CHADEMA, Kikwete alikuwa dhaifu kama mlivyosema, Magufuli je?

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
49,681
39,013
Wanaukumbi,

Hii ni kauli ya kiongozi wa Chadema John Mnyika, alisema nasikitishwa na jambo moja. Tumefika hapa kutokana na udhaifu wa Rais Kikwete.

Dua lake limekubaliwa yeye pamoja na wafuasi wa Chadema JK kaondoka sasa yupo Dr.John Magufuli siyo dhaifu.

Mbadala wa dhaifu ni kupata mtu jasiri bahati nzuri mmefanikwa muungeni mkono rais jasiri John Magufuli, dhaifu kaishaondoka.

"Pamoja na udhaifu alikuwa nao JK alikuwa sio mwoga wa kusikia maoni na ushauri kutoka upinzani hata kama hakuyatekeleza yote , hapo sina budi kumsifu, Mh. Magufuli anaonyesha udhaifu mapema sana anaogopa kukosolewa"

Huyu ni Mchungaji Msigwa
 
Ungejiuliza wewe kwa nini wakati CHADEMA wakisema JK ni dhaifu wewe ulikuwa unakataa? ukimaliza kujijibu ndio unaweza kuendelea na maswali mengine
 
Sawa tunamuunga mkono, miguuu, kichwa, akili na kila kiungo cha mwili.

Huyu anayatenda na kuyaishi yale yaliyokuwa yakipiganiwa na Chadema kwa muongo mmoja uliopita. Huyu ndiye anayefukunyua kwa uhakika madudu na maovu makubwa ya Ccm kiasi ambacho hata wao wanakereka.

Mambo ya kurekebisha kwa Magufuli ni machache sana kulinganisha na kipindi cha mzee wa Msoga. Magufuli karejesha heshima ya Taifa hili kitaifa na kimataifa, kwanini asiungwe mkono.?

Kumbuka wakati tunamuunga mkono ktk mambo flani, si kila kitu itakuwa hewala baba, hapana. Kazi yetu kama UPINZANI itabaki palepale, kamwe hutatuona tukimuunga mkono kwa kila jambo, je tutakuwa na tofauti ganj na ccm. Nanyi ccm vilevile ni lazima ufike wakati mkakubali kazi ya Upinzani, Upinzani unapokuwa unakosoa jambo fulani msijenge chuki kwetu, jengeni chuki juu ya jambo hilo linalokosolewa. Hapo tutaijenga Nchi kwa namna ambayo haijawahi kutokea.

Nadhani nimeeleweka mkuu Ritz

BACK TANGANYIKA
 
Kamanda JK hagombei tena kaishaindoka nyie mlikuwa mnampiga kuwa ni dhaifu hayupo tena kaja Magufuli muungeni mkono bahati nzuri tunaambiwa anaiga sera za Chadema.
 
Wanaukumbi,

Hii ni kauli ya kiongozi wa Chadema John Mnyika, alisema nasikitishwa na jambo moja. Tumefika hapa kutokana na udhaifu wa Rais Kikwete.

Dua lake limekubaliwa yeye pamoja na wafuasi wa Chadema JK kaondoka sasa yupo Dr.John Magufuli siyo dhaifu.

Mbadala wa dhaifu ni kupata mtu jasiri bahati nzuri mmefanikwa muungeni mkono rais jasiri John Magufuli, dhaifu kaishaondoka.

Waku kurupuka
 
Chadema wamekuwa kama wafa maji, hawana pa kushika wanatapatapa, wamebaki kulia lia tu, hayo yote kasababisha mbowe kubadili gia angani kwa kuwaruhusu mafisadi kukamata chama.
 
"Pamoja na udhaifu alikuwa nao JK alikuwa sio mwoga wa kusikia maoni na ushauri kutoka upinzani hata kama hakuyatekeleza yote , hapo sina budi kumsifu, Mh. Magufuli anaonyesha udhaifu mapema sana anaogopa kukosolewa"

Huyu ni Mchungaji Msigwa

Lipi jema!!?
 
Watanzania nashindwa kuwaelewa kuhusu utendaji wa Dr Magufuli, ........... tulifika muda tukatamani kuwa na mtu kama yeye,..... na ndo ashapatikana yeye na jopo lake tumuache maana ile ni TAASISI kwani hapa wengi mapovu yanatutoka 7bu ya kutojua maana yeye anapewa taarifa na usalama wa taifa
 
Sawa tunamuunga mkono, miguuu, kichwa, akili na kila kiungo cha mwili.

Huyu anayatenda na kuyaishi yale yaliyokuwa yakipiganiwa na Chadema kwa muongo mmoja uliopita. Huyu ndiye anayefukunyua kwa uhakika madudu na maovu makubwa ya Ccm kiasi ambacho hata wao wanakereka.

Mambo ya kurekebisha kwa Magufuli ni machache sana kulinganisha na kipindi cha mzee wa Msoga. Magufuli karejesha heshima ya Taifa hili kitaifa na kimataifa, kwanini asiungwe mkono.?

Kumbuka wakati tunamuunga mkono ktk mambo flani, si kila kitu itakuwa hewala baba, hapana. Kazi yetu kama UPINZANI itabaki palepale, kamwe hutatuona tukimuunga mkono kwa kila jambo, je tutakuwa na tofauti ganj na ccm. Nanyi ccm vilevile ni lazima ufike wakati mkakubali kazi ya Upinzani, Upinzani unapokuwa unakosoa jambo fulani msijenge chuki kwetu, jengeni chuki juu ya jambo hilo linalokosolewa. Hapo tutaijenga Nchi kwa namna ambayo haijawahi kutokea.

Nadhani nimeeleweka mkuu Ritz

BACK TANGANYIKA
Sasa kama mbona unatofautiana na kiongozi wako msome kidogo.

Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji amemtaka Rais Magufuli apunguze utumbuaji majipu. Adai inadhalilisha Watumishi wa SerikaliAlisema pamoja na kuwa CHADEMA wanaunga mkono kitendo cha kuwashughulikia mafisadi pamoja na watumishi wasio timiza majukumu yao ipasavyo lakini hawako tayari kuendelea kushuhudia ambavyo amekua akivunja sheria za nchi. “Watumishi wengi wamedhalilishwa na serikali hii ambayo imekuwa ikitumia mabavu kuwawajibisha watu bila kufuata sheria za nchi,” alisema Dk, Mashinji. “Suala la rushwa katika nchi ni jambo la kimfumo ambapo kila unapoona kunamtu katumbuliwa kwaajili ya rushwa basi kuna idadi kubwa ya watu ambao wanashiriki katika rushwa hiyo,” aliongeza Dk Mashinji.Aidha, alisema kuwa utaratibu wa Rais kuwatumbua watumishi kwenye mikutano ya hadhara kwa kutumia ushabiki wa wananchi hauwezi kulisaidia taifa kufanikiwa katika kuwaletea mabadiliko ya kweli wananchi wake. “Magufuli ametumbua watumishi wengi sana tangu aingie madarakani lakini niwaulize sukari imeshuka bei au mchele umeshuka bei lakini kila siku tunasikia watu wametumbuliwa bila kuwa na tija kwa taifa,” alisema.
 
Kaka Mnyika amejifia mwenyewe. Mwaka jana aligundua nani daifu kati ya JK na Mbowe. Ametulia, hasikiki si kwa kuwa anaumwa bali anafikiria kilichotokea juu la Edo.
Sasa kama mbona unatofautiana na kiongozi wako msome kidogo.

Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji amemtaka Rais Magufuli apunguze utumbuaji majipu. Adai inadhalilisha Watumishi wa SerikaliAlisema pamoja na kuwa CHADEMA wanaunga mkono kitendo cha kuwashughulikia mafisadi pamoja na watumishi wasio timiza majukumu yao ipasavyo lakini hawako tayari kuendelea kushuhudia ambavyo amekua akivunja sheria za nchi. “Watumishi wengi wamedhalilishwa na serikali hii ambayo imekuwa ikitumia mabavu kuwawajibisha watu bila kufuata sheria za nchi,” alisema Dk, Mashinji. “Suala la rushwa katika nchi ni jambo la kimfumo ambapo kila unapoona kunamtu katumbuliwa kwaajili ya rushwa basi kuna idadi kubwa ya watu ambao wanashiriki katika rushwa hiyo,” aliongeza Dk Mashinji.Aidha, alisema kuwa utaratibu wa Rais kuwatumbua watumishi kwenye mikutano ya hadhara kwa kutumia ushabiki wa wananchi hauwezi kulisaidia taifa kufanikiwa katika kuwaletea mabadiliko ya kweli wananchi wake. “Magufuli ametumbua watumishi wengi sana tangu aingie madarakani lakini niwaulize sukari imeshuka bei au mchele umeshuka bei lakini kila siku tunasikia watu wametumbuliwa bila kuwa na tija kwa taifa,” alisema.
 
"Pamoja na udhaifu alikuwa nao JK alikuwa sio mwoga wa kusikia maoni na ushauri kutoka upinzani hata kama hakuyatekeleza yote , hapo sina budi kumsifu, Mh. Magufuli anaonyesha udhaifu mapema sana anaogopa kukosolewa"

Huyu ni Mchungaji Msigwa
Unafiki,elimu ya kuunga unga ya Msigwa!
 
Mkuu Ritz,

Haya ndiyo yumayoyakataa kwenu nyie wamaccm, siyo kila anachosema kiongozi wako ni sahihi, mara nyingine nao hughafilika. Sasa wajinga wachache hasa wanaccm hupakachuka tu kwa kila anachosema kiongoxi wao na kuunga mkono hata kama ni Upumbavu.

Nakupa mf kidogo, Hebu angalia suala la Bunge kuonyesha live, Hivi kuna mantiki gani kuzuia Bunge kuonyeshwa live? Sasa ukitaka kuona namna akili za wanaccm vilivyooza angalia wanavyounga mkono, na kama vile haitoshik muangalie, Msukuma, Halima Bulembo na wengine wakitetea hoja hiyo......!!!

Nakupa mfano mwingine, Hebu angalia suala la Kuzuia sukari ya nje kuingia Nchini. Wanaccm na viongozi wao walipiga mayowe kwa furaha baada ya Serikali kuzuia sukari kuingia Nchini, Lakini mara baada ya Serikali kukiri kukurupuka kuchukua uamuzi huo, bado micccm ilikeneka kwa furaha kwa uamuzi huo...!!! Huu ujinga wa kuunga mkono kila linalosemwa na kiongozi wako ndio uliotufikisha hapa kama. Kama mngekuwa na utamaduni wa kukosoana kama tufanyavyo sisi kamwe tusingekuwa hapa.

Nakupa mfano wa mwisho, Hebu angalia Obama anavyolia na kujutia pale alipoamua kuivamia Libya kijeshi, lakini kama kungekuwa na mtu mwenye uthubutu akamwambia mzee hapa unakosea, kamwe majuto haya yasingekuja. Upumbavu wa mtu mmoja umesababisha maisha ya wanalibya kuwa shakani kila sekude inayopita. Hii ni kutoka na ZIDUMU FIKRA ZA KIONGOZI WANGU. huu ujinga acheni ndugu yangu Ritz

Kwa kudhihirisha kwamba siyo utamaduni wenu kukosoana ndiomaana unashangaa mimi kutofautiana na kiongozii wangu. Tambua, mimi si mwanaccm na naomba usiku na mchama Mwenyezi Mungu azidi kunilinda na choyo na chachu ya ccm, kwani kuishi ktk ujinga sijazoea maishani mwangu.

Ni hayo tu mkuu wangu Ritz

BACK TANGANYIKA
 
Sio tu kwamba chadema walisema, bali Mgufuli kadhihirisha hilo, bado unasema mnyika hana adabu? Kuhusu Magufuli hataki kukosolewa akikosolewa wayu wanafikishwa mahakamani, kwa hiyo ni vyema tu kusema anatumia madaraka yake vibaya, hafuati sheria na katiba ya nchi.
 
Wanaukumbi,

Hii ni kauli ya kiongozi wa Chadema John Mnyika, alisema nasikitishwa na jambo moja. Tumefika hapa kutokana na udhaifu wa Rais Kikwete.

Dua lake limekubaliwa yeye pamoja na wafuasi wa Chadema JK kaondoka sasa yupo Dr.John Magufuli siyo dhaifu.

Mbadala wa dhaifu ni kupata mtu jasiri bahati nzuri mmefanikwa muungeni mkono rais jasiri John Magufuli, dhaifu kaishaondoka.

Umepiga chembe ya moyo...lazima wakae...kule Mnyika anasema Rais ana mamlaka ya kuondoa vifungu kwrnye bajetu....leo Ukawa wsnalia rais hana mamlaka ya kufanya lolote bila kumbembeleza kamishna wa bajeti...Bwana Mbowe...burudani..inaendelea.hapa watabaki kuzungusha ndimi kwenye midomo kama wanatafuna kiazi cha moto.
 
