Crashwise katika uzi wa Octoba 2012 alijibu baadhi ya tuhuma hizi, majibu ambayo yanapatikana https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la...azi-print.htm. Kwa kifupi alielaza kuwaIli kuweka mambo sawa, kiwanja cha hospital iliyoahidiwa na Lema kipo Burka kilomita tatu kutoka barabara kuu na kwa sasa michoro ya hosp. inaendelea, trekta lilikabidhiwa kwa wamama wasiojiweza lakini itakuwa chini Arusha Dev Fund (ArDF).
Naye Mkurugenzi wa Afya na Elimu (ArDF) alitoa taarifa hii:
Awali ya yote napenda sana kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kutujaalia uhai.
Nimeisoma na kuielewa vema mada yako ndugu Lengio, wenye kichwa cha habari Lema katupapeli shamba alilo omba kujenga hospital ya Wazazi.
Napenda kueleza mambo machache ambayo yatakuwa na umuhimu kwetu na taifa kwa ujumla, na hasa kuondoa uvumi huu ambao hauna tija kwa taifa na ambao umekuwa ukienezwa na watu wenye fikra mgando. Awali ya yote naomba kueleza kwamba mimi ni mmoja wa Waasisi wa Taasisi ya Maendeleo ya jimbo la Arusha mjini,(Arusha Development Foundation -ArDF) Naitwa Kamanda Magoma Jr Magoma, kwa sasa ni Mkurugenzi wa Elimu na Afya katika taasisi ya ArDF (nikiwa na jukumu kubwa la kuhakikisha tunafanikiwa kutimiza malengo ya taasisi ya ArDF katika nyanja za Afya na Elimu) si kama ambavyo mleta mada ameeleza bila kuwa na haya wala soni hata tone kwa kufanya upotoshaji wa hali ya juu bila kupima madhara yake kwa jamii kwamba Lema katutapeli shamba alio omba kujenga hospital ya Wazazi. Napenda nileezee historia ya awali ambayo ninahisi wanachi wengi hasa waishio nje ya Arusha hawaifahamu na wangependa kuifahamu. Mwaka 2010 katika kampeni za uchaguzi mkuu Kamanda Lema aliahidi kwamba atajenga hospitali ya mama na mtoto katika jimbo la Arusha mjini endapo atapewa dhamana ya kuliwakilisha jimbo la Arusha mjini katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kamanda Godbless Lema alisema ili kuondoa adha ya huduma za afya kwa mama na mtoto, hasa ikizingatia kuwepo kwa msongamano na wagonjwa katika hostpitali ya Mkoa wa Arusha (Mount Meru) mkinichagua nitajenga hostiptali ya mama na mtoto. Baada ya kamanda Lema kushinda alikutana na wadau wengine wa maendeleo katika jimbo la Arusha na kuamua kuanzisha Taasisi ya Maendeleo ya jimbo la arusha (ArDF). Aidha moja na malengo ya msingi ya ArDF ni kujenga hospitali ya mama na mtoto, hivyo ili kuweza kufanikisha malengo ya kujenga hospitali kiwanja ni semehu ya vitu muhimu katika utekelezaji wa ujenzi, hivyo wadau wa Maendeleo walitupatia eneo la ukubwa wa ekari tano katika eneo la Burka, na ili kuweka kumbukumbu sahihi kiwanja hicho kiko chini ya ArDF kikiwa kinasimaniwa na Mama na Mtoto Foundation (Taasisi tanzu ya ArDF) na kwamba si kweli kiwanja hicho kinamilikuwa na Kamanda Godbless Lema na wala hakijabadilishwa umiliki wake wa awali kama ambavyo ndugu Lengio atanaka kuupotosha umma. Hivyo napenda kuwajulisha kwamba alicho andika ndugu Lengio ni uongo na hali ya juu na ni uposhaji uliopiliza mipaka. Chadema ni chama chenye viongozi makini wenye lengo la dhati la kuijenga Tanzania. Aidha nichukue fursa hii kuwajulisha wanachi wa Arusha kwamba tumekuwa tukiwasiliana na wadau na wataalum wa Afya na baada ya muda tutaanza ujenzi wa Hospitali ya mama na watoto, ikisimamiwa na Mama na Mtoto Foundation. Umoja Wetu ndio Silaha yetu
Naomba kuwasilisha,
Asanteni Wana JF.
Kamanda Magoma Jr Magoma
(Mkurugenzi wa Elimu na Afya ArDF)
(M/Kiti Mstaafu CHADEMA Wilaya Arusha Mjini)
Hoja na viroja vya nyongeza?
Tuwekee hati ya kiwanja hapa ili kuondoa utata simple as that watu waone jina la kiwanja na hata ikibidi weka michoro kwani kuna siri gani hapa?