Godbless Lema akamatwa Kajiado akitorokea Kenya yeye na familia yake. Kurudishwa nchini kesho Novemba 9, 2020

Siasa bila watu unaweza wehuka, mtaji wa mwanasiasa ni watu.

Wewe ni mzima Kweli?

Una uelewa mdogo sana ndio maana unatoa tuu mitusi bila kujenga hoja.

Haya nenda kaandamane sasa
Mzima kabisa wala si nusu. Uelewa mdogo sana wa kishetani. Matusi ni kuona uelewa wangu mdogo na wewe bonge la GT. Vile unaona mabandiko yako ni hoja? Pole. Simple mind ndiye awezaye kusema : kaandamane sasa. Diabolic thinking, mama Devil. Sijatukana binadamu. I call a spade a spade. If the cap fits you wear it.
 
Ahaaa mada ina uzito gani? Nauliza hivi wananchi kumg'oa dictator anayetawala mpaka iwe nguvu ya ndani tu?

Sasa unashangaa nini akina Lema kukimbilia nje wakati nguvu ya kumng'oa dictator sio lazima iwe ya ndani tu?
 
Rais wa sasa wa Egypt baada ya maandamano ya kumng'oa Mubarak hakuingia kwa kura, maana box la kura huko lilishapoteza maana kama ilivyo hapa Tanzania sasa. Misingi ya katiba ya chama kimoja imepitwa na wakati na ndio maana tumefikia hali hii. Tuna katiba iliyokataliwa na mtawala ili aburuze watu. Subiri uone kitakachofanywa na bunge hili ili ujue dhamira ya kunajisi uchaguzi huu, lengo lake lilikuwa ni nini.
Tanzania inafuata misingi ya chama kimoja?
Hapa Tanzania kuna rais aliyeingia kwa kupindua?

Chadema kukosa wabunge ndio sababu ya kusema uchaguzi ulikuwa najisi? Wapi imeandikwa kwenye katiba Chadema

Nashangaa wao kukimbia nchi wakati kuna amani na nchi inatawaliwa kwa misingi ya sheria
 
Mzima kabisa wala si nusu. Uelewa mdogo sana wa kishetani. Matusi ni kuona uelewa wangu mdogo na wewe bonge la GT. Vile unaona mabandiko yako ni hoja? Pole. Simple mind ndiye awezaye kusema : kaandamane sasa. Diabolic thinking, mama Devil. Sijatukana binadamu. I call a spade a spade. If the cap fits you wear it.
Nimekupuuza kama ulivyo mwenyewe
 
Stunt

Lema hakuuawa alipokuwa mbunge leo sio mbunge kabakiwa na suruali nani anataka kumuua?

Lema ni threat kwa nani??

Kama personal issue alikabili tu
Small mind. Wanaouwawa wote lazima wawe wabunge tu? Akina Azori Gwanda wako wapi nao walikuwa ni wabunge?

Mkakati unaonekana kuwalenga viongozi waandamizi wa Chadema ili wasipate mwanya wa kujipanga kwa siku zijazo.

Inavyoonekana kuna mkakati umeandaliwa wa kuifanyia katiba mabadiliko fulani ili kukidhi matakwa ya mtu mmoja na ndio sababu ya uchaguzi kuhujumiwa lkn huko tuendako hii nchi historia yake itabadilika sana. Tuweke macho.
 
Hii ni ajabu sana, yaani Kenya mtu ameingia na kuomba hifadhi ya usalam wa kisiasa na anakataliwa mara moja na kurudishwa alikotoka ilhali anajulikana kabisa kuwa ni mwanaharakati wa siasa za upinzani? Kenya naona wanajitafutia matatizo na umoja wa mataifa!
 
Tanzania inafuata misingi ya chama kimoja?
Hapa Tanzania kuna rais aliyeingia kwa kupindua?

Chadema kukosa wabunge ndio sababu ya kusema uchaguzi ulikuwa najisi? Wapi imeandikwa kwenye katiba Chadema

Nashangaa wao kukimbia nchi wakati kuna amani na nchi inatawaliwa kwa misingi ya sheria

Toka awamu hii imeingia madarakani vyama vingi vipo kinadharia na sio kiuhalisia. Hakuna aliyeingia kwa kupindua nchi, ila sasa anayetawala hana tofauti na aliyeingia kwa kupindua nchi. Si lazima cdm kupata wabunge, ila kukosa huko isiwe kwa hiki kilichofanyika juzi. Hofu sio amani, nchi ina amani kisha mitandao ya kijamii inazimwa!?
 
Wangekuwa wanaogopa gharama tusingewaona wakitumia ma VX kwa mizunguko isiyo na tija.
Mkuu, suala la uhai wa mtanzania awaye yeyeote siyo la mzaha ni kwa msingi huo huo suala la kufanya uchunguzi juu ya nani hasa walishiriki kumshambulia ndugu Antipasu na walikuwa na lengo gani, pia haliwezi kufaanywa kimzaha!

Lazima kila kitu kichunguzwe ambacho kinaweza kurahisisha kupatikana taarifa za kufikia lengo la uchunguzi huo. Dereva aliyekuwa na Antipasu wakati wa shambulizi hilo ni shahidi muhimu sana na ndiye hasa aliyeona tukio zima hata baada ya ndugu Antipasu kuwa katika hali ya hatari zaidi kiafya.

Kitendo cha kutetea kumficha dereva huyo wakati ni muhimu katika uchunguzi huu! Kinazalisha maswalj mengi zaidi ya majibu. Maswali mojawapo ni je dereva ana siri gani ambazo hata yeye mwenyewe Ndugu Antipasu hataki wachunguzi wa kushambuliwa kwake na watanzania kwa ujumla hataki wazijue!?
 
Rais wa sasa wa Egypt baada ya maandamano ya kumng'oa Mubarak hakuingia kwa kura, maana box la kura huko lilishapoteza maana kama ilivyo hapa Tanzania sasa. Misingi ya katiba ya chama kimoja imepitwa na wakati na ndio maana tumefikia hali hii. Tuna katiba iliyokataliwa na mtawala ili aburuze watu. Subiri uone kitakachofanywa na bunge hili ili ujue dhamira ya kunajisi uchaguzi huu, lengo lake lilikuwa ni nini.
Ww unaona mfumo wa chama kimoja umepitwa na wakati. Sawa.

Jiulize hivi, nn madhara mabaya ya mfumo wa vyama vingi kwa taifa letu?? Na mfumo huo unatupeleka wapi??

Kwa mtazamo wangu, mfumo wa vyama vingi unatupeleka kwenye migogoro endelevu inayokua nchini kama kipele cha cancer kinavyoota mwilini. Mifumo hiyo inatujengea chuki kati ya watu wa taifa moja, na kuishia kugombana au kuuana cc kwa cc.
 
Wangekuwa wanaogopa gharama tusingewaona wakitumia ma VX kwa mizunguko isiyo na tija.
Vipi yule aliyekua anatembelea helicopter wakati wa campaign za uchaguzi ? Hivi akipata uraisi si ndio atakua na private jet!!
 
Toka awamu hii imeingia madarakani vyama vingi vipo kinadharia na sio kiuhalisia. Hakuna aliyeingia kwa kupindua nchi, ila sasa anayetawala hana tofauti na aliyeingia kwa kupindua nchi. Si lazima cdm kupata wabunge, ila kukosa huko isiwe kwa hiki kilichofanyika juzi. Hofu sio amani, nchi ina amani kisha mitandao ya kijamii inazimwa!?
Ahaaa, malalamiko ni haya haya tokea utawala wa hayati Mkapa.

Ulitaka wakose vipi ili ulidhike? Mitandao kuzimwa kwa usalama ni jambo la kawaida hasa kwa serikali makini ambayo inajitambua.
 
Mkuu, suala la uhai wa mtanzania awaye yeyeote siyo la mzaha ni kwa msingi huo huo suala la kufanya uchunguzi juu ya nani hasa walishiriki kumshambulia ndugu Antipasu na walikuwa na lengo gani, pia haliwezi kufaanywa kimzaha!

Lazima kila kitu kichunguzwe ambacho kinaweza kurahisisha kupatikana taarifa za kufikia lengo la uchunguzi huo. Dereva aliyekuwa na Antipasu wakati wa shambulizi hilo ni shahidi muhimu sana na ndiye hasa aliyeona tukio zima hata baada ya ndugu Antipasu kuwa katika hali ya hatari zaidi kiafya.

Kitendo cha kutetea kumficha dereva huyo wakati ni muhimu katika uchunguzi huu! Kinazalisha maswalj mengi zaidi ya majibu. Maswali mojawapo ni je dereva ana siri gani ambazo hata yeye mwenyewe Ndugu Antipasu hataki wachunguzi wa kushambuliwa kwake na watanzania kwa ujumla hataki wazijue!?

Mkuu ni kwamba unaona unajadili na mtoto au? Lisu amekuja hapa na kukaa zaidi ya miezi mitatu, mbona hajahojiwa chochote wakati yeye ndio aliyeshambuliwa? Dereva anatakiwa sio kuhojiwa bali kutishiwa ili kukishwa maneno ili apoteze ushahidi. Tunafahamu utendaji kazi wa vyombo vyetu vya uchanguzi.
 
Vipi yule aliyekua anatembelea helicopter wakati wa campaign za uchaguzi ? Hivi akipata uraisi si ndio atakua na private jet!!

Private Jet zina tofauti gani na huyu mzalendo ambaye kila aendapo kuna helicopters za ulinzi zinazunguka angani?
 
Hizo helicopters unazosemea ni kwa ajili ya usalama wa wananchi na usalama wake yeye kama raisi (kwani alikua hajavuliwa uraisi wakati huo) . Mm naona alikua na haki zote za kulindwa na hizo helicopter za ulinzi kama raisi.
 
Private Jet zina tofauti gani na huyu mzalendo ambaye kila aendapo kuna helicopters za ulinzi zinazunguka angani?
Mkuu wa nchi lazima apewe ulinzi wa kutosha,hasa rais mzalendo ambae analinda rasilimali za nchi,anakuwa na maadui wengi hasa mabeberu na mafisadi.
 
Ahaaa, malalamiko ni haya haya tokea utawala wa hayati Mkapa.

Ulitaka wakose vipi ili ulidhike? Mitandao kuzimwa kwa usalama ni jambo la kawaida hasa kwa serikali makini ambayo inajitambua.

Unadhani hatujui tofauti ya sasa na awamu zilizopita? 2015 mbona haikuzimwa
Hizo helicopters unazosemea ni kwa ajili ya usalama wake yeye kama raisi (kwani alikua hajavuliwa uraisi wakati huo) na usalama wa wananchi

Huyo unayesema akiwa madarakani atatumia private jet na yeye atasema ni kwa ajili ya usalama wake, kisha watatokea wapambe kama ww watetee huo uhuni. Tumekuwa na marais wa nne mpaka sasa, mbona hatukuwahi kuona ulinzi wa helicopters na makomandoo kama sasa, kipi cha maana sana kwa huyu?
 
Unadhani hatujui tofauti ya sasa na awamu zilizopita? 2015 mbona haikuzimwa

Huyo unayesema akiwa madarakani atatumia private jet na yeye atasema ni kwa ajili ya usalama wake, kisha watatokea wapambe kama ww watetee huo uhuni. Tumekuwa na marais wa nne mpaka sasa, mbona hatukuwahi kuona ulinzi wa helicopters na makomandoo kama sasa, kipi cha maana sana kwa huyu?
Hujui? Au unajifanya hujui? Hujui kuwa ana maadui wengi? Unadhani wanafurahi anavyolinda rasilimali za nchi? Unadhani wanafurahi anavyodhibiti ufisadi?
 
Mkuu wa nchi lazima apewe ulinzi wa kutosha,hasa rais mzalendo ambae analinda rasilimali za nchi,anakuwa na maadui wengi hasa mabeberu na mafisadi.
Kweli kabisaa. Halafu tukumbuke pia mabeberu, makaburu na mafisadi (vibaraka wa wakoloni), wamekasirika sana sababu raisi wetu aliwaumbua kwenye vipimo vya corona 🙈. Yeleuwii
 
Mkuu wa nchi lazima apewe ulinzi wa kutosha,hasa rais mzalendo ambae analinda rasilimali za nchi,anakuwa na maadui wengi hasa mabeberu na mafisadi.

Nyerere alikuwa ndio mzalendo wa kweli nchi hii, acha hawa walioanza uzalendo baada ya kupewa madaraka. Mbona hatukuwahi kumuona na ulinzi wa mbwembwe hivyo? Ni hivi hakuna la zaidi, zaidi ya ulevi wa madaraka fullstop.
 
Back
Top Bottom