Uzi huu ni mchango wangu wa mawazo, taarifa, uzoefu, na maoni kuhusu kukabili usikivu hafifu, hususan utokanao na kelele; kwa nia ya kubadilishana uzoefu na taarifa baina ya waathirika wa hali hiyo, kutiana moyo, na pia kupendekeza suluhu kwa mamlaka husika.

Uzi huu huu unafuatia post ya mwana-Facebook aliyezungumzia kadhia iliyomkumba kwenye daladala kutokana na tatizo hilo.

Tatizo la usikivu hafifu laweza kumkumba mtu yeyote, na wakati wowote; kutokana na mazingira ya kelele, madhara ya dawa (medication side-effects), na visababishi vinginevyo.

Hapa naomba ieleweke kuwa nazungumza kama mtaalamu wa mazingira na muathirika; na si kama daktari.

Natamani madaktari wa ENT (masikio, pua, na koo), ama public health (afya ya jamii) watoe mchango wao kitaaluma kuhusu tatizo hili.

Tofauti na uziwi, uhafifu wa usikivu hauko bayana, na inachukuwa muda kudhihirika kuwa sasa ni tatizo. Na kama kisababishi kinaendelea, hali hii inaweza kupelekea mtu kuwa kiziwi.

Tatizo la usikivu hafifu lina changamoto kadhaa, kutegemea na aina ya tatizo lenyewe na jamii inayomzunguka muathirika.

Wataalamu wanaweza kutusaidia kuainisha aina mbalimbali za usikivu hafifu na visababishi.

Kwa hapa nitazungumzia yaliyonikumba mimi, sababu, adha zake na safari ya kupona; kwa vile ndiyo ninayoyafahamu zaidi. Lakini pia ni aina ya usikivu hafifu inayoongezeka kwenye jamii yetu kwa kasi kutokana na visababishi kuongezeka.

Na pia ni aina ya usikivu hafifu inayoweza kupunguzwa; kama siyo kukomeshwa kabisa.

TATIZO LENYEWE. Uhafifu wa kusikia ulianza zaidi ya miaka 15 iliyopita. Nilitambua nina tatizo hilo ilipofikia kutoelewa kinachohubiriwa kanisani, ama hotuba, japo nilikuwa nasikia sauti.

Mwanzoni nilidhani ni mwangwi kwenye kanisa moja, na nikajiridhisha kuwa ni mazingira ya kifizikia kutokana na jengo lilivyo ndani (acoustics), nikihisi kuta zilikuwa zinaakisi sauti kwa viwango tofautitofauti! Nilipoona hali inakuwa ileile hata kwenye majengo yasiyokuwa na kuta zenye nakshi, nikajua kuwa tatizo ni langu, na si la jengo.

Baadaye niligundua kuwa kama muongeaji haongei kwa kasi, na kama hakuna sauti nyingine karibu, niliweza kusikiasikia kiasi.

Kitu kingine nilichogundua ni kwamba nikiwa mahali penye sauti kutoka pande kadhaa, au sauti mchanganyiko, inakuwa vigumu kumsikia ninayejaribu kumsikiliza. Kwa lugha nyingine, masikio yanashindwa kuchanganua/kuchuja.

Aidha tatizo lilithibitika kitaalamu katika hospitali za Regency na Aga Khan na kushauriwa kutumia visaidizi vya kusikia (hearing aids).

Wakati natafuta tiba niliendelea kufanya "uwanaharakati" dhidi ya kelele, kukwepa sehemu za kelele na kutumia hear plugs dhidi ya kelele za kanisa jirani ambalo ndilo naamini ni chimbuko la tatizo langu.

Kanisa hili limajengwa kwenye kiwanja kidogo cha makazi, likiwa na umbali ndani ya mita 20 kutoka kwangu, na ukuta wa kanisa ni wa matundu kama uonekanavyo kwenye picha. Kibaya zaidi kanisa hilo walikuwa wanapiga magoma na kutumia spika zenye sauti kubwa kiasi cha kutetemesha kuta za nyumba yangu!

Isitoshe walikuwa na mikesha ya mara kwa mara, na wakati mwingine siku kadhaa mfululizo. Walipokuwa wakipiga hiyo miziki na makelele ya kutoa mapepo...mtu hulalii!

Japo kanisa hilo wamepunguza magoma na mikesha, bado wanapiga kelele mara kwa mara na ukuta wa kanisa bado una uwazi, na hawajajenga hata uzio! Hata kampeni ya NEMC ya mwezi Mei 2023 dhidi ya kelele haijawagusa!

SAFARI YA KUPONA: Inasemekana siyo jambo la kawaida kupoteza usikivu halafu ukaupata tena; na kwamba mara nyingi usikivu unaendelea kupungua hadi mtu anakuwa kiziwi, hasa kama kisababishi kinaendelea. Hii ina maana ukiondokana na kisababishi unaweza kuokoa usikivu kiasi fulani, kutegemea na kiwango cha kuathirika.

Siku hizi unaweza kuwekewa vifaa vya kukusaidia kusikia vizuri (hearing aids). Ni watu wachache sana wanaweza kumudu gharama.

HATA HIVYO NINA HABARI NJEMA KUTOKANA NA UZOEFU WA TATIZO LANGU. Inaelekea upo uwezekano wa kupata tena usikivu baada ya kuupoteza. Mimi baada ya kelele za kanisa kupungua na kutumia mbinu kadhaa kukwepa kelele, nimeweza kupata usikivu wa kutosha kusikia tena mahubiri na matangazo. Bado kidogo kuweza kumsikiliza mtu katikati ya kelele mchanganyiko.

RAI: Tafiti zinaonesha kuwa kuna watu wengi wenye matatizo ya usikivu hafifu yanayotokana na mazingira wanamoishi, ama kufanya kazi; na tatizo linaendelea kukua.

RAI YANGU ni kwamba NEMC, Halmashauri za miji/manispaa, na polisi wahimize sheria ya Mazingira kuhusu kelele bila upendeleo, ama ubaguzi; kwa maana kupoteza usikivu kunategemea ukubwa wa sauti bila kujali ni ya kanisa, baa, ama msikiti. Isitoshe, madhara ya usikivu yanaweza kumkumba yeyote anayekumbana na kisababishi, na hivyo yanaweza kuwakumba hata wenye mamlaka, ama ndugu na marafiki zao.

Theonestina Kaiza-Boshe
Email address:tkaiza@gmail.com

@NEMC
@Manispaa Kinondoni
@Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira
Mhe. Selemani Jaffo @Hardofhearing
#Usikivu Hafifu
Wizara ya Afya Tanzania
20230509_121357.jpg
20230509_121412.jpg
 
No photo description available.

Watu wazima nao wamo katika hatari ya kupoteza usikivu, Jielimishe sababu zinazoweza kupelekea hali hiyo





hearingAid-513885121-770x533-1-745x490-1.jpg

Tatizo la Masikio Kupoteza Usikivu,Chanzo,Dalili na Tiba yake.​

Tatizo la Kupoteza Usikivu kwa Mtu huweza kusababishwa na Sababu mbali mbali ikiwemo Uzee(Umri mkubwa) Pamoja na mtu kukaa kwenye mazingira ya makelele mengi makubwa kwa muda mrefu,

Sababu zingine kama vile masikio kuwa na Nta kupita kiasi(excessive earwax), pia huweza kupunguza usikivu wa masikio kwa Muda.

Wakati mwingine kulingana na chanzo cha tatizo hili huwa vigumu kwa masikio kurudisha usikivu wake kama Mwanzo,ila tiba ikasaidia tu kupunguza baadhi ya madhara,

Tatizo la Masikio Kupoteza Usikivu,Chanzo,Dalili na Tiba yake,


hearingAid-513885121-770x533-1-745x490-1.jpg

Tatizo la Masikio Kupoteza Usikivu,Chanzo,Dalili na Tiba yake,

Tatizo la Kupoteza Usikivu kwa Mtu huweza kusababishwa na Sababu mbali mbali ikiwemo Uzee(Umri mkubwa) Pamoja na mtu kukaa kwenye mazingira ya makelele mengi makubwa kwa muda mrefu,
Sababu zingine kama vile masikio kuwa na Nta kupita kiasi(excessive earwax), pia huweza kupunguza usikivu wa masikio kwa Muda.
Wakati mwingine kulingana na chanzo cha tatizo hili huwa vigumu kwa masikio kurudisha usikivu wake kama Mwanzo,ila tiba ikasaidia tu kupunguza baadhi ya madhara,

DALILI ZA TATIZO HILI LA MASIKIO KUPOTEZA USIKIVU WAKE NI PAMOJA NA;
– Mtu kuanza kupata shida ya kuelewa maneno kutoka kwa watu wengine hasa wakiongea mazingira yenye kelele au watu wengi
– Mtu kuanza kuongea kwa Sauti kubwa sana, bila kujua anaongea kwa sauti kubwa zaidi kwa wengine
– Kuomba mara kwa mara watu wengine kuongea taratibu ila kwa Sauti kubwa ili usikie vizuri
– Kuhitaji Sauti ya TV au REDIO kuwa Juu Zaidi ili usikie vizuri
– Kuhitaji Sauti ya Simu Kuwa Juu zaidi ili uweze kusikia vizuri wakati wa mazungumzo n.k

