MakeneTwo things wakuu. Walipanga kufanya hila na hujuma Arumeru Mashariki ili washinde huku pia wakituwinda Arusha Mjini ili wafanye kama walivyofanya. Thinking yao ikiwa ni kulenga total demoralization kwa chama mbadala CHADEMA na upinzani wenye nguvu kwa ujumla dhidi ya Watawala. Arumeru Mashariki ikashindikana.
Bahati mbaya risk calculation zao ni mbovu sana. Hazifanyia kazi sawasawa kwa sababu wamefika mwisho. Huwezi kutegemea mahakama kushinda ubunge Arusha Mjini dhidi ya CHADEMA. Watu wa Arusha wanaamini kwa dhati katika hii struggle. Wanakiamini na kukipenda chama chao. Wako pamoja na mbunge wao. Wasubiri waone.
Usisahau chupa kubwa za UHAI!...shindilia nyingi kwenye buti kule, najua zitasaidia group nzima!
batilda? yule aliye sema atavunja radio safina ajenge msikiti?hata waislam wenzake walimchukia kwahilo..akagombee uamirati..lile shangingi anapewa batilda!!
Mkuu, umesomeka vema....Makene
Mimi nililiona hilo mapema kabisa walitaka wapige double blow, imeshindikana.Kitu wasichojua ni kwamba wanafanya publicity ya bure kwa CDM. CDM wasiwe wanyonge kwa hili kwa sababu siasa si kukaa ofisini siasa ni kuwa karibu na wananchi kuongea nao. Hasara za kuvuliwa Lema kichama ni CCM na serikali yake kwa sababu inazidi kudumaza maendeleo ya wana Arusha hivyo kuongeza hasira za wananchi dhidi ya serikali ya CCM.
Ushauri wangu kwa chama na kwa Lema asikate rufaa kwani miezi mitatu si mingi,kwa sababu nina uhakika uchaguzi ukirudiwa atashinda vizuri ya alivyofanya lasttime. Hii itakuwa ni advantage kwa CDM, itavunja rekodi yake ya kushinda chaguzi ndogo mfululizo, kwa hiyo watu watazidi kukiamini.
Ushauri mwingine ni kuwa, strategically kampeni za Arusha mjini zitajipiga zenyewe, nguvu kubwa (50-60%) kama ni kwenye budget au mali watu ipelekwe kwenye ulinzi wa kura, vituo vijulikane mapema na wapiga kura wajulikane mapema, nafikiri kama ni mtaji wa vijana basi Arusha mjini mnao mkubwa kuliko Arumeru Mashariki.
Mbona mimi siwalewi, wewe na PJnini maji ya uhai....nakuja na maski na ovaroli.... M4C...
Ni mawazo mazuri.
Lakini mtazamo kama huu wa kukiona CCM kama vile ni chama chenye mbinu nyingi, chenye "uwezo wa kipekee", chenye makali n.k., kiasi kwamba tunakiwa tunakiogopa, siyo mzuri. Halafu kibaya zaidi, kama tunafahamu hivyo, nini tunafanya? Je, tunaendelea kukubaliana na hali hiyo? Hivi mbona tunasahau kwamba sisi ndiyo wenye nchi!?! Inasikitisha kwa kweli.
Sidhani kama ni mtazamo chanya sana, kama sisi ambao "angalau" tuna mwanga mwanga kiasi, tunawaza hivyo, je wale ambao bado wako gizani kabisa, si wanakiona CCM kama mungu-chama!!
Kwa hali ya sasa CCM haina ujanja wowote, zaidi ya kutumia "uwoga" wa watanzania wengi, kama inavyojidhihirisha hapa JF mara kadhaa.
Hapana hakuna haja ya rufaa juu ya hili,
kwa hukumu hii mahakama inatia mashaka makubwa,
turudi kwenye uchaguzi wapiga kura tutaamua.
Formula ni ileile, piga kura linda kura.
Mimi nililiona hilo mapema kabisa walitaka wapige double blow,