Guelle Faure: Uchaguzi ni kama ardhi yenye rutuba yenye kumea taarifa nyingi za uongo

JamiiCheck

Member
Nov 3, 2023
54
41
1708690373972.jpeg

Nyakati za Uchaguzi zimekuwa chanzo cha mlipuko wa habari nyingi potofu. Makundi mbalimbali yamekuwa yakipotosha kwa makusudi ili kuwadunisha au kuwanufaisha Wagombea na Vyama vya Siasa.

Mwandishi wa AFP, anawatahadharisha Wanahabari kuwa makini zaidi na habari na madai yanayozuka wakati huu ili kuepuka kupotosha jamii.

Akiwa anatoa utangulizi katika kozi AFP kuhusu Upotoshaji wa Kidijitali wakati wa uchaguzi Guelle Farure amesema:

Taarifa za uongo zinaweza kuwa na athari kubwa katika uchaguzi, yanayotokea mtandaoni yanaweza kufanyiwa kazi haraka katika mitaa, vituo vya kupigia kura na mara kwa mara yanaweza kuathiri mchakato wa kidemokrasia ulimwenguni kote.
Uchaguzi ni kama ardhi yenye rutuba yenye kumea taarifa nyingi za uongo. Waandishi wa habari wanapaswa kuwa waangalifu zaidi wanapochunguza vyanzo vya taarifa na kuthibitisha madai mbalimbali.
Je ni aina gani ya upotoshaji unayoifahamu ambayo hutokea wakati wa Uchaguzi.

Zaidi, tembelea Jukwaa la JamiiCheck kwa kubofya HAPA.
 
Back
Top Bottom