Gumzo: Makatibu CCM Singida Wasafirishwa na Mfanyabiashara kwenda Arusha kuandaa Mazingira ya Kuchukua Jimbo 2025

Dr Hamisi

New Member
Sep 30, 2022
1
2
Huko Mkoani Singida Makatibu wa CCM kata wilaya ya Mkalama inasemekana walisafirishwa na mfanya biashara ajulikanae kwa jina la Baraka Kwenda jijini Arusha kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi wa 2025, ikiwa ni moja ya ukiukwaji wa kanuni za uchaguzi ndani ya CCM pia ni ajabu kwa Uongozi wa CCM Mkoa wa Singida kulikalia kimya suala hilo ambalo wazi ni uvunjifu wa kanuni za uchaguzi na uteuzi za wagombea uongozi katika vyombo vya dola ndani ya CCM, Toleo la 2020.

Kudharau na kutokutii maagizo ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman kinana Tarehe 05 Septemba, 2023 siku ya jummanne katika jimbo la Hai huko Mkoani Kilimanjaro “nawaonya wana CCM wanaosaka nafasi za uongozi wakitafuta uungwaji mkono kwenye nafasi za Ubunge, Udiwani, Mwenyekiti wa Mtaa na kitongoji. Kabla ya kipindi cha uchaguzi kufika.

Kufuatia kauli hiyo, kinana aliziagiza kamati za siasa zikisaidiwa na zile za kanuni za maadili kufuatilia na kuchukua hatua kwa wote walioanza kuzunguka wakitafuta kuungwa mkono kwenye nafasi hizo, aliyasema hayo wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka miwili katika jimbo la Hai, ambayo iliwasilishwa na Mbunge wa jimbo hilo.

Mmoja wa waliokuwa katika msafara huo anasema walilipiwa nauli na walipofika walilazwa kwenye hotel ya kifahari na kufanya kikao na mfanya biashara huyo ikiwa ni moja ya maandalizi ya kuchukua kiti cha ubunge 2025 kuna mengi sana nyuma ya kikao hicho watu wameshakula mlungura tayari.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Pamoja na madiwani imeonekana wako nyuma ya Sakata hilo kwa kumkingia kifua Mfanya biashara huyo ambaye inaonekana kuwa na jeuri na majigambo kwa kuwa ashaaminishwa kuchukua kiti cha Ubunge 2025.

Inasemekana hata uongozi wa Mkoa wa singida Mwenyekiti wa CCM, Martha Mlata alikuwa na ziara yake huko wilaya ya mkalama ila alipofika hakukuta Makatibu wa CCM kata na alipouliza hakukuwa na majibu yanayoeleweka.

02 October 2023, Martha Mlata Mwenyekiti wa CCM Mkoa alikuwa na ziara yake hapo wilaya ya mkalama ila inasemekana ilizua taharuki kwa adhara hiyo kwa kuonekana Mwenyekiti akitetea suala hilo la makatibu kata kusafirishwa na kuomba liweze kufumbiwa macho na liachwe tu bila ufuatiliaji na uwajibishwaji kwa wahusika hao.

Mbunge wa Jimbo hilo la mkalama alionekana pembeni ya gari lake akifuta machozi hali inayoonesha kwamba hakupendezwa na ajenda za mkutano huo zilizotolewa na Mwenyekiti kuonesha kutokutilia maanani suala la makatibu kusafirishwa kwa maandalizi ya kuja kupinduliwa kwenye kiti chake.

Uongozi wa chama wa wilaya mpaka sasa umebaki njia panda hauna la kufanya dhidi ya ukiukwaji huo wa kanuni za maadili na uchaguzi kupitia kauli za mwenyekiti kuomba suala hilo liachwe juu juu bila kufanyiwa kazi.

Mbunge wa jimbo hilo hana Imani na makatibu wa CCM Kata kutokana na kauli alizosikika akiongea na mmoja wa viongozi ambaye ni mjumbe wa kamati ya siasa wilaya hio kupitia tukio hilo la makatibu kata kuonekana wakikata keki na mfanya biashara huko jijini Arusha.

Nimewafikishia ndugu zangu wana jamii forum huko singida hususani wanaotoka wilaya ya mkalama mtuambie bhanwa.
 
We wwacha wawasafirishe,wanaochagua wabunge sio makatibu wala wenyeviti ni wananchi tuu,wakikupiga ya uso,jimbo huna!
 
Back
Top Bottom