God's time is a myth, The strategy of redundancy

God's time is a myth, The strategy of redundancy

Achague upande mmoja tu,


mkuu upo 50/50, sasa kwenye fikra huru mkuu, hizo dini za abrahamic wanakubali fikra huru hapo kwenye mambo ya imani hapo?
Kwenye masuala ya kiimani shida huwa ni kutofautiana uelewa kwenye baadhi ya masuala mbalimbali. Wengi mnafikiri kuhoji hoji hovyo ndio fikra huru.
 
Theists mnadai kuna Mungu, Kitu ambacho Atheists huwa tunawashangaa, Mmewezaje kujua hilo kwa uhakika?
Mbona ni jambo ambalo linaeleweka msingi wa Theist kusema kuna Mungu ni imani, na ndio maana masuala ya Mungu ni masuala ya imani unaweza ukaona sababu za kukubali kuamini ukaamini Mungu au haujashawishika na sababu za kuamini na usiamini.
 
Atheists sio kundi la dini.

Atheist ni mtu asiye na dini wala imani ya aina yoyote ile ya Mungu au miungu.

Theists mnadai kuna Mungu, mmewezaje kujua hilo kwa uhakika?
Atheist haishii kutokuwa na imani ya Mungu na miungu bali ni zaidi ya hivyo.
 
Chochote kinachodaiwa bila ushahidi kinaweza kutupiliwa mbali bila ushahidi

Anything asserted without evidence can be dismissed without evidence.
Tatizo sio hilo bali tatizo ni kukosekana kwa ushahidi wa kuwepo kitu kufanya kuwa ndio uthibitisho wa kutokuwepo hicho kitu.
 
Huyo Mungu wenu ana uwendawazimu.

Mungu ambaye alikuwa na uwezo wa kuumba Dunia isiyo na mabaya. Lakini Akashindwa kufanya hivyo. Badala yake akaruhusu Dunia yenye mabaya iwepo. Ni Mungu mwenye makusudi na ujinga.

Huyo Mungu kama alijua tangu mwanzo kwamba kuna mambo hayampendezi na alikuwa na uwezo wa kuyafuta kabisa yasiwepo, Angefanya hivyo.

Kama Mungu alijua kabisa toka mwanzo kuna mambo hayampendezi lakini akaamua kuyaacha tu mambo hayo yawepo, Haya ni MAKUSUDI ya wazi kabisa. Na uonevu dhidi ya watu wema.

Ni sawa na referee anayeona off-side kabisa lakini anakausha anasubiri goli lifungwe halafu ndio aanze kusuluhisha mzozo baina ya timu mbili.
Wagalatia 6:7-8
7 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.

8 Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.
 
waseminary ni decent sana simuoni kwenye useminary,ndiyo uje kuaminisha watu Mungu hayupo🤣🤣
Hakuna sehemu nime muaminisha mtu Mungu hayupo.

Una uhuru wa kuamini chochote hata jiwe, mti, mlima n.k

Mimi naonyesha contradictions zilizopo katika suala la kuamini uwepo wa Mungu.

Nimekuwekea contradictions za huyo Mungu bado unazikataa tu, kutetea imani ya huyo Mungu.
FB_IMG_1771821867981.jpg

Mungu ambaye ni "perfect" angekuwepo, kusingekuwa na hizi contradictions.

Contradictions zipo, lakini bado mnatetea Mungu wenu ni perfect, mara ni muweza wa vyote, mara ana upendo na huruma.

Contradictions mnaziona, lakini mnapiga mikausho tu. Mnatetea hivyo hivyo kibishi bishi.
 
Mkuu, si kwa ajili ya Mungu kupata taarifa — Yeye tayari ni Mjuzi wa yote. Mtihani ni kwa ajili yetu sisi, si kwa ajili Yake. Unaleta haki, uwajibikaji, na maana ya uchaguzi wetu.
Kama hakuna mtihani, basi hakuna tofauti kati ya mema na mabaya, wala hakuna uwajibikaji wa kweli. Uovu haukuumbwa ili kushinda mema, bali ili kutoa nafasi ya kuchagua mema kwa hiari. Bila uchaguzi, hakuna maadili; bila maadili, hakuna ukuaji wa kiroho.
Mungu kujua matokeo hakumaanishi anatunyima uhuru wa kuchagua. Maarifa Yake hayalazimishi matendo yetu — sisi bado tunachagua.


View: https://www.instagram.com/p/DUnBv60jcLP/?igsh=MWV5bjFtbGl2YnYxYQ==

Kwa kutunia mfano wa kisa hicho hapo juu , nieleweshe test hapo imeenda kwa nani nk.
 
Back
Top Bottom