KILA MTU ANAIJUA NIA YA MCH MSIGWA NA MARAFIKI ZAKE NI KUJINASIFU KUWA WANAWEKA MADUDU HADHARANI YA HUYO RAIS WA AWAMU YA NNE WANAYEMSIFIA. WENYE UFAHAMU TUMEELEWA.

HONGERA JPM KWANI ZIPO NAMNA NYINGI WABUNGE WA UPINZANI WANAWEZA KUZITUMIA KUKULETEA TAARIFA ZA MADUDU YA SERIKALI IKIWA NI PAMOJA NA HATA KUJA KUKUONA, KAMA KWELI WANALINDA MASLAHI YA WANYONGE, NA SIO HII TABIA YA KUMTUKANA JK NA FAMILIA YAKE KWA MGONGO WA UHURU WA BUNGE.

LEO HAWA WALIOKUWA WANAJINASIFU KUWA WATETEZI WA WANYONGE WANAKASIRISHWA PALE PESA ZINAPOELEKEZWA KUSAIDIA WANYONGE!!!! WATANZANIA TUMEWAELEWA NA 2020 SANDUKU LA KURA LITAAMUA MSIJE KUSEMA MMEIBIWA KURA.

JUZI WAMEPINGA KWANINI PESA NYINGI IMEENDA KWENYE MIUNDOMBINU, NADHANI KWA HIZI MVUA ZINAZOENDELEA NA HALI YA MIUNDOMBINU WATAKUBALIANA NAMI HATA KIMOYOMOYO KUWA MIUNDOMBINU NI MUHIMU KAMA MISHIPA YA DAMU KWENYE MWILI.

KASI YA MHE RAIS INAWAUMIZA ROHO SANA WAPINZANIA. PANDENI TAX NA DALADALA MSIKIE MAONI YA WANANCHI KUHUSU UTENDAJI WA MHE RAIS, MKIMALIZA NENDENI VIJIJINI NDIO MTAJUA KUWA TAYARI MNAISOMA NAMBA.

Queen Esther

"Pamoja na udhaifu alikuwa nao JK alikuwa sio mwoga wa kusikia maoni na ushauri kutoka upinzani hata kama hakuyatekeleza yote , hapo sina budi kumsifu, Mh. Magufuli anaonyesha udhaifu mapema sana anaogopa kukosolewa"

Huyu ni Mchungaji Msigwa
 
Sio tu kwamba chadema walisema, bali Mgufuli kadhihirisha hilo, bado unasema mnyika hana adabu? Kuhusu Magufuli hataki kukosolewa akikosolewa wayu wanafikishwa mahakamani, kwa hiyo ni vyema tu kusema anatumia madaraka yake vibaya, hafuati sheria na katiba ya nchi.
Lini na wapi Magufuli kasema hataki kukosolewa?unaweza kututajia watu hawa wawili tu waliofikishwa mahakamani kama unavyosema kwa kumkosoa rais Magufuli?
 
Sasa kama mbona unatofautiana na kiongozi wako msome kidogo.

Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji amemtaka Rais Magufuli apunguze utumbuaji majipu. Adai inadhalilisha Watumishi wa SerikaliAlisema pamoja na kuwa CHADEMA wanaunga mkono kitendo cha kuwashughulikia mafisadi pamoja na watumishi wasio timiza majukumu yao ipasavyo lakini hawako tayari kuendelea kushuhudia ambavyo amekua akivunja sheria za nchi. “Watumishi wengi wamedhalilishwa na serikali hii ambayo imekuwa ikitumia mabavu kuwawajibisha watu bila kufuata sheria za nchi,” alisema Dk, Mashinji. “Suala la rushwa katika nchi ni jambo la kimfumo ambapo kila unapoona kunamtu katumbuliwa kwaajili ya rushwa basi kuna idadi kubwa ya watu ambao wanashiriki katika rushwa hiyo,” aliongeza Dk Mashinji.Aidha, alisema kuwa utaratibu wa Rais kuwatumbua watumishi kwenye mikutano ya hadhara kwa kutumia ushabiki wa wananchi hauwezi kulisaidia taifa kufanikiwa katika kuwaletea mabadiliko ya kweli wananchi wake. “Magufuli ametumbua watumishi wengi sana tangu aingie madarakani lakini niwaulize sukari imeshuka bei au mchele umeshuka bei lakini kila siku tunasikia watu wametumbuliwa bila kuwa na tija kwa taifa,” alisema.

sheria ipi haya manyumbu ya chadema?

hivi cdm walikuwa wanataka nchi hii....waifanye
nini?
 
Mkuu Ritz,

Haya ndiyo yumayoyakataa kwenu nyie wamaccm, siyo kila anachosema kiongozi wako ni sahihi, mara nyingine nao hughafilika. Sasa wajinga wachache hasa wanaccm hupakachuka tu kwa kila anachosema kiongoxi wao na kuunga mkono hata kama ni Upumbavu.

Nakupa mf kidogo, Hebu angalia suala la Bunge kuonyesha live, Hivi kuna mantiki gani kuzuia Bunge kuonyeshwa live? Sasa ukitaka kuona namna akili za wanaccm vilivyooza angalia wanavyounga mkono, na kama vile haitoshik muangalie, Msukuma, Halima Bulembo na wengine wakitetea hoja hiyo......!!!

Nakupa mfano mwingine, Hebu angalia suala la Kuzuia sukari ya nje kuingia Nchini. Wanaccm na viongozi wao walipiga mayowe kwa furaha baada ya Serikali kuzuia sukari kuingia Nchini, Lakini mara baada ya Serikali kukiri kukurupuka kuchukua uamuzi huo, bado micccm ilikeneka kwa furaha kwa uamuzi huo...!!! Huu ujinga wa kuunga mkono kila linalosemwa na kiongozi wako ndio uliotufikisha hapa kama. Kama mngekuwa na utamaduni wa kukosoana kama tufanyavyo sisi kamwe tusingekuwa hapa.

Nakupa mfano wa mwisho, Hebu angalia Obama anavyolia na kujutia pale alipoamua kuivamia Libya kijeshi, lakini kama kungekuwa na mtu mwenye uthubutu akamwambia mzee hapa unakosea, kamwe majuto haya yasingekuja. Upumbavu wa mtu mmoja umesababisha maisha ya wanalibya kuwa shakani kila sekude inayopita. Hii ni kutoka na ZIDUMU FIKRA ZA KIONGOZI WANGU. huu ujinga acheni ndugu yangu Ritz

Kwa kudhihirisha kwamba siyo utamaduni wenu kukosoana ndiomaana unashangaa mimi kutofautiana na kiongozii wangu. Tambua, mimi si mwanaccm na naomba usiku na mchama Mwenyezi Mungu azidi kunilinda na choyo na chachu ya ccm, kwani kuishi ktk ujinga sijazoea maishani mwangu.

Ni hayo tu mkuu wangu Ritz

BACK TANGANYIKA
Mkuu wangu wa Boda,

Mada yangu na hoja yangu viongozi wako kila siku walikuwa wanasema hii serikali ya JK ni dhaifu na lege lege sasa amekuja rais jasiri Magufuli, viongozi wako wanalalamika kupita kiasi msome Mbowe hapa chini.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amemshitaki Rais John Magufuli mbele ya maaskofu kadhaa wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Mbowe amedai kuwa Serikali yake ya Awamu ya Tano imekuwa ikiwatimua watumishi mbalimbali wa umma bila kuwapa nafasi ya kuwasikiliza kupitia kampeni ya kupambana na ufisadi, inayotambulishwa kwa kaulimbiu ya ‘utumbuaji majipu’. Akizungumza jana katika ibada maalumu ya shukrani kwa kumaliza uchaguzi mkuu salama, iliyofanyika kwenye Usharika wa Nshara wa Dayosisi ya Kaskazini ya KKKT na kuhudhuriwa na Mkuu wa KKKT, Askofu Dk. Frederick Shoo, na maaskofu wastaafu Dk. Erasto Kweka na Dk. Martin Shao, Mbowe alisema (wapinzani) hawaridhishwi na hatua ya serikali ya Rais Magufuli kuendeleza timuatimua na kuwasimamisha kazi watumishi wa umma 160 tangu aingie madarakani bila kuwapa nafasi ya kuwasikiliza."

Labda mzee wa boda, mnataka Magufuli aongoze vipi?
 
Back
Top Bottom