Kwa sisi wenye akili timamu hakika hatuachi kuwacheka na kuwashangaa hawa wabunge wa upinzani kwa huu undumilakuwili na uendawazimu wanaoionesha. Sijajua hasa ni nini kinawapanda vichwani mwao mpaka wanashindwa kutunza kumbukumbu zao vizuri na kusahau nini walifanya jana yake ili waoanishe na wanachofanya leo.
Ameanza Godbless Lema kummiss Rais Jakaya Kikwete ambaye amemaliza muda wake Novemba tano 2015. Wamesahau kuwa ni huyu huyu Kikwete ndiye walimuita Rais dhaifu kuweza kutokea Tanzania.
Sasa wameanza kilio kipya cha kumlilia Spika Job Ndugai wakidai kuwa Naibu Spika Dr Tulia Akson anawakandamiza na kuwaziba midomo ili wasisikike. Hakika madai haya yamenishangaza sana na kuniacha mdomo wazi. Je ni nini hasa wanachokitaka hawa wapinzani? Je wana madai mapya ama ni kuendeleza kile walichofanya miaka iliyopita?
Hebu soma habari hii hapa chini then Uniambie kama Wapinzani wanatumia akili kufikiri ama wanatumia viungo vingine vya miili yao.
WAPINZANI WAUNGANA KUMSUSIA NAIBU SPIKA JOB NDUGAI
KWA mara ya kwanza tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa 2010, wabunge wa vyama vya upinzani Februali Mosi 2013 waliungana pamoja na kumsusia Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, wakipinga hatua yake ya kupindisha hoja binafsi ya Mbunge wa kuteuliwa na Rais, James
Mbatia (NCCR-Mageuzi) na kuitetea serikali bila maelezo yanayoeleweka.
Kwa pamoja, wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), National Convention for Construction and Reform (NCCR- Mageuzi), United Democratic Party (UDP) na Chama cha Wananchi (CUF) walitoka nje ya ukumbi wa Bunge wakaenda ukumbi wa kambi ya upinzani kufanya kikao cha dharura juu ya hatua za kuchukua dhidi ya ubabe wa Ndugai.
Hatua kama hiyo ya kutoka nje ya ukumbi wa Bunge, imekuwa ikitumiwa na wabunge wa CHADEMA ambayo inaunda kambi rasmi ya upinzani bungeni kupinga baadhi ya masuala kadhaa.
Hata hivyo, kwa mara mbili tofauti CHADEMA waliposusia Bunge, wenzao wa vyama vingine hawakuwaunga mkono, hatua iliyotafsiriwa kama kutokuwapo kwa mshikamano.
Kwa mara ya kwanza, CHADEMA walisusia hotuba ya Rais Jakaya Kikwete ya kufungua Bunge, wakipinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliyomleta madarakani na mara ya pili walitoka nje ya ukumbi wakipinga kupitishwa kwa sheria ya mabadiliko ya katiba mpya.
Hali hiyo ni tofauti na Februari Mosi 2013 ambapo wabunge wa vyama hivyo vya CHADEMA, CUF, UDP, TLP na NCCR-Mageuzi waliungana kwa kutoka nje ya ukumbi wa Bunge, kupinga hatua ya Ndugai kuwaburuza katika kupitisha hoja ya Mbatia.
Hoja hiyo binafsi iliyoainisha udhaifu katika mfumo wa elimu nchini, iliwasilishwa na kuibua mjadala mzito bungeni, huku kambi ya upinzani ikikubali hoja ya Mbatia kutaka kuunda kamati teule wakati wabunge wa CCM wakipinga.
Mzozo wa jana ulianza baada ya Mbatia kufunga hoja yake na kutaka Waziri wa Elimu na
Kwa muktadha huu, nawaomba wasomaji wa uzi huu muuweke kwenye makabrasha yenu ili tukikutana baada ya uchaguzi wa 2020 tuje tujikumbushe. Kwa hakika hamtaamini. Hawa hawa wanaompinga leo Dr Tulia ndio watakaomlilia. Ni kawaida yao kwani walifanya kazi kubwa ya kunadi ufisadi wa Lowasa na genge lake lakini ni hao hao leo wanamsafisha. Kazi wanayo