Unasema sheria ni upumbavu, Je unadhani watu kuwa na imani ya Mungu tu, bila sheria ingetosha kudhibiti maovu?
Sheria haina maana isipokuwa na msimazi
Unaweza ukawa mbwamwitu unatungia sheria kondoo kila siku unawapeleka malishoni wa nakuona mwema ila kila jioni unaomba mmoja wao akakutandikie kitandani na harudi
Leo tuna mifano inaonekana wazi lakini inaonekana kama hadithi za kutunga viongozi wanaotumainiwa kama wasimamizi wa sheria lakini ndio wahujumu washeria
Sheria inakuwa na maana unapokuwa juu yake na siyo chini yake
Sheria ni kama chanting za kiimani kufanya mpumbavu aone yupo salama
Iwe ulaya hata kwa mtogole sheria ni upumbavu
Wakati nipo mdogo sikudhani dini haiepukiki hata ukikataa Mungu bado binadamu watakufundisha kutii Mungu wa mamlaka kwa jina la sheria
Toka kitambo dini na imani za Mungu zilifeli kuwafanya watu wasitende maovu.
Ndio maana zikaanzishwa sheria dhidi ya makosa mbalimbali, mahakama zikaanzishwa, vituo vya polisi vikaanzishwa, mahabusu zikaanzishwa.
Hii yote ni kwa sababu
imani kwa Mungu haikuleta matokeo yoyote chanya ya kudhibiti maovu duniani.
Hakuna kitu kinaitwa sheria nzuri ikiwa anayehukumu ni binadamu
Wahalifu wengi ni watu wa dini na imani kwa Mungu. Lakini bado wanatenda maovu.
Bila uwepo wa sheria, unadhani hiyo imani ya Mungu ingetosha kudhibiti maovu ya Dunia?
Wewe angalia kina Kibwetere walivyo choma watu kwenye makanisa.
Angalia yule mchungaji wa Kenya Paul Mackenzie aliyeua maelfu ya watu kwa kuwaambia waumini wake wafunge mpaka kufa wakamwone Yesu.
Angalia waislamu wanaoamini ukiua makafiri unapata thawabu kwa Allah.
Unafikiri bila sheria za kibinadamu, mauaji si yangekuwa mengi sana, kila mmoja akijaribu kumtetea Mungu wa imani yake.
Imani kwa Mungu ndio UPUMBAVU kwa sababu imeleta machafuko, mabishano na mauaji mengi duniani.