Great Thinker, Sugua Kichwa kama Unaweza

Bwana mabel mbona umeanzisha hii topic wakati huu ambao vichwa vimeshachoka na pilika pilika za siku nzima!
Ungeuliza asubuhi hakyanani mimi ningetoa jibu sahihi lakini sasa hivi nipo hoi hapa.
Ndibalema wee ni noma.
Kwa hiyo tukikupa nafasi ya kujibu kesho asubuhi utatupatia jibu sahihi au utakuja na stori zingine?
 
kwa vile unaweza kuuliza mmoja na unaweza kutoka kwenye mlango wowote, unamfuata mlinzi moja unamuuliza huundo lango wa kwenda kunyongwa?
Mlinzi mkweli atasema ndiyo, soo, utatoka kwenye mlango wa pili, yule mwongo atasema hapana, then unatoka hapo hapo.

SIMPLE/
 
Siyo simple kama hivyo. Ukiuliza mlinzi huyu atakujibu hilo swali moja tu na hatakupa maelezo mengine, na baada ya kuwa umemuuliza huyu, yule mwingine hatafanya maongezi yoyote na wewe.
 
Nilishasikia hili swali. Jibu lake lilikuwa refu kidogo na kwa kweli sikulielewa pamoja na kurudiwa mara mbili.

Jibu lake kwa wale watakaotaka kufikiri ni kuwa:

Inabidi umuulize swali ambalo linakuwa kama vile limebeba maswali mawili. Hili swali linamlazimisha Mlinzi kusema NDIYO hata kama anataka kukudanganya. Sintajibu kwa maana ya kumpigia simu mshikaji anipe jibu maana lilishanishinda kulielewa pamoja na kupewa jibu. Labda nikilisikia kutoka kwako ndiyo hatimaye ntalielewa. NASUBIRI JIBU.
 
Uko gerezani umefungwa kifungo kisicho na mwisho, unapewa nafasi moja ya kutoka gerezani iwapo utapita mtihani ulio mbele yako.

Hii ni true statement kwamba hapo ni gerezani.

Unaonywesha milango miwili, kila mlango unamlinzi mmoja, mlango mmoja unaelekea kunyongwa na mlango mwingine unakurudisha uraiani kula maisha na jamaa zako.

Hapo nimesha ambiwa kuwa kila mlizi analinda mlango wake

...umepewa nafasi ya kumuuliza mlinzi mmoja wapo kati ya hao wawili swali moja TU ilikutambua ni mlango upi utokee/ufungue na upate kupona.Katika hao walinzi wawili, mmoja anasema uongo tu na mwingine anasema kweli tu, na hawa wawili wanajuana tabia zao na wewe hujui yupi ni mkweli na yupi ni muongo.

Hapa ndo unauliza swali ambalo jibulake la ukweli linajulikana, mf je hapa ni gerezani? au je huu ni mlango?

utafanya nini ili ujue mlango utakao kupeleka uraiani kufurahia maisha na si kwenda kunyongwa?

Baada ya kupata majibu liwe ndiyo au hapana utaweza kujua muongo ni yupi na kwasababu kila mlizi anamlango wake basi utajua wapi kwa kwenda based on the answer.
 
Polenni wandugu, na hili ndio jibu sahihi.

Kwanza kabisa mimi sihitaji kujua mkweli ni yupi na muongo ni yupi, mimi nataka kurudi uraiani.

Hivyo nitamfuata mlinzi yeyote nitamuuliza swali hili la kizushi, "Eti kama nikimuuliza mlinzi mwezako nitokee mlango upi ili nisinyongwe atanionyesha upi?"

Akisha kupa jibu fanya kinyume cha jibu lake pasipo kujali ni muongo au mkweli.

Proof.
Kama utakuwa umemuuliza muongo, atakuonyesha mulango wa kunyongwa (anajua mwenzake anasema kweli tu) hivyo kufungua kinyume utapona
Kama utakuwa umemuuliza mkweli, atakuonyesha mulango wa uongo(anajua mwenzake anasema uongo tu) hivyo kufungua kinyume chake utafungua mlango wa uzima.

