My Take: Chadema isipokuwa makini umaarufu wake utapungua kutokana na migogoro mingi inayokikumba chama hicho. Mwaka 2015 si mbali jahazi linaonekana kuyumba ukilinganisha na huko nyuma. Wengi wataumia ndani ya chama hicho kwani umaarufu wa mtu unakuwa juu ya chama. Hizi tuhuma dhidi ya Lema hazikijengi chama bali zinakibomoa. Arusha hali si shwari.
![]()
![]()
Zaidi, angalia attachments chini
Hawa wanaosimamia ArDF ndio beneficiaries wa huo ufisadi, unategemea waseme nini? Kama chadema iko serious imtume Kitila akafanye uchunguzi huru Arusha juu ya hizi tuhuma.
Kwanza tumia akili ndogo tu, Development foundation gani haina ripoti ya mwaka? Anachotakiwa kufanya ni kuleta ripoti ya mwaka ya mapato na matumizi pamoja na majina na anuani za walionufaika na ArDF.
Nimezisoma hizo nyarakafeki, sijaona ukashfa wala chembe ya kuiua chadema!
Mods: kumekuwa na taswira flani ya uachaji wa mijadala ya kizushi inayotupotezea mda na kushusha hadhi ya jukwaa hili!
Uzushi kama huu haina haja ya kuuacha watu waendelee kuangalia!
Huna lolote na tutangoa mpaka mizizi...A time wil tell.Mbona hawa si wakwenda nao haraka,taratibu kila mmoja atawekwa wazi kwa uchafu wake.Hapa nasubiria document zinifikie muda wowote kutoka makao makuu ya chama za uozo wa CHADEMA COLLEGE pale KIBAHA.Pesa zilishatoka,Katibu mkuu akaelekeza tumboni kwake
NIMECHUKUA HAYA MAWILI; mh lema ww binafsi toa majibu ya ukweli / majungu ya haya , 1, uwanja kwa ajili ya ujenzi wa hospitali. 2, trekta . majibu yako ni muhimu kuliko vizuizi au majibu ya jumlajumla ya mashabiki wako wanaotaka mabadiliko ya haki na maendeleo toka CCM na kuzuia UOZO ndani ya CDM
Crashwise katika uzi wa Octoba 2012 alijibu baadhi ya tuhuma hizi, majibu ambayo yanapatikana https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la...azi-print.htm. Kwa kifupi alielaza kuwaIli kuweka mambo sawa, kiwanja cha hospital iliyoahidiwa na Lema kipo Burka kilomita tatu kutoka barabara kuu na kwa sasa michoro ya hosp. inaendelea, trekta lilikabidhiwa kwa wamama wasiojiweza lakini itakuwa chini Arusha Dev Fund (ArDF).
Naye Mkurugenzi wa Afya na Elimu (ArDF) alitoa taarifa hii:
Awali ya yote napenda sana kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kutujaalia uhai.
Nimeisoma na kuielewa vema mada yako ndugu Lengio, wenye kichwa cha habari "Lema katupapeli shamba alilo omba kujenga hospital ya Wazazi".
Napenda kueleza mambo machache ambayo yatakuwa na umuhimu kwetu na taifa kwa ujumla, na hasa kuondoa uvumi huu ambao hauna tija kwa taifa na ambao umekuwa ukienezwa na watu wenye fikra mgando. Awali ya yote naomba kueleza kwamba mimi ni mmoja wa Waasisi wa Taasisi ya Maendeleo ya jimbo la Arusha mjini,(Arusha Development Foundation -ArDF) Naitwa Kamanda Magoma Jr Magoma, kwa sasa ni Mkurugenzi wa Elimu na Afya katika taasisi ya ArDF (nikiwa na jukumu kubwa la kuhakikisha tunafanikiwa kutimiza malengo ya taasisi ya ArDF katika nyanja za Afya na Elimu) si kama ambavyo mleta mada ameeleza bila kuwa na haya wala soni hata tone kwa kufanya upotoshaji wa hali ya juu bila kupima madhara yake kwa jamii kwamba "Lema katutapeli shamba alio omba kujenga hospital ya Wazazi". Napenda nileezee historia ya awali ambayo ninahisi wanachi wengi hasa waishio nje ya Arusha hawaifahamu na wangependa kuifahamu. Mwaka 2010 katika kampeni za uchaguzi mkuu Kamanda Lema aliahidi kwamba atajenga hospitali ya mama na mtoto katika jimbo la Arusha mjini endapo atapewa dhamana ya kuliwakilisha jimbo la Arusha mjini katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kamanda Godbless Lema alisema "ili kuondoa adha ya huduma za afya kwa mama na