Planet FSD
JF-Expert Member
- Oct 24, 2019
- 455
- 938
Leo nimeona mjadala mkubwa umekuwa ukiendelea kuhusiana na utofauti wa bei ya lita moja ya mafuta kati ya Zanzibar na Tanganyika.
Na picha zikisambaa mitandaoni kuonesha Zanzibar lita moja ni 2600+ TZS wakati Tanganyika ni 3100+ TZS, huku swali kubwa likiwa inakuaje bei iko chini Zanzibar kuliko Tanganyika.
Lakini kubwa hasa ambalo limenifanya niandike uzi huu ni kuwa, swali hili linaulizwa kwa insinuation ya kwamba huenda Zanzibar wanalipa kidogo kwa lita kwa sababu ndiko anakotokea Hangaya. Kusema ukweli sifurahishwi na jinsi Hangaya anavyotupeleka, lakini hapa naomba nimtetee.
Kabla hata hajawa rais wote tunajua gharama za kuingiza bidhaa kutoka nje kwa Zanzibar ziko chini kuliko Tanganyika. Iwe gari iwe TV, Zanzibar unavipata kwa gharama ndogo kuliko Tanganyika. Imekuwa hivyo miaka nenda rudi, sio jambo jipya.
Ukweli ni kwamba kinachotuletea tabu watanganyika ni msururu na lundo la kodi na tozo zisizo na kichwa wala miguu. Bidhaa ndogo tu ila ina utitiri wa kodi. Jaribu kununua gari kutoka Japan halafu peleka Zanzibar, na jaribu kuleta model ya gari hiyo hiyo Tanganyika ndiyo utajua hujui. Unaweza kujipatia kitv chako cha bei rahisi kule kisiwani, wazenji hawana tabu na wewe, balaa litakukuta pale bandarini utakapokutana na watanganyika wenzako.
Kwahiyo kama lita ya mafuta mpaka ifike bandari zetu za Tanzania CIF yake ni 1162 TZS, yakiingizwa Zanzibar na Tanganyika, hayawezi kuwa sawa. Na wenzetu wanajaliana, wanapeana relief muda huu wa mgogoro huko ulaya mashariki.
Kwahiyo watanganyika tusimtafute mchawi. Hangaya asilaumiwe kabisaaaa. Tumuache atukune na kutupuliza fuuu!