Kuna aneyebisha?
 
Sawa kabisa mkuu. Hilo ndiyo jibu lake maana mwanzo niliambiwa kwa Ki-Chechnia na sikuelewa vizuri.

Jibu ni hilo maana nakumbuka kuwa jibu lake lilikuwa kama kwenye mahesabu ya -()x-()=+() au -()x(+-)=-().

Asante kwa jibu. Kweli mahesabu ukiyafahamu, utafanikiwa sana mambo mengi dunia hii.
 
Polenni wandugu, na hili ndio jibu sahihi.

Kwanza kabisa mimi sihitaji kujua mkweli ni yupi na muongo ni yupi, mimi nataka kurudi uraiani.

Hivyo nitamfuata mlinzi yeyote nitamuuliza swali hili la kizushi, "Eti kama nikimuuliza mlinzi mwezako nitokee mlango upi ili nisinyongwe atanionyesha upi?"

Akisha kupa jibu fanya kinyume cha jibu lake pasipo kujali ni muongo au mkweli.

Proof.
Kama utakuwa umemuuliza muongo, atakuonyesha mulango wa kunyongwa (anajua mwenzake anasema kweli tu) hivyo kufungua kinyume utapona
Kama utakuwa umemuuliza mkweli, atakuonyesha mulango wa uongo(anajua mwenzake anasema uongo tu) hivyo kufungua kinyume chake utafungua mlango wa uzima.

Kuna aneyebisha?

Hakuna anayebisha, that's correct!
 
Hakuna anayebisha, that's correct!
kunatofauti gani na jibu hili mkuu??

kwa vile unaweza kuuliza mmoja na unaweza kutoka kwenye mlango wowote, unamfuata mlinzi moja unamuuliza huundo lango wa kwenda kunyongwa?
Mlinzi mkweli atasema ndiyo, soo, utatoka kwenye mlango wa pili, yule mwongo atasema hapana, then unatoka hapo hapo.

SIMPLE/
kwamba fanya viceversa?
 
kumbuka mkuu unaruhusiwa kuuliza swali moja tu na utapajibu moja na huruhusiwi kuo na mlinzi zaidi ya mmoja.

Hi haitafanya kazi.
 
Ntamuuliza swali la kizushi askari kama "nackia mnanyonga kwa kutumia sumu?" najua askari mwongo atakataa wakat askari mkwel anaweza jibu "sio mimi ninayenyonga" afu bada apo ntajua tuu.
mkuu watu hawanyongwi kwa kutumia sumu!
 
:smash:

Duh, kumbe IQ yangu iko chini aisee:embarassed2:.... Hadi jasho limenitoka na bado sikupata jibu!
 
Men u made me think this thing 4 hours and here's the answer. Niligundua kuna swali ambalo ukiwauliza wote watatoa jibu moja. What's the question? Here it is, utamuuliza yeyote swali hili "NIKIMUULIZA HUYO MWENZAKO MLANGO WA URAIANI ATANIJIBU NINI?" there,kama ntakua nimemuuliza yule wa ukweli atajibu "atakuonesha mlango huo apo wa kifo' kama ntakua nimemuuliza muongo,atanidanganya kwa kunionesha wa uongo sababu wa ukweli angenionesha mlango wa ukweli.So yeyote ntakayemuuliza hilo swali atanionesha mlango wa uongo na ntaenda mlango mwingine. Men i had to draw logic values to figure it out. Thanx 4 activating ma brain cell which were zzzzzzzz.
 
Hongera Mabel;
Naona mtihani wa kupima IQ utawatoa kamasi bingwa wengi hapa...
 
namuuliza yule muongo tu kua eti ni mlango upi ni wa kwenda kunyongwa lazma atanidanganya kua ni ule wa kutokea basi nakua nishapata jibu
 
Hata jibu la mtoa mada sio, iliyobaki ni bahati tu, huwezi kuwa mtu wa kuhisi ili kugundua ukweli, labda uwe Sheikh Yahya Hussein
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom