FAKE NEWS.jpg


Baada ya kukutana na taarifa yoyote unayoitilia shaka, kuna hatua kadhaa unaweza kuchukua ili kujiridhisha uhalali wa taarifa hiyo. Kuchukua hatua za haraka na kutoa habari sahihi ni muhimu ili kuzuia kuenea kwa habari feki au gushi.

Hizi ni baadhi ya hatua za kuchukua unapokutana na taarifa au habari unayohisi ni gushi au feki:

1. Usieneze Taarifa hiyo mpaka upate uhakika: Usiisambaze au kueneza taarifa hiyo kwa wengine kabla ya kuithibitisha kuwa ni taarifa sahihi ili kuzuia kusambaa kwa taarifa feki. Kusambaza taarifa/ habari unayoitilia shaka kunaweza kuchangia kusambaa kwa habari potofu

2. Tafuta Ukurasa wa Kukosoa au kuhakiki taarifa/habari: Kuna mashirika na tovuti zinazochambua na kukosoa habari feki, moja ya kurasa hizo ni Jukwaa hili la Jamiicheck.

3. Thibitisha habari, Ukishatilia shaka usisambaze kwanza: Ni muhimu kujaribu kuthibitisha habari kwa kutumia vyanzo vingine upate usahihi. Inaweza kuwa ni kosa la kutoelewa au kutafsiri vibaya ndio kumekupa mashaka na baada ya kutazama vyanzo vingine itakupa uhakika wa ukweli au uongo katika jambo hilo.

4. Wasiliana na chombo au mtoa taarifa husika: Ikiwa habari unayohisi ni feki inatoka kwa chombo cha habari, akaunti ya mtu mtandaoni au chanzo kingine, inaweza kuwa na manufaa kuwasiliana nao moja kwa moja na kuwauliza kuhusu ukweli wa habari hiyo.

6. Iwapo ni jambo la kitaalamu tafuta maelezo au usahihi wa taarifa: Husika kwa kutafuta usahihi wa taarifa kwenye vyanzo vingine au kuwasiliaa na wataalamu wa jambo hilo.

6. Ripoti kwenye jukwaa husika la mtandaoni: Wasiliana na watoa huduma wa mtandao husika, eleza juu ya mashaka yako ili waweze kuona iwapo walikosea na waweze kurekebisha au kukupa ufafanuzi ili kuondoa mashaka na kupata taarifa iliyo kamili. Mara nyingi, majukwaa yanaweza kuchukua hatua za kuthibitisha habari ili kuzuia kuenea kwa taarifa potofu.

7. Toa Taarifa kwa watu husika: Ikiwa taarifa inahusiana na watu fulani, unaweza kuwajulisha wadau husika kuhusu uwepo wa habari hiyo ili waweze kukuthibitishia au kama ni kweli ni habari gushi waweze kuchukua hatua stahiki kabla madhara hayajawa makubwa kwa upande wao na kwa jamii.
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom