Godbless Lema kumchakaza Wassira kwa Helicopter

attachment.php


Lema na chopa ni damu damu,hii iliyotolewa na mayor wa london haijafika tu??
 
Naona Lema yuko addicted na chopa,hivi hiyo chopa ndio ile aliyopiga nayo picha katika ziara yake ya UK kumtembelea mayor au ndio michango ya M4C? Ukombozi bila chopa unawezekana..

Mkuu naona usingizi umekuzidia
 
Chadema hivi kwa nini mnapoteza bure pesa mlizowachangisha Wananchi bure kumnunulia Lema Chopa hivi Lema, na Zitto nani anatakiwa atumie Chopa.
 
Mingoi Mkuu ndio hiyo atakayeitumia Bunda?
 
Last edited by a moderator:

jitu lilikuwa limelala ... limeona thread ya lema .... amewashwa jumla ... you are not a Tanzanian ... we just watch you ... una dhamira ya kuchochea machafuko ya kidini na kikabila ... hutafanikiwa ... rudi kwenu
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ndio hiyo atakayeitumia Bunda?
Mkuu Ritz,nahisi manake kwenye kuchangia M4C Serena Hotel Dar Lema alisema anatamani ifike kabla ya x mas labda mayor katimiza ahadi kwa mapenzi yake aliyonayo kwa wakombozi wetu.
 
Watu wa dar kesho huku ya kamanda wetu Lema naamini mtatupa updates za kutosha..
 
Mkuu Ritz,nahisi manake kwenye kuchangia M4C Serena Hotel Dar Lema alisema anatamani ifike kabla ya x mas labda mayor katimiza ahadi kwa mapenzi yake aliyonayo kwa wakombozi wetu.

Lakini juzi M4C ikiongozwa na Lema kule Mwanza walipata hasara. Malengo yao yalikuwa kukusanya bilioni 3 lakini cha kusikitisha walikusanya milioni 6 na ahadi milioni 20.
 
Zitto kabwe ni wa mhimu zaidi ya lema lakini kwa kuwa si mchaga chopa ataiskia angani, duh........ Hawa watu wana ubaguzi sana
 

Chakaza Kamanda jamaa wameshachanganyikiwa.....Msako wa jangili nyumba hadi nyumba uvungu mpaka uvunguni!!!!!!!


....................wameshaanza mazoezi ya kuwa wapinzani watarajiwa ....... wanapambana na Serikali!!!!!
 
Mungu awalinde makamanda wote, mkumbuke kusali ili kazi njema mnayoifanya iwe na manufaa kwa nchi nzima. M4C for life!
 
Chadema hivi kwa nini mnapoteza bure pesa mlizowachangisha Wananchi bure kumnunulia Lema Chopa hivi Lema, na Zitto nani anatakiwa atumie Chopa.

Ritz usiulize nyumba ya jirani kwanini fulani aenda kulima badala ya yule.
 
Last edited by a moderator:
ester wassira nae tunaomba aongezwe kwenye list tafadhali,atasaidia kuhamasisha wakinamama..na pia she is the most lykly person from chadema wakugombea 2015 hilo jimbo.

hii tabia ya kila mtu akitoa hoja nzuri apewe jimbo italeta mgogoro. si kwamba nampinga esther ila hadi sasa kuna watu 7 waisha tangaza nia kwa staili tofauti tofauti hapa Bunda na faida kubwa naona ni makundi tu.
 
Sasa Bunda tumeelewa Kumbe Chadema mnakuja Bunda kushughulikia Wasira. Tulidhani mnakuja kushughulikia matatizo ya wananchi Kumbe kulipa kisasi kutokana na Wasira kuwaumbua kwa kuwa via ukweli ! Karibuni, lakini hakuna mtakachoambulia. Mtakuikuta Bunda na kuacha Kama mtakavyoikuta. Kuja na chopper siyo Hoja Mwaka 2005 Mbowe alitoa nyamatoke na kuambulia Kurt 0. Sisi Bunda siyo limbukeni aw kupapatukia chopper karibuni sana.
 
Afadhali arusha sasa inatawalika maake huyo kamanda wenu lema alikuwa ameifanya kuwa misri kila siku maandamano jaji aliye tengua ushindi wake ameokoa watoto wa walala hoi na mchakamchaka wa maandamano ubarikiwe sana
 
Majangili matumbo moto... Mwisho wa Chukua Chako Mapema (CCM) umekaribia kufika tamati, Nyara za serikali zirudishwe zikiwemo zilizotoka Gombe!
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeanza Operesheni Chakaza Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Bunda, kwa lengo la kumthibitishia mbunge wa jimbo hilo, Stephen Wassira kuwa hana ubavu wa kudhibiti kasi ya kuenea kwa chama hicho kama anavyojigamba.

Operesheni hiyo inakuja zikiwa ni siku chache tangu Wassira ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), kuwaomba wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM wamchague kuwa mjumbe wa NEC ili aweze kudhibiti kasi ya kuenea kwa CHADEMA.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema, ndiye ataongoza operesheni hiyo itakayoanza Desemba 12 kwa kutumia usafiri wa helikopti na magari ili kuhakikisha wanafika maeneo yote ya wilaya hiyo ndani ya siku sita.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Lema ambaye anasubiria uamuzi wa Mahakama ya Rufaa kuona kama atarejeshewa ubunge wake wa Arusha Mjini, alisema kuwa amekuwa akishangazwa na kauli za majigambo zinazotolewa na Wassira, ikiwemo ile ya Dodoma ya kudai yeye ana mwarobaini wa CHADEMA jambo alilosema hana ubavu huo.

Alisema kuwa ili kumdhihirishia kwa vitendo Wassira na CCM kuwa hawana ubavu wa kuzuia mabadiliko yanayoendeshwa na CHADEMA kwenye maeneo mbalimbali nchini, wameamua kuweka kambi kwenye jimbo lake na kuhakikisha wanawavua magamba na kuwavika magwanda wapiga kura wake.

Lema aliongeza kuwa, mbali ya kuendesha mikutano ya hadhara watakuwa na jukumu la kukagua uhai wa chama kuanzia kwenye msingi na matawi, kwa kuhakikisha wanasimika uongozi pale itakapoonekana kuna ulazima wa kufanya hivyo.

Katika oparesheni hiyo, Lema ataongozana na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, mjumbe wa mkutano mkuu wa CHADEMA, Lucas Webiro na aliyekuwa diwani wa Sombetini kupitia CCM, Alphonce Mawazo.


Source: Tanzania Daima

Nadhani huko Bunda patanuka vumbi!!!

 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom