Ninachofurahi na kumshukuru Mungu ni kwamba CHADEMA ina viongozi, waabunge na wanachama wenye akili. Pia ninamshukuru Mungu kuwa Watanzania tumeshafunguka na tunaendelea kufunguka macho kuona uozo wa CCM. Ni masikitiko makubwa kuwa bado CCM inaendelea kutumia kodi za wananchi kughrimia na kuhonga ili kupitisha sera zao ambazo zimeshakataliwa. Kwa sasa serikali haina hela, shughuli za kimaendeleo na za kawaida kwa serikali katika Wizara na taasisi zake zimelalla, hakuna OC (Other Charges) ya kutosha matokeo yake watumishi wake wanaingi aofisini na kusaini vitabu. Je tutapimaje utendaji au mafanikio ya Ilani ya Chama kama serikali haifanyi kazi? Matokeo yake tunapoambiwa kuandika progress report ya robo mwaka, nusu mwaka au mwaka basi hakuna cha kuandika!!!! Pesa ya kurudia uchaguzi ingetumika kugharimia kazi jamani. It is very painful. Tuwe wazalendo. Siasa kwa upande wangu zinapingana sana na maendeleo. Sasa nasubiri pesa itakayotumika Arusha tena, si mngezipeleka kule tulikoahidi ahadi za matrilion ya hela wakati wa uchaguzi wa awamu ya nne awali na huu wa mwisho. Je 2015 tutawaaambiaje wananchi? Hebu tuchambue kwa kutumia akili na si hisia. Nawasilisha, CCM chukuen hatua. Nampongeza NCCR kwa kufuta kesi, jimbo la Kawe dhidi ya Halima Mdee. Naweza kusema Mr. Mbatia aliona mbali zaidi madhara ya uchaguzi kama Mdee angetenguliwa. Tuachane na umimi inapokuja suala la matumizi mabaya ya rasilimali na kodi za walala hoi kwenye chaguzi kisizo na mvuto. Yaani hata ubungo mnathubutu kupoteza muda wa wanasheria, mawakili wa serikali na muda wa mh. Mnyika? Acheni mbofuuuuumbofuuuuuuu.