Gharama za vitambulisho vya Taifa

Si Dar mwezi wa saba nilikuwa Ilemela, kata ya Buswelu hivyo vitambulisho watu walikuwa wanapata huduma zote bure, sijajua huko Tabora halmashauri kama imekubali hili
Mimi siipendi CCM hata kwa sekunde 2 lakini vitambulisho ni bure kwa watanzania wote.
 
Si Dar mwezi wa saba nilikuwa Ilemela, kata ya Buswelu hivyo vitambulisho watu walikuwa wanapata huduma zote bure, sijajua huko Tabora halmashauri kama imekubali hili
labda ni kwa halmashauri zinazoongozwa na wapinzani
 
Ni habari ya kusikitisha kutoka jimboni kwa mhe: Magdalena Sakaya kuhusiana na upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa.Ili upate kitambulisho unatakiwa kulipia Gharama zifuatazo kutokana na Umri.

1.Kijana anatakiwa kulipa tsh 20000.
2.Wakina Mama Tsh 10000
3.Wakina baba Tsh 15000
4.Wazee Tsh 5000.

My take
Mbona dar tuligawiwa bure inakuweje sehemu nyingine ? Au TRA imehamia huko? Nisaidieni wadau
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA)

TAARIFA KWA UMMA

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa kijamii wa “Jamii Forum” kuhusu upatikanaji Vitambulisho vya Taifa kwa tozo kutegemeana na umri wa mwombaji. Taarifa hiyo inadai vitendo hivyo kufanyika jimbo la Mhe. Magdalena Sakaya (Mb), Kaliua mkoani Tabora.

Awali ifahamike kuwa Mamlaka haijaanza rasmi Usajili wa Umma kwenye Mkoa wa Tabora na Wilaya zake na kwamba maandalizi ya kuanza zoezi hilo ndiyo kwanza yameanza. Usajili unaofanyika ni kwa wananchi wa Kata za Karibu ambazo ni Ufukutwa, Ushokola, Kaliua Mashariki na Magharibi.

Ili mwombaji kusajiliwa lazima awe na nakala ya viambatisho vinavyothibitisha umri wake, makazi na urai; na inapobidi kuja na vithibitisho vingine vinavyothibitisha Uraia wa wazazi kujiridhisha urai wa mwombaji.

Madai ya mtoa taarifa yanaonekana kuandikwa kichochezi bila kuwepo ushahidi kwa kumhusisha Mhe. Mbunge; mbali na kukosekana taarifa msingi zenye undani wa matukio yanayodaiwa kufanyika kuhalalisha madai yake na kuisaidia Serikali kufuatilia na kuwafichua wale wote wenye mchezo huo mchafu zinazolenga kuzorotesha jitihada za Serikali.

Baada ya kusoma taarifa hizo Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa imefanya ufuatiliaji wa kina na kuthibitisha pasipo shaka kuwa madai hayo niya uongo na yamelenga kuchafua Mamlaka na kuzorotesha shughuli za Usajili wananchi zinazoendelea kwa sasa nchi nzima.

Tunamuomba mtoa taarifa iwapo ana ushahidi wa madai hayo kutoa taarifa kituo chochote cha Polisi kilichopo karibu naye au kufika ofisi za TAKUKURU wilayani hapo au Ofisi yetu ya Wilaya ya Kaliua ili suala hilo liweze kufuatiliwa na kukomeshwa mara moja.

Mamlaka inasisitiza zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa ni bure na Mwananchi hatakiwi kulipa gharama zozote.

Limetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)
 
Ni habari ya kusikitisha kutoka jimboni kwa mhe: Magdalena Sakaya kuhusiana na upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa.Ili upate kitambulisho unatakiwa kulipia Gharama zifuatazo kutokana na Umri.

1.Kijana anatakiwa kulipa tsh 20000.
2.Wakina Mama Tsh 10000
3.Wakina baba Tsh 15000
4.Wazee Tsh 5000.

My take
Mbona dar tuligawiwa bure inakuweje sehemu nyingine ? Au TRA imehamia huko? Nisaidieni wadau
Umejiridhisha kabla ujaleta Uzi wako humu mjomba?
 
Ni habari ya kusikitisha kutoka jimboni kwa mhe: Magdalena Sakaya kuhusiana na upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa.Ili upate kitambulisho unatakiwa kulipia Gharama zifuatazo kutokana na Umri.

1.Kijana anatakiwa kulipa tsh 20000.
2.Wakina Mama Tsh 10000
3.Wakina baba Tsh 15000
4.Wazee Tsh 5000.

My take
Mbona dar tuligawiwa bure inakuweje sehemu nyingine ? Au TRA imehamia huko? Nisaidieni wadau
Wenyewe washakanusha kule, km una ushahidi peleka kunakohusika usiendelee kujambisha watu tenaa
 
hili mbona liko wazi siku nyingi..kwa dar kijana ni elf hamsini
kama hukufanya kipindi kile wako mitaani
ukienda sasa ndio bei yake hio
Jamani hii serikali siipendi ila vitu vingine tuwe wakweli tu.

Dar kitambulisho ni bure ila ukipoteza ndo utalipia 20,000 ili utengenezewe kingine. Me nimechukua kitambulisho mwez September kama sikosei.
 
hujaelewa
 
Wap huko!
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA)

nida

TAARIFA KWA UMMA

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa kijamii wa “Jamii Forum” kuhusu upatikanaji Vitambulisho vya Taifa kwa tozo kutegemeana na umri wa mwombaji. Taarifa hiyo inadai vitendo hivyo kufanyika jimbo la Mhe. Magdalena Sakaya (Mb), Kaliua mkoani Tabora.

Awali ifahamike kuwa Mamlaka haijaanza rasmi Usajili wa Umma kwenye Mkoa wa Tabora na Wilaya zake na kwamba maandalizi ya kuanza zoezi hilo ndiyo kwanza yameanza. Usajili unaofanyika ni kwa wananchi wa Kata za Karibu ambazo ni Ufukutwa, Ushokola, Kaliua Mashariki na Magharibi.

Ili mwombaji kusajiliwa lazima awe na nakala ya viambatisho vinavyothibitisha umri wake, makazi na urai; na inapobidi kuja na vithibitisho vingine vinavyothibitisha Uraia wa wazazi kujiridhisha urai wa mwombaji.

Madai ya mtoa taarifa yanaonekana kuandikwa kichochezi bila kuwepo ushahidi kwa kumhusisha Mhe. Mbunge; mbali na kukosekana taarifa msingi zenye undani wa matukio yanayodaiwa kufanyika kuhalalisha madai yake na kuisaidia Serikali kufuatilia na kuwafichua wale wote wenye mchezo huo mchafu zinazolenga kuzorotesha jitihada za Serikali.

Baada ya kusoma taarifa hizo Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa imefanya ufuatiliaji wa kina na kuthibitisha pasipo shaka kuwa madai hayo niya uongo na yamelenga kuchafua Mamlaka na kuzorotesha shughuli za Usajili wananchi zinazoendelea kwa sasa nchi nzima.

Tunamuomba mtoa taarifa iwapo ana ushahidi wa madai hayo kutoa taarifa kituo chochote cha Polisi kilichopo karibu naye au kufika ofisi za TAKUKURU wilayani hapo au Ofisi yetu ya Wilaya ya Kaliua ili suala hilo liweze kufuatiliwa na kukomeshwa mara moja.

Mamlaka inasisitiza zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa ni bure na mwananchi hatakiwi kulipa gharama zozote.

Back
Top Bottom