Godbless Lema akamatwa Kajiado akitorokea Kenya yeye na familia yake. Kurudishwa nchini kesho Novemba 9, 2020

Nyerere alikuwa ndio mzalendo wa kweli nchi hii, acha hawa walioanza uzalendo baada ya kupewa madaraka. Mbona hatukuwahi kumuona na ulinzi wa mbwembwe hivyo? Ni hivi hakuna la zaidi, zaidi ya ulevi wa madaraka fullstop.
Zama alizotawala Nyerere unaweza kulinganisha na zama hizi? Sometimes kaa na kutafakari juu ya argument zako.
 
Hujui? Au unajifanya hujui? Hujui kuwa ana maadui wengi? Unadhani wanafurahi anavyolinda rasilimali za nchi? Unadhani wanafurahi anavyodhibiti ufisadi?

Maadui wapi, mnatengeza taswira wenyewe kisha mnataka tuamini hayo maigizo yenu? Kuna rasilimali gani nchi hii ya kusema anatafutwa? Hatukatai ulinzi maana ni sahihi kwa nafasi yake, ila sio kwa huo wa ufujaji wa pesa.
 
Zama alizotawala Nyerere unaweza kulinganisha na zama hizi? Sometimes kaa na kutafakari juu ya argument zako.

Hizo zama za kina Nyerere si ndio waliuliwa viongozi wengine wa kiafrika wazalendo? Au mauaji ya viongozi yameanza baada ya awamu hii kuingia madarakani?
 
Unadhani hatujui tofauti ya sasa na awamu zilizopita? 2015 mbona haikuzimwa

Huyo unayesema akiwa madarakani atatumia private jet na yeye atasema ni kwa ajili ya usalama wake, kisha watatokea wapambe kama ww watetee huo uhuni. Tumekuwa na marais wa nne mpaka sasa, mbona hatukuwahi kuona ulinzi wa helicopters na makomandoo kama sasa, kipi cha maana sana kwa huyu?
Huyo TL hajapata uraisi anatumia helicopter kila anapoenda, jiulize ninani anampa hizo pesa za kutembelea usafiri wa anga ilihali hatujui shughuli au biashara zake hapa Tanzania zinazoweza kumuwezesha kutembelea usafiri wa anga??!!

Hujawahi kuona ulinzi mkubwa wa raisi kama huo sababu huyu baba ni raisi wa kwanza kwa Tanzania kutangaza vita vya uchumi.
 
Utandawazi umeleta mabadiliko makubwa sana. Zama za akina Nyerere na zama hizi ni tofauti japokuwa waliuliwa na kupinduliwa wengi.
 
Huyo TL hajapata uraisi anatumia helicopter kila anapoenda, jiulize ninani anampa hizo pesa za kutembelea usafiri wa anga ilihali hatujui shughuli au biashara zake hapa Tanzania zinazoweza kumuwezesha kutembelea usafiri wa anga??!!

Hujawahi kuona ulinzi mkubwa wa raisi kama huo sababu huyu baba ni raisi wa kwanza kwa Tanzania kutangaza vita vya uchumi.

Tulichanganya pesa zetu kumuwezesha kutumia chopa.

Inaonekana umezaliwa miaka ya 2,000. Alikuwepo Nyerere mzalendo wa vitendo sio mzalendo baada ya kupata madaraka. Alitangaza vita vyote kuanzia vya kuanzia uhujumu uchumi, mpaka ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika.
 
Nyerere alikuwa ndio mzalendo wa kweli nchi hii, acha hawa walioanza uzalendo baada ya kupewa madaraka. Mbona hatukuwahi kumuona na ulinzi wa mbwembwe hivyo? Ni hivi hakuna la zaidi, zaidi ya ulevi wa madaraka fullstop.
Kwa mtazamo wangu baada ya Nyerere kuwang’oa wakoloni nchini hakua na maadui wengi sana kama alionao mzee wangu JPM, sababu wakoloni walipoondoka nchini waliacha vibaraka wao (mafisadi).

Hao mafisadi walikua wakicheza mchezo mchafu wakiruhusu mchanga wa makinikia kwenda kupimwa nchini mwao. TL na wafuasi wake walipoona wale mabwana wa Barrick wanabanwa, Mererani kuzungushiwa ukuta, wakasema JPM anafukuza wafadhili.
 
Tulichanganya pesa zetu kumuwezesha kutumia chopa.

Inaonekana umezaliwa miaka ya 2,000. Alikuwepo Nyerere mzalendo wa vitendo sio mzalendo baada ya kupata madaraka. Alitangaza vita vyote kuanzia vya kuanzia uhujumu uchumi, mpaka ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika.
Mlitoa wapi hizo pesa ilihali mlisema JPM amekaza vyuma ??
Sawa hata kama mlijichangisha, mlikubali vipi wakati kila chama hupewa fungu lake kwa ajili ya kampeini za uchaguzi??

Semeni tu ukweli kuwa Bob Amsterdam na mtandao wake ndio wamesupport huo usafiri wa anga.
 
Lema anatoroka kesi yake ya kupanga maandamano. Lazima arudi ili aisaidie police. Kukosa kula kwenye ubunge kumezua nongwa kwa hii saccos.
 
Unadhani hatujui tofauti ya sasa na awamu zilizopita? 2015 mbona haikuzimwa

Huyo unayesema akiwa madarakani atatumia private jet na yeye atasema ni kwa ajili ya usalama wake, kisha watatokea wapambe kama ww watetee huo uhuni. Tumekuwa na marais wa nne mpaka sasa, mbona hatukuwahi kuona ulinzi wa helicopters na makomandoo kama sasa, kipi cha maana sana kwa huyu?
Daah mzee baba una moyo sana,kubishana na hizo Lumumba bots ni bora huo muda ukapige puliiiiiiiii tu ujue 1
 
Godbless Lema akamatwa Kenya akitafuta hifadhi Ubalozi wa Marekani

Aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini kupitia CHADEMA, Godbless Lema amekamatwa na Polisi katika Kaunti ya Kajiando nchini Kenya baada ya yeye na familia yake kuvuka mpaka wa Namanga.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Standard Media ya Kenya Lema alikuwa na mkewe, Neema Godbless na watoto wao watatu.Lema ameliambia gazeti hilo kuwa maafisa wa uhamiaji walikataa kugonga muhuri nyaraka zilizowasilishwa na mke wake, kwa madai hadi wamuone Lema. Amesema mke wake alipomuita alikwenda lakini akawaambia hana hati yake ya kusafıria kwa sababu alikuwa hasafıri, na kwamba mke na wanae walikuwa wanakwenda kutafuta shule ya kimataifa Kenya.

Maafisa waliruhusu mke na watoto kuvuka mpaka, na Lema aliomba kwenda kutafuta fedha za Kenya ili ampe mke wake ambaye alisema kwamba angeendelea na safari yeye na watoto. Lakini mara tu alipovuka mpaka, Lema na familia yake waliingia ndani ya gari la mwanasheria wake, George Luchiri ambaye alikuwa akifuatilia mchakato mzima wa Lema kuvuka mpaka kuingia Kenya. Maafisa hao wa uhamiaji walitoa taarifa polisi kwamba kuna mtu ameingia nchini humo pasi na kuwa na nyaraka husika. "Polisi walitufuatilia na wakatukamata tukiwa Ilbisil na kutupeleka kwenye kituo cha polisi.

Sikutaka wamuweke Lema hapo kutokana na ukaribu wake na mpaka wa Tanzania," mwanasheria huyo ameiambiba The Standard Media.

Mwanasheria huyo amesema alifahamu kwamba Lema anakwenda Kenya na kwamba alitaka ampeleke Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (UNHCR) mara tu atakapavuka mpaka.

Luchiri amesema kwa mujibu wa UNHCR mtu anayetafuta hifadhi hahitaji kuwa na nyaraka za kumuwezesha kuingia nchi nyingine. Akieleza sababu za kutokutoa hati yake ya kusafıria, Lema amesema alijua kwa kufanya hivyo, maafisa hao wangemshikilia na kumzuia kuvuka.

"Nimeacha kila kitu nyumbani. Hivyo havina umuhimu kwa sasa. Muhimu ni usalama wangu na usalama wa familia yangu. Nipo na wanangu Allbless, Brilliance na Terrence. Sijui kesho itakuja na nini. Kwa sasa natafuta hifadhi," Lema ameiambia The Standard. Mwanasheria huyo amesema atawasilisha taarifa za Lema katika Ubalozi wa Marekani kwani amekuwa akifanya mawasiliano na maafisa wa ubalozi huo.

Wakati hilo likitokea, aliyekuwa mgombea Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA, Tundu Lissu yupo Ubalozi wa Ujerumani jijini Dar es Salaam alipokwenda kuomba hifadhi akidai ametishiwa kuuawa.

Chanzo: swahilitimes
Umesema Tume ya Haki za Binadamuinaitwa

UNHCR ndio tume ya haki za binadamu?
 
Sio jambo jema kuifananisha nchi ya Kidemokrasia inayofuata misingi ya haki za binadamu na Zaire ya Mobutu au Uganda ya Amin

Msitake kusema kuwa watanzania walitiwa hofu,watanzania wanajua hakuna dhuluma,kama kuna dhuluma wao wenyewe wataandamana na kutaka haki.

Pia usifananishe Rwanda na Tanzania, genocide ya Rwanda ilipofanyika kila mtu aliona kilichotokea, acha kupotosha umma kwa mifano ya hovyo.
Tumeulizwa wakati hayo yanafanyika waliridhia hivyo wasiandamane? Unakurupuka na kubwabwaja tu. Unatoa majibu ya Changu wa Madoa!
 
Jamaa naona wanajitahidi kila mbinu kuifanya Tanzania ionekane kua si nchi salama...
Time will tell. Hao watakua kama wale wakimbizi wa kizanzibari waliokimbilia UK kuomba ukimbizi wakidai hawapo salama.
Muingereza akafanya uchunguzi wake wa kina na baada ya kugundua uhalisia wengine walirudishwa kwao Zanzibar.
 
Dunia inauona ukweli, hali ya usalama wa nchi si jambo la kuficha, hii ni kukosa uzalendo, hakuna yeyote katika nchi zilizoendelea anaweza kufanya haya...Taifa kwanza..
 
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom