Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,498
- 9,279
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka Watanzania hususani vijana wasikubali kurubuniwa na makundi ya watu wasio na mapenzi mema na nchi yetu ambao watataka kuwatumia kwa maslahi yao binafsi na hatimaye kuhatarisha usalama na amani ya nchi yao.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Desemba 10, 2020) wakati akifungua mkutano Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma. Amewasisitiza Watanzania wawe wazalendo kwa nchi yao.
“Uzalendo ndio utalifanya Taifa liendelee kujitegemea, hivyo ni muhimu suala hilo likapewa kipaumbele. Tusimkubali kushawishiwa na Mtanzania yeyote anayetumiwa na watu wenye lengo la kutaka kuja kututawala, tusikubali lazima tuendelee kuwa huru na tulinde rasilimali kwa manufaa ya wote.”
Waziri Mkuu amesema uzalendo ni muhimu sana katika kujenga umoja wa kitaifa na Vijana ni zaidi ya asilimia 60 ya wananchi wa Tanzania, hivyo wakipata misingi mizuri ya uzalendo tutajenga Taifa imara, lenye mshikamano, nguvu na kuendelea kudumisha Amani nchini.
Amesema Serikali kwa kutambua hilo, kupitia Ilani ya CCM 2020-2025, imeweka msisitizo wa kuhamasisha na kuelimisha wananchi juu ya masuala ya uzalendo wa Kitaifa. “Suala la uzalendo ni muhimu sana kwa mustakabali na maendeleo ya Taifa lolote.”
Waziri Mkuu amesema amefurahi kuona skauti wenye umri mdogo katika mkutano huo na kwamba wanachama wa chama cha skauti huanzia umri wa miaka mitano na kuendelea, ni dhahiri kuwa malezi na makuzi ya uzalendo kuanzia utotoni yatawezesha ujenzi wa Taifa imara lenye wananchi wenye kuipenda nchi yao, kuilinda na kuithamini.