Kuna walioolewa na miaka 24 wakiwa mabikira na ndoa zao zimevunjika au hazina amani na kuna walioolewa na miaka 35 wakiwa hawana bikira na ndoa zao zimedumu na zina amani
Kuna watoto wamezaliwa ndani ya ndoa na mwisho wa siku wakaja kuwa mashoga na wasagaji na kuna watoto wamezaliwa nje ya ndoa na mwisho wa siku wakaja kuwa watiifu na wacha Mungu tukumbuke ili kupata 10 siyo lazima uchukue 5 + 5 tu au 10 + 0 tu hata 7 + 3 au 9 + 1 nk nazo zitakupa jibu 10
Maisha ni kama mtihani ambao kila mtu ana maswali yake tofauti na ya mwingine na watu wanapokosea ni pale wanapojaribu kuigilizia majibu ya watu wengine badala ya kutafuta majibu yanayoendana na maswali yao na ndipo wanapojikuta wanafeli
Hakuna anayechelewa wala anayewahi kila mtu yupo kwenye timezone yake mwenyewe kulingana na kusudi lake hapa duniani na siku tutakapoujua huu ukweli mchungu basi tutaacha kukariri maisha na tutaacha kulazimisha watu waishi kutokana na matakwa ya watu wengine na ili kufurahisha watu wengine