Godbless Lema avuliwa ubunge

Status
Not open for further replies.
Machungu niliyonao aisee serikali isinipe post ya kua judge siku moja haki itatendeka tu, miaka hii kikwete alichagua majaji kwa criteria za ajabu sana, ukisoma judgment zao ni aibu tupu, hapo ndo napomkumbuka the late Mwalusanya J(as he the wa) alikua hateteleki na serikali, naona hakusoma vizuri criminal, civil na jurisprudence tort ndo alikimbikia kabisa darasani
 
Swala Dr Slaa kugombea A town nijema mno!Sio kwamba Lema hafai ila wanamtega nahukumu ili asipokata rufaa maana yake alitenda kosa so akigombea watamuwekea pingamizi tena wanaweza wasiwe ccm bali vyama vingine vikishinikizwa na ccm!Ili aondelewe wabaki vyama B ili A wapite kiulaini!Asipokata rufaa asigombe Chadema isimamishe mgombea mwingine nahasa DR!
 
wakuu ambaye ana summary ya kesi atuwekee basi sijui mnaita jurisdendi
 

Kabla ya kumshauri kukata rufaa umeshaisoma huku yenyewe na kuilewa? Rufaa hazifanywi kisisa wewe. Nenda kasome hukumu kwanza halafu uje hapa na vigezo vya kisheria vya kukata rufaa.
 
sijui kama bado kuna strategic thinkers ndani ya CCM. kama bado hawajaona umaarufu wa Chadema basi warudi tena kwenye uchaguzi mdogo hivi karibuni. Kwa vyovyte vile watashindwa vibaya sana. na hii ina madhara makubwa sana kwao kama chama na taasis. kwa mtandao wa vyombo vya habari ulivyo na kwa aina ya kampeni zifanywazo kwa sasa, ni vigumu sana kwa kampeni ya uchaguzi mdogo kujikita kwenye masuala ya jimbo husika pekee. linakuwa ni suala la kitaifa ambalo kila raia analifuatilia. sasa kuitisha uchaguzi mwingine hivi karibuni na kushindwa tena vibaya ni mbaya kwa CCM kitaifa. CCM wanaweza jidai kuwa watatafiti na kusuka mikakati mipya na kutumia watu tofauti na waliotumika Arumeru Mashariki. Lakini wajuer kuwa CCM kama taasis haina watu wawezao kusimama na kubadili upepo wa kisiasa. ni kama kupambana na wimbi kubwa dhidi yao. hii ni kujipaka petroli na kupita juu ya moto. nawahurumia sana CCM lkn kwa mwenendo huu wanafanya kampeni ya urais ya Chadema kuwa nyepesi zaidi. na badala ya chadema kutumia muda na resources zao nyingine kwenda vijijini na kujiimarisha, sasa wamepata platform ya uhakika zaidi, ambayo kwa kusimama jukwaani katika jimbo moja, tayari inakujengea umaarufu mbali zaidi na ulipo. kwa kuhitimisha, Lema asikate rufaa mahakamani. arudi kwenye uchaguzi, ambao atashinda bila shida kubwa, mradi awe makini kudhibiti uchakachuaji, ambao CCM ndo silaha yao kubwa kwa sasa. kwa mara nyingine, Mungu anatuonesha watanzania kuwa anaipenda hii nchi na pumba zitajionesha tena hivi karibuni.
 
Iwapo kuvuliwa kwa ubunge kwa Lema kutasababisha vurugu nashauri rais ajiuzuru. Vinginevyo ikulu patafuka moshi, watanzania wanaonekana kujawa na jazba na hasira juu ya kile kinachoonekana kuwa ni hila za CCM kwa CHADEMA na mahakama ikiwekwa kati. Ni vema wahusika wakawa makini na hili
 
 
Mambo yote yawe kama Senegal, unalazimisha kuingia kwenye uchaguzi na wananchi wanakujibu kwa sanduku la kupigia kura!
 
hakuna damu itamwagika Arusha mkuu..........watu wameelewa na tunasubiri kufanya maamuzi yetu kwenye sanduku la kura.....safari hii ni kimya kimya......
 
Dam tena ya nini CDM muwe na subira kama mkiti wenu alivyo wambia
 
Wananchi wa Arusha na maeneo mengine ya Tanzania wapokea taarifa za hukumu ya kesi ilikuwa inamkabili Mhemishiwa Lema kwa hisia kali. Wengine wamekuwa wakijiuliza je mahakama zetu bado zipo huru? mwana JF una maoni gani? uwanja ni wetu.....
 

Acha kauli za kuwatisha watu ww, usicheze na dola na lazima mfuate utawala wa sheria
 
Rais huyu ameletwa kwenu na NEC, Kwa msaada wa watu wa usalama
 
Wala hakuna haja ya kukata rufaa, acheni twende tena kwenye uchaguzi mdogo ndo thithiemu wajue watakavyochapwa. Na waelewe kuwa ccm ni chama cha upinzani kule Arusha!
 
Baada ya CHADEMA na Joshua Nassari kuwadhihirishia CCM huko Arumeru Mashariki kwamba wao wana fanya siasa za kisayansi na kimantiki, natabiri kuwa fursa ya kuendelea na kampeni za Ubunge Arusha Mjini katika siku 90 zijazo ni fursa ya CHADEMA kujiimarisha.

Nawasilisha hoja kwa WanaJF.
 
Hongera mahakama kwa kutenda haki,endeleeni kusimamia sheria kwani ndo kukuza utawala wa sheria
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…