Gharama za umeme zimepanda lini? Tsh.10,000 kwa unit 72 badala ya 82 imekuwaje?

Kwa kawaida, kwa wale wa matumizi ya chini, hawaruhusiwi kununua umeme wa 10,000/= kwa mwezi. Yaani toka tarehe 1 mpaka mwisho wa mwezi. Ukifanya hivyo, mwezi unaofuata, hizo unit zilizozidi kwenye zile unit 75,utazilipia kwa ongezeko la bei kubwa. Kwa hiyo, ukinunua umeme tena, watakata kwanza hicho kiasi, na fedha itakayobaki, utapewa umeme.

Nakushauri kama hizo unit 75 zinakutosha, basi usizidishe. Kwani ukiendelea hivyo, watakutoa, na kukuunganisha kwenye zile bei za juu.
Halafu ni kwa Nini Hawa majizi Tanesco jamani ukiwa chini ya unit 75 mbona hawakupeleki kwenye tarrif 4 ya hiyo matumizi lakini eti mpaka uwafuate ofisini kwao huko.
Na je mbona mtu ukishazidisha tu jamani wanakupeleka huko kwa gharama za juu
 
Ni kweli usemalo. Na natamani TANESCO waje hapa watoe ufafanuzi. Sisi wengine hatufikishi units 75 kwa mwezi lakini tunaambulia units 28.10 kwa Tshs. 10,000 kila tununuapo umeme. Ukiuliza kwa nini unaambiwa uandike barua kwa Meneja kwa Tanesco wa eneo lako kubadilishiwa Tarriff!

Binafsi nimefanya hivyo tangu mwaka jana lakini mpaka sasa sijabadilishiwa hiyo tarriff. Kwa nini wasibadilishe tarriff automatically bila urasimu na mlolongo huo mrefu hivyo maana mita zetu zinarekodi kamili wanaotumia chini ya units 75 na wa juu ya hapo!!?
Uko Mkoa gani Mkuu?
 
Ukitumia reference zilezile alizotumia yule jamaa kuwashtaki Tigo na tcra Basi hili la tariff huku TANESCO unaeza fungua kesi na ukapata fidia yako nzuri tuu Mana hata elimu ya hili tuu wanashindwa kutoa
 
Mimi natumia around 2 units per day,
kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa wananiibia kwa kuniweka kwenye kundi nisilostahili ?, halafu huo utaratibu ni wa kijinga, kwanini wasiweke standard ?, yaani mtu ukitumia zaidi basi unaonekana fisadi, wangeweka standard ili mtu unapotumia zaidi unalipa kadri ulivyotumia, nasikia hata ukienda kuwaomba wakuhamishe wanasumbua sana ??, natamani tungepata shirika binafsi la ugavi wa umeme ili lishindane na kugawana wateja na hawa wezi tanesco
Ni kweli licha ya kuandika barua kwa meneja lakini bado ni shida, wao tanesco siku zote wana sisitiza kutumia umeme kidogo ndio maana wanatoa motisha kwa hao wanaotumia 0-75 units kwa mwezi.
 
Sisi tusiokuwa na tarrif mnatuumiza roho tu jamani. Imagine sh. 10,000 tunapata units 28.1
Watusaidie na sisi jamani. Matumizi yangu yakizidi sana ni unit 25 kwa mwezi. Sijawahi zidi hapo. Hata hivyo nikinunua umeme wa shs 5000 napata unit 14 tuu.
 
Back
Top Bottom