mtoto, hasa ikizingatia kuwepo kwa msongamano na wagonjwa katika hostpitali ya Mkoa wa Arusha (Mount Meru) mkinichagua nitajenga hostiptali ya mama na mtoto". Baada ya kamanda Lema kushinda alikutana na wadau wengine wa maendeleo katika jimbo la Arusha na kuamua kuanzisha Taasisi ya Maendeleo ya jimbo la arusha (ArDF). Aidha moja na malengo ya msingi ya ArDF ni kujenga hospitali ya mama na mtoto, hivyo ili kuweza kufanikisha malengo ya kujenga hospitali kiwanja ni semehu ya vitu muhimu katika utekelezaji wa ujenzi, hivyo wadau wa Maendeleo walitupatia eneo la ukubwa wa ekari tano katika eneo la Burka, na ili kuweka kumbukumbu sahihi kiwanja hicho kiko chini ya ArDF kikiwa kinasimaniwa na Mama na Mtoto Foundation (Taasisi tanzu ya ArDF) na kwamba si kweli kiwanja hicho kinamilikuwa na Kamanda Godbless Lema na wala hakijabadilishwa umiliki wake wa awali kama ambavyo ndugu Lengio atanaka kuupotosha umma. Hivyo napenda kuwajulisha kwamba alicho andika ndugu Lengio ni uongo na hali ya juu na ni uposhaji uliopiliza mipaka. Chadema ni chama chenye viongozi makini wenye lengo la dhati la kuijenga Tanzania. Aidha nichukue fursa hii kuwajulisha wanachi wa Arusha kwamba tumekuwa tukiwasiliana na wadau na wataalum wa Afya na baada ya muda tutaanza ujenzi wa Hospitali ya mama na watoto, ikisimamiwa na Mama na Mtoto Foundation. "Umoja Wetu ndio Silaha yetu"
Naomba kuwasilisha,
Asanteni Wana JF.
Kamanda Magoma Jr Magoma
(Mkurugenzi wa Elimu na Afya ArDF)
(M/Kiti Mstaafu CHADEMA Wilaya Arusha Mjini)
Hoja na viroja vya nyongeza?
kwa uyo utasubiri sana kama wafuasi wa kibwetere, hamna kitu anajua zaidi ya utunzi kama wa shigongo.
NIMECHUKUA HAYA MAWILI; mh lema ww binafsi toa majibu ya ukweli / majungu ya haya , 1, uwanja kwa ajili ya ujenzi wa hospitali. 2, trekta . majibu yako ni muhimu kuliko vizuizi au majibu ya jumlajumla ya mashabiki wako wanaotaka mabadiliko ya haki na maendeleo toka CCM na kuzuia UOZO ndani ya CDM
Majungu hayajengi !
Haya majibu ni mepesi mno halafu hii barua imeandikiwa kamati kuu sio huyu kizabizabina anaekereketwa kuja hapa kuijibia kamati kuu na Lema.inadhihirisha kuwa husomi majibu yaliyotolewa humu, kuhusu tractor jibu limeshatolewa, kuhusu kiwanja jibu limewekwa humu ila kama wewe una hati yenye jina la lema weka tuone, tukiwaendekeza nyie kila siku mtakuja na propaganda za kutaka mpaka tuwawekee humu hadi mipango yetu ya ndani, kwa mfano: wewe usiyehusika na chama unahitaji kujua mchakato wa uchaguzi wa daraja II ili iweje??
Leo kwa Lema ndiyo yamekuwa majungu siyo? Vipi alipoleta majungu kwa madiwani mpaka wakafukuzwa uanachama halafu anasema hii ndiyo siasa. Siasa ya kutojiamini unasingizia watu uongo halafu eti unasema unakesha kanisani kuomba. Kwa Lema mbona mtaona na kuyasikia mengi....
mhh!!!,aya mmoja wa makatibu wenezi,ata ivo ID yako inaonyesha ivo uku!Mmemuandama dr slaa sana tu atikisiki,Mmeanza kumchimba Lema.NIKIWA KAMA Katibu mwenezi wa chadema ktk mojawapo ya kata hapa arusha Mjini napingana nawe.HALI YA CHADEMA ARUSHA NI SHWARI na hapa tulivyo ni vigumu mno hata kuona bendera ya magamba kwa mabalozi ambao nadhani HAWAPO siku hizi ktk jimbo hili.hizi ni siasa za sewage za mama porojo na akina mama chatanda.
hujasoma na kuelewa ndio maana hujaona uzito wa kashfa hizo.
Kweli wewe ni "Mama porojo" kama lilivyo jina lako. Hivi CHADEMA haina NEMBO ya Chama kwenye "Headed letter" zake?!!
Waliotunga huu waraka ni wahuni, kwanza wameingiza majina ya watu safi ambao wakiyaona majina yao humu wanaweza kuchanganyikiwa! Halafu baadhi yao humo walishafukuzwa uwanachama! Kifupi ni watu dhaifu hawana ushawishi wowote hapa Arusha!