GPL na Clouds FM waandaa Tamasha la Kuhamasisha Uzalendo

mwanakwetu

Member
Mar 30, 2008
89
14
mafisadi.jpg


Global Publishers kwa kushirikiana na Clouds group wanaanda tamasha la kuwahamasisha wananchi kuwa wazalendo kwa kile walichodai kuchafuliwa kwa hali ya hewa kulikosabaishwa na maandamano na kauli za wanasiasa dhidi ya serikali hivyo wananchi kupoteza imani kwa serikali yao. Tamasha litafanyika viwanja vya Biafra, tarehe 19/03/2011 kuanzia saa 5 asubuhi na kingilio ni bure.

Swali langu wametumwa na nani kuwafundisha wananchi uzalendo? wakati wote walikuwa wapi wakashindwa kufundisha wananchi uzalendo wa kupinga ufisadi na unyonyaji kwa wananchi? Kuna haja ya kuwaangalia hawa wanaojiita vijana wazalendo wa taifa hili.
 

Attachments

  • MZALENDO1.jpg
    MZALENDO1.jpg
    36.9 KB · Views: 83
Masahihisho kwa mstari wa pili sio wananchi ni wanasiasa. Hivyo isomeke kuwa ni kuchafuliwa kwa hali ya hewa kufuatia maandamano na kauli za wanasiasa.
 
Hao ni wehu, tena waganga njaa. Maandamano yalifanyika kanda ya ziwa wao wanafanya tamasha dar!!!!
 
Jamani hawa watu wanafanya mambo haya tuwafanyaje? Ina paswa tuweke maazimio wa watu wasio tumia akili kama hawa.....hao watu wote vituo vyao vya habari ni upuuzi mtupu...

Nani asiyejua kuwa Clouds inamilikiwa na makada wa CCM (napata hata tabu kukitaja hiki chama) nani asiyejua kuwa Shigongo ni mtumwa wa CCM? Hao publisher na magazeti yao ya udaku na hadithi zao za kuzimu sichelei kusema wanaonyesha namna gani walivyokuwa ni wajinga.......
 
Global publishers na Clouds wanajulikana kuwa ni pro-CCM.Kwahiyo kuandamana,kutetea serikali ya chama chao ni haki yao
 
Hawa watu wananishangaza mno,kwa nini wanakuwa makuwadi wa dhuluma na hali mbaya tuliyo nayo...hivi wana akili timamu kweli?au kwa sababu wao wapo kivulini!Badala ya kutumia jukwaa hilo kupaza sauti kwa niaba ya walalahoi tunaoumizwa na udhaifu wa serikali ya ccm,wao wanautetea udhaifu huo na kuupongeza!mnh....
 
Lazima atokee shujaa mmoja avae vilipuzi awafanyizie hawa mafala.

We can't go on like this.

My parents are sick of poverty back in my home village, yet a fool at the center of Dar es Salaam is organizing such a nonesense gathering!!

Ipo siku hata mimi nikichoka nitavaa mabaruti
 
Amakweli ipo kazi, yani nchi inavamiwa wananchi wako vitani kuikomboa lakini ajabu yake wachache wanageuka nakuwa upande wa wavamizi. Nasema kweli bila kumumunya maneno watanzania tuna ugonjwa wa kutojitambua na kutokujua kwamba hatujui...
 
vyura wa bahari hao hawajui ukame dawa kuwapiga mawe naona amani imewazidi wanaleta dharau watu tunakufa njaa
 
Uzalendo mtu anazaliwa nao labda wangefanya kusanyiko la kuwafundisha wenzao kuimba wimbo wa taifa. Taasisi hizi, CF na GP wanafaidika na mfumo wa kifisadi, tamasha hili litadhaminiwa na kila fisadi unayemjua na hakika kutakuwa na muziki wa nguvu utakaofungwa hapo, tutawaona wasanii wanaoimbia matumbo na viuno huku wale wanaoimbia mioyo na kichwa hawataalikwa.
Nahimiza tujitokeze, ni sehemu nzuri ya kuwajua adui zetu:smash:
 
Wala sitashangaa, hao mawingu si ndo walimuandalia mkwere B'day party? Halafu hawa kweli ni vijana? Huyo wa tatu kutoka kushoto alikuwa sober kweli? na huyo wa nne toka kushoto mbona kama anafikiria mambo mengine wala hayuko nao?
 
kwa hakika ni wana wa mafisadi, na wanastahili kupuuzwa na watanzania, matamasha ya CDM hayakuwa na wanamziki wala wasanii ili kuvutia hadhira, sasa hawana namna ni lazima watafute wasanii wa kuwafarij kidogo
 
View attachment 25163
Global Publishers kwa kushirikiana na Clouds group wanaanda tamasha la kuwahamasisha wananchi kuwa wazalendo kwa kile walichodai kuchafuliwa kwa hali ya hewa kulikosabaishwa na maandamano na kauli za wananchi dhidi ya serikali hivyo wananchi kupoteza imani kwa serikali yao. Tamasha litafanyika viwanja vya Biafra, tarehe 19/03/2011 kuanzia saa 5 asubuhi na kingilio ni bure.
Swali langu wametumwa na nani kuwafundisha wananchi uzalendo? wakati wote walikuwa wapi wakashindwa kufundisha wananchi uzalendo wa kupinga ufisadi na unyonyaji kwa wananchi? Kuna haja ya kuwaangalia hawa wanaojiita vijana wazalendo wa taifa hili.
Mambo kama haya ndiyo huwa yanapelekea mapigano ya wenyewe kwa wenyewe....Hata kama ccm ikiondolewa madarakani,still ni vigumu ku co exist na watu kama hawa....So sishangai kwanini sometime watu wanalimana risasi especially wakati wa mapinduzi ama strategic changes.
Utawezaje kupatana na watu wenye hulka na mawazo kama haya?Hopefully ni siasa tu,ila kama ndivyo walivyo,then tuna kazi.
 
Lakini mbona nimesoma habari yenyewe GP haina mambo ya Mwanakwetu?

PRESS RELEASE
March 15, 2011, DAR ES SALAAM

YAH: TAMASHA LA UZALENDO
Kampuni ya Global Publishers ikishirikiana na Clouds Media Group inapenda kuufahamisha umma wa watanzania kuwa wameandaa tamasha la wazi na la bure lililopewa jina la "TAMASHA LA UZALENDO: TANZANIA KWANZA, SISI SOTE NI NDUGU". Tamasha hili Kubwa, linatarajiwa kufanyika Jumamosi ya tarehe 26 Machi, 2011 katika viwanja vya Biafra, Kinondoni Dar es Salaam kuanzia, saa 5:00 asubuhi hadi saa 12:30 jioni.

Madhumuni ya tamasha hili ni kuwakumbusha watanzania umuhimu wa kuishi pamoja kwa upendo na amani bila kujali tofauti zao. Vilevile kuwahamasisha kuipenda nchi yao na kupendana kama binadamu na kuweka uzalendo mbele kwa maslahi ya taifa. Tamasha hili linakadiriwa kujumuisha watu kati ya 20,000 hadi 25,000 wa rika tofauti na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa makampuni na taasisi mbalimbali wanaoheshimika na jamii, ambao siyo wanasiasa.

Tamasha linatarajiwa kuvuta watu wengi kutokana na maudhui yake pamoja na kauli mbiu yake ya kuhimiza na kuhamasisha mapinduzi ya kifikra kwa kuwajenga watanzania wawe na uzalendo na moyo wa kupenda nchi yao. Kwa kufanya hivyo, wataweza kuongeza upendo miongoni mwao na hii itasaidia kulinda amani na utulivu tulio nao na tunaojivunia.

Kwa kipindi kirefu sasa, nchi ya Tanzania imekuwa katika vita ya maneno kati ya wanasiasa wanaokinzana na hivyo kwa namna fulani kuathiri watanzania wengi kutokana na misimamo na matamshi yanayowakatisha tamaa wananchi wengi. Tamasha hili litakuwa ni fursa ya kipekee ya kurejesha matumaini kwa kufufua chachu ya kutaka kuwa wazalendo, wenye uchu wa kulinda nchi yetu na kuonesha mapenzi kwa kila kitu kinachohusisha Utanzania, bila kujali tofauti zetu za kiitikadi na vyama.

Ujumbe wa tamasha hili ni muhimu sana kwa kila mtanzania atakayefika pamoja na wale watakaosikia habari zake. Ili ujumbe uweze kufika kwa ufasaaha, kunatarajiwa kuwepo wanaharakati watakaozungumza siku hiyo, wakiwemo Eric Shigongo, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Joseph Kusaga, Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group na wengineo.

Tamasha hili linatarajiwa kusindikizwa na burudani mbalimbali kutoka kwa bendi na vikundi mbalimbali vya sanaa. Kati ya burudani hizo ni muziki wa dansi kutoka kwa bendi za African Stars, Msondo Music Band, DDC Mlimani Park, TOT Band na Stone Mayiyasika. Vile vile kutakuwa na muziki wa taarabu ambapo bendi za Jahazi Modern Taarab na Super Shine Modern taarab zitatumbuiza.

Vijana wakiwa ndiyo kundi kubwa linalowakilisha idadi ya Watanzania wengi, burudani ya bongo flava itakuwepo huku wasanii wengi wakionesha nia ya kushiriki. Miongoni mwa wasanii hao ni pamoja na Profesa Jay, AY, H. Baba, H-Mbizo, wasanii kutoka Zizzou Entertainment, mwimbaji wa injili, Flora Mbasha na wengineo wengi.

Mbali ya wasanii hao, atakuwepo pia mwanamuziki mkongwe wa Reggae, Innocent Galinoma, Mtanzania aishiye nchini Marekani, ambaye amejipatia umaarufu kutokana na nyimbo zake za kizalendo kama vile "Sote ni ndugu" na "Kilimanjaro".

Juhudi za makusudi zimefanywa na kamati ya maandalizi kuhakikisha kuwa ulinzi na usalama wa watu na mali zao unakuwa wa kutosha. Vyombo husika vya ulinzi na usalama vimeshapewa taarifa na vinajipanga kuhakikisha tukio hili linakuwa la kihistoria. Vilevile kutakuwa na maninja watakaoongeza nguvu kusaidiana na polisi ili kuhakikisha usalama wa kutosha.

Kamati ya maandalizi ya tamasha inapenda kutoa hamasa kwa watanzania wote kujitokeza kwa wingi siku hiyo na kula kiapo cha uzalendo. Wananchi watakaohudhuria, si tu watapata fursa ya kupokea changamoto ya kuwa wazalendo na kuishi kwa amani na upendo, bali pia wataburudika na burudani zilizotajwa hapo awali. Vilevile huduma mbalimbali muhimu, kama vinywaji, vyakula, vitatolewa kwa gharama nafuu.

Asanteni, Mungu awabariki na aibariki Tanzania.

-Global Publishers & General Enterprises Ltd

-Clouds Media Group

Juma Mbizo,
Mratibu wa Tamasha.
 
Back
Top Bottom