CHANZO CHA TATIZO HILI NI NINI?
mara nyingi tatizo la Masikio kupoteza usikivu wake hutokana na;

1. kuharibiwa kwa sehemu ya ndani ya sikio(inner ear), Na hii husababishwa na sababu mbali mbali kama vile; Uzee(umri mkubwa), mtu kukaa kwenye mazingira yenye makelele mengi makubwa kwa muda mrefu n.k,
Vitu hivi huweza kusababisha shida kwenye vinyweleo au Nerve cells kwenye eneo la cochlea,
Kumbuka vinyweleo hivi au Nerve cells hizi ndyo hutuma taarifa(sound signals) kwenda kwenye Ubongo, Hivo baada ya kuharibiwa haziwezi tena kufanya kazi vizuri hivo tatizo la upotevu wa usikivu hutokea.

2. Kujengwa kwa Nta taratibu ndani ya sikio(Earwax), Nta ikizidi huweza kuziba ear canal na kuzuia upitishwaji wa Mawimbi ya Sauti,
Hivo kuondoa uchafu huu(Nta/earwax) huweza kurudisha usikivu wa sikio lako.

3. Maambukizi ya Sikio, masikio kushambuliwa na vimelea mbali mbali vya magonjwa kama bacteria,fangasi,virusi n.k huweza kuleta tatizo la masikio kupoteza usikivu wake

4. Kuwa na shida ya kimaumbile kwenye mfupa eneo la sikio(abnormal bone growths), hii hutokea tangu ukiwa tumboni

5. Uwepo wa tatizo la Uvimbe ndani ya sikio, hasa sehemu ya nje au katikati ya sikio(outer or middle ear),
Hii pia huweza kusababisha masikio kupoteza usikivu wake.

6. Kupatwa na Tatizo la Kupasuka NGOMA ya SIKIO(Ruptured eardrum),
Makelele mengi,Sauti kubwa sana, mabadilikio ya gafla ya Presha,kuingiza kitu chenye ncha kali sikioni,maambukizi ya magonjwa n.k,
Vyote hivi huweza kusababisha tatizo la Ngoma ya Sikio kupasuka,kisha Mtu kupoteza Usikivu wake. N.K

VITU HIVI HUONGEZA HATARI YA KUPATA TATIZO LA KUPOTEZA USIKIVU MASIKIONI
– kuwa na Umri Mkubwa(Uzee)
– Kufanya kazi kwenye mazingira yenye makelele mengi na makubwa mara kwa mara,
Au kukaa kwenye mazingira yenye makelele zaidi kila mara,makelele ya mziki mkubwa, makelele ya milipuko mikubwa ya mabomu,vyuma kugongwa sana n.k
– Kuwa na Mtu mwenye tatizo hili ndani ya Familia yako(heredity)
– Matumizi ya baadhi ya Dawa hovio pasipo maelekezo ya kina kutoka kwa wataalam wa afya,mfano dawa kama; gentamicin, sildenafil (Viagra) au dawa jamii ya chemotherapy drugs, huweza kuharibu sehemu ya ndani ya sikio(inner ear).
Kutumia Dose kubwa za aspirin au dawa zingine za maumivu(pain relievers), Dawa za Malaria(antimalarial drugs) N.k
– Kupatwa na magonjwa ambayo husababisha Homa kali(high fever), kama vile meningitis n.k, huweza kuharibu eneo la cochlea ndani ya sikio.”

MATIBABU YA TATIZO HILI LA KUPOTEZA USIKIVU
Zipo tiba mbali mbali kulingana na chanzo husika,ila kwa Ujumla,tiba huweza kuhusisha;
– Kuondoa uchafu au Nta zinazoziba masikio(Removing wax blockage).
– Upasuaji kwa baadhi ya matatizo
– Kutumia Dawa za kutibu infections mbali mbali
– Kutumia vifaa vya kuongeza Usikivu(Hearing aids). N.K

Dawa ya asili ya kuweza kutibu Tatizo la kutosikia vizuri aka kupoteza usikivu ipo kwa mtu mwenye kutaka atanifuta kwa wakati wake ili niweze kumtibia apate kupona maradhii yake.
 
Back
Top Bottom